peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 12,824
- 21,428
Amepewa wizara ya malia asili na utalii na utalii umeshakufa siku nyingi. Katiba yetu pia CCM inasema ni nzuri,kujua kusoma na kuandika, unalamba ubunge then uwaziri. Watanzania we zangu,wizara ya fedha,wizara ya madini, wizara ya malia asili na utalii,wizara ya elimu,wizara ya afya na wizara ya sheria na katiba ni wizara muhimu sana na zinahitaji watu mahiri na waadilifu.ila kwa tanzania ni oppositeDamas Ndumbaro anakuwaje Waziri?
Nimemsikia muda mrefu kwenye migogoro ya mpira mara aibukie TFF mara aibukie Simba hadi akafungiwa..
Ni aina ya wale 'watafuta fursa 'popote..
Kaanzia kwenye mpira ambako hakuna achievement yoyote inayoweza kumhusisha zaidi ya migogoro hadi kama kaenda jaribu bahati kwenye Ubunge akashinda Kwa mbeleko za chama
Now eti ni Waziri halafu wizara nyeti Sana..
Wizara ya Utalii huyu mtu hafai hata ukatibu kata Kwa maoni yangu.
Anapewaje dhamana ya vitalu vyote vya uwindaji?.. dhamana ya kutangaza nchi na kutuletea watalii?
Tayari keshaanza kutia shaka..
Je, maamuzi yake Yana 'Green light' kutoka hata Kwa waziri Mkuu?
Mara asimamishe watu kazi mbele ya media mara awape vitalu waliowahi nyang'anywa.
Ile 'lack of coordination ' aliyosema Rais Samia naiona waziwazi Kwa huyu.
Maamuzi yake Yana 'go ahead' kutoka wapi?
Bodi ya utalii?
Idara ya wanayama pori?
Ofisi ya Waziri Mkuu?
Huyu Mtu amefikaje hapo Wizara ya Utalii? Ndo kusema mtu yeyote akiwa mbunge anaweza pewa wizara yoyote?