Mtu kama Damas Ndumbaro anakuwaje Waziri?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,108
115,837
Damas Ndumbaro anakuwaje Waziri?

Nimemsikia muda mrefu kwenye migogoro ya mpira mara aibukie TFF mara aibukie Simba hadi akafungiwa..

Ni aina ya wale 'watafuta fursa 'popote..

Kaanzia kwenye mpira ambako hakuna achievement yoyote inayoweza kumhusisha zaidi ya migogoro hadi kama kaenda jaribu bahati kwenye Ubunge akashinda Kwa mbeleko za chama
Now eti ni Waziri halafu wizara nyeti Sana..

Wizara ya Utalii huyu mtu hafai hata ukatibu kata Kwa maoni yangu.

Anapewaje dhamana ya vitalu vyote vya uwindaji? Dhamana ya kutangaza nchi na kutuletea watalii?

Tayari keshaanza kutia shaka. Je, maamuzi yake Yana 'Green light' kutoka hata Kwa waziri Mkuu?

Mara asimamishe watu kazi mbele ya media mara awape vitalu waliowahi nyang'anywa.

Ile 'lack of coordination ' aliyosema Rais Samia naiona waziwazi Kwa huyu.

Maamuzi yake Yana 'go ahead' kutoka wapi?
Bodi ya utalii?
Idara ya wanayama pori?
Ofisi ya Waziri Mkuu?

Huyu Mtu amefikaje hapo Wizara ya Utalii? Ndo kusema mtu yeyote akiwa mbunge anaweza pewa wizara yoyote?
 
Hao bodi ya utalii alisimamisha mkurugenzi wa kwa ushauri wa kipuuzi kutoka kwa CAG. Hicho kitalu hata PM hawezi kuweka ulimi wake. Wenye nchi wamerudi wanarejesha wanyama wao kibindoni. Tulieni sindano ziwaingie. Mtamkumbuka JPM muda si mrefu.
 
Mpaka hapoa watakapo igundua sura yake halisi, hakika atakuwa amepiga kikweli kikweli! Hata mimi nitakuwa Mtanzania wa mwisho kuamini uadilifu wa huyu Mheshimiwa.

Ni mpambania fursa na ulaji, asiye jificha. Huko waliko muweka, atatajirika mara dufu aisee. Muonekano wake, siyo wa mtu wa kukataa mzigo wa aina yoyote ile. Time will tell.
 
Damas Ndumbaro anakuwaje waziri?
Nimemsikia mda mrefu kwenye migogoro ya mpira mara aibukie TFF mara aibukie Simba had akafungiwa...
Kuna vitanzania fulani hivi vilazaliwa na mapungufu kibao na vinaishi ishi tu kwasababu ya haki ya kuishi,, hivyo ndivyo vinavyoonekana kuwa na haki ya kuongoza nchi hii.

Sisi Watanzania wengine tubaki kuwa wakosoaji na walipa kodi na wapiga kura tu.
 
AENDE NGORONGORO AKAWATOE WALE WAMASAI. WENGINE WALILIPWA HADI FIDIA ILA WAMERUDI NDANI YA HIFADHI.
Mkuu ishu ya Ngorongoro ni zaidi ya wengi waijuavyo.

Kulikuwa na mradi wa kuwezesha jamii na wananyamapori kuishi pamoja kwenye hifadhi. Baadhi ya vijiji vilivyokuwa vinaishi kwenye hifadhi viliruhusiwa kuendelea kuishi humo kwa mkataba maalum, kuhakikisha hawadhuru ikolojia ya hifadhi, lakini pia kuwa sehemu ya ulinzi na vivutio. Mradi huu ulilenga pia kupunguza migogoro ya ardhi kati ya hifadhi na jamii zinazoishi karibu na hifadhi.

Hata hivyo, pasi na matarajio, watu walianza kuitana..baadhi ya wafanyakazi wakajikatia maeneo..mambo ni mengi kwa kweli.
 
Mkuu ishu ya Ngorongoro ni zaidi ya wengi waijuavyo.

Kulikuwa na mradi wa kuwezesha jamii na wananyamapori kuishi pamoja kwenye hifadhi. Baadhi ya vijiji vilivyokuwa vinaishi kwenye hifadhi viliruhusiwa kuendelea kuishi humo kwa mkataba maalum, kuhakikisha hawadhuru ikolojia ya hifadhi, lakini pia kuwa sehemu ya ulinzi na vivutio. Mradi huu ulilenga pia kupunguza migogoro ya ardhi kati ya hifadhi na jamii zinazoishi karibu na hifadhi.

Hata hivyo, pasi na matarajio, watu walianza kuitana..baadhi ya wafanyakazi wakajikatia maeneo..mambo ni mengi kwa kweli.
Hawezi akajua yote hayo huyo mbaguzi.
 
Mawaziri , wakuu wa mikoa na wilaya utopolo wako wengi Sana sio huyo tu mwingine huyu hapa
Screenshot_20210429-211312.png
 
Damas Ndumbaro anakuwaje waziri?
Nimemsikia mda mrefu kwenye migogoro ya mpira mara aibukie TFF mara aibukie Simba had akafungiwa..

Ni aina ya wale 'watafuta fursa 'popote..

Kaanzia kwenye mpira ambako hakuna achievement yeyote inayoweza kumhusisha zaidi ya migogoro Hadi kama kaenda jaribu bahati kwenye ubunge akashinda Kwa mbeleko za chama
Now eti ni waziri halafu wizara nyeti Sana..

Wizara ya Utalii huyu mtu hafai hata ukatibu kata Kwa maoni yangu..
Anapewaje dhamana ya vitalu vyote vya uwindaji?.. dhamana ya kutangaza nchi na kutuletea watalii?

Tayari keshaanza kutia shaka..
Je maamuzi yake Yana 'Green light' kutoka hata Kwa waziri mkuu??
Mara asimamishe watu kazi mbele ya media mara awape vitalu waliowahi nyang'anywa ....

Ile 'lack of coordination ' aliyosema Rais Samia naiona waziwazi Kwa huyu..
Maamuzi yake Yana 'go ahead' kutoka wapi?
Bodi ya utalii?
Idara ya wanayama pori?
Ofisi ya waziri Mkuu?

Huyu Mtu amefikaje hapo wizara ya Utalii? Ndo kusema mtu yeyote akiwa mbunge anaweza pewa wizara yeyote???
Alifungiwa kujihusisha na soka maisha kwa utapeli
 
Back
Top Bottom