Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 205
- 941
Waziri Ndumbaro ni msomi mkubwa wa Sheria, walau kwa kurejea historia ya elimu yake bila kujali uhalisia wa mambo anayofanya.
Kwamba Waziri Ndumbaro hajui kuwa FIFA hairuhusu serikali kuingilia masuala ya mpira wa miguu? na tangu lini uzalendo unalazimishwa? Ni kukosa ubunifu wa kuendeleza michezo nchini, au ni kiburi kinachokuzwa na tabia za wanasiasa kutoa matamko pasipo kujali sheria za nchi?
Binafsi nimeshangaa sana kuona anapiga marufuku mashabiki kuvaa jezi za timu pinzani zinazotoka nje ya Tanzania kwa hoja mufilisi za uzalendo na kwamba wanaovaa watatakiwa kuwa na passport za nchi hizo pamoja na watakaokaidi watashughulikiwa na Polisi.
Tangu lini uzalendo ukalazimishwa? kwa sheria gani?
Kwa maarifa yangu madogo ya Civics ya Form 2, Uzalendo wa mtu ni kuipenda nchi yake, siyo kupenda Chama wala Serikali. Waziri haoni kuwa kuvalisha watu tisheti za Samia na kuweka mabango ya Serikali na mama anaupiga mwingi uwanjani inakwaza watu wengine wasioipenda CCM? Nani alisema uzalendo ni kupenda mambo yanayoifurahisha CCM na Serikali pekee?
Nataka nimwambie Ndumbaro, kama kweli yeye ni mzalendo apige kwanza marufuku tabia hii. Hapo kweli atakuwa amekunywa maji ya bendera ya uzalendo wa Tanzania.
Lakini anapaswa kutambua kuwa hana uwezo wowote wa kufanya anachokipanga, pia Simba na Yanga ni kubwa kuliko yeye, na asipokuwa makini zitamng'oa kwenye uwaziri wake.
Pia soma: Mambo haya ndio yanaidharaulisha Nchi yetu hadi kuonekana imekufa