Mtu anaanzaje kumchukia ndugu yake?

Mtu anaanzaje kumchukia ndugu yake?

We acha tu! Ufukara chanzo cha matatizo mengi sana. Utajikuta unaamini mambo ya uchawi hivi hivi, nadra sana uwe masikini ukawa na roho nzuri na upendo wa kweli. Mungu atujaalie kuvuka huo mtihani.
Hujasikia matajiri wanaoenda na vieite zao kutafuta mambo ya kichawi/kishirikina?
 
Sasa si bora wewe kakutolea povu hajakulaani?
Sipati shida mtu akinilaani wakati sijamkosea. Najua laana yake haitanipata. Kitabu cha Mithali kinasema hivyo pia kwamba "...laana isiyo na sababu haimpigi mtu"
 
Nilikuwa naendesha gari langu kwa kasi, macho mbele bila kutazama tazama kushoto au kulia kwa barabara. Ndugu yangu aliniona akanisimamisha nimpe lifti lakini bahati mbaya mimi sikumuona nikampita. Tulipoonana uso kwa uso alikuwa amejaa hasira, akaniuliza kwanini siku ile alinisimamisha sikusimama. "Kwakuwa siku hizi umenunua Hummer, unatuona sisi ndugu zako hatufai, eeh? Hutaki hata kutusalimia njiani. Haya, we endelea tu." Ndugu yangu alinifokea kisha akaondoka. Japo sikuona kosa langu nilimfuata nikaenda kumuomba msamaha yaishe.

Siku nyingine ndugu yangu huyo alinipigia simu kuniomba nimkopeshe milioni mbili. Nikamjibu kuwa hapa nilipo hata laki mbili sina. Pesa nilizokuwa nazo zimetumika kukarabati nyumba yangu. Kabla sijamaliza kujieleza alikata simu kwa hasira, baadaye akanifuata nyumbani na kuanza kunigombeza: "Sema leo tujue moja, undugu umevunjika? Kwanini siku hizi hutaki kuwasaidia ndugu zako?"

Dawa ya moto sio moto, nikamjibu kwa upole kuwa ni kweli sina pesa. Nikipata nitampa hata bila kudai anirudishie. Aliondoka kwa hasira huku akiongea mwenyewe njia nzima mpaka mtaa wetu wakajua tumekosana. Huo ni mfano tu wa maisha ya ndugu na ndugu wanaokosana na kuchukiana hata kwa mambo madogo madogo.

Najiuliza mtu anaanzaje kumchukia ndugu yake? Anaanzaje kupanga kulipa kisasi au kumfanyia fitina ndugu yake kwa sababu ya mambo kama hayo huku anakiri kwamba yeye ni mcha Mungu? Katika 1Yoh 3: 14-15 tunaambiwa kwamba mtu asiyempenda ndugu yake anakaa mautini. Na kwamba yeyote amchukiaye ndugu yake anafananishwa na muuaji, na kwamba muuaji hana uzima wa milele ndani yake. Katika 1 Yohana 4:20 tunaambiwa pia kwamba Mtu akisema, anampenda Mungu, huku anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hamwoni.

Ulishawahi kuchukiwa na ndugu yako au jirani yako? Ulichukua hatua gani?
Duuu! umenigusa sana nilichukiwa na mdogo wangu, niliye mpenda hasa, kwa dhati ya moyo!! Mungu ni shahidi yangu, tena bila sababu za wazi !! ila kwa sababu ya upendo nikamsamehe sana tu!! nikawa ninawaza huenda karogwa!!

Mbaya zaidi hata akawa hanipi heshima nayostahili ile ya ukubwa ya udada!! km vile ''shikamoo Dada!!! nooo!! akawa ananipa za hivi ''habari yako'' tena kwa dharau mnoo!!.....nikawa namjibu ''safi!''

Nilimsema mara moja kuwa acha '' dogo dharau''! kwa upendo tu! sikurudia tena, neno hilo......yaani hapo ndo km nimechochea moto ndo akazidi kabisaa akawa ananipa '' third class treatment''

mfano alinikalisha kwenye pick up nyuma huko na mahiti ya Babangu!! daa nika nyuti tu! tuka safiri umbali mrefuuu wa siku tatu! yaani dogo alinidharau kweli!! lkn utafanyaje sasa nikapiga kimya tu! hapo ikabidi niukubali ukweli kuwa huyu ana dharau hasa!

Nikajiuliza kwa nini anafanya vile Wakati namzidi Ujuzi, Elimu nzuri tena kwa mbali mnooo, Pesa, EXposure!! kwa vile tu ana kanyumba ka mawazo!! Ok! nikapiga kimya!!

Siku moja akanishusha kwenye Cab aliyo kodi tena waziwazi!! mbele ya umati wa watu wengi.....kwa kuwa tu nilienda panda humo!.....ikanibidi nishuke tu.. nikapiga teke umbali kiasi!!....lkn maajabu ya Mimi! nikampenda ivoivo!! si unajua kipenda roho jamani!

Tena hata na hela nikawa nampa!! yaani hata najishangaa mpaka sasa! so nilicho kifanya nilikamata mkopo kazini wa haja!! nikashushaa kitu cha maana hapo Salasala juu jirani na Gwajima!! Kimya kimya tu! rasmi nika keep distance la maana hasa!!

kilichotokea sasa kabla ya ujenzi nili ishi kimaskini kweli kweli!! bin shida tena wakajua huyu jamaa yetu kapigika hasa,.... tena maksudi kabisaa Baada ya hayo mamikasa, ghafla nikasepa zangu abroad kimya kimya tu!

hakuna cha kwaheri au tutaonana bali watanisikia CNN, liwalo na liwe!! so long as hawaniheshimu na kunijali basi mie ntajijali binafsi jua langu mvua yangu mbelekwa mbele!! mpaka leo ni hivo!! ...

lkn fununu walikuwa nazo kwa mbaali, lkn ajili ya midharau mingi wakaona nachoma manyoya ya kuku Mlevi.....Ok! sawa wa kwanza, pili wa tatu duuu!! wakaona huyu jamaa yuko serious......

sasa hivi majuzi wakanitafuta bana!!!...... Hamad huyooo! wakanipata! kuumbe walijua connections zangu ila sababu ya kiburi tu wakajifanya hawajui ..... yaani kilicho mpata dogo kinatia huruma sana! tena sana!!

Ninaamini sana! Maandiko ya Biblia nanukuu ''usidharau Baba yako na Mama yako, siku zako zipate kuwa nyingi katka nchi upewayo na Bwana Mungu wako!! hili Neno ni kweli na uzima kwa yeyote anaepitia uzi huu.......

Ila sababu hawakunithamini tokea awali baasi.......utawafanyaje sasa?? saana ukijisogeza na kutatua maatizo yake atarudia palepale!! hakika kwa dharau zile nilijua mie nikipata shida ni zangu tu.... hebu nipe ushauri Mleta mada na yeyote anae pitia hapa.....
 
Huyo ndugu yako ana ujasiri sana . Sijui anawezaje kumkaripia mtu anayemiliki Hummer!!!
Una akili sana weye mkubwa!! kwa sababu Gate zake tu!! hapo nyumbani mpaka anifikie!! kazi kweli kweli mara ataambiwa acha mseji getini. mara ana kikao, mara yuko safarini , mara amepumzika, mara ana sali! mara......maramaraaraaramara!!

kwanza km mie ukinifokea ndo kabisaaa!!...hutanijua labda uwe kaka yangu ntajishusha!
 
Pole sana, siyo ndugu tu, kwa ujumla watu wako wa karibu...
 
Back
Top Bottom