Mgeni wa Jiji
JF-Expert Member
- Jul 27, 2017
- 10,488
- 20,039
Wachawi ndugu wachunguze wa kwako
Ndugu lawamaNilikuwa naendesha gari langu kwa kasi, macho mbele bila kutazama tazama kushoto au kulia kwa barabara. Ndugu yangu aliniona akanisimamisha nimpe lifti lakini bahati mbaya mimi sikumuona nikampita. Tulipoonana uso kwa uso alikuwa amejaa hasira, akaniuliza kwanini siku ile alinisimamisha sikusimama. "Kwakuwa siku hizi umenunua Hummer, unatuona sisi ndugu zako hatufai, eeh? Hutaki hata kutusalimia njiani. Haya, we endelea tu." Ndugu yangu alinifokea kisha akaondoka. Japo sikuona kosa langu nilimfuata nikaenda kumuomba msamaha yaishe.
Siku nyingine ndugu yangu huyo alinipigia simu kuniomba nimkopeshe milioni mbili. Nikamjibu kuwa hapa nilipo hata laki mbili sina. Pesa nilizokuwa nazo zimetumika kukarabati nyumba yangu. Kabla sijamaliza kujieleza alikata simu kwa hasira, baadaye akanifuata nyumbani na kuanza kunigombeza: "Sema leo tujue moja, undugu umevunjika? Kwanini siku hizi hutaki kuwasaidia ndugu zako?"
Dawa ya moto sio moto, nikamjibu kwa upole kuwa ni kweli sina pesa. Nikipata nitampa hata bila kudai anirudishie. Aliondoka kwa hasira huku akiongea mwenyewe njia nzima mpaka mtaa wetu wakajua tumekosana. Huo ni mfano tu wa maisha ya ndugu na ndugu wanaokosana na kuchukiana hata kwa mambo madogo madogo.
Najiuliza mtu anaanzaje kumchukia ndugu yake? Anaanzaje kupanga kulipa kisasi au kumfanyia fitina ndugu yake kwa sababu ya mambo kama hayo huku anakiri kwamba yeye ni mcha Mungu? Katika 1Yoh 3: 14-15 tunaambiwa kwamba mtu asiyempenda ndugu yake anakaa mautini. Na kwamba yeyote amchukiaye ndugu yake anafananishwa na muuaji, na kwamba muuaji hana uzima wa milele ndani yake. Katika 1 Yohana 4:20 tunaambiwa pia kwamba Mtu akisema, anampenda Mungu, huku anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hamwoni.
Ulishawahi kuchukiwa na ndugu yako au jirani yako? Ulichukua hatua gani?
Kazi ipoNdugu wakweli siku hizi ni mke, watoto zako, baba&mama na washkaji. Mbali na hapo tegemea maumivu tu.
Mimi siongei na mdogo wangu na wajomba zangu chanzo mali zangu na kazi yangu. Wanatamani nifukuzwe kazi, nimepeleleza wanasema najisikia naringa nimekuwa sasa.
Mkuu unawafahamu vizuri waafrika/waswahili...,??Roho mbaya haijengi,waswahili tusaidiane,tubebane,ndg kwa ndg mbona wenzetu wahindi,waarabu wanainuana?
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Soma Biblia yote yamo humo..Tukiukemea kwa Jina la Yesu huo ushetani unaweza kutoka?
Nilikuwa naendesha gari langu kwa kasi, macho mbele bila kutazama tazama kushoto au kulia kwa barabara. Ndugu yangu aliniona akanisimamisha nimpe lifti lakini bahati mbaya mimi sikumuona nikampita. Tulipoonana uso kwa uso alikuwa amejaa hasira, akaniuliza kwanini siku ile alinisimamisha sikusimama. "Kwakuwa siku hizi umenunua Hummer, unatuona sisi ndugu zako hatufai, eeh? Hutaki hata kutusalimia njiani. Haya, we endelea tu." Ndugu yangu alinifokea kisha akaondoka. Japo sikuona kosa langu nilimfuata nikaenda kumuomba msamaha yaishe.
Siku nyingine ndugu yangu huyo alinipigia simu kuniomba nimkopeshe milioni mbili. Nikamjibu kuwa hapa nilipo hata laki mbili sina. Pesa nilizokuwa nazo zimetumika kukarabati nyumba yangu. Kabla sijamaliza kujieleza alikata simu kwa hasira, baadaye akanifuata nyumbani na kuanza kunigombeza: "Sema leo tujue moja, undugu umevunjika? Kwanini siku hizi hutaki kuwasaidia ndugu zako?"
Dawa ya moto sio moto, nikamjibu kwa upole kuwa ni kweli sina pesa. Nikipata nitampa hata bila kudai anirudishie. Aliondoka kwa hasira huku akiongea mwenyewe njia nzima mpaka mtaa wetu wakajua tumekosana. Huo ni mfano tu wa maisha ya ndugu na ndugu wanaokosana na kuchukiana hata kwa mambo madogo madogo.
Najiuliza mtu anaanzaje kumchukia ndugu yake? Anaanzaje kupanga kulipa kisasi au kumfanyia fitina ndugu yake kwa sababu ya mambo kama hayo huku anakiri kwamba yeye ni mcha Mungu? Katika 1Yoh 3: 14-15 tunaambiwa kwamba mtu asiyempenda ndugu yake anakaa mautini. Na kwamba yeyote amchukiaye ndugu yake anafananishwa na muuaji, na kwamba muuaji hana uzima wa milele ndani yake. Katika 1 Yohana 4:20 tunaambiwa pia kwamba Mtu akisema, anampenda Mungu, huku anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hamwoni.
Ulishawahi kuchukiwa na ndugu yako au jirani yako? Ulichukua hatua gani?
Mungu naye umemuweka wa pili?Jipende mwenyewe ndo ujifunze kumpenda mwingine...hii ndo falsafa yangu
Mh! mke ni ndugu siku hizi tayari ushatengenezwa wewe!Ndugu wakweli siku hizi ni mke, watoto zako, baba&mama na washkaji. Mbali na hapo tegemea maumivu tu.