Saikolojia ya hasira

Saikolojia ya hasira

MIHAYO1710

Member
Joined
Apr 7, 2018
Posts
22
Reaction score
50
SAIKOLOJIA YA HASIRA NA UFALME WA MUNGU

"A Rhapsody For Kingdom Anger Management Strategies"

Amani Na Salama 🙏

Mimi sijambo na Karibu.

MASWALI YA KUJIULIZA.

1.Umewahi kuwa na hasira?
2.Huwa unapata hasira Mara kwa Mara?
3.Ukiwa na hasira huwa unafanyaje?
4. Je, Kuna ndugu, jamaa au marafiki umewafuta kabisa na hutaki hata kusikia habari zao kutokana na hasira?

5.kuna wakati hasira inajaa mpaka unahisi Koo linauma/Kuwaka Moto😥

6. Umewahi kujuta kwa kufanya maamuzi mabaya kutokana na hasira?
7.Hasira imewahi kukugarimu e.g kutozwa faini, kufungwa au kutengwa na jamii?

8. Je, Kuna faida au Hasara kwenye hasira?

SOMA BILA UVIVU

HASIRA ni sehemu ya hisia Kali za ndani zimpatazo mtu hasa anapokutana na upinzani Fulani.

Hakuna binadamu asiyekasirika, kwa Sababu hasira Ni hisia za kawaida za kuzaliwa (Inborn).

Hata hivyo Uwezo na kiwango cha kutawala hisia za hasira hutofautiana kati ya mtu mmoja na Mwingine.

🤔Mwanafalsafa wa zamani Aristotle aliwahi kusema

"Kukasirika kila mtu anaweza, lakini Kukasirika kwa sababu sahihi, kwa mtu sahihi, kwa Kiwango sahihi na kwa wakati sahihi Ni vigumu kwa kila mtu."

👉Lengo la Makala hi Ni kukufanya uwe na Uwezo wa kuhimili Hasira zako! Na ukikasirika Basi iwe ni kwa sababu sahihi, wakati sahihi, kwa Kiwango sahihi na kwa mtu sahihi! Ili usijikute kwenye matatizo.

👇
Ukiwa na Uwezo mkubwa wa kudhibiti hasira zako utaonekana mtu mwema na muungwana kwa mwenzi wako, familia yako na jamii kwa ujumla!

🤔Kama mshauri wa masuala ya kisaikolojia, nimekutana na wateja kadhaa wanaosumbuka na Hasira, Wengi walikiri kuwa, kutokana na kuwa na hasira za ghafla na za Mara kwa mara hujikuta wameleta fujo na madhara makubwa. Zaidi Sana wengine imewapelekea kuepukwa na ndugu, jamaa na marafiki kadhaa! Mmoja Aliniambia

"Kwenye vikao vyetu vya ukoo wananijua, Mara kwa Mara huwa wanaepuka kubishana na Mimi."

Hata hivyo Hali hiyo Ilionekana kumuumiza Sana!

Fikiria, Staff member wenzako wanakuogopa kwa hasira zako!

"Jamaa akifumka Hapa, mtiti wake siyo poa Kabisa"

Ukifahamu wanakwepa hata kukudadisi Mambo ya kawaida kwa sababu ya hasira zako Kama za mkizi, unajisikiaje?

AINA ZA HASIRA KISAIKOLOJIA

Kisaikolojia zipo aina kadhaa za hasira, aina Hizi zimechambuliwa kutokana na kisababishi Cha hasira yenyewe Kama Ifuatavyo.

👉 Hasira ya haki. Hii kwa kimombo tunaita Righteous Anger. Hii ni hasira chanya, Ni hasira inayositahili na kuhitajika! Ni hasira ambayo huinuka ukiona kitu/Jambo Fulani haliendi Sawa Sawa, mfano ukaona mtu anaonewa na kunyanyaswa, hasira hii hupelekea kukupa Nguvu hata za kujitoa mhanga ili umsaidie! Kwa hiyo hii Ni hasira Nzuri!

MFANO WA HASIRA YA HAKI

(Yesu aliwahi kucharaza viboko na kupindua meza za watu waliokuwa wamegeuza nyumba za ibada kuwa sehemu ya harambee na biashara maarufu Kama pango la wanyang'anyi) Soma Luka 19:45-46 au Marko 13:15-17

⛔Kuna siku niliingilia Kati kuzuia mwizi asiuawe kwa kupigwa mawe! Akili zilikuja kujua kuwa Nilikuwa kwenye risk ya Kufa Mimi Mwenyewe, wakati difenda ya polisi ilipokaribia😭 Hata hivyo nilifurahi kwa kuwa jamaa alinusurika!

👉Hasira nyingine hutokana na kuzidiwa au kuelemewa na Mambo mengi, inaitwa overwhelmed anger!

Mfano kutopata usingizi vizuri, kuwa na ratiba iliyosonga sana, kukosa muda wa mazoezi na kuburudika!

👉 Hasira za kutaka kuendesha/kutawala hii kwa kimombo tunaita Manipulative anger,

Ni hasira inayolenga kuwatisha watu ili wakuogope uwaendeshe unavyotaka! Sometimes hii mtaani inaitwa "Kupiga mkwara"

Baadhi ya viongozi madikteta uchwara, hutumia hasira hii ili afanye anavyotaka bila kufuata katiba Wala sheria.

👉 Hasira itokanayo na mapito!

Hii Ni hasira kutokana na matukio aliyopitia mhusika kama vile kusalitiwa na mpenzi, kufiwa, kunyanyaswa kingono nk. (Post traumatic stress Disorder)

👉Pia hasira kwa kiasi Fulani huweza kisababishwa na Hali ya kimaumbile/kifiziolojia kwa mfano Kiwango Cha sukari kuwa Chini Sana mwilini, kukosa mlinganyo sawia wa homoni na kemikali kwenye Ubongo kutokuwa sawa! (Hormonal na brain chemical imbalances.

👉 Sababu zingine-zingine Ni hofu ya maisha na usalama, Mfano michongo hakiendi halafu unasikia serikali kwa kutumia kinywa Cha Mwigulu imeongeza aina 17 za tozo, hapo unakuta mtu ana hasira tu!

HABARI NJEMA

Pamoja na sababu zote, nilizotaja Hapo na zile uzijuazo Mwenyewe, wanasaikolojia wote tunakubalina kuwa hasira inaweza kudhibitiwa/kuzuiwa au kupunguzwa

UNAFANYAJE?
👉Isome hasira vizuri yako bila kujipendelea/kujihurumia

👉Ukisha ielewa vyema, Epuka vitu/Hali/vichochezi vya hasira yako.

👉Ufundishe ubongo wako kubaini mapema Mazungumzo, hali au mazingira yanayoweza kukupelekea kwenye hasira.

HASIRA KWENYE UFALME WA MUNGU IKO HIVI

Tuliozaliwa mara ya pili na kufanyika kuwa watoto wa Mungu kwa kumwamini Yesu Kristo (Yohane 1:12) Tunayo nafasi Nzuri zaidi ya kuishinda hasira na kuwa Wenye furaha.

Kwa sababu gani?

👉Unapozaliwa Mara pili, unakuwa kiumbe kipya na unabeba vinasaba na Hali ya baba wa mbinguni.

Maana imeandikwa "Kama Yeye alivyo, ndivyo na sisi tulivyoona humu Ulimwenguni" (1 Yohane 4:17b)

MUNGU YUKOJE?

Zaburi 103:8 " Bwana amejaa huruma na Neema, Haoni HASIRA upesi, Ni mwingi wa fadhili."

👉Sifa ya Mungu wetu Ni hiyo ☝️

KWA NINI HASIRA HAIFAI?

Pamoja na faida moja ya hasira Kama tulivyoona kule juu, bado Hasara inaonekana kuwa Ni kubwa Sana.

🎤HASIRA HAITENDI HAKI. Mtu mwenye hasira kamwe hawezi kutenda Haki, kwa sababu vitendo vingi huvifanya akiongozwa na hasira kuliko akili.

Yakobo 1:19-20 "Hayo mnajua ndugu zangu wapenzi: Basi kila mtu awe mwepesi wa kusikia, Bali Si mwepesi wa kusema, Wala KUKASIRIKA kwa Maana hasira ya mwanadamu haiitendi Haki ya Mungu."

So, kwenye hasira hakuna Haki. Viongozi wengi Wenye hasira hushindwa kutenda Haki kea wanaowaongoza! Kamata kamata na vitisho Ni dalili za kiongozi mwenye hasira 😥

🎤 HASIRA HULETA UGOMVI na uasi! Bila hasira ugomvi na uasi utatoka wapi?

Mithali 29:22 "Mtu wa hasira huchochea ugomvi, na Mtu mwenye ghadhabu huasi Sana."

🎤 Hasira hutenda mabaya. Kuna watu wanaozea kwenye magereza mbalimbali kutoka na kufanya unyama kwa msukumo wa hasira tu, wanajutia hasira Yao what a tragedy!

Zaburi 37:8 "Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, usikasirike mwisho wake Ni kutenda mabaya."

😭 Kumbuka Kaini alimuua ndugu Yake Abeli kutokana na kujaa wivu na hasira! (Mwanzo 4:3-8)😭

Hata nabii Yona alifikia hatua ya kumwomba Mungu amuue, kwa Maana moyo wake ulijaa wivu na hasira! Soma Yona 3:10 na Yona 4:1-4
⛔Utaona Mungu anamuuliza Yona, Je watenda vyema KUKASIRIKA?

🎤 Hasira nyingi Ni Upumbavu. Umejilaumu na kujuta Mara ngapi kutokana kufanya maamuzi au tendo fulani kwa Hasira?

Mhubiri 7:9 "Usifanye haraka KUKASIRIKA Rohoni mwako, Maana hasira kukaa kifuani mwa wapumbavu."

🎤 Hasira huondoa ulinzi.

😁 Mdomo hukiponza kichwa ndivyo hasira pia iwezavyo kukuponza, mtu Asiye na hasira Ni vigumu kujikwaa katika kusema au kutenda.

Mithali 25:28 "Asiye tawala Roho Yake Ni mfano wa mji uliobomolewa, usio na kuta.

JINSI YA KUFANYA

🔥JIPATIE HEKIMA NA UFAHAMU. Ndiyo maana Nipo Hapa kukufundisha, ukipata UFAHAMU wa kutosha juu ya Jambo Fulani Ni rahisi kukabiliana nalo kwa ufasaha!

Mithali 29:11 "Mpumbavu hudhihirisha Hasira Yake yote, Bali mwenye Hekima huizuia na kuituliza."

👉Umeona 🖕? Mwenye Hekima huizuia na kuituliza Hasira! Kwa hiyo uwezo wa kuituliza na kuizuia hasira yako unategemea Kiwango Cha Hekima na uelewa wako! Glory

Pia Mithali 14:29 "Asiye mwepesi wa hasira anafahamu nyingi. Bali mwenye Roho ya hamaki hutukuza upumbavu."

Zaidi ya hayo Mithali 16:32 "Asiye mwepesi wa hasira Ni mwema kuliko shujaa, na Mtu aitawalaye roho Yake kuliko mtu atekaye mji."

🔥SAMEHE KWA FAIDA YAKO!

kusamehe Ni njia moja Nzuri na rahisi Sana kumaliza hasira! Kama Kuna mtu alikukosea na kukusababishia hasira hizo, Basi dawa Nzuri Ni kumsamehe! Ukimsamehe moyo wako utafunguka na hautasikia hasira juu Yake!

Mithali 19:11 "Busara ya Mtu huiahirisha hasira Yake. Nayo ni fahari Yake KUSAMEHE makosa."

🔥EPUKA UKARIBU na mtu mwenye hasira Kali.

Hasira wakati Mwingine Ni contagious! Inaambukizwa, kuenea na kusambaa! Ukiwa na urafiki na Mtu mwenye hasira Ni rahisi kuiga tabia zake! Ndiyo maana Kuna makabila Hapa Tanzania yanajulikana kabisa kwa hasira na mapanga! Why? Wanaigana tu! Hii huitwa "nurture imitation"

Mithali 22:24-25 "Usifanye Urafiki na mtu mwenye hasira nyingi, Wala usiende na Mtu wa ghadhabu nyingi. Usije ukajifunza njia zake na kujipatia nafsi yako mtego."

⛔Hii ☝️ inanikumbusha kipindi Fulani nikiwa mwanafunzi, kijana mmoja rafiki yangu (mwenye asili ya hasira hasira) alinishawishi tukampige mkwara mwalimu mmoja tuliyekuwa tunaamini Ni mnoko sana pale shuleni!
Nilikubali na tukaenda, tulichokifanya kidogo Mimi nifukuzwe shule🤣

JE, TUSIKASIRIKE KABISA?

Waefeso 4:26-27 "Mwe na hasira, ila msitende dhambi; Jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka." Wala msimpe nafasi ibilisi."

👌🏿Kukasirika kwa muda mrefu Ni kumpa shetani nafasi ya kufanya uhalifu kwa kutumia Mikono au Mdomo wako."

⛔🚫 Kumbuka hasira imetajwa Kama matendo ya mwili yasiyo na kibali kwa Mungu! Mwenye hasira hawezi kuingia mbinguni!

Wagalatia 5:19-20 "Basi matendo ya mwili Ni dhahiri, ndiyo Haya. Uasherati, ufisadi, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, HASIRA, Fitina faraka uzushi husuda etc.

NI IPI SULUHU YA KUDUMU?

🔥🔥 Hakikisha Roho Mtakatifu anakaa ndani yako na kukuongoza, Yeye Ni kinyume na hasira!

👉 Wagalatia 5:22-23 "Lakini tunda la Roho Ni UPENDO, furaha, Amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi juu ya Mambo hayo hakuna sheria."

Umebarikiwa milele 🙏

Kumbuka 👇

#Shetani Anaogopa mtu anayejua kitu

🎤Kama hujampa Yesu Kristo Maisha, Hii Ni fursa kwako kufanya hivyo! Karibu katika Ufalme wa Mungu!
 

Attachments

  • 1784442473751.jpg
    1784442473751.jpg
    49.8 KB · Views: 9
Back
Top Bottom