Ben Zen Tarot
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,392
- 7,875
Na wachaga na wahaya!Roho mbaya haijengi,waswahili tusaidiane,tubebane,ndg kwa ndg mbona wenzetu wahindi,waarabu wanainuana?
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Na wachaga na wahaya!Roho mbaya haijengi,waswahili tusaidiane,tubebane,ndg kwa ndg mbona wenzetu wahindi,waarabu wanainuana?
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Kei kufanyaje sasa, embu fafanua kidogo.
Sasa huyo alimaanisha unamuibia kishirikina.Mimi kuna mtu alinijia ofisini kwangu amechukia sana, akanambia kwanini namuibia wateja wake? Maskini yangu, sijawai kumuibia wateja, wanakuja wenyewe kwangu
Ndugu lawama
Unashangaa mtu mwenye chuki kwenda kanisani?
Hata wachawi uwa wanaenda kusali kanisani..!
Mkuu hakuna nchi isiyo polisi bhana, sema isiyo jeshi.Ni nature ya binadamu wote?
Kuna nchi nilisikia haina Polisi. Ni kweli? Kama ni kweli basi watu katika nchi hiyo hawachukiani
Unaweza ukajipenda mwenyewe lakini akatokea mtu akakuongezea upendo kwa kukupenda.Jipende mwenyewe ndo ujifunze kumpenda mwingine...hii ndo falsafa yangu
Huyo bw mdogo wako jishushe kwake kumuongelesha uone kama hashuki 'temper'.Ndugu wakweli siku hizi ni mke, watoto zako, baba&mama na washkaji. Mbali na hapo tegemea maumivu tu.
Mimi siongei na mdogo wangu na wajomba zangu chanzo mali zangu na kazi yangu. Wanatamani nifukuzwe kazi, nimepeleleza wanasema najisikia naringa nimekuwa sasa.
Hongera bana hammer aise unatiringisha bana ungetaja gari tu inatosha hata hapa utajiongesa maaduiNilikuwa naendesha gari langu kwa kasi, macho mbele bila kutazama tazama kushoto au kulia kwa barabara. Ndugu yangu aliniona akanisimamisha nimpe lifti lakini bahati mbaya mimi sikumuona nikampita. Tulipoonana uso kwa uso alikuwa amejaa hasira, akaniuliza kwanini siku ile alinisimamisha sikusimama. "Kwakuwa siku hizi umenunua Hummer, unatuona sisi ndugu zako hatufai, eeh? Hutaki hata kutusalimia njiani. Haya, we endelea tu." Ndugu yangu alinifokea kisha akaondoka. Japo sikuona kosa langu nilimfuata nikaenda kumuomba msamaha yaishe.
Siku nyingine ndugu yangu huyo alinipigia simu kuniomba nimkopeshe milioni mbili. Nikamjibu kuwa hapa nilipo hata laki mbili sina. Pesa nilizokuwa nazo zimetumika kukarabati nyumba yangu. Kabla sijamaliza kujieleza alikata simu kwa hasira, baadaye akanifuata nyumbani na kuanza kunigombeza: "Sema leo tujue moja, undugu umevunjika? Kwanini siku hizi hutaki kuwasaidia ndugu zako?"
Dawa ya moto sio moto, nikamjibu kwa upole kuwa ni kweli sina pesa. Nikipata nitampa hata bila kudai anirudishie. Aliondoka kwa hasira huku akiongea mwenyewe njia nzima mpaka mtaa wetu wakajua tumekosana. Huo ni mfano tu wa maisha ya ndugu na ndugu wanaokosana na kuchukiana hata kwa mambo madogo madogo.
Najiuliza mtu anaanzaje kumchukia ndugu yake? Anaanzaje kupanga kulipa kisasi au kumfanyia fitina ndugu yake kwa sababu ya mambo kama hayo huku anakiri kwamba yeye ni mcha Mungu? Katika 1Yoh 3: 14-15 tunaambiwa kwamba mtu asiyempenda ndugu yake anakaa mautini. Na kwamba yeyote amchukiaye ndugu yake anafananishwa na muuaji, na kwamba muuaji hana uzima wa milele ndani yake. Katika 1 Yohana 4:20 tunaambiwa pia kwamba Mtu akisema, anampenda Mungu, huku anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hamwoni.
Ulishawahi kuchukiwa na ndugu yako au jirani yako? Ulichukua hatua gani?
Ndugu Wa kweli ni yule mnayeendana naye,kumbuka yesu alipofuatwa na wazazi wake na kuambiawa mama yako na baba yako wanakutafuta , yeye alijibu baba Yangu na mama Yangu ni wale wanaolitii na kuliheshimu neno la Mungu.Ndugu wakweli siku hizi ni mke, watoto zako, baba&mama na washkaji. Mbali na hapo tegemea maumivu tu.
Mimi siongei na mdogo wangu na wajomba zangu chanzo mali zangu na kazi yangu. Wanatamani nifukuzwe kazi, nimepeleleza wanasema najisikia naringa nimekuwa sasa.
Hapo kwenye kuchukia umasikini hunifikii hata kwa nukta moja 😄Sasa si bora wewe kakutolea povu hajakulaani?
Mie niliambiwa najidai, mtu akasema naombea apate ajali na gari lake na hiyo kazi afukuzwe tuone kama ataendelea kujidai
Hao watu wanasema hivyo ni wale ndugu zako umekua nao bega kwa bega katika hali zote na kuna wakati umejinyima ili uwawekee sawa mambo yao. Kumbe vyovyote unavyofanya hauwaridhishi.
Nilichokuja kugundua, binadamu wote kama sio wengi wetu tuna roho ya ubinafsi ( kwanini isiwe mimi) tofauti inakuja pale unapojitahidi kuishinda hiyo roho mbaya na inakupa furaha ya kuishi na watu.
Hivyo basi, ukiwa kwenye jamii, ukiwa kazini, ukiwa na ndugu, jua kabisa watu hawafurahii mafanikio yako, kuanzia wanaosema hadi wale walionyamaza, enenda kwa tahadhari.
Si kazi ndogo kuifunza nafsi iushinde ubaya kwa wema. Ufurahie kwa dhati mafanikio ya mwingine, sio rahisi, lakini ukiweza kufikia hapo, utajiepusha na maradhi mengi sana.
Mwisho, nauchukia umasikini sana!
Ndugu wakweli siku hizi ni mke, watoto zako, baba&mama na washkaji. Mbali na hapo tegemea maumivu tu.
Mimi siongei na mdogo wangu na wajomba zangu chanzo mali zangu na kazi yangu. Wanatamani nifukuzwe kazi, nimepeleleza wanasema najisikia naringa nimekuwa sasa.
Hapo kwenye kuchukia umasikini hunifikii hata kwa nukta moja 😄
NaamWe acha tu! Ufukara chanzo cha matatizo mengi sana. Utajikuta unaamini mambo ya uchawi hivi hivi, nadra sana uwe masikini ukawa na roho nzuri na upendo wa kweli. Mungu atujaalie kuvuka huo mtihani.
Naam
Mwalimu Nyerere alipatia alivyosema, maadui wa mwanadamu ni:-
1. Maradhi
2. Ujinga
3. Umasikini
Ukipambana na matatu haya sawasawa unapata amani ya kutosha moyoni. Kinyume chake ni mateso.
Kabisa mkuu unakuta kitu kidogo ambacho mngeweza kusuruhisha ila na likaisha lakini mwishowe watu wabaya wanalikuzaNi maroho ya mafarakano utupwa kwenye ukoo hivyo upelekea ndugu kabisa kuwa PAKA na panya.
No huyo ni wa kwanza....nimezungumzia kidunianiMungu naye umemuweka wa pili?