Ajira yangu inanipa laki 5-6.
Nina mchumba na mtoto mmoja
Kwanza nikupongeze kwa kuweza kusave na kupata hicho kiasi, kuzichanga laki 6 kwa mwezi hadi kufikisha >7m ni jambo kubwa sana.
Kwa tafsiri yangu unaonesha una njaa sana ya mafanikio ndiyo maana umeweza kufanikisha kusave that amount.
With that into my mind nitashauri
1. Jipe malengo na mipango ya muda wa wastani, achana mipango ya muda ufupi mfupi.. Itakufanya ujione haupigi hatua. Weka mipango ya miaka mitatu hadi mitano, then unaji evaluate progress kila baada ya miezi kadhaa. Mfano: Unaweza kusema naendelea na kazi hii hii kwa miaka mitano ijayo, hapa hapa mji huu huu ninaoishi.. Nafungua biashara yangu ya mtaji wa 4m (japo sijui upo mji gani), then hiyo biashara kwa miezi mitatu ya mwanzo sitoona faida.. Baada ya miezi 6 itakuwa inanipa faida ya sh elf 80 kwa mwezi.. Unaendelea ku manourve kadiri unavyoendelea.
2. Kwa uzoefu wangu: Kuhamia nchi ya mbali hasa nchi za Dunia ya kwanza (kama tunavyoziita) at 33 is a big risk.. Kuna chance kubwa sana ukaukumbuka huo mshahara pamoja na opportunity uliyo nayo ya huo mtaji
3. Sitokushauri uitumie hiyo saving kwenda kulipa ada sijui veta au wapi, kuna vijana tayari wana ujuzi mtaani.. Ni suala la kuweka vigezo unavyovihitaji vya kimaadili, kinidhamu na uwajibikaji, utapata kijana mtafanya kazi.. Wewe utakuwa msimamizi mkuu
4. Achana kabisa na siasa mzee utajuta.
Nina mengi ya kuandika lkn napenda nihitimishe kwa kusema- nakutazama kama kijana mwenye maisha ya kati tayari, sema una nia ya dhati ya kufika maisha ya juu ndani ya muda mfupi, its better to retreat kidogo, relax kidogo huku unaweka mipango yako vema..
More importantly, hiyo ni cutting age.. Maamuzi unayoamua yana maana sana kwa keshokutwa yako.
Wish you luck!!