Mtu aliye intelligent, mwenye exposure na street-oriented anipe ushauri

Mtu aliye intelligent, mwenye exposure na street-oriented anipe ushauri

Kwanza nikupongeze kwa kuweza kusave na kupata hicho kiasi, kuzichanga laki 6 kwa mwezi hadi kufikisha >7m ni jambo kubwa sana.
Kwa tafsiri yangu unaonesha una njaa sana ya mafanikio ndiyo maana umeweza kufanikisha kusave that amount.

With that into my mind nitashauri
1. Jipe malengo na mipango ya muda wa wastani, achana mipango ya muda ufupi mfupi.. Itakufanya ujione haupigi hatua. Weka mipango ya miaka mitatu hadi mitano, then unaji evaluate progress kila baada ya miezi kadhaa. Mfano: Unaweza kusema naendelea na kazi hii hii kwa miaka mitano ijayo, hapa hapa mji huu huu ninaoishi.. Nafungua biashara yangu ya mtaji wa 4m (japo sijui upo mji gani), then hiyo biashara kwa miezi mitatu ya mwanzo sitoona faida.. Baada ya miezi 6 itakuwa inanipa faida ya sh elf 80 kwa mwezi.. Unaendelea ku manourve kadiri unavyoendelea.

2. Kwa uzoefu wangu: Kuhamia nchi ya mbali hasa nchi za Dunia ya kwanza (kama tunavyoziita) at 33 is a big risk.. Kuna chance kubwa sana ukaukumbuka huo mshahara pamoja na opportunity uliyo nayo ya huo mtaji

3. Sitokushauri uitumie hiyo saving kwenda kulipa ada sijui veta au wapi, kuna vijana tayari wana ujuzi mtaani.. Ni suala la kuweka vigezo unavyovihitaji vya kimaadili, kinidhamu na uwajibikaji, utapata kijana mtafanya kazi.. Wewe utakuwa msimamizi mkuu

4. Achana kabisa na siasa mzee utajuta.

Nina mengi ya kuandika lkn napenda nihitimishe kwa kusema- nakutazama kama kijana mwenye maisha ya kati tayari, sema una nia ya dhati ya kufika maisha ya juu ndani ya muda mfupi, its better to retreat kidogo, relax kidogo huku unaweka mipango yako vema..

More importantly, hiyo ni cutting age.. Maamuzi unayoamua yana maana sana kwa keshokutwa yako.

Wish you luck!!
Mkuu samahani cutting age maanake nini
 
Number 1 ni kamari ya sokoni mkuukikiumana meza inapangwa nyanya na mboga
Mtaa unahitaji kipawa chako,ubunifu wa hali ya juu
Kujilipua nje uwe na targeted countries kama una technical/mechanical skills unapata mchongo
mtaa unahitaji elimu yako wa kiasi kidogo sana
 
Sema veta kwenyewe magumashi ungeeleza una digrii ya Nini ili niangalie vilivyomo hafu nikushauri vizuri
 
Kifupi mkuu sasa hivi nafanyia kazi kula na nauli tu. Mshahara wote hautoshi hata kununua nguo kila mwezi. Jinsi nilivyoipata hiyo hela sio kwenye mshahara ila kwenye issue nyingine kabisa
Hata mm nilijua kabisa umeipata nje ya mshahara mkuu...hali tete sana kwa waajiriwa!
 
Ndgu; zingatia kujifunza kuanza biashara bila cash.. yaani kma unaweza ficha hiyo pesa kisha ukaomba kujiunga na one of garage.. ukasota huku unajifunza mapambano ya kimtaa.. ukafaulu .. ulichokusanya garage+ ulemtaji... Fungua spare part shop nunua hizo diagnoses mashine.. piga KAZI kma fundi mfanyabiashara.. hutajuta kaka..
Shukran kwa mchango wako.
Hapa itabidi niache kazi ili nifanye kazi
 
Kaza roho.. jifanye huna kitu kaka..Mimi huwa najipenda bure man..maana ni m'bahili Hadi kuna ndugu hawanipendi.. pesa MAALUM kwa MATUMIZI MAALUM sio eti kisa Nina kiasi fulani basi nile nile hovyo sijui nini. No [emoji41]
Pamoja sana
 
Mkuu.. namba tatu hapa ndiyo pa kudeal napo..
Hata mimi nipo kwenye mchakatok kama huo..!

Unaweza kutafuta nafasi za kusoma nje, au kazi ikiwezekana.

Zipo nchi ambazo kupata visa ni rahisi na zimepiga hatua kuliko hapa bongo
Visa free/ visa on entry
Kama
hong kong
Malaysia
Unaweza anza na hizi kupata mishe na exposure
Na nchi hizi za waarabu matajiri kama UAE UAE Dubai, Qatar - nchi tajiri duniani
Pia unaweza pata fursa - ukapata hata pesa zaidi kutosha ..kwenda nchi
Za ulaya
Na USA

Ila ukipata connection mkuu zama mbele tu!!
Huko kwa waarabu sina hata idea ya maisha yalivyo walau Ulaya kidogo kuna watu wawili watatu wamenipa ABC
 
Shida ni kwamba biashara ikifa nachukua muda mrefu sana kupata mtaji mwingine huku nikiugulia makato ya benki
Biashara haina dhamana broh, tafuta ujuzi VETA..

Mfn, unaweza ukajifunza ufundi cm, utakuwa fundi na duka lako la vifaa vya cm.. Demands is still high than supply, what you needs is market strategies , to win you're customers
 
Back
Top Bottom