Mtoto wa nje ya ndoa

Mtoto wa nje ya ndoa

Mimi naungana na Shishi kukwambia kwamba ni bora usiseme chochote maana mumewe wako atachanganyikiwa sana na kujiuliza maswali mengi ambayo wewe huwezi kuyajibu. Atakuuliza maswali kama yafuatayo: Umetembea na huyo jamaa kwa miaka mingapi wakati wa ndoa yenu? Kama mna watoto wengine anaweza kuuliza je na hawa watoto kuna uwezekano kuwa si wangu? Ni wakati gani ambapo mlikuwa mnakutana na mlikutana mara ngapi labda kwa wiki au kwa mwezi? Kama mumeo huwa anasafiri kikazi au kibiashara atakuuliza uliwahi kumleta nyumbani kwenu na mkafanya naye mapenzi labda kitandani kwenu? Na mengine mengi tu.

Kwa kifupi ukimwambia ndio itakuwa mwisho wa ndoa yenu. Najua hiki kitu kinakutesa sana na kukukosesha raha katika maisha yako ya kila siku, lakini siafikiani na wewe kumwambia mumeo. Unajua kwa sababu halinihusu mimi ni rahisi mno kusema mwambie atakusamehe, lakini ukweli mkuki kwa nguruwe kwa mwanadamu ni mchungu. Wanaume tulivyo katika maswala haya hasa kunapokuwa na mtoto aliyemlea miaka yote hiyo akijua kwamba ni mwanae halafu anakuja kuambiwa si mwanae basi inakuwa ni kasheshe ya hali ya juu. Ndio wako wanaume wachache wanaweza kusamehe lakini zaidi ya asilimia 80 ya wanaume hawawezi kusamehe na ndoa inakuwa imeingia dosari kubwa na itadorora na hatimaye huvunjika. Kila la heri lakini kumwambia mumeo IS A NO NO maana ndio itakuwa mwisho wa ndoa yenu. Na huyo taahira fanya juu chini ukate mawasiliano naye kabisa kama mnafanya kazi pamoja basi aanza kutafuta kazi nyingine kwa juhudi zako zote.

well said mpendwa, but hapo kwenye baba wa mtoto naweza sema hawezi kuitwa tahaira hata kidogo, kuna watu wengine damu zao hazipotei hovyo, ndio mana anania na mwanae, na kama huyu mama alishamwambia ni mimba yake then wat do u espect? ana haki zote za kumtaka mwanae, kasheshe ni kwa mume namuonea huruma kweli atakavyokabiliana na hii ctuation, wewe mama mwenzangu hebu roho ikuume ki vyako, ucumize za wenzio, 2lia na hicho kitu! sio kidogo kama unavyofikiria, nakwambia utaachwaaa na watoto wote baba atakuwa na wacwac nao kasheshe aende kupima hiyo DNA kwa wote, hapana ucwaaweke watoto kwenye risk ki hivyo.
 
Kidzogolae,
Yaelekea wewe umeshatoa adhabu kabisa maana unavyoonekana ni ungempa talaka mkeo tu akaanze maisha mapya, hayo unayoyasema.

wanaume mnajifanya mna mahasira sana, na ndio maana hamuambiwi jambo. Busara zenu tuzione katika vitendo na maneno yenu na sio MANGUMI na KUCHINJANA. Mbona sisi wanawake tunawafumania na bado tunawaandalia chakula na kuwatunzia siri? Hapa sitafuti sympathy, nataka tu kuonyesha kuwa mko tofauti.

Sijui kama umesoma alivyosema Abunuwasi - yeye ana wake baba mkubwa sasa na anamtunza. Labda "kifua" chako kidogo tu.

Nataka kujaribu kumpa mume wangu mtihani kumpima pressure kabla sijampa ishu, any idea how?.

kwani unadhani wewe hustahili talaka? unadhani ni jambo dogo hili?ucfananishe na cc kuwafumania kabisa! ur not serious sis.
 
This is serious!!!
My dear, pole sana kama ni kweli.
But you have to change the attitude. (THIS YOU HAVE TO LEARN) you are still deffensive. You are thinking more for yourself now and protecting your interests.(MY VIEWS)
Try to think and act like a selfless mother and wife. You will get a positive solution
 
"You have no right to call me father and I got no right to call you son" aliwahi kuimba Lucky Dube akielezea tukio kama la Da'Maindainda!
Japo nimechelewa pls let me share a live example related to this one:
Nina rafiki yangu wa karibu mno ambaye alililewa katika mazingara kama haya, yeye ni mzaliwa wa kwanza kwa wazazi wake, akifuatiwa na wadogo zake watatu wawili wa kike na mmoja wa kiume kwenye familia yao ya watoto wanne! Kimaisha wazazi wake hawa hawakuwa na maisha mazuri sana na huyu rafiki yangu alijitahidi mno kujaribu kuweka mambo sawa ikiwa ni pamoja kuwahudumia wadogo zake pamoja na wazazi wake.
Huyu rafiki yangu pia alijitahidi kufungua biashara ndogo ndogo kijijini kwao pamoja na kununua mashamba na BABA zake wadogo walikuwa ndio wasimamizi. Maisha yalisonga mbele kwa staili hii hadi mwaka 2005 alipougua baba yake mzazi, Rafiki yangu alifanya juhudi zote za kumpatia matibabu baba yake kwa muda mrefu bila mafaniakio na bahati mbaya baba yake alifariki mwaka huo huo. Alifanya taratibu zote za mazishi na baada ya kumaliza mambo yaliendelea kama kawaida!
KASHESHE! iliibuka mwaka 2007, ikiwa ni miaka miwili baada ya kumzika baba yake! Aliibuka baba mwingine na kudai kuwa ni mwanae! (HUYU rafiki yangu keshaoa tangu mwaka 1998 na ana watoto wawili!) Huyu baba kila kitu anafanana naye! Hiii ilimuweka huyu rafiki yangu katika hali ya kuchanganyikiwa na kutoamini na hadi leo hii hataki hata kumuona huyo baba yake mzazi (japokuwa ni mtu anayejiweza kiuchumi na rafiki yangu mambo yake sio mazuri) huyu baba kamuahidi mambo kibao lakini jamaa kagoma kabisa
KIBAYA ZAIDI baada ya huyu baba kujitokeza jamaa ilibidi amvae mama yake ambaye yuko kijijini na kumuuliza, mama alishindwa kumjibu akamuelekeza kwa wajomba zake ambao walimwambia kuwa ni kweli na hata BABA aliyemzika alikuwa anafahamu kuwa hakuwa mwanae! Baba zake wadogo nao pia walikuwa wanalifahamu hilo na walipoona kuwa ameshafahamu wakaanza kumuwekea mipaka, biashara na mashamba wamechukia na imekuwa kama wamemtenga! Jamaa amekuwa mpweke sasa kwani ndugu wa upande wa baba aliyemlea hawamtaki na wa upande wa bilogical father hawafahamu na wala hataki kuwasikia!
Honestly hii hali imemuathiri sana kisaikolojia na hata kiutendaji ameshuka sana pamoja na ushauri anaoupata mara kwa mara!
Tofauti kwa huyu rafiki yangu ni kuwa watu wengi katika familia walikuwa wanalifahamu hili baada ya mama kuamua kumueleza ukweli baba'ke kuwa wakati anaolewa alikuwa na mimba ya mtu mwingine, na huyu bwana (mwenye mimba) hakuwahi hata mara moja kujitokeza kwa mtoto.

Da'Mainda hili jambo ni gumu na lahitaji busara za ziada, ila kama ulivyoamua mueleze mumeo na pia mtoto kuepusha mabalaa ya uzeeni!
 
...pheeeeeeeeewww! hii ni kali...imeniacha mdomo wazi!

panahitajika busara ya hali ya juu sana kutoa ushauri juu ya hili, ukitilia maanani jamaa keshakuwa mtu mzima.
 
Haki lazima itendeke ,baba wa kubambikiziwa aambiwe ,mtoto nae aambiwe ,kuendela utasulubiwa na kosa jingine la kudanganya unamdanganya mtu mzima.Mtoto hana kosa kabisa ni haki yake kujua ,halikazalika huyo baba wa kambu nae hana kosa kosa lake ni kutokujua na kupoteza mahesabu ya mkewe
 
YOU BETTER FACE THE REALITIES OF LIFE,BY TELLING THE TRUTH.
if he was meant to be yours,he will understand

otherwise,
SO SORRY DEAR
 
Pole sana dada. Haupo peke yako, haya mambo yanatokea sana!

Ingawa unaonesha huna shaka juu ya baba halisi wa mtoto lakini ingalikuwa vema ukupata 'scientific proof' kwamba huyo mtoto si wa mume wako. Hili litakusaidia kufanya maamuzi sahihi.

Ukishapata hiyo proof kwamba mtoto si wa mume wako, kinachofuata ni kumwambia mumeo ukweli. Ni lazima ujiandae na mtikisiko utakaofuata baada ya hapo.
 
makosa makubwa uliyafanya mwanzo kabisa baada ya kugundua kuwa una mimba ambayo si ya mumeo bac hapo ndipo ungeanza mchakato wa kuyaweka haya mambo wazi, kwa sababu sasa tatizo kubwa litakalo ku(wa)face ni jamii inayowazunguka na maanisha ndugu wa upande wa mwanaume kwa sababu mwanaume anaweza kukusamehe lakini tatizo ndugu wakishakuja kujua itakuwa ni balaa kubwa, na uwezekano wa kujua lazima utakuwepo tu kwani mnaweza kusema iwe siri lakini nauhakika kabla ya mumeo hajatoa uhamuzi ni lazima atawauliza jamaa na marafiki ili apate ushauri kama wewe ulivyofanya hapa JF
kwa ushauri wangu japokuwa umeshachelewa bac jaribu kutochelewa zaidi wewe muite mumeo na taratibu mpe ukweli wote na pia uwe tayari kwa maamuzi yoyote,
 
Pole dada, Mimi binafsi nina jambo linalofanana na lako,miaka sita iliyopita nilikuwa na uhusiano na dada mmoja ambaye kwa wakati ule alikuwa na mchumba wake, ambaye walikuwa wakiishi sehemu tofauti tofauti,kazi ya huyu dada ilikuwa inamfanya awe asafiri mara kwa mara na hivyo kuwa anakutana na mwenza wake .Lakini katika mahusiano yetu huyu dada alipata uja uzito,kilichotokea ni kwamba alikuwa ajasafiri katika kipindi cha miezi mitatu hivi, hiyo ilifanya ajue wazi muhusika ni nani, na wakati huo maandalizi ya Ndoa yao yalikuwa yamekamilika.Baada ya miezi minne wakafunga ndoa wakati yule dada akiwa mja mzito,tulipojadiliano juu ya huo huja uzito alikubali kutotoa ,lolote na liwe.Kweli akajifungua mtoto wa kiume copyright na baba mimi,na akawa anataka niendelee kuwa baba wa mtoto wakati yeye ni mke wa mtu?Nilikataa katakata.
Na jambo baya zaidi nilipoamia kwenye makazi yangu mapya nikagundua kuwa tunaishi wote mtaa mmoja kwa tofauti ya nyumba kama 10 hivi.
Nime-avoid sana mawasiliano naye.Japo yeye analazimisha.Sipendi mke wangu ajue wala mume wake.
Hivyo kumueleza au kutomueleza mume wako kunategemeana na jinsi yeye alivyo kitabia, kama high tempered utalimwa talaka ya haraka.Kumueleza kunategemeana na tabia ya mtu.kumueleza kutamfanya akose imani kwako.
 
Sister, ushauri umeshatolewa sana na watu tofauti na nahisi mpaka sasa labda umeshafanya maamuzi.

Kama bado, ushauri wangu ni huu: NEVER NEVER EVER TELL YOUR HUSBAND!!

Ukithubutu tu, yatafuata maswali kama 100 hivi ambayo either utashindwa kuyajibu au majibu yake hayataeleweka kwa mumeo. Life will never be the same again. Utakuwa umemuharibia kabisa mwanao, wewe mwenyewe na hata mume wako anaweza kuchanganyikiwa na kazi asifanye tena, hasa kama kazi zake ni za kusafiri safiri sana. Utakuwa umewaharibia wanao wengine kwani jamaa ataanza kuwa na mashaka nao pia.

In the worst case scenario, mumeo anaweza kumuua huyo mtoto, kukua wewe na hata kujiua mwenyewe. Yes, nasikia kuna makabila wanajiua faster inapotokea kesi kama hizi.

Kuna watu wamekushauri ati you have to pay for your mistake by telling the truth, mimi nasema no, nakushauri upay kwa kuendelea kutunza siri hiyo moyoni mwako. Ni bora uendelee kuumia PEKE YAKO kwa kukaa kimya kuliko kuwaumiza watu wengine wengi kwa kusema

Ilikuwaje ukwamwambia huyo mshakaji aliyekumega ati huyo ni mwanae? hapo ndo umebore sister. Anyway, mkimbize mtoto kwa bibi yake au nduu zako wengine wa mbali ili awe mbali na wewe/na huyo mwizi. Tafuta jinsi ya kumsuka mumeo akubali huyo mtoto atoke hapo.....one lie always leads to the other!
 
Pole dada, Mimi binafsi nina jambo linalofanana na lako,miaka sita iliyopita nilikuwa na uhusiano na dada mmoja ambaye kwa wakati ule alikuwa na mchumba wake, ambaye walikuwa wakiishi sehemu tofauti tofauti,kazi ya huyu dada ilikuwa inamfanya awe asafiri mara kwa mara na hivyo kuwa anakutana na mwenza wake .Lakini katika mahusiano yetu huyu dada alipata uja uzito,kilichotokea ni kwamba alikuwa ajasafiri katika kipindi cha miezi mitatu hivi, hiyo ilifanya ajue wazi muhusika ni nani, na wakati huo maandalizi ya Ndoa yao yalikuwa yamekamilika.Baada ya miezi minne wakafunga ndoa wakati yule dada akiwa mja mzito,tulipojadiliano juu ya huo huja uzito alikubali kutotoa ,lolote na liwe.Kweli akajifungua mtoto wa kiume copyright na baba mimi,na akawa anataka niendelee kuwa baba wa mtoto wakati yeye ni mke wa mtu?Nilikataa katakata.
Na jambo baya zaidi nilipoamia kwenye makazi yangu mapya nikagundua kuwa tunaishi wote mtaa mmoja kwa tofauti ya nyumba kama 10 hivi.
Nime-avoid sana mawasiliano naye.Japo yeye analazimisha.Sipendi mke wangu ajue wala mume wake.
Hivyo kumueleza au kutomueleza mume wako kunategemeana na jinsi yeye alivyo kitabia, kama high tempered utalimwa talaka ya haraka.Kumueleza kunategemeana na tabia ya mtu.kumueleza kutamfanya akose imani kwako.

Mnh, Renegade, pole bro. Naomba kukuuliza maswali matatu...

...1; kwanini unakataa kuwa baba wa huyo mtoto?

...2: Kwanini hupendi mumewe ajue, wala mkeo ajue huyo mtoto ni wako?

...3; unaonaje ukipata vipimo vya kitaalamu zaidi, i.e DNA test kuhakikisha ukweli wa paternity?
 
Kwanza pole sana Mainda,
Katika vitu ambavyo sitokushauri kama unaipenda ndoa yako basi UMWAMBIE huyu baba. Fikiria walivyo marafiki, fikiria anavyojituma kwa huyu mtoto, fikiria anavyomhangaikia shule nk. Leo hii unamwambia kuwa Unajua baba nanii, huyu mtoto sio wako nili,,,,, sijui nini! Ndugu yangu ni hatari! Hatari tupu! Unaweza mpoteza baba na ukamzika kabsaaaaaaa. Anaweza akasababisha maafa makubwa kwenye familia yenu ambayo yatakuwa ya kukumbukwa daima. Mdogo wangu acha kabisa. Unafikiri kama utamwambia na akakwambia kama unataka basi mpeleke huyo mtoto kwa baba yake mwendelee kuishi unafikiri utakubaliana nalo wewe? Na yeye hatakubaliana kuendelea kumwona hasa kama atamjua kabisa baba yake ni yule anayemfahamu.
Nafikiri linakutesa sana basi enedelea kulibeba hili kwa uvumilivu.
 
Kwanza pole sana Mainda,
Katika vitu ambavyo sitokushauri kama unaipenda ndoa yako basi UMWAMBIE huyu baba...

Eeka Mangi na wote mnaokataa 'asimwambie',... hapo nyuma umesoma mkasa aliotuletea ndugu yetu KILAMBI? niwakumbushe;

KASHESHE! iliibuka mwaka 2007, ikiwa ni miaka miwili baada ya kumzika baba yake! Aliibuka baba mwingine na kudai kuwa ni mwanae! (HUYU rafiki yangu keshaoa tangu mwaka 1998 na ana watoto wawili!) Huyu baba kila kitu anafanana naye! Hiii ilimuweka huyu rafiki yangu katika hali ya kuchanganyikiwa na kutoamini na hadi leo hii hataki hata kumuona huyo baba yake mzazi (japokuwa ni mtu anayejiweza kiuchumi na rafiki yangu mambo yake sio mazuri) huyu baba kamuahidi mambo kibao lakini jamaa kagoma kabisa

KIBAYA ZAIDI baada ya huyu baba kujitokeza jamaa ilibidi amvae mama yake ambaye yuko kijijini na kumuuliza, mama alishindwa kumjibu akamuelekeza kwa wajomba zake ambao walimwambia kuwa ni kweli na hata BABA aliyemzika alikuwa anafahamu kuwa hakuwa mwanae! Baba zake wadogo nao pia walikuwa wanalifahamu hilo na walipoona kuwa ameshafahamu wakaanza kumuwekea mipaka, biashara na mashamba wamechukia na imekuwa kama wamemtenga! Jamaa amekuwa mpweke sasa kwani ndugu wa upande wa baba aliyemlea hawamtaki na wa upande wa bilogical father hawafahamu na wala hataki kuwasikia!

...sumu hii haifichiki, utaficha leo, lakini ipo siku tu itakuja toka hadharani! Mw'Mungu atakuumbua tu, hata kama sio kwenye mambo ya mirathi, huenda hata pale wanandugu watapokuomba umchangie damu, au magonjwa ya kurithi, nk... Siku hizi safari za Uingereza zinahusisha sana DNA testing iwapo watoto wanahusishwa...

Kuna mengi tu yakuumbua...! siri hiyo isipomdhuru mume, itakuja wadhuru watoto huko maishani mwao iwapo litatokea jambo ambalo litawataka wathibitishe undugu wao...
 
Mnh, Renegade, pole bro. Naomba kukuuliza maswali matatu...

...1; kwanini unakataa kuwa baba wa huyo mtoto?

...2: Kwanini hupendi mumewe ajue, wala mkeo ajue huyo mtoto ni wako?

...3; unaonaje ukipata vipimo vya kitaalamu zaidi, i.e DNA test kuhakikisha ukweli wa paternity?

Naomba kukujibu kama ifuatavyo,
1.Sikatai kuwa baba wa mtoto, lakini hakuna mtoto anayeweza kuwa na baba wawili,pia kukubali kwangu akuwezi kumsaidia huyo dada na hasa ukizingatia kuwa tulipokuwa na uhusiano kila mmoja alikuwa na mtu wake.Na isitoshe itahadhiri ndoa yake.

2.Kwa upande wa mke wangu ,nitaazaje kumueleza?Mume wake akijua nini itakuwa hatima ya ndo yao, lengo hasa ni nini?

3.Kuhusu DNA sawa unaweza kufanya hivyo kama una mashaka hivi,kwa upande wangu sina mashaka, maana sura ya mtoto ni yangu na pia anafanana sana na watoto wangu.
 
KASHESHE! iliibuka mwaka 2007, ikiwa ni miaka miwili baada ya kumzika baba yake! Aliibuka baba mwingine na kudai kuwa ni mwanae! (HUYU rafiki yangu keshaoa tangu mwaka 1998 na ana watoto wawili!) Huyu baba kila kitu anafanana naye! Hiii ilimuweka huyu rafiki yangu katika hali ya kuchanganyikiwa na kutoamini na hadi leo hii hataki hata kumuona huyo baba yake mzazi (japokuwa ni mtu anayejiweza kiuchumi na rafiki yangu mambo yake sio mazuri) huyu baba kamuahidi mambo kibao lakini jamaa kagoma kabisa

KIBAYA ZAIDI baada ya huyu baba kujitokeza jamaa ilibidi amvae mama yake ambaye yuko kijijini na kumuuliza, mama alishindwa kumjibu akamuelekeza kwa wajomba zake ambao walimwambia kuwa ni kweli na hata BABA aliyemzika alikuwa anafahamu kuwa hakuwa mwanae! Baba zake wadogo nao pia walikuwa wanalifahamu hilo na walipoona kuwa ameshafahamu wakaanza kumuwekea mipaka, biashara na mashamba wamechukia na imekuwa kama wamemtenga! Jamaa amekuwa mpweke sasa kwani ndugu wa upande wa baba aliyemlea hawamtaki na wa upande wa bilogical father hawafahamu na wala hataki kuwasikia!

Mbu.,
Hiyo kali, nakumbuka nilivyokuwa undegraduate nillishi na kijana mmoja yeye akiwa mwaka wa kwanza huku mimi nikimalizia ka-degree kangu,yule kijana alikuwa akiishi na mama yake na baba yake wa kambo bila kujua.Jinsi yule baba alivyokuwa akimhangaikia kuliko watoto wa kuwazaa mwenyewe.Siku ya siku huyo kijana akagombana na mdogo wake huko nyumbani kwao,unajua kilitokea nini? Yule mdogo wake akamueleza bayana kwa hasira kwamba yeye siyo ndugu wa baba mmoja! alishtuka sana na akuamini saa hiyo hiyo aliibuka na kwenda kwa ma mkubwa wake ambaye ni kigogo wa serikali.Kwenda kutaka ukweli wa habari ile, huyo mammkubwa alikubali na kumwita mdogo wake ili waweke mambo wazi, dogo akaambiwa ukweli wa mambo na akurudi nyuma akasema kama baba yake yupo yeye amtambui anayemtambua ni huyo aliyepo.
ukawa mwisho wa habari.
nawasilisha
 
Eeka Mangi na wote mnaokataa 'asimwambie',... hapo nyuma umesoma mkasa aliotuletea ndugu yetu KILAMBI? niwakumbushe;

...sumu hii haifichiki, utaficha leo, lakini ipo siku tu itakuja toka hadharani! Mw'Mungu atakuumbua tu, hata kama sio kwenye mambo ya mirathi, huenda hata pale wanandugu watapokuomba umchangie damu, au magonjwa ya kurithi, nk... Siku hizi safari za Uingereza zinahusisha sana DNA testing iwapo watoto wanahusishwa...

Kuna mengi tu yakuumbua...! siri hiyo isipomdhuru mume, itakuja wadhuru watoto huko maishani mwao iwapo litatokea jambo ambalo litawataka wathibitishe undugu wao...

Mkuu you are right,

Hii kitu huwezi ficha. Whether you like it or not, the day shall come when truth will catch up with you.

Nadhani kama mistake imeshatokea imeshatokea. If you break it, you own it. Najua ni challenge kubwa na inaweza kusababisha ndoa ya huyo mama kuvunjika hata ya mwanaume. LAKINI HEBU JIULIZE. ITOKEE SIKU MOJA AMBAYO WEWE NA MIMI HATUJUI..MZEE ANAKULA BIA YAKE MITI MIREFU NA MSHKAJI AMBAYE ana habari na hivi vitu vya DNA......Katika mazungumzo..jamaa anaamua kwenda kufanya vipimo vya DNA (just know in this world ANYTHING is possible-so dont assume)..si unaona hali itakuwa mbaya zaidi?

Hata hapa kwenye hii Thread naamini ni wengi wameshaanza kulifikiria hili la DNA..especially kama jamaa ana hata chembe ya mashaka juu ya mwenzake. Iko siku jamaa ataenda kuomba vipimo..by the way usisahau kizazi cha leo..ni tofauti na wazee wetu....hata hapa JF wengi tunajifunza mengi sana ambayo yanatusaidia..

Kikubwa ni kuwa wakweli katika nafsi zetu especially watu ambao wako kwenye mahusiano... hata sisi vijana ambao tumeoa na hatujaolewa. Whatever you do today, will ALWAYS catch up with you in a diffrent way.

Na kama wazungu wasemavyo- Two people can keep a secret when one is dead! Ni vema kama limetokea..ujue kabisa namna ya kutoka kwenye huo mtego.

Kwa mfano mimi personally na hii technology iliyokuja..I cant rule out kwamba haipo siku nitamwambia mke wangu tukachukue DNA za watoto wetu. (when I get one-lol) Kwa nia njema tuu. I know wengi tuna concept tufauti..na mwenzako anaweza ona ni kama ishara ya kutokuwa na imani naye..lakini ndo hapo..dunia imebadilika..huwezi kumuamini yeyote. Au unaweza hata ukafanya kwa siri mwenzako hajui...nisikilizie sasa..ajue kwamba yeye si muhusika wakati ulimficha..na kwa akina baba ni worse..maana kama yupo responsible kwa mimba anajua kabisa.

So wakubwa wote humu: kuficha siyo solution kamwe. Ukificha ni kwamba unaahirisha matatizo kwa mda. Ila iko siku ambayo wewe hujui na yeye hajui...itajulikana. So forwarned, is forearmed. Hapo ndo kutakuwa na kilio cha kusaga meno.
 
Naomba kukujibu kama ifuatavyo,
1.Sikatai kuwa baba wa mtoto, lakini hakuna mtoto anayeweza kuwa na baba wawili,pia kukubali kwangu akuwezi kumsaidia huyo dada na hasa ukizingatia kuwa tulipokuwa na uhusiano kila mmoja alikuwa na mtu wake.Na isitoshe itahadhiri ndoa yake.

2.Kwa upande wa mke wangu ,nitaazaje kumueleza?Mume wake akijua nini itakuwa hatima ya ndo yao, lengo hasa ni nini?

3.Kuhusu DNA sawa unaweza kufanya hivyo kama una mashaka hivi,kwa upande wangu sina mashaka, maana sura ya mtoto ni yangu na pia anafanana sana na watoto wangu.

naanza kwa kumpa pole huyo mdada, kwakweli najua anawakati mgumu sana, hichi kitu kinawasumbua sana akina mama, unajua inauma sana, na hii inawafanya akinamama wengi wanakuwa depressed na kukosa raha katika maisha, ingawa kwa wanaume nadhani ni tofauti

1.kutokana na majibu yako sidhani kama huyu dada anahitaji mume wake afahamu kuwa mtoto ni wako, ila nadhani anachohitaji ni kuona ww kama baba wa mtoto unafahamu na unaonyesha mapenzi kwa mtoto kama biological father angalau kutaka kujua maendeleo ya mtto, ingawa baba mlezi anabaki na status yake kama baba, na pengine inawezekana asigundue hili kama nyie wawili mna ushirikiano unajua pana masuala mengine yanweza tokea ikahitajika msaada wako kama baba mzazi, kama mnawasiliana unaweza ukaokoa jahazi hata pengine bila mzee kujua, imagine kuwa mtoto huyo damu yake haifanai na ya baba mlezi, na ghafla maepata tatizo linalohitaji huduma ya damu je kama mnalijua hili mapema lolote linaweza fanyika likaokoa maisha ya mtoto, MIMI NADHANI UNAHITAJIKA KUWA NA MAWASILIANO NA NI MUHIMU KUJUA VINASABA VYA MTOTO KAMA VINAFANA NA VYA KWAKO; NA MUANGALIE MAMBO MUHIMU KAMA DAMU; MAGONJWA YA UKOO ETC ni muhimu katika kumsadia huyu mtoto. haina maana kuwa mtto anakuwa na baba wawili, baba wa mtoto ni ww na huyu mwingine ni mlezi ingawa mwenyewe hajui, maana ni kosa lenu nyie huwezi kuukwepa ubaba . na pengine huyu dada haihitaji chochote toka kwako anahitaji tu uonyeshe unajali.

2. mimi pia nakubaliana na ww nadhani ni ngumu mno kuwaeleza wenzi wenu juu ya hili, lakini bado nasisitiza mnaweza kuwa na mawasiliano ya siri kujua maendeleo ya mtoto, bila kuwa na mahusiano yeyote zaidi. na wala mtoto asijue hili, hii kisaikolojia itamsaidia huyu mama pia, nafikiria kuwa je anajisikiaje akimuangalia mtot hasa unasema kuwa amefanana na ww, je anapata feeling gani anapokosa japo salamu au kuulizwa hali na baba ya mtoto!!
3. pamoja na kufanana bado pana vitu mnatakiwa mvipime ili kumfahamu zaidi mtoto na hii itasaidia hata litakapotokea tatizo, ni bora ujue kuliko kutokujua !!!
 
Mama pole sana kwani napenda kukutia moyo uwe tu mkweli kwa mumeo. Mimi haya yalikuta miaka 18 iliyopita baada ya mamsapu wangu kufanya tendo kama lako na akazaa mtoto ambaye kwa kweli ni kijana mzuri sana na mwenye akili sana> Nimemsomesha na hata sasa yuko USA kwenye chuo kikuu huko. Hili pendo lilitokea baada ya mke wangu kunieleza ukweli na kunisihi sana nimfichie hii siri kama mwenzanke kwenye ndoa inayotambulika tulifanya hivyo and now the boy is 21 yrs old. Baadaye nilizunguza na Bilogical father wake kuhusu hili jambo na kuwa kijana anatumia sir yangu. Huyu bwana naye kanishukuru sana na kuniomba hata mtoto asiambiwe yaliyopita yasije yakamfanya akaumia roho. Hivyo kama mumeo ni mtu aliyekomaa kindoa naona hili halitakuwa jambo la ajaabu kwake na bila shaka atalipokea kwa moyo wa kutaka kukusaidia pia maana ni kitu ambacho uanakijutia hadi leo.

Sikutaka kutoa comments kwanza kuhusu suala hili lakini hapa uzalendo umenishinda... aisee ABUNUWASI am not sure kama huyo wife wako hajakupa limbwata. Hivi haya unayoeleza hapa na jinsi unavyoelezea yaani upo very confortable kabisa na hiyo situation iliyokutokea.. sidhani kama mwanaume aliyekamili anaweza kupokea situation quite easily kama wewe na kuendelea nayo kama ulivyoeleza. otherwise mkuu u have some serious problem.. Mamaa kaishamaliza kila kitu aisee.
 
Unahangaika bure, huyo mtoto ni wa mumeo. Kuzaa hata kuku anazaa. Baba ni kulea na upendo wa dhati. Siamini kuwa mama ndiye mwenye kujua ameshika mimba ya nani kwa uthabiti. DNA imeshawaibisha akina mama wengi wanaodai kuwa mtoto wao ni wa fulani.

Ungekuwa unampenda kweli mumeo, usingekaa muda mrefu kiasi hicho bila ya kumwambia.

Kuna matatu yanayoweza kutokea. La kwanza, unyamaze uendelee kutukutia, ndiyo adhabu inayokustahilia. La pili umwambie, uachike, ndiyo adhabu inayokustahilia. La tatu umwambie akusamehe, lakini asikuamini tena, ndiyo adhabu inayokustahilia.

Kabla ya kufanya lolote katika hayo matatu, jiweke katika viatu vya mwanao. Usifanye lolote la kumwadhinisha yeye. Hana kosa.
 
Back
Top Bottom