3. Unaproof gani huyo MZINIFU MWENZA ni mwanae?...sura..tabia..mwili? DNA? au wewe wajua siku ulipozini ndio uliopata mimba?
NI WA KWAKE, MPAKA KUPIGA MIAYO WANAFANANA. HAPO HAMNA MASWALI. NDIO TATIZO LA WATOTO WA NAMNA HII, NA HILI LINANIDUHI NA KUHUZUNISHA, MAANA NAMUONA JAMAA KILA SIKU KATIKA MTOTO HUYU, NAKUMBUKA MAKOSA YANGU
Dada, Kila jambo lina chanzo chake. Ndio maana huwa wanasema, lazima mtu awe makini na decisions za maisha yake wakati wowote ule,kwasababu mtu huvuna kile anachopanda. Ukipanda uharibufu, utavuna uharibifu....hata ukilia sana, lazima uyale yale matunda ya uharibufu kwanza yaishe ndo maisha mazuri yawepo. Labda, Mungu aweza kukusamehe, ila kwa vitu halisi kama hivyo(mtoto katokea), itabidi ujikaze ule hiyo pilipili hadi iishe, na ikiisha, ndo utaanza maisha ya kawaida ya kula sukari..yaani utaanza upyaaa, maisha mapya. ukijua kuwa yale ya zamani yameshavurugika kabisa na utaanza chapter mpya.
sisemi ili kukuumiza. ukweli ni kwamba, itabidi umwambie huyo jamaa haraka sana ili asiendelee kujiridhisha na mtoto akijua ni wake kumbe sio. unavyozidi kunyamaza ndo unavyozidi kuongeza pilipili kwenye mboga. bora hapo ulipofikia upate adhabu ya hapohapo na uanze maisha mapya kuliko kuja kuanza hayo maisha mapya baadae na jamaa akijua kuwa wewe ni mtu mbaya sana kwani siku zote hizo ulikuwa unamfanyia unafiki. atajua kuwa wewe unao uwezo hata wa kumuua wakati wowote kama unao uwezo wa kuweka mambo hayo moyoni kwa muda wote huo, inamaana haikuumi?
itabidi uwe responsible for your faults. kwetu sisi wanaume, hasa ukiona tunawapenda sana, huwa tunaumia sana kama mkitudanganya. kwa ufupi, jamaa anaweza hata akakuua kama ni kwenye sport na akasingizia ni "provocation" ambayo kisheria hata haendi ndani. wale wanasheria mnajua hili. lakini itabidi tu, umwambie ili kama noma na iwe noma mapema. kama kukusamehe akusamehe mapema, kama kukuacha akuache mapema. ili uanze maisha mapya starting from where jamaa atafikia. ni kweli, kama akiamua kukuacha, hauwezi kumlaumu kwasababu wewe mwenyewe unajua kuwa ni kosa lako, hovyo utaanza na wewe maisha mapya....na kama ataamua kukusamehe, ndo hivyo tena.
Lakini hili liwe fundisho kwa wanawake wengine humu ndani, kwasababu, kwa wanaume wengine, kama mkewe ndo kafanya hivyo, hata akikusamehe, ujue na wewe anaweza akakutafutia watoto wa nje ya ndoa hata watano ili tu akukomeshe. sio rahisi kwa mwanaume wa kawaida kukusamehe hivihivi,ndo maana nasema uwe tayari kula matunda ya yale uliyoyafanya, na wala usipate shida, wewe mwenyewe nenda yachume anza kuyala hadi yaishe....na hauna mtu wa kumlaumu. ila nakushauri, unapomwambia,usiwe peke yako, uwe na watu kama wanne ivi hasa wanaume na wenye nguvu, jamaa asije akachanganyikiwa na hasira akakuchinja. Pole sana. Mrudie Mungu, Okoka, nenda kanisani ukaombewe, na Mungu anaweza akapunguza hiyo sumu, ukashangaa mambo yameenda vizuri tu lakini. ila ukienda kichwakichwa, kuna mawili. .......