Mtoto wa nje ya ndoa

Mtoto wa nje ya ndoa


...duh, ha ha haa..Bubu nawe hasa mshabiki, loh!

Dont underestimate JF opinions, ...akija sema mumewe kamsamehe kuna wataomhukumu kuwa Mume Bwege, kama sio dada kumlisha mumewe 'kipapai!'!

Dada Maindainda, iwe siri yako hiyo na mumeo, wasikia sana? ...siri sirini mtavyooongea na kukubaliana, wala huyo mzazio usimwambie kilichojiri, labda kama mumeo kakusudia kumtoa roho ili akimbie mji!

Sio ushabiki, ni katika kujifunza kutokana na mifano hai. Wanaume wengi hapa tutasema mke wangu kama alitembea nje na kuzaa mtoto ambaye anajua si wangu ningependa anafihamishe haraka sana, ukiuliza wangapi watakuwa tayari kumsamehe mwenzi wao na kuendelea kumlea mtoto kama ilivyokuwa mwanzo basi sidhani kama watafika hata asilimia 5! Kina abunuwas dunia ya leo ni wachache mno!!! labda limbwata limewakolea barabara! (a joke)

Mie Mainda akisamehewa na mumewe nitafurahia sana kuliko kusikia ndoa yake imevunjika au kuna baya zaidi limetokea, I hope mapenzi waliyojenga katika kipindi cha miaka 10 ya ndoa yatawasaidia kuwavusha katika majaribuni haya mazito ndani ya ndoa yao.
 
Sio ukiuliza wangapi watakuwa tayari kumsamehe mwenzi wao na kuendelea kumlea mtoto kama ilivyokuwa mwanzo basi sidhani kama watafika hata asilimia 5!

Kina Abunuwasi ni nadra sana!! Kusamehe na kulea ni vitu viwili tofauti. Mtoto si ana baba yake? Anyway, ni delicate issue na ni vigumu kuamua kwa kutumia akili tu. Inaweza ikawa bond imejengeka kiasi kikubwa kati ya baba mlezi na mtoto. In any case, mtoto ni vyema ajue biologiocal parents wake.
 
Nimesikia hasira umenifanya niishiwe imani na mwenzangu huyu kuanzia sasa itakuwa ni vipimo kwa vipimo kama sio vyangu pale pale namtwanga karata aah sorry taraka 3.

Lakini anyway kuwa muangalifu sikushauri kumwambia mumeo kuhusu jambo atakukimbiza mara moja dadangu.Kama kosa ushafanya so tubu kwa Mungu wako tu huu ushauri sijui umwambie mumeo sure am telling you utapewa taraka
 
Dada Pole Na Matatizo Pamoja Na Mzigo Ulionao Moyoni.najua Ni Mzigo Mkubwa Sana Kwako Na Unaitaji Kuutua Ndio Maana Umeamua Kuomba Msaada.mimi Binafsi Kama Mwanaume Nineumia Na Sijui Huyo Jamaa Akijua Itakuaje?ila Ninachoweza Kukuambia Ni Kwamba Kwa Nguvu Ya Mawazo Unayojaribu Kukusanya Kutoka Kwa Wadau Wa Jamii Forum Yatakusaidia Kwa Kiwango Kidogo Sana.unachotakiwa Kufanya Ni Kumshirikisha Mungu Kwanza Katika Hili Hata Kama Wewe Sio Mwenda Kanisani Sasa Inakubibi Uanze Nasema Hivi Nikiwa Na Maana Ya Dhati Kutoka Moyoni.anza Maombi Ya Binafsi Ikiwezekana Anza Kufunga Kula Kwa Ajili Ya Jambo Hili Zito Kwa Ajili Ya Kunusuru Familia Yako Pamoja Na Ndoa Yako, Hata Yesu Aliupokua Na Mambo Mazito Alijitenga Peke Yake Na Kuanza Kuomba Nguvu Ya Ziada Ili Kuyashinda Majaribu Mazito.kwa Kufanya Hivyo Nguvu Za Ajabu Ambazo Ujawahi Kuziona Wala Kuzihisi Zitakutokea Na Utajikuta Unamweleza Mumeo Mambo Haya Naye Atakuelewa Na Utapata Matumaini Katika Maisha Yako.kuna Kitabu Cha Biblia Kina Waalika Wale Watu Wote Wasumbukao Na Mizigo...... Wamfuate Yesu Nae Atawatua, Amini Nakuambia Akuna Lililo Gumu La Kumshinda Mungu Baba.

Please Fuata Hayo Niliyo Kuambia Nawe Utaona Maajabu Ya Mungu, Kama Kosa Umeshalifanya Na Inaonesha Ni Jinsi Gani Unavyolijutia Na Mungu Amesukia Kilio Chako.hakuna Njia Ambayo Itaweza Kufanya Mambo Haya Yawe Mepesi Zaidi Ya Hiyo I Am Saying That With Confidence Coz Nimesoma Maoni Karibu Yote Yaliyotolewa Na Wadau.
Belive In God EVERYTHING WILL BE EASY FOR U.
 
Nilikuwa namtafuta Mchongoma maana sijamuona siku nyingi hapa ukumbini hivyo nikataka niwaulizie waungwana Mchongoma kapotelea wapi!? Katika upelelezi wangu nilioufanya hapa ukumbini nmegundua kwamba Mchongoma sasa kawa Mbu 🙂 Mbu, mbona hukutoa taarifa kwamba umebadilisha jina?
 
dada siyo rahisi kama unavyodhani. Wengi watakushauri ila ukweli ni huu wewe ni binaadamu na kila binaadamu ni mpungufu mana ni mungu tu ndiye mkamilifu, yapo makosa tunaweza kusamehe na yanavumilika na yako makosa hata ukisamehe kila siku yatakutesa wewe na huyo uliyedhani utapata salama yako, badala yake sasa utajenga chuki ya milele na milele.
Mimi ni mwanaume ila kwa hili naomba nikushauri kwa nia safi kosa la aina hili lnabaki kuwa siri na siri yako pekee na ndio mambo ambayo mama zetu wanasema unakufa nayo. Vyenginevyo kama nilivyosema athari si kwako tu, bali kwa mume wako na baya zaidi na kwa mtoto pia na inawezekana utaumia zaidi mana sisi mola ametumba wadhaifu tunapenda tuwe sisi wa kutenda yote kila siku kwa wake au marafiki zetu ila tukitendewa ni dhambi kuu na uvumilivu ni zero, hivyo dada yangu hii ni siri yako na kufa nayo, sahau na samehe kama ni kujisikia mkosa ni kweli wewe ni mkosa ila omba kwa mola atakusamehe mana yeye ndiye mkamilifu na msamehevu. Usiiharibu familiia. Hili kufa nalo wewe na hesabu za kawaida 1 is not equal to three, usidhani utaleta amani bali kisirani kwa familia yako na hutaiweza tena.
Nakusihi hii ndiyo moja ya kuambiwa mama zetu wana siri nyingi na wewe ni mmoja wa mama zetu kufa na tai shingoni. Angalia mbele nyuma mwiko.
 
Hatari lakini salam sasa umenifanya nirudi Arusha nikawakaguwe watoto DNA zao
 
Pole dada kwa yote. Kwanza hili sakata si rahisi kama linavyoonekana na wengine. Kama ulibakwa na huyo jamaa na ukamficha mumeo kwa miaka kadhaa kwa vyovyote wewe ni mkosaji. Ningekushauri tu ujukaze kike, na hiyo ibaki kuwa siri yako. Huyo unayedhani kuwa ni baba wa mtoto wewe achana naye. Hakuna mwanamme mwenye akili zake anayeweza kudai mtoto kutoka kwa mke wa mtu. Kisheria mtoto huyo ni wako mama. Ningekuwa mimi ningetangaza kubakwa maapema tangu siku uliyoisaliti ndoa yako. Haya yasingekukuta. Kwa kuwa uliamua kumtunzia siri mhalifu, hizi ni gharama zake. Endelea kula jiwe. Lakini kukupunguzia matatizo mshauri mwenzio mtoto aende boarding school. Angalau utakutana naye hapo kwako wakati wa likizo tu.

Kama unataka ndoa yako iendelee, usithubutu kumtamkia mumeo jambo hili. Si rahisi kusamehe usaliti wa ndoa na hasa kama huyo bwana mumeo anamjua.

Yani kaka hapa umelenga...very good idea. Maana na mimi niko kwenye ndoa sasa kama mwaka na nusu hivi... mwenzangu haonyeshi muelekeo wowote kama anahitaji tupate mtoto (may be bcoz he has already 2 children from the x-wife)! nimejaribu kutunga mimba hola...sijui kala dawa? Ni bora nitumie hii njia ya kubakwa sasa. Lol!
 
Yani kaka hapa umelenga...very good idea. Maana na mimi niko kwenye ndoa sasa kama mwaka na nusu hivi... mwenzangu haonyeshi muelekeo wowote kama anahitaji tupate mtoto (may be bcoz he has already 2 children from the x-wife)! nimejaribu kutunga mimba hola...sijui kala dawa? Ni bora nitumie hii njia ya kubakwa sasa. Lol!

LOL!!!! Mwambie unataka mtoto ili ujue msimamo wake kwenye swala hilo uko wapi, kama yeye hataki tena mtoto mwingine maana tayari anao wawili basi uanze kutafuta wabakaji 😉 wanakubaka mpaka mambo yajipe ndiyo unatangaza umebakwa na aliyekubaka alivaa kitu usoni wakati anakubaka hukuona sura yake 🙂
 
Wasiwasi wangu mimi hapo ni kuwa,
kwanza kabisa mzee ataquestion watoto wote katika familia, kama wapo.
Pili atascan mambo yoooote aliyomfanyia mtoto, akidhani kama wa kwake kumbe kulikuwa na mjanja kamdabo krosi.
Tatu atakuwa na hilo swali siku zote, kama ulifanya before, atakuwa na uhakika gani kuwa hautofanya tena...?!?!
Yote hayo yatakuwa ni maswali ambayo itabidi ujiandae kuyajibu yakiambata na vithibitisho anuai...Samahani pekee haitotosha hapo mamaa
Lastly hakikisha mzee anapafu la ziada, maana from nowhere kumuweka chini na kumwambia "we need to talk", kamanda anaweza akafleti buree, ikawa mada kesi.....Ni ushauri tu!!
 
LOL!!!! Mwambie unataka mtoto ili ujue msimamo wake kwenye swala hilo uko wapi, kama yeye hataki tena mtoto mwingine maana tayari anao wawili basi uanze kutafuta wabakaji 😉 wanakubaka mpaka mambo yajipe ndiyo unatangaza umebakwa na aliyekubaka alivaa kitu usoni wakati anakubaka hukuona sura yake 🙂

Bubu eeeh, nilishaongea sana na mifano juu...ila haonyeshi hata dalili yoyote bwana...achanikabakwagee. Nasikia eti kuna sindano pia za kuzuia mayai ya kiume kufanya kazi hivi nikweli! asanteni sana wanajiefu kwa kutupa maarifa na muendelee na mwendo huu huu.
 
Bubu eeeh, nilishaongea sana na mifano juu...ila haonyeshi hata dalili yoyote bwana...achanikabakwagee. Nasikia eti kuna sindano pia za kuzuia mayai ya kiume kufanya kazi hivi nikweli! asanteni sana wanajiefu kwa kutupa maarifa na muendelee na mwendo huu huu.

Haya kubakwa kwema 😉
 
Dada Maindainda!
Uliongea na husband kuhusu hii ishu yako?Ilikuwaje?Tupashe tafadhali ilivyokuwa.
Au hujamweleza? Tuhabarishe tu yaliyojiri maana naona hii thread ya muda kidogo lazima kuna habari utakuwa nazo!
Kumbuka yote maisha,kila mtu ana ishuz hapa duniani!
 
Bubu eeeh, nilishaongea sana na mifano juu...ila haonyeshi hata dalili yoyote bwana...achanikabakwagee. Nasikia eti kuna sindano pia za kuzuia mayai ya kiume kufanya kazi hivi nikweli! asanteni sana wanajiefu kwa kutupa maarifa na muendelee na mwendo huu huu.

Mtegeshee bila kumwambia huyo mumeo,kama unajiamini unaweza kushika mimba wewe mtegee siku zako za hatari kwenye mzunguko. Kubakwa sidhani kama ni kitendo ambacho mwanamke anapenda kufanyiwa! Umenishtua kwakweli..
 
Nilikuwa namtafuta Mchongoma maana sijamuona siku nyingi hapa ukumbini hivyo nikataka niwaulizie waungwana Mchongoma kapotelea wapi!? Katika upelelezi wangu nilioufanya hapa ukumbini nmegundua kwamba Mchongoma sasa kawa Mbu 🙂 Mbu, mbona hukutoa taarifa kwamba umebadilisha jina?

...kuna 'mwanga' alikuwa anaweka usiku, by the time anakuja gundua nime 'mutate', tayari nishakata mitaa... pole kaka! 😀
 
Mtegeshee bila kumwambia huyo mumeo,kama unajiamini unaweza kushika mimba wewe mtegee siku zako za hatari kwenye mzunguko. Kubakwa sidhani kama ni kitendo ambacho mwanamke anapenda kufanyiwa! Umenishtua kwakweli..

Belinda, kubakwa huku anakosema Mrs ni tofauti na kubakwa kwa kawaida maana anaweza kabisa akamtafuta mbakaji wake kama anavyotaka yeye na muhimu afananefanane na Mr 🙂, labda kwa urefu, rangi na hatapiga ukelele kwamba amebakwa mpaka mambo yajipe 😉
 
Mh Dada Maindainda pole kwa yalokusibu. Mengi yeshasemwa na wenzangu sina haja ya kurudia ila tu ninachopenda kukwambia fuata ushauri wa Da NaimaOmari. Reactions za wanaume wetu hazitabiriki na wala si za kuzijaribu.
 
you know your husband better than all of us .. mwengine ukimwambia ukweli atakuchukia maisha it can kill him as well ... eeh its very painful

one mistake you did ni kumwambia that thieeeef kwamba you have his baby ... why did you do that for christs sake ... unakimbelembele kweli

Mi I suggest ... study the situation carefully reverse the order umwambie yule bazazi the child is not his and then kwa mume wako .... just swallow ... because you will distabilise and dismantle him kabisa.

Kila mtu ana madhambi ..... so go wisely on this


hapo tu mie ndipo panaponimaliza, kwanini ulimwambia? yani hii thread inaccmua kweli, jamani mie sioni urahic kwa hili jambo, huyo baba mwenye mtoto ana haki na mwanae na kama 2juavyo huyo baba anaweza kuongea na mkewe wakakubaliana mtoto wamchukue, huyu mama atamwambia nini mumewe? ndio aje amwambie mtoto sio wako kwasasa na ameshajitahidi kumsomesha na makorokoro yote sasa hv aje amwambie sio wake?umesema hutaki kulaumiwa but hapa najiuliza ulienda kufanya vp mapenzi na lim2 unalosema hulipendi na mpaka umwambie tena una mimba yake? jamani looo ndoa zina mambo aisee, hapo tena ni shughuli kwa mtoto aliemzoea huyo anaedhani ni baba yake mzazi leo aje aambiwe sio, ni kwamba cjui ni mwanaume gani atakae ielewa hii debate, uanze tu "eti baba junia, huyu junia sio wa kwako cjui nini na nini" haaa ni ngumu kuliko unavyofikiria, kama bado una wazazi kaanze kuwaelezea wazazi wako kwanza ndio ujue step ya pili ya game. oteee mai kanyi looo ni gumu.
 
Ndugu yangu Msanii

Tatizo hapa ni the emotional battle that will ensue ... facing the situation ... how long the recepient will take to digest the situation ... the emotional trauma ... mengine ya sheria yatakuja later after mumewe recovering and accepting the situation


Maana anybody can be given any news lakini there is limitation this is what this lady is worried about ... the aftermath of the situation

I suggest maybe amlishe limbwata kwanza ... maana hapa hata kumface simba afadhali


mami cna la kuongeza! take 5.
 
Mama pole sana kwani napenda kukutia moyo uwe tu mkweli kwa mumeo. Mimi haya yalikuta miaka 18 iliyopita baada ya mamsapu wangu kufanya tendo kama lako na akazaa mtoto ambaye kwa kweli ni kijana mzuri sana na mwenye akili sana> Nimemsomesha na hata sasa yuko USA kwenye chuo kikuu huko. Hili pendo lilitokea baada ya mke wangu kunieleza ukweli na kunisihi sana nimfichie hii siri kama mwenzanke kwenye ndoa inayotambulika tulifanya hivyo and now the boy is 21 yrs old. Baadaye nilizunguza na Bilogical father wake kuhusu hili jambo na kuwa kijana anatumia sir yangu. Huyu bwana naye kanishukuru sana na kuniomba hata mtoto asiambiwe yaliyopita yasije yakamfanya akaumia roho. Hivyo kama mumeo ni mtu aliyekomaa kindoa naona hili halitakuwa jambo la ajaabu kwake na bila shaka atalipokea kwa moyo wa kutaka kukusaidia pia maana ni kitu ambacho uanakijutia hadi leo.



hizi busara zinahitaji moyo haswaa, hongera kwa hilo.
 
Back
Top Bottom