Mtoto wa nje ya ndoa

Asanteni kwa ushauri wenu mzuri. I am still caught up between the two - nicheme nichicheme? Nakubali nisingesema kwa biological father, ila nilichanganyikiwa wewee, sikujua nifanye nini. Na kwa kweli kutoa mimba sikuwahi kufikiria.

Kwa kweli hata kama naachika leo singependa mtoto akae na biological father, alelewe na mama wa kambo? Nina reservations katika hili, pamoja naye pia. Halafu pia mtoto akijua na ukija kumkanya akikosea baadae atasema-wewe na baba nyote hamna akili!

Bado nahitaji muongozo wa kisheria, wajua siwezi kwenda kwa lawyer juu ya hili. Kama nimeelewa, mnasema mtoto kisheria ni wa biological father unless anakuwa adopted. Naomba kama kuna mtu anaijua hiyo sheria aniambie ni ipi niitafute.

Abunuwasi hongera sana, I wish ningekutuma wewe uongee na mume wangu. Ila sina uhakika kama mzee anafanana na Chuma au la, maana amesema angenisambaratisha kwanza, maskini mie.

Hivi wababa mnaopeleka watoto wa nje home inakuwaje, au nyie ni mteremko tu, unampiga mama kiswahili na doti ya Khanga / Wax basi.

Kuna mtu aliuliza umri wa mtoto, naomba nisiseme maana wanaume wote humu ndani wataenda kukagua watoto wao wa umri huo, mwajuaje mzee ni mwana JF?

Ukishafanya uamuzi useme au usiseme basi tufahamishe pia. Na kama utaamua kumwambia mumeo pia tungependa kujua matokeo ya hili bomu utakalomuangushia. Bado ushauri wangu ni ule ule kwamba usimwambie mumeo.
 
Kidzogolae,
Yaelekea wewe umeshatoa adhabu kabisa maana unavyoonekana ni ungempa talaka mkeo tu akaanze maisha mapya, hayo unayoyasema.

wanaume mnajifanya mna mahasira sana, na ndio maana hamuambiwi jambo. Busara zenu tuzione katika vitendo na maneno yenu na sio MANGUMI na KUCHINJANA. Mbona sisi wanawake tunawafumania na bado tunawaandalia chakula na kuwatunzia siri? Hapa sitafuti sympathy, nataka tu kuonyesha kuwa mko tofauti.

Sijui kama umesoma alivyosema Abunuwasi - yeye ana wake baba mkubwa sasa na anamtunza. Labda "kifua" chako kidogo tu.

Nataka kujaribu kumpa mume wangu mtihani kumpima pressure kabla sijampa ishu, any idea how?.

Trust me wanaume kama abunuwasi ni wachache mno katika dunia ya leo sidhani kama wanafika hata 5% ya wanaume wote duniani.
 
Kosa limeshatendeka na ni kosa kubwa kwa mila za kiafrika. Kwa hatua iliyofikia ni Bora ukakaa kimyaa, ila mwangukie mungu wako anayejua kila kitu . Kama kuchukua tahadhari ulipasaswa kuichukua mapema kama kutoa mimba ingali changa. Ukijitoa hadharani kwa sasa miongoni mwa athari ni kuwa Mtoto wako atajisikiaje atakapoambiwa kuwa yule baba anayempenda na kumtunza si baba yake mzazi, na huyo anayedhaniwa kuwa ni mzazi wala hamjui wala kumjali. Na mume ambaye kwa miaka yote alimchukulia kuwa ni muadilifu atapokea vipi ukweli huo. ndoa itasambaratika ama kuwa na nyufa kubwa zisizozibika.
 
Kidzogolae,
Yaelekea wewe umeshatoa adhabu kabisa maana unavyoonekana ni ungempa talaka mkeo tu akaanze maisha mapya, hayo unayoyasema.

wanaume mnajifanya mna mahasira sana, na ndio maana hamuambiwi jambo. Busara zenu tuzione katika vitendo na maneno yenu na sio MANGUMI na KUCHINJANA. Mbona sisi wanawake tunawafumania na bado tunawaandalia chakula na kuwatunzia siri? Hapa sitafuti sympathy, nataka tu kuonyesha kuwa mko tofauti.

Sijui kama umesoma alivyosema Abunuwasi - yeye ana wake baba mkubwa sasa na anamtunza. Labda "kifua" chako kidogo tu.

Nataka kujaribu kumpa mume wangu mtihani kumpima pressure kabla sijampa ishu, any idea how?.

Dadangu, ninachosema mimi ni cha kweli, sio nakuhukumu. ila nakupa tahadhari. kitu cha muhimu ni kwamba, kama utaendelea kukaa kimya, ndo jipu linaendelea kutunga kwa ndani.bora ulitumbue mapema ili kama litaleta kidonda, ukipeleke kwa daktari mapema upone na uanze kutembea vizuri. inauma sana kudanganywa,kulea mtoto ukijua ni wako kumbe sio. inauma sana, kwa hiyo ni lazima uwe tayari kwa lolote. Inavyoonyesha ni kwamba, wewe sio mtu mwaminifu. na sio mtu wa dini, mtu wa kawaida hawezi kudanganyika kirahisi hivyo.

Hiyo ilikuwa ni tabia yako, ndo maana nasema lazima ule pilipili uloiunga mwenyewe. nanilazima iishe, ndo upakue mboga ingine isokuwa na pilipili. jitahidi kufumba macho, to face this prob, na hakuna wa kumlaumu.ila Mungu ni wenye rehema, anaweza akakusaidia jambo hili likawa rahisi, lakini ni kwa miujiza ya Mungu, sio hivihivi.

Unavyoonekana ni kwamba, wewe sio mwanake layman. unaonyesha umesoma kidogo, hivyo hata mwili wako unaujua. ulijua kabisa siku zako za hatari ni zipi, na ambazo sio za hatari ni zipi. uliamua tu kuzaa na huyo mtu.mtu msomi kama wewe hawazi kuwa reckless kama hivi. ulifanya makusudi kabisa,na huyo mtoto ulitarajia iwe hivyo,ndo maana hata ulipopata mimba ulienda kumwambia jamaa hata kabla hajazaliwa, kwasababu ulijua kuwa umeamua kufanya ngono wakati wa siku za hatari ili umzalie jamaa huyo mtoto. siajabu huyojamaa alikuwa mtu wako wa zamani, au pengine jamaa ni handsome hivyo ulipenda tu upata photocopy yake kwenye tumbo lako.

the only remedy hapa kwako dada, piga magoti,mwombe Mungu, Okoka, ubadilishe maisha yako ili Mungu akusaidie uwe makini katika nyendo zako. katika maisha siku zote, kuwa nje ya Mungu ni hasara kama hizo. ona sasa shetani alikushauri ufanye ngono na huyojamaa, lakini sasa hivi ukiwa na matatizo amekuacha peke yako. shetani amekutelekeze? ndo maana nasema, jibu lako lipo kwa Mungu tu sasa hivi. kama ukifanya moyo wako kuwa mgumu, I tell you, this issue sio rahisi, itakugarimu sana. bora utafute msaada wa Mungu ndo pona yako, na ndo utaweza kufikia solution ya heri. Nenda kanisani, mara moja haraka sana, kaokoka na uanze kuwa mtaua.asante.
 
Dada Maindainda,
Mwambie mumeo na liwalo na liwe.
Ningekubaliana kabisa na wote wanaokushauri usimwambie:
1. Kuhofia reaction yake;
2. Kumuonea huruma huyo mtoto;
3. Kuionea au kuepusha kuvunjika kwa ndoa yako nzuri na yenye wingi wa upeno;
4. Kuwaonea huruma wanao wengine kama wapo .nk.

Lakini the fact kwamba huyo pressumptive father ameshakutishia kuwa kuna siku atakuja kumchukua mwanae, linakuweka mahali pabaya kweli. Ninamini mumeo atafedheheka na kudhalilika zaida kama atashtukizwa tu siku mmoja na mwanaume mwingine(presumptive father) kuwa huyo mtoto sio wake. Ni vyema ukadeal nalo mwenyewe.

Ingekuwa unaweza kutoa facts zaidi kuhusu mumeo na fikra zake katika tu maisha yenu ya ndoa, naaimini ungeweza kupata msaada wa how to go about it. Mfano: unaweza kushirikisha watu wengine kwenye mazungumzo hayo kumbe Mungu wewe kakupendelea kuliko wanawake wengine kakupa mume mvumilivu, muelewa kama Abunuwasi. Utakuwa umetoa siri iliyokuwa si lazima itoke nje. Lakini huenda mumeo ni kiboko, basi bila msaada wa watuliza ghasia unaweza ukajikuta mortuary pasipo kutarajia. Huenda wewe huwezi kujieleza labda unahitaji msaada, hapo then unahitaji wa kukusaidia kufanya hivyo.

Kwa vile kuna information nyingi inakosekana inakuwa vigumu kweli kukushauri ni njia ipi bora. Ukisema ina madhara tena makubwa. Ukinyamaza si sahihi na what "IF".

Dada endelea kusali na kuzingatia ushauri mbalimbali unaotolewa na ambao ukiuassess unaona unaswihi situation yako.

Good Luck.
 
sina zaidi ya kusema, pole sana, japo najua hujapoa, lakini kupata raha na peace of mind it to aim a little too high, sometimes we have to live with the consequences of our past mistakes.
you are not alone my dear, that may console you.
but you will have to brace for the future, praying it will be a little kind to you.
in the mean time, think for the husband, for the kid and less of yourself.
you have had your enjoment, now its time to consider others in turn.

Just have strength, and do not let despair get you down.
 
Dada.

For the sake of the child, mwambie mumeo. Ushauri wangu ni kwamba tafuta wazee wenye hekima ambnao mumeo anawaheshimu ndio wakamwambie na isiwe wewe. Haya kaa kimya. Siku baba wa halali akifuata mtoto wake au ukaletewa mkweo na mtoto wako huyo kumbe mkewo ni dada/kaka yake na kitumbo juu (kama ni dada!!). Utatamani dunia ifunguke ikumeze.

Sikubaliani kabisa na kitendo cha kumficha mtoto biological parents wake!!!!
 
Kwa wale wajuao sheria - Kisheria, huyu mtoto ni wa nani?

Kama ni wa Biological father, naweza kufanyaje awe wa kwangu?

Kama alivyoshauri Pundit, hata kama hayupo katika birth certificate, anaweza kushinda kwa kuangalia Vinasaba-DNA, kama ni mtu anaependa fujo au kuna watu hawajali ndoa zao au zimewashinda na wanaweza kutumia chochote ili mke/mume apate EXIT way. Najaribu kuwa mwangalifu hapa.
Pole dada kwa yote. Kwanza hili sakata si rahisi kama linavyoonekana na wengine. Kama ulibakwa na huyo jamaa na ukamficha mumeo kwa miaka kadhaa kwa vyovyote wewe ni mkosaji. Ningekushauri tu ujukaze kike, na hiyo ibaki kuwa siri yako. Huyo unayedhani kuwa ni baba wa mtoto wewe achana naye. Hakuna mwanamme mwenye akili zake anayeweza kudai mtoto kutoka kwa mke wa mtu. Kisheria mtoto huyo ni wako mama. Ningekuwa mimi ningetangaza kubakwa maapema tangu siku uliyoisaliti ndoa yako. Haya yasingekukuta. Kwa kuwa uliamua kumtunzia siri mhalifu, hizi ni gharama zake. Endelea kula jiwe. Lakini kukupunguzia matatizo mshauri mwenzio mtoto aende boarding school. Angalau utakutana naye hapo kwako wakati wa likizo tu.

Kama unataka ndoa yako iendelee, usithubutu kumtamkia mumeo jambo hili. Si rahisi kusamehe usaliti wa ndoa na hasa kama huyo bwana mumeo anamjua.
 
Kidzogolae, naomba kukujibu kama ifuatavyo:

Hiyo ilikuwa ni tabia yako, ndo maana nasema lazima ule pilipili uloiunga mwenyewe. --- HIZI TUHUMA ZAKO SI ZA KWELI. KAMA KWELI WEWE NI MTU WA MUNGU, ANZA KUTUBU KWA KUSEMA UONGO MBELE YA KADAMNASI HII


Unavyoonekana ni kwamba, wewe sio mwanake layman. ....kwasababu ulijua kuwa umeamua kufanya ngono wakati wa siku za hatari ili umzalie jamaa huyo mtoto. siajabu huyojamaa alikuwa mtu wako wa zamani, au pengine jamaa ni handsome hivyo ulipenda tu upata photocopy yake kwenye tumbo lako. ----- SI MZURI KABISA KAMA UNAVYOFIKIRI AU KUSEMA KWA HIYO SIHITAJI COPY YAKE. WALA HAJAWAHI KUWA JAMAA WANGU WA ZAMANI AU SIKU NYINGI. SIWEZI KUKULAZIMISHA UKUBALI NINACHOSEMA ILA UKWELI WA KILICHOTOKEA NIMEUELEZA
 
Bibie Mandainda,

Kazi unayo kwelikweli....

Anyway, wengi wametoa mawazo/ushauri wao kuhusu nini ufanye...

Binafsi napendela kuigawanya Dunia mara tatu - Spiritual World, Moral World, na Reality World. Sasa basi, kabla sijaanza mchakato wa kulipangua kila jambo linalonikinga mbele yangu, kwanza najaribu kuli-fit katika kila moja ya hizo Dunia kuona ni Dunia ipi hilo jambo lita-fit haswa.....halafu nalipangua. Muda mwingine napatia, na muda mwingine nakosea. Kukosea ni sehemu ya misukosuko ya maisha.

Sasa nikijaribu ku-fit ishu yako kwenye hizo Dunia tatu, tutaona kwamba:
Spiritual World - Unachotakiwa kufanya kiko wazi kabisaaaa....MWAMBIE MUMEO. Kwenye hii dunia hakuna mjadala zaidi ya kufanya hivyo.
Moral World - Kinachoendelea katika Dunia hii hakina tofauti sana na ya Spiritual. Tofauti ziko chache mno. Kwa hiyo jibu ni kama la hapo juu.
Reality World - Siku ulipogundua kuwa kipande kilichokatia tumboni mwako sicho cha mumeo, ulihamua kuminya. Sasa kwanini usiendelee kuminya hivyo hivyo? Anyway, hapa unachotakiwa kufanya kinategemea na watu wangapi wataathirika. Je ukisema, ni watu wangapi wataathirika na taarifa hizo? Vivyo hivyo usiposema. Pima matokeo ya ukisema versus usiposema. Fuata uamuzi ambao utabebwa na matokeo mepesi.
 
Wafikirie na wahusika wengine katika familia yenu. Sasa hivi wewe pekee ndiyo unakosa raha kwa hili. Utakapoamua kusema hujui uamuzi wa mume wako utakuwaje anaweza kuchanganyikiwa, anaweza kabisa kumchukia mtoto na kutotaka kujihusisha na lolote kuhusiana na mtoto huyo. Ndoa itakua mashakani na inaweza kuvunjika, kama mna watoto wengine nao pia watakuwa affected kwa kuwa familia yao ndiyo itavunjika. Ndugu, jamaa na marafiki wanaweza kabisa kukuchukia. Kwa hiyo wafikirie wote wanaohusika katika sakata hili je, kama utaamua kusema wataathirika vipi na maamuzi mbali mbali ambayo mengi yatakuwa nje ya uwezo wako.
 
I keep wondering, when did you realise that you have made wrong?
After the action? no...............
after you met him and decided to enter into a discussion about your pregnancy? no...............
( ia ma sure you have had more than a single encounter with him)

after growing older and came back you some of your senses? no...............

What are you afraid of any way? the child will survive it, the husband will survive it too, provided you come CLEAN. Not like what you told us here in the board.
You know there ias a lot unsaid, a lot of twisted and hiden information in this story, and all of us have noted it.

you are afraid of what the community will think of you, YOU!!! YOU!!! only.
Stop being selfish.
As it has been said, earlier, if you wait until your children get married that will be worse.
For further advise please search for information on the internet about breaking a wrong relationship.
 
Haika,

Kama nilivyokwishaliambia baraza hili na kutia msisitizo kwa Kidzogolae, story yangu ndiyo hiyo, amini au usiamini. Singependa kubadilisha mwelekeo wa mjadala huu kwa kuhamia katika nilifanya mara ngapi, wapi, kivipi, nk. Hapa swali ni nifanye nini sasa? Hayo mengine hayanihusu. Hili jambo latia aibu, wala si mimi tu bali na mume wangu, familia yangu nk, kwa hiyo sihitaji kukumbushwa hilo.

Nashangaa comments zenu zinazoonyesha kama vile hamuijui sayansi ya upatikanaji wa mimba? Hivi unahitaji kufanya mara ngapi ndio ubebe mimba? Anayebakwa na kupata mimba wakati huohuo mtasemaje? Kama wanajamii hii kasumba ya kuona mshichana/mwanamke kabeba tumbo lake halafu mnaanza kumhesabia kafanya mara kibao haina mantiki kabisa. Mimba ni Sperm na Ova, BASI, sio frequency.

Hivi One Night Stand ndio maana yake nini labda? Ikikutokea ndio utajua ninachosema.

Najua consequences zangu nikisema kwa mume wangu (si lazima ziwe sawa au zitokee), na wala sitaki kuwa selfish. Sitaki asiyehusika apate shida.
 
Dada.

Kweli inaonekana unajutia sana tendo lililotokea.

Face the consequences. Uzuri ni kwamba si lazima zitokee. Kama nilivyosema, usimwambie wewe bali tafuta mzee/wazee wa heshima wamwambie. Kama baba mkwe wako yupo hai, huyo ni the right person kwa kukuombea msamaha, na naamini atakuelewa. Mimi ni mwanaume na nina-imagine kama ni mke wangu amefanya hivyo na hajaniambia mpaka nikagundua mwenyewe. Mhh. Patakuwa hapatoshi.
 
Inategemea huyo baba yuko je. kuna wengine wenye soft hearts na wengine hawana. Inategemea pia amewahudumia miaka mingapi. Kuna mwingine hatajali hilo ila utaondoka kwake na ataoa demu mwingine. Mwingine atakuchanachana kwanza kusikia tu habari kama hiyo. Ningekuwa wewe ningesubiri ,maana hiyo ni dhambi yako ya mauti. Na inawezekana hata akikusamehe ikawa inaendelea kukuuma hadi mwisho.Halafu kwa sasa wewe ndio unaumia ila ukisha mwambia leo mtakuwa manumia watatu. Wewe , yeye, na huyo mtoto.

Hata wewe unajua siku moja itajulikana, ila hujui time is a big problem solver.
 
mainda,pole sana mpenzi,naamini umesoma majibu yote kwamakini,na naelewa how ua feeling now,sasa mume wak ni binadamu ,so na yeye pindi utakoppmwambia atajisikia kimojawapo kama watu walivyojibu ,either +ve or -ve itategemea jinsi alivyo na anavyokuchukulia wewe kwakweli,
sielewi mpenzi wangu umejitayarisha vipi kwamatokeo ambayo yatatokea iwapo atalijua hili kwanjia yoyote ile,LAKINI MAINDA LOLOTE LITAKALOTOKEA PLEASE TRY TO BE STRONG,NAAMINI LITAISHA TU,HAMNA HAJA LA WEWE KUKUUMIZA ,MAANA LIMESHATOKEA NA HUWEZI KURUDI NYUMA ,MIUSHAURI WANGU NI WEWE JINSI GANI YA KUMOVE ON,NA KUZOEA KWAMBA HII JAMBO LIMETOKEA,WETHER AKIJUA BILA KUMWAMBIA OR UKIMWAMBIA,MAINDA MOVE ON,KUWA BUSY ANZISHA BUSINESS YOYOTE IKUWEKE UWE BUSY,TENA INGEKUWA MAJUU,UNGEAZISHA COUNSELLING FIRM,MAANA UMESHAYABEBA YA KUOSHA ,NANAAMINI USINGEPENDA MTU MWINGINE AYAPATE HAYA KAMA UNAVYOJISIKIA NOW,WEWE KUANZIA LEO ENDEEA NA MISHA YAKO KAMA KAWAIDA,USIMWAMBIE NA AKISIKIA ,MWAMBIE MUME WANGU NAKUPENDA SANA,SIKUTAKA TUACHANE,NISAMEHE,NA NILIPENDA WEWE UWE BABA WA UYU MTOTO .
MIMI NI HAYO TU MPENZI WANGU.
 
Haika,

Hivi One Night Stand ndio maana yake nini labda? Ikikutokea ndio utajua ninachosema.

Najua consequences zangu nikisema kwa mume wangu (si lazima ziwe sawa au zitokee), na wala sitaki kuwa selfish. Sitaki asiyehusika apate shida.

1. Hutaki mtu apate shida ( THAT IS A LITTLE TOO LATE TO WISH FOR)
2. lazima watu wataumia, be prepared, ila know what you should do and do it.
3. Yes it was one night stand in bed , but it lasted for longer our of bed. (that is my stand)

My dear, ndoa haijengwi wala kubomolewa na kosa moja.
Usijipe woga kiasi hicho, we mwambie tu!!
Trust your good concious which pushing you now.
unless there is something else GOING ON IN YOUR LIFE TOGETHER WITH THE MAN, WHICH YOU HAVENT DISCLOSED HERE.
kama unaogopa hutasamehewa, ina maana wewe huwezi kumsamehe mumeo???
Lazima atakusamehe (provided kuna uelekeo wa kujuta na si kujuta kwa sura)
 
Kitu ninachokwambia ni cha kweli kabisa. Unatakiwa ukubali kuface chochote kitakachotokea. and you should not underestimate it. ni kitu kigumu sana na hatari sana. kama dadangu, ningekushauri uchukue ushauri wa jamaa mmoja hapo juu, upitie mgongo wa mtu mzima, yani mzee, eg.baba mkwe, wazazi wako waende wakaongee kwa babamkwe nk. ukienda wewe mwenyewe pekeyako, tutakukosa kwenye hii JF. usijaribu kuvuka mto wakati kuna mamba.

pili, kama utaendelea na hiyo tabia yako ya kunyamaza wakati ulishafanya kosa, kuna siku jamaa akija kugundua yatakuwa makubwa. bora uanzishe wewe mwenyewe ili ajue lilikuwa linakuuma na ulikuwa hauna nia ya kulificha, ila tu ulikuwa unatafuta nafasi appropriate ya kumwambia. Ukificha, damu nzito kuliko maji, na hakuna siri ya watu wawili duniani. Hilo lijamaa lenye mke lililo kubanjua, halitakubali mtoto wake aendelee kubaki na mwanaume mwingine. kuna siku tu ataamua atoe siri, akijua kuwa yeye hayuko kwenye hatari sana kwasababu hakai na mme wako uliyemdanganya,,,,wewe ndo unakaa na mumewako kwahiyo hadi afike kwa hilo lidume lililo kubanjua, hasira zitakuwa zimeshaishia kwako. hivyo, lazima tu kuna siku jamaa ataamua kuweka siri wazi ili akomboe mtoto wake.

hivi unafikiri ni kitu cha kweli, mtu awe na mtoto wake halafu akue hadi awe mkubwa bila kujitambulisha ili ampe mtoto wake upende wa dhati? asikudanganye mtu. siku mme wako akija kugundua kuwa ulikuwa unamficha, utashindwa hata hicho kidogo cha kujitetea. period.
 
Maindainda acha kubweteka. hapa utapata kila aina ya jibu au mampendekezo. wewe angaliwa what best you can do....

ANGALIZO
Ninamtafuta kimahaba mwanamke aliyeachika mwenye mtoto wa nje ya ndoa yake....
 
Pole Dada,

Nakuomba, kama ulivyoamua kukaa kimya kwa muda wote huo bila kumwambia your beloved husband!! basi uendelee kunyamaza, at least unayeumia for the time being ni wewe peke yako, imagine ukilitoa hilo bomu ni wangapi wataathirika????????? kaa kimya wewe na Mungu wako.
 
Back
Top Bottom