Mtoto wa Jicho, Kisukari ni chanzo kikuu cha Upofu Kanda ya Ziwa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
James Shimba, Daktari Bingwa wa Macho kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando amesema uchunguzi wao umebaini kuwa magonjwa ya Mtoto wa Jicho na Kisukari ndio chanzo kikuu cha Upofu kwa kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Shimba ameeleza kuwa Hospitali hiyo kwa mwezi inapokea Wagonjwa wa Macho zaidi ya 1000 wakiwemo watoto ambapo idadi ya watoto wenye tatizo la Macho wanaoonwa na Daktari kwa siku imefikia 70.

Aidha ametaja sababu nyingine ya ongezeko la wagonjwa macho na tatizo la Upofu kuwa ni watu kupuuza matumizi ya Miwani wanapoagizwa na watalaam wa Macho.
 
Upasuaji wa jicho na kuweka lenzi mpya ya jicho inawezekana kama vifaa vitanunuliwa na wataalamu wetu watawezeshwa. Ikiwezekana kila mtaa watu wapimwe na wenye mtoto wa jicho wafanyiwe upasuaji.

Huko ndiko kodi ilitakiwa kupewa kipaumbele badala ya V8.
 
Back
Top Bottom