GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,695
- 6,398
Unaweza ukashindana na watu wa Kanda ya Ziwa kwa mambo fulani fulani, lakini usithubutu kwenye uendeshaji wa baiskeli kama wewe si mmoja wao. Utaumbuka! Nazungumzia baiskeli za kawaida au za kazi, siyo zile za "starehe".
Sina uthibitisho wa kitakwimu, lakini kwa makisio yangu, Kanda ya Ziwa inaongoza kwa uendeshaji baiskeli.
Najua Singida nako wako vizuri, lakini sidhani kama wanawafikia "Wasukuma"
Ni nadra kwa mkoa niliokulia kumkuta mwanamke akiendesha baiskeli, lakini ni kitu cha kawaida kwa Geita, Shinyanga, na Mwanza, hasa maeneo ya vijijini. Huko, si ajabu kukutana na mwanamke amebeba mzigo mkubwa kwenye baiskeli ambao mwanaume wa mikoa mingine asingeweza.
Najua kuendesha baiskeli, lakini watu wa Kanda ya Ziwa walinifanya nijione Chekechea kwenye uendeshaji baiskeli.
Wakati fulani, nilikuwa Misungwi maeneo ya vijijini mkoani Mwanza, nilipoamua kukodi baiskeli kwa lengo la kuitumia kama usafiri wa kunifikisha mahala fulani. Usafiri uliokuwa ukipatikana huko ni wa pikipiki na baiskeli za kukodi. Niliamua kukodi baiskeli.
Nikiwa njiani, mama mmoja wa Kisukuma akiwa na baiskeli, alikuwa amebeba mzigo juu ya baskeli na mtoto mgongoni, alinipita kama vile nimesimama.
Sikutaka ligi naye, ingawa sikupenda alivyonipita kwa "dharau". Niliishia kumwambia kimoyo moyo, "nenda salama mama"
Kanda ya Ziwa hongereni!!!