Mtihani, zawadi ya krismasi..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtihani, zawadi ya krismasi..!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbu, Dec 23, 2011.

 1. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  [​IMG]....ushauri wandugu...maana huu utamaduni unaonifanyisha nifikirie kwa lugha ya kigeni karibu naadhirika ugenini...

  nimeletewa zawadi na mlimbwende (namshukuru mungu sina wa kuniuliza nimepewa zawadi na nani na kwanini,) kaniambia ndio zawadi yangu ya krismasi...kilichomo ndani ya boksi na u thamani wake mnh...

  ...sasa je? niuchune, au inabidi nami nimtafutie kilicho na thamani sawa au kuzidi hiyo? nasikia krisimasi zawadi lazima zikabidhiwe eti kabla ya tarehe 26?!...mbu anaadhirika ugenini, lol!
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,268
  Likes Received: 19,412
  Trophy Points: 280
  kakupa nini?
  mpe hii
  PORC-RB33.jpg
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mbu sena kwanza umepewa zawadi gani ili tukushauri vizuri. . . au angalau inahusiana na nini.
   
 4. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #4
  Dec 23, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mbu HONGERA saana kua na mpenzi ambae hukununulia zawadi... Wengine hilo limewashinda kabisa tokana na selfishness.. Or ile tu kutotambua kua kila mmoja uhitaji zawadi once in a while....

  B2T IMHO Naomba niseme kua uelewa wangu ni siri ya nyuma ya zawadi ulotumiwa ndo hufanya iwe nzuri ama mbaya (hasa kama kweli mwapendana kweli - achana na haya Mapenzi ya kuhongana!); Kumnunulia Mpenzi wako zawadi muafaka ya kumfurahisha utegemea saana na jinsi gani mwaishi, nini yeye apenda, kitu gani katamani recently labda ikawa nje ya uwezo wenu na pia experiences na kumbukumbu mlizojenga kama wapenzi kama wapenzi. Kwa mantik hio naamini kua bei ya zawadi does not always matter... What matters ni ile zawadi yasema nini? Mfano labda katika mahusiano yenu Mpenzi wako kisha wahi zungumzia "maybe nilikua na kitabu fulani cha mwandishi fulani - hua chaniuma saana kilipotea for I loved the book".... I am taking it kama utafanikiwa kukitafuta hicho kitabu na ndo ikawa zawadi.... Ataifurahia mno for the following reasons....  • Itaonesha wamkumbuka akiwa hayupo.
  • Itaonesha wajali saaana kwa kuhakikisha anapata the one thing anapenda.
  • Itaonesha you remember every moments (hata kama sio kweli wakumbuka).
  • Itaonesha kweli wampenda. Ni tofauti kama ungemnulia tu zawadi ya thamani kubwa mno... YES atafurahi but it portrays a different message in the relationship kama sio tu kusema I can buy anything for you....

  Mbu... Happy Festive Greetings to you....
   
 5. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Inategemea huyo mtu unampango nae gani wewe binafsi na sio yeye.

  Kwahio aina ya zawadi utakayompa wewe ni kutokana na na uzito gani unampa kwenye malengo yako na sio uzito wa zawadi yake.

  Yeye kashakupa zawadi kutokana na jinsi anaona umuhimu wako kwake na wewe zawadi yako inatakiwa itokane hivyo na sio kupima kwa kutumia zawadi yake. Zawadi zina ujumbe mkuu kwahio na wewe peleka ujumbe ambao nafsi yako inamaanisha na sio kulingana. Na zawadi yake.
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Dec 23, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  It's the thought that counts. Ndicho hicho ulichomaanisha hapo?
   
 7. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ohoooo,....sasa nyie msilete za kumwaga mtama hapa,....naweza jitutumua kutaja zawadi halafu kina klorokwini waje nishushua bure hapa na uluga luga wangu...btw, nilipewa sharti la kutoifungua mpaka eti boxing day...

  all in all, mnaniambiaje sasa....Ivuga na Lizzy imagine zawadi ina thamani approx £150 (tu)...(tshs laki nne kasoro za bongo?)
  Kabla hamjanishawishi nijifunge mabomu, mkumbuke nategemewa na kijiji........wanasubiria sikukuu yao niwatumie pesa... :(
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  well bro... it is indeed her thoughts of you that count more than a million dollars bro

  love and friendship can never be quantified or at least measure in terms of $$$$

  count your blessings bro...
   
 9. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  mnh, AshaDii....unantakia balaa weye ee? soulmate akija soma humu itakuwaje yarabi?
  astaghafirullah, huyu si mpenzi wangu....ni rafiki tu wa kike ambaye amenitia majaribuni
  kiasi cha mbu miye usiku wa manane huu nawaza nikiwazua kwa lugha za kigeni....

   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Dec 23, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Huu kweli unaweza ukawa ni mtihani. Lakini inategemea na yeye mtoa zawadi ni mtu wa aina gani.

  Kuna aina ya watu ambao wao wakimpa mtu zawadi basi na wao wanategemea kupewa zawadi na huyo mtu waliyempa zawadi. Tena unakuta wengine wanategemea zawadi yenye thamani sawa na waliyotoa au hata yenye thamani kuizidi waliyoitoa.

  Pia kuna aina ya akina mimi. Tukitoa zawadi tunachotaka ni angalau ka asante tu, basi tunakuwa tumeshamalizana.

  Sasa Mbu wewe huyo mtu wako wewe ndiyo unamjua vizuri zaidi yetu sisi. Kama umeshamsoma vizuri ni mtu wa aina gani basi utakuwa na dhana nzuri ya nini ufanye.

  Kama yupo kwenye kundi la akina mimi basi hata ka 'Thank you' card katatosha. Ila kama yupo kwenye lile kundi lingine hapo unaweza ukawa usiwe na ujanja zaidi la sivyo unaweza usieleweke kabisa.
   
 11. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...duhhhh!?....wewe umenipa mtihani zaidi!....
  inanibidi nikeshe sasa nikijaribu kutafsiri hii zawadi ina maana gani...
  aisee?....nilidhani zawadi ni zawadi tu....kumbe kuna ujumbe ndani!
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Khaaaa. . . Mbu siri haizai bana!!

  Nwy kusema ukweli hamna haja ya kujitutumua ufikie bei (kijijini watu watakosa pilau) kwahiyo we tafuta kitu cha bei ya kawaida kinachoendana na uhusiano wenu. Vitu kama PERFUME hua havijali mahusiano wala jinsia, so kama ni mtumiaji mtafutie ambayo iko kwenye SALE basi biashara imeisha. Chochote utakachompa zingatia bei (isiwe juu) na ujumbe. Hatutaki kushauri namna ya kuondoa ruba wakati ulimwita mwenyewe!!!
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,268
  Likes Received: 19,412
  Trophy Points: 280
  ingekuwa mimi natoboa box nachungulia..hawachelewi kukupa peni hawa
  mimi nakushauri angalia post #2 kanunue zawadi boy
   
 14. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #14
  Dec 23, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mkuu zina ujumbe na ndio maana unahisi kama mtego na kuona ni mtihani mpaka umekuja kuomba msaada.


  Kama angekuwa mtu wa kawaida tu nadhani wala usingefungua thread.

  Ndio mkuu zawadi zinatumika kutuma ujumbe .
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  Dec 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Na wewe ukipewa. . . . . ?
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...kamanda huu nao ni mtihani,....si nasikia hawa wenzetu (wadhungu) kipindi kama hiki ndicho cha kubadilishana zawadi, si ndio bana? sasa nikisema asante na card tu mnh...si ndio nitaonekana mi mandingos ndivyo ilivyo?
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Dec 23, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Nitaipokea kwa mikono yote miwili na kwa moyo mkunjufu kabisa kwani kukataa zawadi si uungwana.

  Mwenzio kukufikiria na kutumia muda wake kwenda kutafuta na hatimaye kuinunua hiyo zawadi si jambo dogo la kuletea masikhara.

  Wewe unaonaje?
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Dec 23, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Loh! Kumbe imetoka kwa hao watu. Ngoja nikupe pole kabisa kabisa.
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Dec 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mmmh. . . .
  Na baada ya kupokea?Unaona kuna uhitaji wa kurudisha (na wewe kutoa zawadi)?
   
 20. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #20
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...khaa, SALE hapa mpaka boxing day bana...halafu mtu kajitutumua zawadi ya gharama halafu unanishauri nikamtafutie PRIMARK kizawadi cha sale? Lizzy usinifanye nionekane cheap bana, krismasi comes but once a year bana...ila mnh, bajeti na recession hii!...


  ...Ivuga, sijachungulia tu...nishachana wrapping paper zamani, na zawadi nishaitoi kwenye boksi ndio maana nikakwambia mpaka na makisio ya uthamani wake! Mswahili mie bana, ngoja ngoja nikifa je kabla ya krisimasi?

   
Loading...