Mtihani wa kesho huu hapa!!

kutokana na watu humu ndani kudai kwamba mitihani imekuwa inavuja kila mwaka na kilichobadilika ni aina ya teknolojia inayotumika kuivujisha,nimeamua kuweka mtihani Historia wa taifa wa kidato cha nne utakaofanyika kesho ili kwamba kila mwenye kuuhitaji basi ajipakulie hapa, asije akafeli bure!!

Kitu!!

1. Why did British adopt indirect rule system in their colonies?
2. Explain the factor of the rise and consolidation of the centralized states in different African societies
3. how did the outbreak of World War I and world War II intensify the rise of nationalism in Africa
4. Describe various methods used in the establishment of colonial economy
5. explain the factor of exploitation in mode of production in Africa around 15th Century
6. Political instability is inevitable to Africa. Verify this statement and measures taken to prevent them
7. Factors of abolition of slave trade
8. how did USA support the decolonization of African colonies
9. In which way colonial education destroy African culture
10. Effective mass education maintained resistance against colonialism .Discuss
11. Discuss form and the motive of African nations reaction against colonial occupation

And then there is a map on which a candidate needed to spot the East Africa costal cities historical Sites and answer the Questions about African resistance against Colonialism and who was involved

As far as i know format ya mtihani haiko hivo.Anyway lets see.Hivi haijaundwa tume kuchunguza kwa nini mitihani imevuja?
 
Umefika wakati sasa kubadilisha mfumo mzima wa utungaji, ufanyaji na usahihishaji wa mitihani hususan ya sekondari.

Mfumo wa sasa umepitwa na wakati kutokana na ongezeko kubwa la mashule ( sijui zile sekondari za kata za Lowassa zitakapofika form 4 itawakuwaje) ya sekondari na ukuwaji wa teknolojia ( mobile internet etc) vilevile na kuota mizizi kwa rushwa kona zote za nchi. Ni ukweli usio na shaka udhibiti wa mitihani utakuwa hatarini miaka yote imagine shule ya sekondari ipo mpakani huko na Uganda nyingine mpaka na Msumbiji nyingine zipo kwenye visiwa vidogo vidogo ni mitumbwi tu ndio inafika huko. Katika hali kama hii mtihani unaotungwa Dar Es Salaam unatakiwa atoke Dar kwenda huko ( remote areas) walau wiki moja kabla. Kwa hali ya kawaida udhibiti hapo unakuwa mgumu kosa dogo tu mtihani ukiangukia kwa mjanja unasambaa kama moto wa nyika nchi nzima nahili ndio tunalo shuhudia sasa.

Nadhani ipo haja ya kufuata mfumo wa shule msingi ambao upo kikanda au kimkoa hivi. Hapa hata hivyo panatakiwa pawe na usimamizi mzuri isije ikawa mikoa au kanda nyingine zikawa na mitihani poa wakati wengine wana mitihani migumu kunaweza leta balaa jingine.

Kuwatia kitanzi mama Ndalichako na Maghembe ni kukata matawi na kuacha shina suala hapa ni mfumo sio utendaji.
 
MMh mbona hiyo format ya maswali ya kujieleza (normally section B) huwa haina maswali 15? hata language na aina ya maswali ni "utata" kidogo... Im not rulling out anything but mmmhh haya....

Wala usibabaike mkuu, bado inaweza kuwa ndio pepa yenyewe. Katika kunakili maswali kuyaweka hapa pengine ndiko kasoro ulizoziona zilikotokea. Kwa technolojia ya sasa hivi maswali yanaweza kusambazwa na sms za simu hadi yote yakatimia. Na kwa kuwa yanasambazwa mtindo huo, huwezi kuona instructions zote (ambapo nyingine zinasema kwa mfano jibu maswali mawili kila section etc, maana yake hayajibiwi yote). Niliwahi mimi kupata "tenda" ya kufundisha part time, tena jioni tu katika shule moja maarufu mkoani Kilimanjaro, mwezi mmoja kabla ya mtihani wao wa form 6. Walikuwa wananilipa vizuri kwa kweli, malipo kwa saa! Lakini wanafunzi hao hawakuwa na mwalimu wa hilo somo tangu walipoingia A-level, lakini mkuu wa shule akawa ananisisitizia atanipa ushirikiano wowote nitakaohitaji. Mimi sikuwa na lolote zaidi ya kuwafundisha kwa "kubahatisha" kwenye yale maeneo yanayouliziwa maswali mara kwa mara, angalao vijana waambulie japo S au E kwa wenye bidii sana. Wiki ya mwisho, kama siku 4 kabla ya mtihani, mkuu wa shule akaniita ofisini akanitajia vitu vya kufundisha, alinisomea kutoka kwenye karatasi aliyokuwa nayo nikaandika kwenye notebook yangu (nadhani aliamua kunifanyia dictation kuepuka kunipa "ushahidi" ukizingatia nilikuwa "mpitaji" tu!). Na seriously, alikuja darasani kukagua kama nafundisha yale mambo (ingawa alizuga anakuja kuwapa "morale" wanafunzi wake). Niliyafundisha nikayarudia tena na tena! Ajabu, katika mtihani yalitoka yale yale! Wanafunzi walipotoka nje ya chumba cha mtihani wakanibandika jina la "Hassan Affif" (alikuwa kocha na pia mchezaji wa Simba, na kipindi hicho alikuwa anawika sana sikumbuki kwenye michuano gani, lakini nadhani ya kimataifa). Matokeo yalipotoka, hakukuwa na A wala F, lakini katika wanafunzi 49 watano walipata B, wanane S, waliobaki katikati hapo.

Kwa uzoefu huu ni kwamba mitihani hii inaibiwa kwa njia nyingi, na zote zinapaswa kufuatiliwa kwa umakini mkubwa.
 
mmekosea mngeleake hii pepa ..muda mfupi kabla ya mtihani...hapa hamtawapata mmewapa muda wa kutangaza kuahirishwa kwa huu mtihani [kama ni kweli]

Obviously utapigwa stop wataleta whatever they call their emegerceny paper ili kuzuia hiyo aibu!
 
nime-paste na kusave then nita-print na jambo la kwanza kesho ni kwenda huko shuleni nikikuta ni wenyewe kwa kweli moto utawaka huu ni mwendolezo wa ufisadi hadi kuharibu watoto wetu
 
Nini taarab give me a break!sema jingine na si taarabu!niambie basi wewe mfumbuzi Mwanakijiji alimaanisha nini?

Kit_Kat_Mini_Bag_332_gram.jpg

hiyo hapo mini, chukua!!! lol

You seem so furious...seriously, you don't need to get angry mwaya... take it easy, yalikuwa mawaidha tu, yasikusumbue na tuendelee na libeneke.
 
AU UPO INTERNET CAFE GANI TUKULETEE PORTABLE SCANNER ? , au kwanini hata usiupiga picha huo mtihani page ya kwanza kwa njia ya simu uuweke hapa ? so simple
 
mmekosea mngeleake hii pepa ..muda mfupi kabla ya mtihani...hapa hamtawapata mmewapa muda wa kutangaza kuahirishwa kwa huu mtihani [kama ni kweli]

1....ukiahirishwa ndio itakuw anamna moja ya kuthibitisha
2......ikithibitika hiyo kesho.....

............Mkuu Ben nitakuwa pamoja na wewe kuwaambia Maghembe na Ndalichako wawajibike
 
Kit_Kat_Mini_Bag_332_gram.jpg

hiyo hapo mini, chukua!!! lol

You seem so furious...seriously, you don't need to get angry mwaya... take it easy, yalikuwa mawaidha tu, yasikusumbue na tuendelee na libeneke.
asante sana ubarikiwe
 
AU UPO INTERNET CAFE GANI TUKULETEE PORTABLE SCANNER ? , au kwanini hata usiupiga picha huo mtihani page ya kwanza kwa njia ya simu uuweke hapa ? so simple

mkuu,umeshaambiwa hataki,mbona uang'ang'aniza ofa?
 
Kigarama kama uko dar es salaam wilaya ya kinondoni au ilala nijulishe nitakuelekeza kwa kwenda kuscan na utume hapo hapo bure kabisa

Kigarama jiepushe na huyu jamaa anayejiita Shy, usijaribu wala usilogwe ukampa contacts zako! Atakuingiza mkenge wa ajabu sana. Kama unaweza kuwa na digital camera ukaipiga picha mwenyewe hiyo pepa ukurasa wa kwanza fanya hivyo umtumie invisible. Kama hilo haliwezekani basi njia nyingine utakayoweza, lakini nasisitiza sio huyu Shy atakutia matatani, anajulikana kwa hilo!
 
katika hali hii niliyoiona mimi mwenyewe ninaamini paper linavuja kila mwaka.

Si kweli! Waliomaliza darasa la 7 mwaka 1991, kidato cha 2 mwaka 1993, kidato cha 4 mwaka 1995 na kidato cha 6 mwaka 1998 mitihani ya miaka hiyo ilivuja. Ila waliowatangulia, yaani waliomaliza darasa la 7 mwaka 1990, kidato cha 2 mwaka 1992, kidato cha 4 mwaka 1994 na kidato cha 6 mwaka 1997 mitihani haikuvuja labda kwa watoto wachache sana wa Vingunge. Nini siri ya kutovuja huko?
 
Aliyepost anaweza ku-scan hiyo paper na kuweka hapa... tutamrudishia fedha yake!

---siyo kwamba atakamatwa na kupelekwa polisi kama Kubenea ali/navyofanyiwa, kwa madai kuwa JF ina-leakisha mitihani wakati anakabidhiwa pesa yake?!

---either way, i hope not!
 
Umefika wakati sasa kubadilisha mfumo mzima wa utungaji, ufanyaji na usahihishaji wa mitihani hususan ya sekondari.

Mfumo wa sasa umepitwa na wakati kutokana na ongezeko kubwa la mashule ( sijui zile sekondari za kata za Lowassa zitakapofika form 4 itawakuwaje) ya sekondari na ukuwaji wa teknolojia ( mobile internet etc) vilevile na kuota mizizi kwa rushwa kona zote za nchi. Ni ukweli usio na shaka udhibiti wa mitihani utakuwa hatarini miaka yote imagine shule ya sekondari ipo mpakani huko na Uganda nyingine mpaka na Msumbiji nyingine zipo kwenye visiwa vidogo vidogo ni mitumbwi tu ndio inafika huko. Katika hali kama hii mtihani unaotungwa Dar Es Salaam unatakiwa atoke Dar kwenda huko ( remote areas) walau wiki moja kabla. Kwa hali ya kawaida udhibiti hapo unakuwa mgumu kosa dogo tu mtihani ukiangukia kwa mjanja unasambaa kama moto wa nyika nchi nzima nahili ndio tunalo shuhudia sasa.

Nadhani ipo haja ya kufuata mfumo wa shule msingi ambao upo kikanda au kimkoa hivi. Hapa hata hivyo panatakiwa pawe na usimamizi mzuri isije ikawa mikoa au kanda nyingine zikawa na mitihani poa wakati wengine wana mitihani migumu kunaweza leta balaa jingine.

Kuwatia kitanzi mama Ndalichako na Maghembe ni kukata matawi na kuacha shina suala hapa ni mfumo sio utendaji.

MKuu Masatu

Nadhani kuwa na shule nyingi si sababu ya mitihani kuibiwa....shida ni rushwa ilishamili kila sehemu, wenye shule binafsi huiba mitihani ili watoto wafaulu zaidi ili wazazi waendelee kupeleka watoto huko. Tukiamua tunaweza kabisa kuondoa tatizo hili, kwanini mitihani isipelekwe kwenye mfumo wa Kibenki? Ninaamini Bank ni salama zaidi. Kwa Kuanzia Dr Ndalichako na Prof Maghembe lazima wachukue accountable responsibility kwa kuanzia na wale wafanyakazi wengine wanahusika kwa njia moja ama nyingine wachukuliwe hatua.

Sijui tunajenga taifa la aina gani? Kuna watu wanaiba mitahani ya darasa la saba, form four, six na hata ya chuo kikuu kuna watu wanapeta na kupata degree fake...kuna ushahidi university exams huvuja SUA, UD, MU, IFM, MUHAS huenda ni sababu ya kukutana na graduates wa ajabu sana siku hizi
 
kigarama jiepushe na huyu jamaa anayejiita shy, usijaribu wala usilogwe ukampa contacts zako! Atakuingiza mkenge wa ajabu sana. Kama unaweza kuwa na digital camera ukaipiga picha mwenyewe hiyo pepa ukurasa wa kwanza fanya hivyo umtumie invisible. Kama hilo haliwezekani basi njia nyingine utakayoweza, lakini nasisitiza sio huyu shy atakutia matatani, anajulikana kwa hilo!

mimi na wewe nani ni shushushu ?? Au nitaje jina lako na tuhuma zako humu ? Mbona unasema vitu ambavyo huna uhakika navyo ?
 
mimi na wewe nani ni shushushu ?? Au nitaje jina lako na tuhuma zako humu ? Mbona unasema vitu ambavyo huna uhakika navyo ?

Hebu anza kutaja moja baada ya nyingine. Anza na jina halafu endelea.
 
Back
Top Bottom