GS,
Tatizo ni kuwa tuna sehemu kubwa kati yetu ambao tunang'ang'ania ushabiki na kuamini kuwa Chadema ndicho chama mbadala. Labda ni ule mvuto wa Dr. Slaa, Chacha Wangwe, Zitto na Kitila. Lakini, hatuwezi kuendelea kuburuzwa kama enzi zile za kuwa Chipukizi wa CCM ambazo tulivutiwa na kunogewa na kusahau kuwa wadadisi na kuhoji mambo.
Humu ndani ya JF, kuna ngome kubwa sana inayoilinda Chadema, wala sitashangaa kuwa sehemu kubwa ya wana JF ni washabiki kama si wanachama wa Chadema. Sasa ukiandika kuwakosoa Chadema, fukuto litakalokufuata ni kubwa la kubezana na wala si kujenga hoja au kujibu hoja.
Mambo ya ubinafsi na kushambulia nafsi na si kuchambua hoja huanza, na ndio maana sehemu kubwa ya majadiliano hapa yamegeuka si kuchambua hoja na kujenga hoja za kukubaliana au kupingana bali ni kudai Mwanakijiji kapotoka au kaanza ku-dilute the message kisa kaongea dhidi ya Chadema.
Kama umeona, Shalom kanirukia na kudai eti nafuata nyayo za Mwanakijiji, na siku nikionyesha uhuru wa mawazo atatoa zaka! EBO!
Watu wameichoka CCM, lakini hawajui kupanga hoja ziuzike kwa kila roho Tanzania ili CCM ianguke. Ukitoa ushauri kwa mtazamo mwingine, unitwa msaliti au hujui unachokisema. Lakini kama nilivyomwwambia Dr. Slaa kwenye ile mada yangu ya Udhaifu wa Operesheni Sangara, ni kuwa huu ni mwaka karibu 20 tangu vuguvugu la Chadema na Upinzani kuanza kudai ni lazima CCM iondoke na kuondolewa, lakini kila siku zinavyozidi kusonga mbele, unaona CCM inazidi kushika hatamu pamoja na migongano waliyonayo ndani mwao.
Najiuliza kama Watanzania wameichoka CCM kama tunavyodhania, iweje ile kasi liyofanywa na TAA na TANU kumn'goa mkoloni ilifanikiwa kwa haraka, lakini vyama vya upinzani vinashindwa kuiangusha CCM? Je tuendelee na majaribio kuamini TLP, Chadema, CUF, NCCR, DP na hata sasa kukimbilia mgombea huru ndiyo suluhisho mpaka lini kama si kwa vyama hivi kujipima na kuanza kujiuza kwa kutuambia Itikadi zao ni zipi ili tuwe na uchaguzi basi wa kuamua tumtakaye?
Hatuwezi kujenga mfumo bora wenye msingi mzuri wa kisiasa bila kuwa na utambulisho wa kiitikadi ambao utatoa tofauti za kichama na kuwapa Watanzania uwezo kuchagua itikadi wanayopenda, sawa na dini zilivyo.
Hivyo tunaacha kujenga hoja, tunaanza shambuliana kisa hatutaki kusikia kukosolewa na hivyo kuwaacha CCM wakiendelea kukenua meno na kutamba ushindi mwingine ile Jumatatu bada ya uchaguzi mkuu.