mkalamo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 324
- 347
.Wahoji ushawishi wao ulipoishia
.Wasifu Uamuzi wa serikali kutoyaingilia
Na James Mtokambali
Zikiwa zimepita siku 11 tokea Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,Freeman Mbowe atangaze maandamano yaliyohitimishwa leo, mwitikio wake umewasikitisha wananchi wengi na kuhoji chama hicho kinapoelekea tofauti na nguvu iliyokuwa nayo miaka 10 iliyopita
Wakizungumza katika maeneo tofauti yalipopita maandamano hayo baadhi ya wakazi wa jiji la Dar esSalaam, walieleza kuwa mwitikio mdogo wa wananchi si kiashiria kizuri cha maendeleo ya Chadema katika kuwashawishi wananchi kama walivyokuwa zamani
Mustapha Morie Mfanyabiashara wa Matunda katika soko la Buguruni, alieeleza kuwa hakutarajia mwitikio mdogo wa wananchi katika maandamano hayo yaliyoongozwa na viongozi wa kitaifa wa Chadema
Mimi nilijua baada ya serikali kuruhusu maandamano wananchi wengi wangejitokeza kwa kuwa miaka kadhaa nyuma chama hiki kilipoitisha maandamano licha ya kuzuiwa kwa nyakati tofauti lakini uungwaji mkono ulikuwa mkubwa kuliko hivi sasa”alisema Morie.
Dereva wa boda boda Mjulusi Mganza aliyejitambulisha kuwa anatokea kituo cha Buguruni Malapa, alisema kilichomsukuma kushiriki na kubeba bendera ya chama hicho katika maandamano hayo ni malipo na mafuta aliyopatiwa kwa makubaliano ya kuishia katika kituo cha Manzese
Aliongeza kuwa katika hali ya kawaida usafiri wa mara moja wa kutoka Buguruni Malapa kwenda Manzese haifiki shilingi 14,000 na kutaja kiasi hicho ndicho alichopokea kwa sharti la kuingiza pikipiki yake kwenye maandamano.
“Nilidhani tutakuwa wengi katika hili mimi ninaishia Manzese Darajani hii bendera nasepa nayo hata wenzangu nadhani nao wataishia hapo hapo kwa kuwa kijiweni kwetu mkataba ulitutaka tuishie Manzese”alisema Mganza
Mariam Stephano Mkazi wa Kimara Baruti alisema kilichomvutia kushiriki maandamano hayo ni ngoma zilizokuwa zikipigwa maarufu kigoma cha Uruguay.
“Wala sikuwa na taarifa nikaona watu wanapita na ngoma akiwemo shoga yangu Mwajey namuuliza ananiambia twende twende name nikaunga baadae ndiyo tukakutana na Lissu pamoja na Mbowe lakini sijafika mpaka mwisho”alisema
Mwandishi wa habari hizi aliyekuwa katika msafara wa maandamano hayo alishuhudia makundi ya watu wachache wachache wakiungana kabla ya kuongezeka walipofika katika eneo la Magomeni Usalama
Juma Mkilai aliyejitambulisha kuwa ni dalali wa ndizi katika soko la Mabibo, alisema kinachomskitisha ni kuona mvuto wa viongozi wa kitaifa wa Chadema ukishuka kila mwaka kiasi cha kushindwa kukonga nyoyo za watu kama walivyokuwa zamani
Alisema miaka 12 iliyopita akiwa nyumbani kwao Morogoro, alishuhudia maandamano makubwa ya chama hicho katika mji wa Morogoro licha ya kuwa na upinzani kutoka jeshi la Polisi wakati huo.
“Haya si mafanikio kwa ninavyoijua Chadema, kitendo cha Serikali kuruhusu wafanye maandamano kimewashusha sana na kuonyesha uwezo wao wa kukubalika ni mdogo, nimenafurahia jambo hili kuliko wangezuiwa kwa kuwa wangekuja na sababu nyingine ya kudai maandamano”alisema Mkilai