Rev Kishoka said:
TUache mambo ya kulazimishana hapa. Ukweli ni kuwa Vyama vya Siasa Tanzania havina mwelekeo, sera imara wala Itikadi zinazoeleweka
.
Reverand hili hata hao ccj ambao wanasema wao ni mbadala bado hawajaweza kuliweka wazi,hata hivyo tujifunze kutoka kwa wenzetu ie labor party na conservative huko UK ambao wamekuja pamoja regardless of the tremendous difference,all for the National interest....For the people,na hata US,kuna voting blocks kutoka mrengo wa kati kulia,na kati kushoto ambao huwa wanapiga kura either Republican ama democrats depending on sera za anayetaka kuingia madarakani kwamba watalifanyia nini taifa na wananchi wake especially kwenye yale wanayokabiliana nayo ie uchumi, terrorism,job creations nk.na wasipofanya huwa wako held accountable kwa kutokuchaguliwa tena,na si kama Tanzania ambapo mtu atakuja kusema uongo wa wazi ie maisha bora "Kwa kila mtanzania" wakati ni uongo mtupu halafu bado wanasahau....Sasa tunakabiliwa na ufisadi na wananchi wanaelewa kuwamaisha bora hayawezi kuja kama ufisadi ukiendelea kuwepo kwa kasi hii....
Ni muhimu tukajikita kwenye reality,shida tumeona si kufanya yale yaliyomo kwenye makaratasi,shida ni watendaji,uzuri wa sera na itikadi ni utekelezaji wake na si makaratasi,tumeweza kuona wazi ccm wenyewe wameshindwa kuekeleza sera zao za kwenye makaratasi,umeshasema mwenyewe kuwa unaweza kufanya tofauti na ulichoandika kama wanavyofanya ccm,preac this and do fifferenttly...cha muhimu ni uthubutu wa mabadiliko ndiyo haswa nguzo kuu ya kuelekea kwenye mabadiliko ya kweli na ya muda mrefu na tija kwa Taifa,la sivyo ni sawa na kucheza "gombania goli" ambapo kufunga upande wowote ni halali madhali unapiga bao,basi unaweza hata kujipiga bao wewe mwenyewe,naona ndiko tunaelekea sasa....
TUanze na CCM, Katiba inasema CCM ni chama cha Kijamaa na kinafuata siasa za Ujamaa. Lakini hata baada ya mabadiliko ya kinafsi ya Watawala wakuu wa CCM kuwa Mabepari na CCM na Serikali yake kuukumbatia Ubepari, bado kin adai chenyewe ni chama cha kijamaa!
Hiyo ndiyo haswa definition ya ccj kwasababu wao wamesema wanayo hiyo "combination" ya ubepari na ujamaa na hata kusema kuwa ujamaa una misingi ya ideologies za mrengo wa far right.
Sasa ukija kwa wengine, hakuna mwenye msimamo kamili wa kusema "sisi ni mabepari" "sisi ni wajamaa" "sisi ni wakomunisti" "sisi ni maliberali" "sisi ni wahafidhina-conservative" kwa kuwa Tanzania na siasa zake bado hazijaweza kujitambulisha na kueleweka kuwa siasa zipi ni za mrengo wa kushoto na ni kushoto ipi, mrengo wa kati kati ya namna gani na mrengo wa kulia, kulia ya mbali au ya karibu.
Kwenye dunia ya sasa vyama vinategemea wapiga kura kutoka kwenye ideologies na misimamo ya tofauti,kwa hiyo ni rahisi kukuta chama kina behave kama ni far right kwenye baadhi ya maamuzi na wakati mwingine center etc,mfano kuendelea kwa Obama kwenye vita ya Afganistan ni msimamo mzuri kwa wale wanaodai ni far right ambo walimpa Obama kura kutokana muendelezo wa sera hiyo,hata hivyo hakuwatupa wale wa far left na hata center left kwani pia walifurahishwa na yeye kufunga guatanamo nk licha ya kwamba vita hakujitoa Afghanistan,hata hivyo aliweka misingi ya kufanya hivyo huko Iraki,unaweza kuona ni tafauti ambazo hata hivyo zote zina lengo moja yaani maslahi ya Taifa la marekani na wananchi wake....Issues ni nyingi zitakazoweza kuchangia namna wananchi watakavyochagua viongozi wao na mara nyingi iantegemea na Taifa linakabiliwa na mambo gani,hata US pia kuna mambo kama abortion,issue ambayo inawagawanya wamarekani vilivyo,lakini shangaaa mtu asiye aimini in abortion anampigia kura rais asiye na msimamo mkali kuhusu hilo,mwenye ku beleive in freedom to choose ama kama maisha ya mzazi yamo hatarini....cha msingi ni sababu na nia ya kuing'oa ccm...Kama Taifa,tuangalie kwanza ni nini tunataka,then we build on it,huwezi tu kukaa na kutayarisha sera na kudhani it just magically works....Wananchi hivi sasa wanakerwa na ufisadi,hilo ndo la kwanza,sera za ccm haziruhusu ufisadi,neither would any parties policies initiate ufisadi,ufisadi unafanyika...Sasa wananchi wanataka viongozi waaminifu,waadilfu wenye nia njema na Taifa....Wananchi wapewe wanachokitaka na wasilishwe mambo ya kwenye makaratasi...
Ni kweli lazima chama kiwe na msimamo ambao ndiyo utakuwa na msingi wa base ya wapiga kura,kwa mfano republicans base yao ni far right where as democrats ni far left,hao hawawezi ku cross over,lakini always kuna moderates ambao wao huwa ndiyo mara nyingi wanaamua uchaguzi ama ushindi uelekee wapi base on sera za wanaogombea...Siasa zimebadilika Rev na ni lazima tubadilike accordingly.
Pasipokuwa na Chama chochote kutambulika Itikadi yake na ikaeleweka, ni vigumu tuamini kuwa eti Vyama vikiungana, kutakuwa na mafanikio hata kama lengo ni kuing'oa CCM.
Wanadai topic si kuungana bali "kuhamia" Hata hivyo hayo mambo ya kuwa na "itikadi na ikaeleweka" hayazidi nia ya wenye nia kukaa chini na sababu za kufanya hivyo kama zipo...Ikiwa sababu ni pamoja na kuweka mikakati kwa malengo ya kulinufaisha Taifa na vizazi vijavyo,the hakutaharibika jambo...tunapozungumzia "mafanikio" tujiulize in what context do we hold the term mafanikio....?Tuangalie kwa mapana zaidi...Kwamba malengo ya mafanikio yetu yaelekezwe wapi....?Tukielekeza kwenye maslahi ya Taifa certainly hakuna kitakachoharibika.
Leo hii muungano wa CUF na Chadema unafanikiwa, wanashika madaraka ni siasa za nani tutazifuata? Kama tayari tushadai CUF ni wadini na Chadema ni wachagga, je tutaongozwa kichagga au kidini? je kama mmoja ni mkomunisti na mwingine ni bepari, je tutafuata la nani na kumuamini nani? Je hatuoni kuwa udhaifu huu ni rahisi kwa CCM ambao japo kimatendo si wajamaa, lakini ni rahisi kwa wao kudai wao ni wajamaa na kupokelewa na wananchi?
Hatuwezi kusonga mbele kama tuna migogoro ya kutugawanya,haijalishi kidini ama kikabila....certainly hilo haliwezekani,haiwezekani kabisa tukaendelea kama misngi ya mmamuzi yetu imejikita kwenye hayo ya udini na ukabila....kama hatuna yanayotuunganisha kama taifa,na tukawa tunaamini kabisa kuwa nothing comes above them.....basi haijalishi,tutakuwa mbayu wayu kikweli kweli kwa kuyumbishwa hovyo hovyo tu,hatuwezi kuongozwa kwa hear says,half backed stories and innuendos na kutegemea better outcomes,kama ni kweli vyama hivyo vinaongozwa na hayo mnayoyasema basi sioni ni kwanini issue hizo hazitatuliwi kama ni kweli tuna agenda moja ya maslahi ya taifa....
Taifa la marekani ni watu wenye imani tofauti za kisiasa nk,lakini kuna national interest issue ambazo zinalileta taifa pamoja na kuiweka identity yao intact no matter what,na ndio maana kuna maendeleo tangible na si bla blah za kisiasa....sisi tumebakia kutumia madhaifu yetu sisi wenyewe dhidi yetu sisi wenyewe na dhidi ya vizazi vijavyo,tumegeuka kuwa adui yetu sisi wenyewe.....Ni kama mtoto anayecheza na wembe,vyote wembe na utoto ni adui wa mtoto huyo....We're our own enemies...Na ushauri ambao tumeshawapa vyama hivyo na bado tutaendelea kuwapa;kwamba wasiyapuuzie malalamiko ya wananchi kama kweli ni valid,basi shurti yafanyiwe kazi na wananchi waonyeshwe evidence of whatever is done to correct it,hata kama ni kwa nia njema,kutokana na uelewa wa wananchi,there is always something that can be done,its politics...However kama siyo valid,basi ni ya kuyapuuziwa.
Hivyo ni lazima vyama vindelee kujijenga kwa ubinafsi na kuongeza nguvu za kuuza si sera za kuking'oa CCM pekee, bali kuwahubiria Watanzania Itikadi wao ili Watanzania wawe waumini wa Itikadi kwa kujifananisha na kuelewa Itikadi za Chama kuendana na maisha yao na si adha ya kushindwa kuivumilia CCM.
Hatuna hiyo luxury,honestly rev hiyo ni ya kufikirika kwa mtanzania wa kawaida,wananchi walio wengi hawaitaki ccm sema hawajui wafanye nini na pengine labda hawajui waende wapi,vyama vya upinzani vinaweza kulitumia hilo kama somo la kujifunza,hao walioenda ccj,na sizungumzii the so called "mamluki" bali nazungumzia wale valid ambao hawakujiunga na vyama vingine vya upinzani hadi ccj ilipojitangaza....na pengine wale wana ccm wenye kutaka na wanaotaka kumeguka ila pa kumegukia pakawa ama ni shida...Wapinzani waangalie what went wrong na ama what is wrong,as in kwanini wananchi hao hawakujiunga na vyma vyao na ama hawajiungi nao, ili kama kuna mabadiliko na marekebisho kwa upande wa upinzani basi wayafanye....Na validity ya mabadiliko hayo ikawa established,yani kama mabadiliko hayo hayataathiri well being ya vyama hivyo kiujumla,basi yawepo.....Pengine inaweza kuwa sababu ama kichocheo kwa wale waloshauriwa kuhamia kwenye vyama flani flani kusita kufanya hivyo...?Again kama maslahi ya Taifa ndiyo mbele basi sioni kwanini watu wasikae chini na mazungumzo kufanyika?
Pia ukweli ni kwamba lazima kutakuwa na tofauti za kuwagawa baadhi ya wananchi ambao wanapenda wenyewe ubaguzi ubaguzi...Ama kugawanyika kama ilivyo asili ya watu flani flani....Kuna ma anti this and anti that....Siasa si dini....Kama chama cha republican,voting block yao kubwa ni pamoja na wale tea partiers ambapo kuna wale birthers ambao hawaamini kama Obama kazaliwa marekani,wengine wakiamini ni muislam nk....ni wabaguzi wakubwa,lakini hiyo haina maana kwamba wale ambao si wabaguzi watasema kuwa chama cha republican sasa ni cha wabaguzi na kwa hivyo siwezi kumpigia kura mgombea wake,hilo halipo...Tukifikiria kwa mapana zaidi tutalikwamua Taifa,kuna wale waumini wa kusema hawa ama wale hawafai kuongoza nk,hayo ni ya kuturudisha nyuma,tukiamini kuwa tutaweza kuleta mabadiliko na si kujikata kata wenyewe kama vile tunaongozwa na suicidal mind set.....Ama pia labda sijaelewa ulimaanisha nini kusema vyama vijiendeshe kibinafsi binafsi kwanza?naona kama tumepoteza malengo ama tunajilazimisha kupoteza malengo....?!Jamii tuliyo nayo ya watanzania kwa ukweli reverand Kishoka, haina hiyo luxury ya kusoma sera na itikadi kwenye makaratasi na kusahau kuiondoa ccm madarakani,nani asome na wakati hajui atakula wapi?wananchi walio wengi hawafanyi hivyo,wananchi walio wengi hawazungumzi haya tunayoyazungumza humu....Hawana hiyo luxury......Maisha ni ya taabu na wanataka something other than ccm,kinachohitajika ni kukaa pamoja for the sake of the people...Ni muhimu kutafuta njia rahisi ya kuwapatia wananchi haya tunayoazungumza humu kwa lengo la kuwafungua macho kuwa ni mwelekeo gani unawafaa...Hiyo luxury ya kukijenga chama kiipite ccm kwa sera ni ndoto ya alinacha,certainly umeshakiri mwenyewe kuwa ccm wenyewe wameshindwa kuyafanya yale yaliyomo kwenye makaratasi ie ujamaa na wao kupractice ubepari kwa hivyo tatizo si sera na itikadi flani,haya unayoyataka yameshindikana na ccm licha ya kwamba wako madarakani toka uhuru.....Halafu Since when kuiondoa ccm kukawa si priority tena the first one?
Lets not get our eye off the ball.