Tukuelewe vipi? Mbona unauma na kupuliza? Hilo suala la Vatican limehusishwa kujiunga na OIC na nani? Unaishi wapi Tanzania ambako husikii/huoni jinsi udini ulivyoishaota mizizi? Hilo la kodi za waislamu kuwalipia watumishi wa ubalozi wao Vatican linahusiana nini na topic hii?
Unataka tuzungumzie competence ya hao wajumbe. Tutazungumzia based on what? Ushiriki wao katika kuandika Katiba nyingine? Si nyinyi ambao mnadai kuwa Justice si itendeke tu bali ni lazima ionekane kutendeka. Unadhani tume kama hii, hata ikifanya mchakato diligently, kwa uhaki kabisa halafu wakaja na hoja kuwa wananchi wanataka Mahakama ya Kadhi itambulike kikatiba watakuwa na credibility yeyote?
Mahakama ya Kadhi ilikuwepo wakati wa ukoloni kwa sababu tu mhimili mkubwa wa taifa hili alikuwa Malkia wa Uingereza, Mkuu wa Church of England. Kwa wao kilikuwa kitendo cha appeasement ambacho walijua hakina uwezo wa kuathiri utawala wao. Vile vile nchini Kenya, ambako the great majority ni wakristu. Kwa wao, hakuna uwezekano wa chombo hicho kuonekana kama Trojan Horse ya Islamization ya taifa lao.
Sisi ni tofauti. Hasa bara, ambako tumeoleana, tumezaa pamoja na tunaishi katika delicate balance ambapo tukifanya mchezo mmoja wetu anaweza ku-tip the scales upande wake. Tofauti na wakati wa ukoloni au kwa jirani zetu, ni wachache sana kwetu ambao hawana ndugu, rafiki au jirani asie wa dini nyingine. Katika mazingira kama hayo secularism ni imperative. Ndio maana tunasema Mahakama kama hii iundwe nje ya mfumo wa serikali. Mahakama ya kitaifa ni lazima itoe haki sawa kwa raia yeyote bila kujali dini, rangi au jinsia yake. Upendeleo uolewe kwa wale tu ambao sisi sote kama taifa tunakubaliana kuwa wanahitaji kulindwa, k.m wenye ulemavu na watoto.
Badala ya kumkebei Mtei, inabidi tumshukuru kwa kuzungumzia huyo tembo aliye katika sebule yetu. Si kwenye udini tu bali katika uwakilishi wa pande mbili za Muungano. Ni kujidanganya kuwa Muungano wetu uko imara wakati wenzetu wamegeuza Bunge lao kuwa sehemu la kuelekeza mapigo dhidi ya wale wanaowaita machogo. Tatizo si Jussa kuwaita watanzania bara wageni bali ni kwa kiasi gani hoja yake ilikubalika na kuungwa mkono na wenzie bila kujali itikadi zao!
Hap tunazungumzi tume itakayotuongoza katika kupata sheria mama ya taifa letu, sio viranja au wajumbe wa bodi za mashirika. Ni lazima tuzungumzie kwa undani yale yote ambayo tunadhani yanaweza kutufanya tukose imani na uongozi wao, udini na mustakabali wa Muungano vikiwemo.
Amandla.......