nimekusikia mkuu. awali ya yote, na-declare position yangu kwenye hii debate..... mimi ni mkristo.
the irony behind my earlier post ni kwamba kuna mambo ambayo kwenye mchakato huu wa katiba mpya kama hatutayapekenyua to the finest details (inside-out, upside-down, back n forth, black n white), kuna uwezekano wa kupata katiba yenye mizizi ya kinafiki. so, let's put everything on the table now and chew it to the last bit.
uchokonozi aliouanzisha mtei usinge-attract a heated and intense debate like this kama uchokonozi huu ungekuwa umeanzishwa na a nobody like "m-mbabe". that's why nimependezewa sana kwamba ni mtei (or hata kama ingekuwa equivalent dignitaries like mkapa, lipumba, mwinyi, etc) ndiye aliyechokoza mada hii.
otherwise, arguments zako katika huu mjadala kuhusu position ya uislam ni more than valid.
This is not a heated debate ila ni kuonyesha jinsi Udini unavyoweza kutusambaratisha. Hakuna mtu hapa anakubaliana na mwenzake na wala hakuna mtu hapa anakubali kutokubaliana, isipokuwa Kujitenga na WAO kuwa wao against SISI.. Hii ndio hatari ya maneno baadhi ya maneno.
Mkuu wangu maana ya kupiga vita Ubaguzi wa aina yoyote imeelezwa vizuri sana ndani ya katiba iwe wanawake, Ukabila au Udini.. Nitatoa mfano japokuwa ni mbaya sana lakini yachukulieni kama maneno ya mwendawazimu kwa muda..
Nikisema:- "Wanawake hawafai kuongoza nchi maana ni wazembe na sehemu yao ni jikoni..."
Maneno haya yanaweza kuwa na ukweli kwa baadhi ya wanaume na yakazua heated debate kuhusiana na maneno haya lakini japokuwa yanaonekana kubeba ukweli fulani kwa baadhi ya watu lakini ni maneno ya mazito ya uchonganisha, kubeza na sio right kuyasema hata kama unafikiria ni haki yako kusema ukweli unaofikiria wewe. katiba inakataza na ndivyo inatakiwa hata ktk maswala ya Udini na Ukabila.
Unapopinga Udini ni lazima uwe na kigezo cha kuonyesha UPENDELEO kwa waislaam/wakristu na ndivyo mzee wetu Mtei alitaka kuonyesha lakini alishindwa kuonyesha jinsi gani wajumbe wa Zanzibar wangeweza kuchaguliwa ili huo uuwiano uwepo. Na kisha hii habari ya UUWIANO ni kuni kavu au mafuta ktk kuchochea Udini ama Ukabila uliopo. Toka tumefanya Uuwiano ktk maswala ya Muungano ndivyo muungano wetu umekuwa na kero zaidi tofauti na nchi nyinginezo ambazo zimejenga sheria kuhakikisha kila mmoja wao anayo haki sawa ya kushiriki ama kupewa huduma na sio kutazama uuwiano baina yao.
Hata kuwezeshwa kwa watu weusi Marekani haikulenga ati watu weusi wapewe uuwiano sawa na weupe au wazungu isipokuwa haki sawa ya kushiriki bila kubaguliwa. Ukitazama affirmative action ya Marekani imewezeshwa kwa sababu shule zao nyingi ni Private na zinahitaji wanafunzi walipe karo (fedha), weusi wengi sii tu walitengwa ila pia kutokana na umaskini wao walishindwa kumudu karo za shule hizo hivyo affirmative action ililenga zaidi kuwawezesha watoto wa maskini kupata usajili wa shule nzuri na imetokea tu kwamba maskini wengi ni weusi japokuwa wapo wazungu ambao wanafaidika pia na sheria hiyo kuwezeshwa kuingia shule nzuri..
Kwa hiyo kinachotazamwa ni malengo, hapa tunajadili mzee Mtei pasipo kuwa na majawabu isipokuwa kulaani kitendo cha JK kuchagua wajumbe wa Zanzibar ambayo amepewa na Wazanzibar kuwakilisha nci ya Zanzibar kwa maslahi ya Wazanzibar na leo kuwa ati ni maslahi ya waislaam hali zanzibar yenyewe ina asilimia 99 waislaam. Inaingia akilini hii jamani?
Huu ni upumbavu mkubwa sana tunaufanya..Maana hakuna kati yetu anaweza kumtaja hata mkristu mmoja wa Zanzibar anayetakiwa kuwepo ktk wajumbe hao mbali kabisa na kwamba hawa wajumbe wamechaguliwa kutetea maslahi ya Zanzibar, sisi wabara tunaumia vichwa kwa sababu gani? Mbona wao hawatazami wajumbe wa Bara na kuanza kusema kuna wakristu wengi, kuliko waislaam hali bara wakristu na waislaam ni nusu kwa nusu!. Hakuna Mkerewe au Mgogo au wachagga wengi na kadhalika...inawahusu nini wajumbe wa Zanzibar kuzungumzia uchaguzi wa wetu ikiwa ni kwa maslahi ya bara?..
Halafu jamani hivi kweli mnapenda kuona Tanzania ambayo kesho itakuwa ikifuata Uuwiano ktk teuzi zake wakati watu hawa hawachaguliwi kusimamia maslahi ya kundi lao. Wewe unajenga nyumba yako unataka kusema kweli lazima mchora ramani na mjenzi awe Muislaam au Mkristu kwa sababu watakaoishi ndani ya nyumba hiyo ni waislaam au wakristu? Heee jamani tuache unafiki huu ni mbaya na hatari sana kwa Utaifa wetu...
Mwisho nasema hvi tumeshindwa kuijenga nchi yetu kwa katiba iliyopo ambayo ni KAVU inayokata kama kisu, tutaweza vipi kulijenga Taifa na katiba mpya ambayo itakuwa legelege. katiba itakayo ingiliwa na vyombo vya dini, makabila na jinsia wakivutia upande wao ilihali watu wote tunaitaka haki sawa?.. Kwa watu gani basi SISI watanzania maskini wanafiki wenye uchu na greed ya Utajiri sii ndio tutajimaliza kabisa!.