Mkuu labda nikujibu tena na tena. Nachosema Hospital za Bugando KCMC na nyinginezo zijiendeshe zenyewe kama private Hospital na wananchi wanaotibiwa hapo ndio wapewe nafuu kwa kulipiwa kiwango fulani cha huduma zipatikanazo. Tunachopinga sisi ni serikali kuwa mbia na kanisa wakati katiba inapinga swala hilo. Sasa kama wameweza kurudisha shule na hospital zote za makanisa wameshindwa nini kurudisha shule za AghaKhan kama Tambaza?.. na iweje shule za waislaam na watu wengine waliojitolea kufungua shule na kutoa huduma kwa watu wote zisiwe na fungu la kupewa fedha isipokuwa zile za kanisa? Tazama shule za waislaam na Private nyinginezo zinapokea tu watoto waliofail mitihani na kuwapa nafasi ya kujiendeleza wakati za kikristu zinachukua walioshinda mitihani kwa ushirika na serikali kwa kutumia fedha za walipa kodi lakini zile nyingine kila mtu anajitegemea yeye mfuko wake..Huoni kasoro hapo halafu unasema ni Huruma?
Kila mara mnapenda sana kuepa ukweli, wewe huwezi kuishi nyumba ya kupanga ati kwa sababu unapewa huduma hiyo, utapenda ujenge chako na wewe uwe na sehemu yako. Unafikiri shule na hospital nyinginezo hawapendi kuziboresha hospital zao ili wapate kuhudumia watu wote kwa ufanisi bila kuwatenga kwa dini au makabila yao?.. Eeeh, nakuuliza wewe inakuwaje serikali bado inajenga shule na Hospital zake ambazo ziko chini ya kiwango halafu tunaambiwa ati walishindwa kuzihudumia ndio maana makanisa wakarudishiwa, sasa zile za waislam au za watu private serikali iliweza kuzihudumia au ndio wametengwa kiaina.
_ Namalizia kwa kusema muafaka wa MoU haufai, aidha shule na hospital zote nchini ziwe na mfumo mmoja na wapewe wote nafasi sawa za kifedha na kadhalika au kila shule na hospital isiyokuwa ya serikali ijiendeshe yenyewe (ktk ushindani) na serikali ijikite ktk kuwasadia wananchi wanaokwenda kusoma au kutibiwa huko.
Hii ni story ya kweli at Mbagala Mission (La Sainte Union Sisters)
Kuna siku masheikh kadhaa waliendesha mhadhara karibu na hii hospitali maarufu sana mbagala
masheikh hawa walitukana sana ukristo na wakawatukana masisters wa ile hopsitali kuwa hawana lolote, ni wahuni tu, na ni wake wa mapadre! bila wao kujua kuwa hao masister wanajua kiswahili vizuri tu
Vipaza sauti vikaendela kutoa maneno yote mabaya! pamoja na kuwa eti wanapendelewa na serikali kwa mambo mengi..kama ulivyosema!
siku ya pili yake wagonjwa wengi wakaja kama kawaida yao
sister akaanza kuwauliza majina na dini zao
ukisema Asha na ni mwislamu anasema toka nje kwani waislamu wametutukana sana jana, siku hiyo ya alhamisi alifanya hivyo kwa waislamu wote waliokuja hopsitali na alisema hakutakuwa na huduma ya hospitali kwa waislamu!....wakastuka
wakristo waliokuwepo walikuwa wachache sana....labda asilimia 20 ya walioondoka!
wale akina mama waislamu wakaenda kuwaeleza waume zao (kumbuka ina hudumia sana akina mama na watoto) na mkutano mkubwa ukaitishwa wa kuwaomba msamaha masister..tangu kipindi kile mpaka wa leo hii hakuna tena mihadhara na huduma zinaendelea kama kawaida
Kwa hiyo mr. Mkandara unachokisema ni sahihi kwako ila kwa waislamu wa mbagala hawatakuelewa.
capital cost ya kujenga hospitali nani anaitoa?? je zinapata ruzuku ya serikali on time?
Nimekupa mfano tu.....hii hospitali tajwa hapo juu inaserve asilimi 80 ya waislamu ambao ndio wengi huku mbagala!
Njoo na hoja zako hapo juu umweleze mwanamke anayeumwa au mzazi anayeuguliwa na mtoto......uone utakavyotukanwa
Mwisho:
sikutegemea mtu kama wewe utatoa mawazo ya kijinga na kipumbavu kama haya ambayo hata zuzu Kikwete ameyakataa!! yaani unatoa wazo mpaka mwislamu mwenzako anakuona mjinga!! what a shame!
grow up!! nikiona unaendeleza ujinga huu na sumu hii, nitadeal na wewe nina hasira na wewe maana ni kingunge humu, unajua JF ilivyo na bado unaleta vi-element vya udini udini, tofauti yako
wewe Mtei na Jusssa ni nini??
usirudie