Mtei amefilisika kimawazo - Zitto

Mtei amefilisika kimawazo - Zitto

1. Hivi ni shule ngapi za wakristu na ngapi za waislamu zilitaifishwa? Tukizungumzia sekondari, mimi najua katika maeneo ya Dar es Salaam, kanisa lilikuwa na shule za sekondari zifuatazo:
a. St. Xavier ambayo ilitaifishwa ikaitwa Kibasila.
b. St.Joseph iliyogeuzwa na kuitwa Forodhani.
c. St. Andrews iliyotaifishwa na kuitwa Minaki.
d. St. Francis iliyotaifishwa na kuitwa Pugu.

Katika hizi ni Forodhani peke yake iliyorudishwa.

Waislamu mlikuwa na shule za sekondari zifuatazo:

a. Aga Khan Boys Secondary iliyotaifishwa na kuitwa Tambaza.
b. Aga Khan Girls Secondary iliyotaifishwa na kuitwa Zanaki.
c. Mzizima Secondary ambayo haikutaifishwa.
d. Kinondoni Muslim ambayo haikutaifishwa.

Ukienda Moshi, wakatoliki walikuwa na Weruweru na Ubwe. Katika hizi, ipi wamerudishiwa?

Katika hizo, ninavyojua, Zanaki amerudishiwa Aga Khan. Hapa ni nani kaonewa? Huyo aliyetaifishiwa shule 4 akarudishiwa moja au yule aliyetaifishiwa mbili akarudishiwa moja? Wewe unaesema wakristu walipendelewa, unaweza kunitajia shule ya sekondari ya kikristu ambayo haikuwa seminari ambayo haikutaifishwa?

Ukweli ni kuwa ukiangalia idadi ya shule, vyuo na hospitali zilizokuwa zikimilikiwa na kanisa ni chache ambazo wamerudishiwa.

2. Kwa vile inaelekea hii MoU imekuwa ni ishu sana kwenu basi hebu tuiweke tuone wapi mnakwazika. Hii hapa kama alivyoileta mwenzenu: https://www.jamiiforums.com/jamii-i...a-katoliki-na-taasisi-nyingine-za-kidini.html
Ukiangalia article XII inazungumzia kutaifishwa kwa shule, hospitali au chombo chochote kinachotoa huduma ya afya au/na elimu kinachomilikiwa na kanisa. Hii ilikuwa ndiyo sababu kubwa ya MoU hii, kuwalinda wale ambao waliishang'atwa na serikali wasing'atwe tena. Hayo hayo ambayo wakina Mkandara wanataka kurudia.

Article XIII ambayo imekuwa underlined inasema serikali ita-endeavour (ITAJITAHIDI) kuingiza suala la misaada kwa ajili ya institutions hizi za kanisa katika majadiliano yao na nchi zinazotufadhili haswa Ujerumani. Watajitahidi na si lazima.

Sasa nyie mnaosema kuwa MoU hii inataka serikali itoe ruzuku kwa kanisa katika utoaji wa huduma hizi, tuonyesheni article inayoelezea hivyo. Mnataja bilioni kumi bila kutuambia kwa uhakika imetoka wapi kwenye bajeti!

2. Naam, kweli shule za kikristu zitakuwa na mlengo wa kikristu kama vile ambavyo zilivyo za kiislamu. Lakini hakuna shule inayotambulika na serikali (isipokuwa zile zinazowatayarisha wahudumu wa baadae wa imani hizi) inayozuia muumini wa dini nyingine kujiunga nazo. Waislamu wengi walikataa kwenda kwenye shule za kikristu kwa sababu ya kuhofia kuwa watabadilishwa dini au uwezo mdogo wa kipesa. Pamoja na haya, ni wengi tu ambao wameelimishwa katika shule hizi bila kuathirika, rais wetu akiwa mmoja wao. Wakristu wengi hawapeleki watoto wao katika shule za kiislamu kwa wasiwasi wasi huo huo. Lakini nao kama shule hizo zina matokeo mazuri kama Feza, Al Muntazir n.k. hawachelei kuwaruhusu binti zao kuvaa hijab ili mradi wanapata elimu.

Kusingizia kuwa waislamu wanaathirika kutokana na shule hizo kurudishwa kwa wakristu ni uchimvi maana waislamu wamekuwa wakilega nyuma kielimu hata wakati karibu shule zote zilikuwa ni za serikali. Badala ya kutafuta visingizio kama hivi ( incl. kuibiwa mitihani), waislamu mnatakiwa kujiangalia wenyewe na kuhimizana kwenda shule.

Huko kubaguliwa mnakodai kunafanyika katika shule hizo za kikristu dhidi ya waislamu inabidi mtolee mifano. Au mnazungumzia seminari ambazo hata mkristu wa dhehebu lingine hapewi nafasi kwa sababu lengo ni kuelimisha watu watakaokuwa makasisi, mapadri n.k.?

3. Mnazungumzia hadithi za alinacha. Hata kama mlipewa ili kuwapooza juu ya MoU, ukweli unabaki kuwa MLIPEWA BURE. Itakuwa vyema kama mtatutolea mfano wa namna ambavyo hayo mabilioni serikali inayotoa kwa kanisa mnayoyazungumzia yamewafaidia vipi wa kristu kwa kuhudumia shule na hospitali wanazoelimishwa na kutibiwa peke yao. Tutajieni shule au hospitali moja inayopokea ruzuku hiyo ambayo inahudumia wakristu peke yao. Moja tu.

4. Waberoya amewapa mfano wa Mbagala Mission lakini hamtaki kumsikia. Au mnataka kutuambia kuwa katika maeneo yenye waislamu wengi hakuna shule au dispensari za kanisa? Hamna hata aibu!

5.Yale yale. Insinuations bila substantiation. Toa ushahidi wa shule au chuo kinachopewa ruzuku na serikali ambayo inatoa huduma zake kwa kupendelea waumini wa dini yake.

Amandla......
Mkuu swala la kutaifisha shule soteb tunajua wazi kwamba shule zilitaifishwa nyingi zilikuwa za kikristu na sababu yake ilikuwa kuondoa matabaka ambayo yaliathiri UMOJA wetu, hata ukienda Zimbabwe au South Afrika utaona waliowekeza zaidi ni wazungu na waliofaidika vile vile ni wazungu..Hivyo huwezi kuleta usawa katika nchi hizo kwa kutazama nani ataumia zaidi..

Tatizo linakuja ni kwamba kama kutaifisha mashule na Hospital ilikuwa kuondoa ubaguzi uliokuwepo toka mkoloni kwa nini leo tumeurudia tena kule na Udini umerudi?. tatizo lako unazungumzia kwa niaba ya makanisa wakati sisi tunahoji serikali sio wakristu ama Ukristu. Nakumbuka vizuri sana kwamba Lake socondary - Mwanza, Shaaban Robert, Mzizima - Dar, na kadhalika hizi hazikutaifishwa kwa sababu zilikuwa za watu binafsi kwa hiyo haikuwa kutaifisha hovyo tu bali zile zilizosababisha kutugawa. Kinondoni Sec na Seminary hazikutaifishwa kwa sababu zilitakiwa kuwa shule za DINI zikifundisha pia elimu dunia. Kwa nini tumebadilisha mfumo huu?.

Nitakupa hadithi moja ya kweli nayoikumbuka vizuri. baba mmoja katika kuendesha familia yake alimpeleka mwanaye wa kiume shule akamwacha wa kike kwa sababu alitegemea huyo ni mwanamke na mwisho wake ataolewa na hivyo kuwa ktk familia nyingine lakini wa kiume ataendele kulinda jina la familia hata akioa. Miaka imeenda mzee akamwandikishia mtoto wa kiume nyumba yao kama urithi, yule mtoto wa kike akamuuliza baba yake kulikoni umrithishe nyumba mtoto wa kiume..

Wakati akisubiri jibu, mtoto wa kiume akadakia na kusema "Dah! leo nimeelewa, kumbe dada yangu mwenyewe hupendi mafanikio yangu? mbona nyumba yenyewe tunaishi wote sijakubagua leo umefikia kuhoji hata kuandikishwa mimi jina langu?.."

Yule binti akasema "Kaka haihusiani kabisa na mapenzi yangu kwako, isipokuwa sielewi kwa nini baba hakunipeleka shule na sasa imefika hadi urithi anakupa wewe kwnai mimi sii mwanaye?"

Kaka mtu akasema "Aaah si unajua wewe utakuja olewa na kuondoka, lakini mimi kama mwanamme nitaendeleza mali za baba na kuilinda familia ndilo jukumu nililopewa na utamaduni wetu." Dada mtu akasema "Basi kama hofu yenu ndio hiyo bora uniowe wewe maanake navyojua mimi nikiolewa tutapewa mahari ya millioni 10 na ukioa wewe tutatozwa mahari ya millioni 10 nani anayeigharimu familia?"

Ubishi ukawa ubishi na nisemavyo sasa hivi yule kijana yuko Marekani, nyumba aliuza na sasa mzee wa watu analelewa na mtoto wa kike ambaye hakujaliwa kuolewa ila anafanya kazi nzuri tu Benki kuu na kamjengea baba yake nyumba nyingine anakoishi sasa hivi.

Habari hii ni kukuonyesha kwamba hakuna sababu ya kushinda hapa kati ya waislaam na wakristu, sisi sote ni ndugu na tunachohoji sisi ni serikali, serikali kuwa na Ubia na kanisa wakati katiba yetu inakataza kutokana na experience tuloipata enzi za mkoloni kufikia mwaka 1966. Haijalishi kabisa nini malengo ya kanisa wala wanafanya nini kwa sababu hata zile zisizo za kanisa zinalenga kuwaelimisha na kuwatibu watu wote bila kujali dini na makabila yao. Kwa nini uundwe muafaka kama huu pasipo kuvihusisha vyombo vyote?.. hili kosa jamani..Mbona sote tunatazama kwa makini uundwaji wa Katiba mpya tukitaka asasi zote za kijamii zihusishwe? kwa nini seikali isifanye jambo hili na asasi mojawapo tu ambayo itakuwa na malengo ya kulinufaisha Taifa zima?..
 
Fundi Mchundo,
Na kuhusu MoU nakuomba rudia kausome vizuri nje ya box... Halafu pia kuna kipande hiki kutoka site RomanCathoilic kinasema hivi:-

To strengthen their social services sector, the two Church bodies that is the Protestants under the Christian Council of Tanzania (CCT) and the Catholics under the Tanzania Episcopal Conference (TEC), in 1992 assisted by the German partner Churches negotiated a "Memorandum of Understanding" with the Tanzania government. In this memorandum the government recognized the important role played by the Churches in the social services sector of the country, pledged to help the Churches by sharing with them grants from foreign government and promised never to nationalize the church institutions again. The "Memorandum of Understanding" authorized the forming of the "Christian Social Services Commission"(CSSC). TEC and CCT are each represented by the General Secretary and four bishops. The Commission has two executive organs, the Christian Medical Board of Tanzania (CMBT) and the Christian Education Board of Tanzania (CEBT) for health and education respectively. This commission formulates common policies for the Education and medical Services of the Churches and negotiates with the Tanzania government in the name of the churches. The two executive organs run common programs. The churches together run more than 50% of the Medical Services and secondary schools in the country.

Sasa kama kipande hiki hakikutatizi sijui nikwambie nini zaidi...
 
Mkandara, mie huenda kiingereza kilinipita kando lakini nukuu hii "In this memorandum the government recognized the important role played by the Churches in the social services sector of the country, pledged to help the Churches by sharing with them grants from foreign government" hususan kwenye wino uliokolezwa na kupigiwa mstari unaeleza mgawanyo wa misaada inayotolewa na mahisani wa nje kwa makanisa au taasisi za kikristo. Haielezwi ni msaadsa kutoka serikali ya JMT. Kama uelewa wangu ni tenge, basi wanaoelewa kiingereza vizuri wafafanue.
 
Hivi huelewi kwamba mpango wa millenium goals kuhusu Elimu na Afya tunapewa mikopo mikubwa ya kuendesha shughuli hizo? Pengine jaribu kuelewa nini maana ya Grants na taratibu zake labda itakurahishia kuelewa.
 
Mkandara, ni busara kutojaribu kuchanganya watu. MDGs ina vipengele zaidi ya elimu na afya na misaada hiyo inatolewa kwa mataifa masikini bila kujali kama wakazi wake wengi wanafuata madhehebu ya kikristo au kiislamu, kibuda n.k. Tujaribu kukaa kwenye mada na tuelimishane vizuri kwa sababu wapo watu ambao hawajui MDGs ni nini na mchakato uliofanikisha azimio hilo katika Umoja wa Mataifa.
 
Fundi Mchundo,
Na kuhusu MoU nakuomba rudia kausome vizuri nje ya box... Halafu pia kuna kipande hiki kutoka site RomanCathoilic kinasema hivi:-

To strengthen their social services sector, the two Church bodies that is the Protestants under the Christian Council of Tanzania (CCT) and the Catholics under the Tanzania Episcopal Conference (TEC), in 1992 assisted by the German partner Churches negotiated a "Memorandum of Understanding" with the Tanzania government. In this memorandum the government recognized the important role played by the Churches in the social services sector of the country, pledged to help the Churches by sharing with them grants from foreign government and promised never to nationalize the church institutions again. The "Memorandum of Understanding" authorized the forming of the "Christian Social Services Commission"(CSSC). TEC and CCT are each represented by the General Secretary and four bishops. The Commission has two executive organs, the Christian Medical Board of Tanzania (CMBT) and the Christian Education Board of Tanzania (CEBT) for health and education respectively. This commission formulates common policies for the Education and medical Services of the Churches and negotiates with the Tanzania government in the name of the churches. The two executive organs run common programs. The churches together run more than 50% of the Medical Services and secondary schools in the country.

Sasa kama kipande hiki hakikutatizi sijui nikwambie nini zaidi...

Mkuu Mkandara. Nimekuwekea MoU yenyewe na inasema wazi kuwa serikali ita-endeavour kuziombea misaada taasisi za dini katika makubaliano na nchi wahisani hususan Ujerumani. Endeavour maana yake itajitahidi. Hakuna mahali kwenye hiyo MoU ambapo serikali inashurutishwa kusaidia taasisi za kikristu. Sasa kwa nini mnapenda kuandikia mate wakati wino upo?

Wakati mwingine msipende kutufanya wengine mazezeta. Mnajifanya si wadini lakini kama mnayoandika yanawaumbua. Kama si udini, mtakuwa na tatizo gani na serikali kuona umuhimu wa kushirikiana na taasisi ambazo zinaendesha zaidi ya asilimia 50 (quote yako) ya shule za sekondari na huduma za afya nchini? Hawa wanachangia zaidi ya serikali katika sekta hizo lakini mnataka serikali iwaache kivyakevyake tu kwa vile ni za kikristu? Pamoja na kwamba hamjatoa ushahidi wowote kuwa hizo taasisi zinatoa huduma hizo kwa kuwapendelea wakristu. Hivi unaamini kweli serikali inaweza kutimiza malengo ya MDGs bila kuzishirikisha taasisi hizi? Na grant ni ruzuku, si mkopo. Kupewa hizi taasisi hakumuongezei mzigo wa kulipa deni mtanzania wa kawaida. Badala yake kunamboroshea huduma ambazo anazihitaji sana. Utapingaje hili kama si mdini? Unatofauti gani na wale wanaopinga kuingia OIC kwa sababu tu ni ya waislamu? Pamoja na kwamba kama watasaidia kujenga dispensari zitawasaidia wakristu, wahindu, wenye imani za asilia n.k.?

Kweli hamuitakii mema nchi yetu na watu wake.

Amandlaa...........
 
ningependa kukujibu kwa kutumia post moja ya mzee mwanakijiji katika mjadala huu unaohusisha mambo ya mou kati ya serikali na kanisa, post ambayo nakubaliana nayo kwa kiasi kikubwa: Kitu cha kwanza fahamu kabisa kwamba lawama zetu zipo kwa serikali na si kwa kanisa, kama kanisa limeweza kuishawishi serikali ivunje katiba ya nchi juu ya kutokuwa na upendeleo wa taasisi moja dhidi ya nyingine katika "biashara" lawama zinaiangukia serikali.

Mzee mwanakijiji anasema hivi ifuatavyo:

nadhani mwanakijiji amekuwa objective na ameweka mambo mengi into perspective katika suala hili:

Mzee Mwanakiji alikosea kama nyinyi mnavyokosea.

Mwalimu alitaifisha shule kutoa fursa sawa kwa raia wa Tanzania kupata elimu bora bila kujali uwezo wao wa kifedha. Siamini kuwa alifanya hivi kwa sababu shule hizi zilikuwa zikibagua kidini kwa sababu ninawajua wenye dini tofauti wengi waliosoma katika shule hizo bila kujificha dini zao. Ukweli ambao tunajifanya kuusahau ni kuwa shule bora nyingi zilikuwa za misheni, wahindu na waislamu wa dhehebu la Shia na zilikuwa zikitoza ada ambazo mtanzania wa kawaida wa wakati ule asingeweza kumudu. Ndio maana pamoja na zoezi la kutaifisha, alifuta ada.

Baada ya zaidi ya miaka 30 ya kuendesha shule hizi (na hospitali) serikali ilitambua kuwa ni mzigo ambao haiwezi kuendelea kuubeba kama kweli inataka kutoa huduma inayoeleweka. Tulitoka kwenye wanafunzi kupewa vitabu, madaftari bure hadi kufika mahali ambapo shule za serikali ( incl. zile zilizotaifishwa) kuonekana si lolote si chochote. Tulitoka mahali ambapo walioenda praivet ni wale ambao walifeli kufikia mahali ambao wanaoenda shule za serikali ni wale ambao wazazi wao hawana chaguo. Mtu yeyote akiangalia hali ya majengo na huduma (vyoo, maabara n.k.) katika shule hizi atatambua ukweli huo. Serikali ilishindwa.

Kutokana na ukweli huu, serikali ikaona ni heri kumkaribisha mbia ambae ataweza kuwekeza katika shule hizi (na hospitali) ili kuzinusuru. Taasisi zenye uwezo huo zilikuwa ni zile ambazo hapo awali ndio zilikuwa zinamilki shule na hospitali hizo yaani taasisi za kidini. Taasisi za kikristu hazikuwa na tatizo na hili lakini walitaka garantii kwamba mara baaada ya wao kuziboresha serikali haitarudia kamchezo kake na kuzitaifisha tena. Kwa vile ilikuwa vigumu kuingia mkataba baina ya wabia hawa wawili, MoU ilikuwa ni njia pekee ya kuzihakikishia kuwa serikali haitazitaifisha tena shule na hospitali hizi na badala yake watazipa ushirikiano unaotakiwa. MoU ikasainiwa, baadhi ya shule na hospitali zikarejeshwa kwa taasisi hizo za kidini na wote tunaona matokeo yake.

Hayo matabaka mnayoyazungumzia yanatokana na uwezo wa kipesa. Leo hii moja ya shule inayotoza ada ya juu sana ni ya kiislamu ya Feza. Wakina Loyola, St.Joseph hawaoni ndani. Wale wenye uwezo zaidi wanapeleka watoto wao nje kufuata elimu bila kujali kuwepo kwa hizo shule zinaondeshwa na taasisi za kidini nchini. Hayo matabaka yangekuwepo hata kama shule hizo zisingetaifishwa. Badala yake yangekuwa makubwa zaidi kwa sababu wale wenye uwezo wangepeleka watoto wao nje ( na hivyo kuondoa ajira kwa watanzania, kutochangia uchumi kwa kununua mahitaji ya shule nchini n.k.) wakati wakina Fundi Mchundo tusingekuwa na alternative bali kuendelea kuangalia watoto wetu wakikalia matofali. Leo tuna uwezo wa kudunduliza na angalau kuwapeleka watoto wetu St. Marian, Al Muntazir au Feza. Cha msingi ni elimu bora na si hadithi hizo za alinacha.

Badala ya kusakama taasisi za dini, mngesakama serikali ambayo pamoja na kupunguziwa mzigo wa kuhudumia shule zote hizo bado inashindwa kutoa huduma stahili kwenye shule ilizobaki nazo. Kaangalie hali ya shule iliyokuwa ikiitwa Aga Khan Boys Sekondari ulie. Madirisha yamevunjika, shule haijapakwa rangi miaka kibao, chafu n.k. Inaisha kufikiria ingekuwa na hali gani kama serikali ingetakiwa kuendelea kuhudumia shule za Forodhani, Zanaki n.k.

Mzee Mwanakiji amekosea kwa kuingiza udini kwenye hili. Affirmative action haina maana kumilki shule zote. Huko Marekani ambako kuna Affirmative Action mbona shule za misheni bado zipo? Kwa nini hatujiulizi, kwa nini katika maeneo ambayo yana waumini wa dini zote mbili, na shule ni za serikali, waislamu bado wanakuwa nyuma kielimu? Mnataka kutuambia kuwa huko Kilwa, Lindi n.k. hakuna shule ndio maana wako nyuma kielimu? Tatizo ni kubwa kuliko mnavyotaka kutuambia. Affirmative Action haisaidii kama walengwa hawana mpango na elimu (kwa sababu mbalimbali). Marekani pamoja na upendeleo wa aina hiyo lakini walengwa ambao ni weusi na latino bado wamebaki nyuma ukilinganishwa na waasia waliokuja hivi karibuni. Na hata katika hao weusi na walatino, wanaobaki nyuma ni wavulana. Shule zipo lakini mtizamo wao ni kuwa elimu ni kutaka kuwaiga watu weupe. Hei uuze unga kulikokuwa sell out. Sasa kama baadhi ya waislamu wanaona kuwa elimu ni kuingia ukristu, hata ufanye affirmative action ya aina gani, hawatakuja.

Mzee Mwanakijiji amekosea. Hakuwa objective hata kidogo.

Amandla......
 
Mzee Mwanakiji alikosea kama nyinyi mnavyokosea.Mwalimu alitaifisha shule kutoa fursa sawa kwa raia wa Tanzania kupata elimu bora bila kujali uwezo wao wa kifedha. Siamini kuwa alifanya hivi kwa sababu shule hizi zilikuwa zikibagua kidini kwa sababu ninawajua wenye dini tofauti wengi waliosoma katika shule hizo bila kujificha dini zao. Ukweli ambao tunajifanya kuusahau ni kuwa shule bora nyingi zilikuwa za misheni, wahindu na waislamu wa dhehebu la Shia na zilikuwa zikitoza ada ambazo mtanzania wa kawaida wa wakati ule asingeweza kumudu. Ndio maana pamoja na zoezi la kutaifisha, alifuta ada.Baada ya zaidi ya miaka 30 ya kuendesha shule hizi (na hospitali) serikali ilitambua kuwa ni mzigo ambao haiwezi kuendelea kuubeba kama kweli inataka kutoa huduma inayoeleweka. Tulitoka kwenye wanafunzi kupewa vitabu, madaftari bure hadi kufika mahali ambapo shule za serikali ( incl. zile zilizotaifishwa) kuonekana si lolote si chochote. Tulitoka mahali ambapo walioenda praivet ni wale ambao walifeli kufikia mahali ambao wanaoenda shule za serikali ni wale ambao wazazi wao hawana chaguo. Mtu yeyote akiangalia hali ya majengo na huduma (vyoo, maabara n.k.) katika shule hizi atatambua ukweli huo. Serikali ilishindwa.Kutokana na ukweli huu, serikali ikaona ni heri kumkaribisha mbia ambae ataweza kuwekeza katika shule hizi (na hospitali) ili kuzinusuru. Taasisi zenye uwezo huo zilikuwa ni zile ambazo hapo awali ndio zilikuwa zinamilki shule na hospitali hizo yaani taasisi za kidini. Taasisi za kikristu hazikuwa na tatizo na hili lakini walitaka garantii kwamba mara baaada ya wao kuziboresha serikali haitarudia kamchezo kake na kuzitaifisha tena. Kwa vile ilikuwa vigumu kuingia mkataba baina ya wabia hawa wawili, MoU ilikuwa ni njia pekee ya kuzihakikishia kuwa serikali haitazitaifisha tena shule na hospitali hizi na badala yake watazipa ushirikiano unaotakiwa. MoU ikasainiwa, baadhi ya shule na hospitali zikarejeshwa kwa taasisi hizo za kidini na wote tunaona matokeo yake.Hayo matabaka mnayoyazungumzia yanatokana na uwezo wa kipesa. Leo hii moja ya shule inayotoza ada ya juu sana ni ya kiislamu ya Feza. Wakina Loyola, St.Joseph hawaoni ndani. Wale wenye uwezo zaidi wanapeleka watoto wao nje kufuata elimu bila kujali kuwepo kwa hizo shule zinaondeshwa na taasisi za kidini nchini. Hayo matabaka yangekuwepo hata kama shule hizo zisingetaifishwa. Badala yake yangekuwa makubwa zaidi kwa sababu wale wenye uwezo wangepeleka watoto wao nje ( na hivyo kuondoa ajira kwa watanzania, kutochangia uchumi kwa kununua mahitaji ya shule nchini n.k.) wakati wakina Fundi Mchundo tusingekuwa na alternative bali kuendelea kuangalia watoto wetu wakikalia matofali. Leo tuna uwezo wa kudunduliza na angalau kuwapeleka watoto wetu St. Marian, Al Muntazir au Feza. Cha msingi ni elimu bora na si hadithi hizo za alinacha.Badala ya kusakama taasisi za dini, mngesakama serikali ambayo pamoja na kupunguziwa mzigo wa kuhudumia shule zote hizo bado inashindwa kutoa huduma stahili kwenye shule ilizobaki nazo. Kaangalie hali ya shule iliyokuwa ikiitwa Aga Khan Boys Sekondari ulie. Madirisha yamevunjika, shule haijapakwa rangi miaka kibao, chafu n.k. Inaisha kufikiria ingekuwa na hali gani kama serikali ingetakiwa kuendelea kuhudumia shule za Forodhani, Zanaki n.k.Mzee Mwanakiji amekosea kwa kuingiza udini kwenye hili. Affirmative action haina maana kumilki shule zote. Huko Marekani ambako kuna Affirmative Action mbona shule za misheni bado zipo? Kwa nini hatujiulizi, kwa nini katika maeneo ambayo yana waumini wa dini zote mbili, na shule ni za serikali, waislamu bado wanakuwa nyuma kielimu? Mnataka kutuambia kuwa huko Kilwa, Lindi n.k. hakuna shule ndio maana wako nyuma kielimu? Tatizo ni kubwa kuliko mnavyotaka kutuambia. Affirmative Action haisaidii kama walengwa hawana mpango na elimu (kwa sababu mbalimbali). Marekani pamoja na upendeleo wa aina hiyo lakini walengwa ambao ni weusi na latino bado wamebaki nyuma ukilinganishwa na waasia waliokuja hivi karibuni. Na hata katika hao weusi na walatino, wanaobaki nyuma ni wavulana. Shule zipo lakini mtizamo wao ni kuwa elimu ni kutaka kuwaiga watu weupe. Hei uuze unga kulikokuwa sell out. Sasa kama baadhi ya waislamu wanaona kuwa elimu ni kuingia ukristu, hata ufanye affirmative action ya aina gani, hawatakuja.Mzee Mwanakijiji amekosea. Hakuwa objective hata kidogo.Amandla......
Wewe unazungumzia sababu ya Kifedha tu Wakati Fedha ilikuwa ni sababu mojawapo tu[hususan shule za wahindi], sababu nyingine ilikuwa ni Ubaguzi wa Kidini na wa Kirangi katika shule hizo. KWA MAANA SUALA LINGEKUWA NI UBAGUZI WA KIFEDHA, WATANZANIA WOTE YAANI WAISLAMU NA WAKIRISTO WALIKUWA WAMEPIGIKA KIFEDHA LAKINI SHULE ZA KIDINI BADO HAZIKUKOSA WANAFUNZI.Ila tofauti na wezao Wakiristo, Waislamu walikuwa kama Watoto wa kambo, kwa maana hawakuwa na Taasisi Imara na nyingi kulinganisha na wenzao Wakiristo ambao tokea Mkoloni Taasisi zao zilipata kila aina ya Usaidizi Kutoka Serikalini, na hivyo pamoja na umasikini waoWakiristo kupitia Taasisi za zao walikuwa much better kuliko Waislamu.NA TAMBUA KWAMBA KANISA LILITUMIA HUDUMA HIZI KAMA NJIA YA KUSAMBAZA IMANI/DINI YAO NA HUO ULIKUWA UGOMVI MKUBWA SANA BAINA YAKE NA WAZEE WA KIISLAMU AMBAO WENGI KWA SABABU HIZO WALIGOMA KUWAPELEKA WATOTO WAO KATIKA SHULE HIZO, HATA HIVYO WAPO WAZEE WALIOAMUA KUWA WABISHI NA KUAMUA KUWAPELEKA WATOTO WAO HIVYO HIVYO, WAKAVUMILIA CHRISTIAN TEACHINGS INDOCTRINATION, LAKINI AT THE END OF THE DAY WAKAPATA ELIMU YAO NA VYETI VYAO, NDIYO HAO BAADHI YA WAISLAMU WACHACHE TULIOKUWA NAO WALIOPITIA SHULE ZA KANISA ENZI HIZO. NA KITU KINGINE FAHAMU KWAMBA PALE FEDHA ILIPOTUMIKA KATIKA SHULE ZA WAHINDI, ILITUMIKA KAMA NJIA TU YA KWASIDELINE LOW CLASS AMBAO WENGI WALIKUWA NI WATANZANIA WEUSI ILI WAWEZE KUENDELEZA AJENDA YAO YA URACISM. Sababu zangu za kutaifishwa shule hizi inathibitishwa na Tamko la Serikali kupitia kwa Hotuba ya Raisi Jakaya Kikwete alipokuwa anawajibu Waislamu kwenye baraza la Iddi August 2011. Kikwete katika hotuba hiyo Anazungumzia Ubaguzi wa Kidini na Wa Kirangi na wala hajagusia Ubaguzi wa Kifedha, nadhani alifanya hivyo kwa kutambua kuwa FEDHA ILITUMIKA KAMA EXCUSE TU ILA SABABU BEHIND THAT ILIKUWA NI RACISM!. Kikwete alisema hivi nanukuu.
Shule za Taasisi za Kiislamu Mheshimiwa Mufti; Ndugu Zangu Waislamu na Watanzania Wenzangu; Nimesikia maelezo na maombi yenu kuhusu shule zilizokuwa zinamilikiwa na taasisi za Kiislamu zilizotaifishwa na Serikali baada ya Uhuru. Ni kweli kwamba mara baada ya Uhuru shule zote za msingi, sekondari na vyuo vilivyokuwa vinamilikiwa na mashirika ya dini na jumuiya za kijamii zilitaifishwa. Ni kweli pia chache kati ya hizo zilirejeshwa kwa wamiliki wa awali katika miaka ya 1990. Ni kweli vile vile, kwamba mashirika ya dini ikiwemo BAKWATA na jumuiya za kijamii zimekuwa zikiomba kurudishiwa shule hizo lakini Serikali haijayakubali maombi hayo. Mheshimiwa Mufti; Waheshimiwa Masheikh; Katika mkutano wangu wa tarehe 22 Julai, 2011 na Jukwaa la Wakristo suala hili lilijitokeza na nililitolea ufafanuzi ambao napenda nirudie kuueleza hapa leo. Baba wa Taifa na Rais wa Kwanza wa nchi yetu, Mwalimu Julius Nyerere aliamua kutaifisha shule zote za mashirika ya dini na jumuiya za kijamii hasa za Wahindi na Wazungu kwa lengo la kutoa fursa sawa ya kupata elimu kwa watoto wa dini zote, wasiokuwa na dini na wa rangi zote bila kubaguliwa. Kutokana na uamuzi ule hakuna mtoto aliyebaguliwa kupata elimu kwa sababu ya rangi yake au dini yake. Hata wale waliotoka kwenye jamii ambazo kwa dini zao au rangi zao hawakuwa na shule kabisa au walikuwa nazo kidogo waliweza kupata nafasi, bora tu wawe na sifa stahiki hasa za kufaulu mitihani na nyinginezo. Lakini si hivyo tu, ili kujenga usawa kwa upande wa sekondari Mwalimu alikwenda mbali zaidi. Serikali iligawa sawia nafasi za kwenda sekondari kwa mikoa na wilaya nchini na siyo tu kufuata kigezo cha mtu kufaulu mitihani. Mheshimiwa Mufti; Baada ya kutaifisha shule hizo, ukiacha shule za msingi zilizojengwa karibu kila kijiji, Serikali haikuwekeza sana katika ujenzi wa shule mpya za sekondari. Matokeo yake wakati ule katika mikoa yetu, ukizungumzia shule za sekondari za Serikali, kwa kweli nyingi, kama siyo zote, ni hizi zilizotaifishwa kwani Wakoloni hawakuacha shule nyingi na Serikali haikujenga nyingi mpya. Kwa kweli uwekezaji uliongezeka kwa wingi sana kwa shule za sekondari za Serikali katika Awamu ya Nne kwa ujenzi wa Sekondari za Kata. Kwa kutambua ukweli kwamba shule za Serikali ni kidogo hata baada ya Serikali kutiliana saini Itifaki ya Makubaliano (MoU) na TEC na CCT mwaka 1992, kasi ya kurejesha shule ilikuwa ndogo sana na baadae ikasimama kabisa. Kilichosimamisha ni ule ukweli kwamba zingerudishwa zote Serikali ingejikuta kama vile haina shule za sekondari na badala yake shule zingekuwa mikononi mwa makanisa. Kitendo hicho kingezua manung'uniko na mgogoro katika jamii hasa baada ya zaidi ya miaka mingi shule hizo kuwa mali ya Serikali. Kwa ajili hiyo, pamoja na nia njema iliyokuwepo ya kuziboresha na kuziendeleza uamuzi huo ulikuwa mgumu kutekelezeka. Serikali ikajipa dhima ya kuziboresha na kuziendeleza. Mheshimiwa Mufti; Viongozi wa Dini Zote; Ushauri na maombi yetu kwa BAKWATA na mashirika mengine ya dini na jumuia zilizokuwa na shule wafikirie kuwekeza katika ujenzi wa shule na vyuo vipya badala ya kuendelea kudai shule zao za zamani. Ahadi kubwa ya Serikali inayotoa kwenu ni kuwa hazitataifishwa tena. Source: Hotuba ya Rais ya Idd, picha za kuashiriki swala ya Idd - wavuti.com*
 
Wewe unazungumzia sababu ya Kifedha tu Wakati Fedha ilikuwa ni sababu mojawapo tu[hususan shule za wahindi], sababu nyingine ilikuwa ni Ubaguzi wa Kidini na wa Kirangi katika shule hizo. KWA MAANA SUALA LINGEKUWA NI UBAGUZI WA KIFEDHA, WATANZANIA WOTE YAANI WAISLAMU NA WAKIRISTO WALIKUWA WAMEPIGIKA KIFEDHA LAKINI SHULE ZA KIDINI BADO HAZIKUKOSA WANAFUNZI.Ila tofauti na wezao Wakiristo, Waislamu walikuwa kama Watoto wa kambo, kwa maana hawakuwa na Taasisi Imara na nyingi kulinganisha na wenzao Wakiristo ambao tokea Mkoloni Taasisi zao zilipata kila aina ya Usaidizi Kutoka Serikalini, na hivyo pamoja na umasikini waoWakiristo kupitia Taasisi za zao walikuwa much better kuliko Waislamu.NA TAMBUA KWAMBA KANISA LILITUMIA HUDUMA HIZI KAMA NJIA YA KUSAMBAZA IMANI/DINI YAO NA HUO ULIKUWA UGOMVI MKUBWA SANA BAINA YAKE NA WAZEE WA KIISLAMU AMBAO WENGI KWA SABABU HIZO WALIGOMA KUWAPELEKA WATOTO WAO KATIKA SHULE HIZO, HATA HIVYO WAPO WAZEE WALIOAMUA KUWA WABISHI NA KUAMUA KUWAPELEKA WATOTO WAO HIVYO HIVYO, WAKAVUMILIA CHRISTIAN TEACHINGS INDOCTRINATION, LAKINI AT THE END OF THE DAY WAKAPATA ELIMU YAO NA VYETI VYAO, NDIYO HAO BAADHI YA WAISLAMU WACHACHE TULIOKUWA NAO WALIOPITIA SHULE ZA KANISA ENZI HIZO. NA KITU KINGINE FAHAMU KWAMBA PALE FEDHA ILIPOTUMIKA KATIKA SHULE ZA WAHINDI, ILITUMIKA KAMA NJIA TU YA KWASIDELINE LOW CLASS AMBAO WENGI WALIKUWA NI WATANZANIA WEUSI ILI WAWEZE KUENDELEZA AJENDA YAO YA URACISM. Sababu zangu za kutaifishwa shule hizi inathibitishwa na Tamko la Serikali kupitia kwa Hotuba ya Raisi Jakaya Kikwete alipokuwa anawajibu Waislamu kwenye baraza la Iddi August 2011. Kikwete katika hotuba hiyo Anazungumzia Ubaguzi wa Kidini na Wa Kirangi na wala hajagusia Ubaguzi wa Kifedha, nadhani alifanya hivyo kwa kutambua kuwa FEDHA ILITUMIKA KAMA EXCUSE TU ILA SABABU BEHIND THAT ILIKUWA NI RACISM!. Kikwete alisema hivi nanukuu.

Mheshimiwa Rais ana haki ya mawazo yake kama ilivyo wewe na mimi. Lakini tukumbuke kuwa nae alisomeshwa na wamisheni na sikumbuki kama kuna mahali alisema kuwa walijaribu kumbadili dini au alibaguliwa kwa aina yeyote. Na yeye alienda hizo shule mara baada ya uhuru wetu wakati jotojoto la ukoloni lingalipo.

Mbona unajikanganya? Mwenyewe unasema wazee wa kislamu walikataa kuwapeleka watoto wao kwenye shule za misheni kwa kuogopa indocrination halafu unadai shule hizi ziliwabagua? Nina ndugu zangu kibao waliosoma kwenye shule za misheni na wamenihakikishia kuwa hakukuwa na hiyo indocrination unayoizungumzia. Tutoleeni mfano wa shule ambako ubaguzi huo wa kidini ulifanyika katika shule za kimesheni. Hata hizo shule za kihindi hazikugua maana wangefanya hivyo ndugu zetu wengi wasingesoma Aga Khan Boys Sekondari. Wakati wa ukoloni, ubaguzi mkubwa ulikuwa wa rangi na ulifanyika haswa kaika utoaji wa huduma za afya. Wazungu walijifungua Ocean Road na waswahili Makuti Muhimbili. Kama tatizo lilikuwa ni ubaguzi wa kidini basi baada ya miaka 30 ya elimu kutolewa bila ubaguzi wowote, pasingekuwa na tofauti kati ya idadi ya waliosoma wakristu, waislamu, bahai, wahindu , wasio na dini n.k.

Ni ufinyu wa kufikiri kutaka shule ambayo imeanzishwa na inayoendeshwa na taasisi ya kidini isifuate maadili ya dini hiyo. Mkristu ukienda Al Muntazir hauwezi kukataa kujifunika hijab. Unachoweza kukataa (na ni haki yako) ni kuingia msikitini (kama wanafanya hivyo) wakati wa kuswali. Vile vile, muislamu akimpeleka mtoto wake katika shule ya kikristu ni lazima akubali kuwa kabla ya kula watasali na kama ni wakatoliki patakuwa na msalaba darasani. Ni haki ya mtoto huyo kukaa kimya wakati wenzake wanasali na kukataa kupiga ishara ya msalaba. Ukienda katika Projects ufaransa ambako wakazi wengi ni waislamu, shule zinazogombaniwa (hata na ma-imamu) ni za kikatoliki. Hii ni pamoja na ukweli kuwa kuna shule za serikali ambazo hazina dini.

Umedai mwanzo kuwa waislamu na wakristu walkuwa wachovu kifedha wakati wa ukoloni. Naam, lakini tulitofautiana uchovu. Wafanyakazi wengi wa serikali walikuwa wakristu na hivyo walikuwa na kipato zaidi ya wenzao. Hali hii iliendelea na inaendelea hata baada ya kupata uhuru wetu. Wakristu kwa ujumla wao wana uwezo zaidi wa kipesa ambao unawafanya waweze kuhakikisha watoto wao wanapata elimu bora na kuweza kuchangia miradi ya maendeleo ya makanisa yao. Kwa sababu kutaifisha hizo shule hazikuondoa tofauti hiyo, inabidi jamii iangalie ili suala kwa undani zaidi badala ya kushinda kudai serikali inawapendelea wakristu. Kwenye hilo, wakristu nao wanatakiwa watambue kuwa wana jukumu la kupunguza tofauti hii maana hali kama
hii inaweza kutufikisha pabaya.

Amandla......
 
Hivi uhuru wa kutoa mawazo unakomea wapi? Mzee Mtei yeye kaangalia vigezo kadhaa mojawapo ni takwimu kwamba wale 15 kutoka Zanzibar wote ni Waislamu na 15 kutoka bara ni 4 yaani zaidi ya 63% ni kutoka dini moja tu. Je mtu katika ubinafsi wapi wake, kuna kosa gani akiuliza kukosekana kwa usawa katika hili?

Katika uteuzi wa tume hii uwazi na ushirikishwaji wa wadau mbalimbali ulikuwa unatakiwa zaidi. Kwa kuwa mtu mmoja tu amepewa dhamana hii tutarajie mapungufu mengi zaidi na zaidi kutoka kwenye tume na katiba yenyewe.

Hivi kigezo cha usawa ni dini tu? Na je kinapimwache hicho? Ninyi mmejuaje kuwa hao watu waliotajwa ni wakristo au waislamu, mnasali na kuswali nao? Yaani kusikia majina tu na dini zao mmeshazijua? Hivi Adolf Hitler alikuwa mkristo? Mnanishangaza sana kwa kweli. Unaijuaje dini ya mtu kwa kumsikia jina tu? Hivi mwenye jina Noel kama mimi basi tayari ni mkristo sababu ya jina la kizungu? Hata kama siendi kanisani, ni mzinzi, sitoi zaka nk? Hao mnaosema ni waislamu wamependekezwa na masheikh na maimam wao? Mnajuaje kama mashekhe wao wangeulizwa kama wasingependekeza watu tofauti? Hao mnaosema ni wakristo je walipendekezwa na maaskofu wao? Mimi naona mjadala wote huu ni upuuzi mtupu! Hao watu wangekuwa wametumwa na viongozi wa dini zao ningejua wanawakilisha interest za dini hizo, lakini jamani mbona siyo hivyo? Tuacheni upunguani.
 
ccm tulivu kwa ufisadi na vita vya makundi ya tripple alliance na tripple ententee. sijui wewe kundi gani? wanaokula? waliokula? watakaokula?
 
Hatima ya mustakabali wa tanzania itaamuliwa na kakundi kadogo sana ka watu zaidi kidogo ya milioni moja dhidi ya milioni 44. Bado hatupo salama. ngoja mlazimishwe kufuga midevu!

umenichekesha mdau! na hili joto mbona tutakomaaa! ila mkuu si wanadai mamushka wake ni crusader mwenzetu? au yeye haoni hilo akamkanya mwanawe?
 
Mkuu Mkandara. Nimekuwekea MoU yenyewe na inasema wazi kuwa serikali ita-endeavour kuziombea misaada taasisi za dini katika makubaliano na nchi wahisani hususan Ujerumani. Endeavour maana yake itajitahidi. Hakuna mahali kwenye hiyo MoU ambapo serikali inashurutishwa kusaidia taasisi za kikristu. Sasa kwa nini mnapenda kuandikia mate wakati wino upo?

Wakati mwingine msipende kutufanya wengine mazezeta. Mnajifanya si wadini lakini kama mnayoandika yanawaumbua. Kama si udini, mtakuwa na tatizo gani na serikali kuona umuhimu wa kushirikiana na taasisi ambazo zinaendesha zaidi ya asilimia 50 (quote yako) ya shule za sekondari na huduma za afya nchini? Hawa wanachangia zaidi ya serikali katika sekta hizo lakini mnataka serikali iwaache kivyakevyake tu kwa vile ni za kikristu? Pamoja na kwamba hamjatoa ushahidi wowote kuwa hizo taasisi zinatoa huduma hizo kwa kuwapendelea wakristu. Hivi unaamini kweli serikali inaweza kutimiza malengo ya MDGs bila kuzishirikisha taasisi hizi? Na grant ni ruzuku, si mkopo. Kupewa hizi taasisi hakumuongezei mzigo wa kulipa deni mtanzania wa kawaida. Badala yake kunamboroshea huduma ambazo anazihitaji sana. Utapingaje hili kama si mdini? Unatofauti gani na wale wanaopinga kuingia OIC kwa sababu tu ni ya waislamu? Pamoja na kwamba kama watasaidia kujenga dispensari zitawasaidia wakristu, wahindu, wenye imani za asilia n.k.?

Kweli hamuitakii mema nchi yetu na watu wake.

Amandlaa...........
Mkuu wangu nadhani haya ndio matokeo ya MoU maana hukubali kabisa tunachoongea na unaendelea kutumia swala la NYIE against wakristu japokuwa nimekwambia mara mia kidogo kwamba lawama zetu ni kwa serikali. Wakristu hawahusiki na lawama zetu isipokuwa mfumo uliopo. Na nashangaa sana siku hizi kila kitu cha Waislaam lazima kipingwe na Wakristu hata kama kinaelekezwa kwa serikali ambayo nyote mnailaumu kwa ukandamizaji wake. Kama wameweza kufanya mengine yoote mabaya serikali hii inashindwa vipi tukugawa ili waendelee kututawala kwa Udini..Hii nni mbinu ya kizamani kabisa lakini nashangaa inafanya kazi nchini na watu bado mnashindwa kuishtukia. Hivi ni kipi hasa kinachokufanya ujione mbora zaidi ya Waislaam kiasi kwamba maandishi yako yamejaa dharau tupu kwao..

Halafu kwa utetezi ktk MoU mbona umechukua kipande kidogo sana cha Muafaka huo na kukiweka hapa? weka muafaka wote watu wausome halafu wauchambue wenyewe kwa macho yao maana tunarudi nyuma sana ambako tuliisha pita miaka.. Na please usitake kudanganya watu, ndani ya Muafaka huo hakuna jina Ujarumani wala nchi iliyotajwa kushiriki na misaada yao, japokuwa unajua fika kwamba bajeti ya serikali inategemea donors kwa kiwango kikubwa na msisitizo mkubwa uliwekwa kwa Elimu na Afya toka mwaka 1990. Halafu unasema ati serikali haijalazimishwa? haya kweli majibu ya kuandika hapa wakati watu tunajua fika kwamba hakuna mikopo inayotolewa bure wala pasipo masharti...Mungu wangu leo Grants ni ruzuku!! ama kweli tuna wakati mgumu sana kuelimishana. Ebu nambie hizo fedha za MDG zinatumika vipi ktk Elimu na Afya maana nijuavyo mimi gharama za huduma hizi nchin zipo juu sana pengine kuliko hata Mataifa makubwa, na hao wadau wengine wanafaidika vipi?

Nimerudia hata kukwambia kwamba hata mjadala wa Katiba unashika moto leo kwa sababu watu wana wasiwasi wa kuhusishwa, iwe muafaka au Mkataba na kundi moja la kijamii. Majuzi tu, Dr. Slaa kazungumzia kuna hatari ya muafaka baina ya CCM na Wakuu wa mikoa kuhusiana na Katiba mpya. Dr.Slaa hazungumzi hivyo kwa sababu yeye ni Chadema na anafanya upinzani na CCM bali lawama zake anazielekeza kwa serikali iliyopo madarakani, angeyafanya hayo hata kama angekuwa NCCR au CUF maana sii haki kwa serikali kuandaa mipango kwa minajiri ya CCM. Muafaka kama huu unaweza kuharibu kabisa ushirikiano wa wananchi ktk utunzi na hata kuikubali katiba mpya. Bado huoni nyuma ya pazia hili mkuu wangu?

Ni ktk maudhui hayo hayo, sisi tunasema serikali haikufanya busara ilipoweka muafaka na Kanisa kuhusiana na swala la ELIMU na AFYA bila kuwahusisha wadau wengine wote. Leo hii ni miaka 20, hatuna bora lilofanyika zaidi ya huduma kuwa mbovu zaidi, Udini kushika kasi ya ajabu na wewe unakataa katakata kuliona hili kwa sababu unachoona ni upande wa dini yako na sisi ni maadui wa wakristu hali wanafaidika ni watu wengine kabisa. Kina Jokakuu huko nyuma wameandika mengi kuhusu lawama za Waislaam, na ukizitazama juu juu utafikiri hazina maana lakini ndizo zitakazo vunja UMOJA wetu na nakuhakikishia hata kama wangekuwa Bainiani ningewaunga mkono kwa sababu binafsi yangu huu mpango wa kulitazama Taifa hili kama nchi ya Wais;laam na Wakristu sikubaliani nalo.. Muafaka wowote unawaweka Waislaam au wakrisut mbele ya jumuiya nyinginezo siwezi kuunga mkono..

Na mwisho, mkuu wangu kuhusu Nyerere umedanganywa sana, Kwani wakati wa Mwinyi hata kabla ya kurudishwa kwa shule hizi wanafunzi walikuwa wakilipa Ada na UPE kwa shule zote za Primary school, haikuwa swala la uwezo wa watoto bali itikadi nzima ya siasa ya Ujamaa na Kujitegemea inazungumzia vyanzo hivi kuwa mikononi mwa serikali ili kuondokana na Ubepari, Ukabila, Unyonyaji, Udini, Ukabila na makundi mengineyo..Ni baada ya Muafaka ndio tumeona bei zikiongezeka zaidi japokuwa tunapewa misaada mingi ya kuboresha Elimu na Afya nchini. Mkapa ndiye alokuja rudisha elimu ya primary iwe bure..

Hatuna noma kabisa na makanisa kuendesha shule na Hospital zake na tena wanaifanya kazi kubwa na nzuri lakini tatizo linakuja tu pale serikali inapoingia Ubia na chombo cha kidini kuwapa nafuu ya kodi na mabillioni kwa mwaka wakati hizi ni private schools sio kanisa kama tulivyofundishwa kwamba kazi ya kanisa ni kutoa huduma bure - Ndio tukaupata msemo wa sifanyi kazi ya kanisa. That is wrong na maadam hatutaweza kubaliana wala kuelewana tokana na tofauti zetu nadhani tuishie hapa.. Wewe endelea kuamini serikali ilifanya jambo bora nami kivyangu maana sintotegemea kabisa Musilaam na Mkristu kukubaliana ikiwa swala la imani zetu tu imekwisha kuwa label - Uadui..
 
Unasoma kweli wanachobandika wenzako? Mbona nakala ya Mou niliishaibandika halafu leo unadai niibandike tena? Hata hivyo, nimeibandika tena hapo chini.

Kama unayo MoU iliyo kamilifu na yenye vipegele unavyokazania zaidi ya hii niliyoibandika iweke humu tuione. The Memorandum of Understanding between the Christian Council of Tanzania and Tanzania Episcopal Conference and the United Republic of Tanzania ulioandaliwa na Prof. Dr. C.R Mahalu na kuidhinishwa tarehe 21 February 1992 (nakala iliyobandikwa hapa JF na Game Theory tarehe 30 June 2009 15.21, unaweza kuusoma hapa Na please usitake kudanganya watu, ndani ya Muafaka huo hakuna jina Ujarumani wala nchi iliyotajwa kushiriki na misaada yao, japokuwa unajua fika kwamba bajeti ya serikali inategemea donors kwa kiwango kikubwa na msisitizo mkubwa uliwekwa kwa Elimu na Afya toka mwaka 1990.) ina sehemu 4. Sehemu ya 4, article XII I inasema:
The Government shall endeavour to include financial assistance to Church run services in its bilateral negotiations particularly with the Government of the FEDERAL REPUBLIC OF GERMANY. Consideration shall be made during such bilateral negotiations with other donors.

Maneno yako

Na please usitake kudanganya watu, ndani ya Muafaka huo hakuna jina Ujarumani wala nchi iliyotajwa kushiriki na misaada yao, japokuwa unajua fika kwamba bajeti ya serikali inategemea donors kwa kiwango kikubwa na msisitizo mkubwa uliwekwa kwa Elimu na Afya toka mwaka 1990.

Inawezekana nimekosea kutumia neno ruzuku kuhusiana na grant. Grant hailipwi. Ukipewa Grant hautakiwi kuirejesha tofauti na mkopo. Lakini kuwepo na grant hakumaanishi kuwa hakuna gharama nyingine. Grant zinatumika katika kutusaidia kufikia malengo ya MDG lakini sio kwamba yanatuondolea sisi wajibu wa kulipia sehemu ya gharama zake. Unaposema gharama zetu za elimu na afya ni zaidi ya zile za mataifa makubwa tutolee mfano wa gharama hizo. Au unadhania watu wote wanawapeleka watoto wao Feza na kuuguziwa Aga Khan Hospital?

Utasemaje kuwa hauna tatizo na wakristu wakati lawama zako juu ya muafaka ni hususan kuwa umeingiwa na wakristu? Hivi leo ukiilaumu serikali kwa kutoa upendeleo kwa wakina mama, utaepuka lawama kuwa hauwapendi wakina mama? Na hasa ukitoa lawama hizi ukijua thika kuwa ni mama, dada, shangazi zako ambao wanasaidiwa!

Ni chuki hiyo hiyo dhidi ya ukristu inayokufanya udai kuwa gharama za elimu zimepanda kwa sababu ya MoU hiyo kana vile shule zote zisizo za serikali zinaendeshwa na kanisa. Badala ya kuona kuwa hili ni matokeo ya kufungua milango katika nyanja za elimu na utoaji wa huduma za afya na kuruhusu soko huria kutawala, unawanyooshea mkono kanisa. Hebu tutolee mfano wa hospitali gani ya kanisa inayotoa huduma kwa bei mbaya? Uwe muangalifu, usichanganye zile zinazotumia majina ya kikristu lakini zinaendeshwa na watu binafsi. Linganisha na bei za Aga Khan Hospital ( waislamu), Hindo Mandal ( wa-hindu), Ibrahim Haji (waislamu), TMJ ( sijui nani), Regency (watu binafsi), Tumaini (watu binafsi) n.k. Wote hawa hawakuwemo kwenye muafaka lakini bei zao bado ni juu. Linganisha gharama za St. Marian, Loyola na za Feza. Badala ya kushukuru kuwa pengine kutokana na muafaka huo ndio maana bei za hizo shule za wakristu zimekuwa nafuu, unabaki kulaumu. Hii pamoja na kuwa ni baadhi tu ya shule zilizorudishwa.

Badala ya kulalamikia MoU, hebu angalia hali ya shule ambazo zilirudishwa kwenye taasisi hizo (ubora wa majengo, vifaa, ufundishaji n.k.) na zile ambazo serikali imebaki nazo. Wewe furaha yako ingekuwa St. Joseph hali yake ingekuwa kama Tambaza au Azania?

Unasahau kuwa ni kutokana na MoU hiyo ndio taasisi za kikristu zimepata confidence ya kuwekeza kwenye elimu na afya. Au roho yako inakuuma kuona kuwa wanajenga Vyuo Vikuu, mashule, dispensari na hospitali. Yote haya ni kutokana na kuhakikishiwa kwenye Article XII ya MoU yao kuwa:
The Government shall not nationalize schools, hospitals or any education or health institutions owned by the Church.

Maneno ya jukwaani hayana uzito kama MoU.

Unazungumzia UPE? nani ambaye alikuwa na uwezo alimpeleka mtoto wake kwenye shule za UPE? Ni kama vile ilivyo shule za Kata sasa hivi. Mimi nazungumzia hali ilivyokuwa wakati shule zinataifishwa. Shule zenye elimu bora zilikuwa za taasisi za kidini na karo zake zilikuwa juu. Walioweza kuzimudu walikuwa wafanya biashara wakubwa na viongozi serikalini. Na wengi waliwapeleka watoto wao huko. Na wengi wa hao walikuwa wakristu na wahindi. Mara baada ya shule hizo kutaifishwa, kiwango cha elimu na huduma kilibaki juu katika shule zote za serikali. Ndio maana hakuna mtu alikataa kumpeleka mtoto wake shule hizo akichaguliwa kuingia huko na badala yake ampleleke private (kwa Dar wakati huo, hii maana yake likuwa Kinondoni Muslim, Shaaban Robert na Mzizima). Watu walijivunia kuwa watoto wao wanasoma Kibaha, Ilboru n.k. Tofauti na sasa. Hali ilipoanza kuwa mbaya, hata kabla ya MoU hiyo, wenye uwezo walianza kuwapeleka watoto wao nje ya nchi kwa kukosa imani na viwango vya elimu nchini. Kenya, Uganda, Swaziland zimefaidika sana na karo inayolipwa na watanzania. Ni baada ya watu binafsi (St. Mary's), taasisi za dini kukaribishwa kuwekeza kwenye elimu bila kiwingu cha kutaifishwa ndipo alternative ya kupeleka watoto nje imeanza kupatikana. Pamoja na hizo gharama unazozingumzia, watu wanaona ni afadhali amlipie moto wake kuliko kumuacha katika shule za serikali zenye bei nafuu. Wengi wanaowabakiza watoto wao huko ni wale wasio na choice. Hivi unaamini kama serikali ingeboresha huduma zake angalau zifikie hizo za praivet, wangapi wangepeleka watoto wao Loyola?

Unarudia tena uongo. Wapi katika MoU panaposema sema taasisi za kanisa zitapewa nafuu ya kodi? Misamaha ya kodi inatolewa kwa taasisi zote za kidini zinazowekeza kwenye elimu na afya. Bila shaka hata Aga Khan anapata nafuu hii. Lakini kwa vile taasisi za kanisa ndio nyingi zimejiingiza humu basi nafuu yao kwa ujumla itakuwa kubwa.

Hatari kubwa hii! Ulifundishwa na nani kuwa kazi ya kanisa ni kutoa huduma BURE? Kanisa linawajibika kuhudumia jamii lakini sio bure. Au unadhani sadaka za wakristo (wa nchini na nje ya nje) zinatosha kutoa huduma hizi bure kwa kila mtu? Ni mawazo ya kupenda dezo huku ndiko kunakofanya wenzako wengine wafanye misaada ya bure kuwa ndio hoja kuu ya kujiunga na O.I.C. Kanisani tunafundishwa kuwa Mungu atamsaidia yule anayejisaidia. Hakuna free lunches kanisani.

Kama unaona kwa kusema kuwa waislamu walikuwa na wanaendelea wachovu kielimu na kipato ukilinganisha na wakristu, ni kuwadharau waislamu, hiyo ni juu yako. Mimi naamini hivyo na ndio maana nasema kuwa tatizo ni zaidi ya kuwepo kwa MoU. Kwa zaidi ya miaka 30 pamekuwa na equal opportunities katika elimu lakini tofauti hiyo bado ipo. Kuilaumu MoU ni kuionea serikali na wakristu.

Naona nimefikia tamati katika suala hili. Kama haujanielewa basi heri tubaki na tofauti zetu.

Amandla......
 
The Government shall endeavour to include financial assistance to Church run services in its bilateral negotiations particularly with the Government of the FEDERAL REPUBLIC OF GERMANY. Consideration shall be made during such bilateral negotiations with other donors.

hiki Kipengele ni Kipengele Hatari sana, ni kipengele kinachoifanya SERIKALI IANZE KUFANYA KAZI KWA NIABA YA KANISA KITU AMBACHO NI KINYUME CHA KATIBA . huko nyuma umejaribu "KUPLAY DOWN SIGNIFICANCE YA NENO ENDEVOUR", wewe unalitafsiri kama "ITAJITAHIDI", Mimi nalitafsiri kuwa "ITAFANYA JUHUDI" kuiombea kanisa misaada kwa ajili ya miradi yake inapofanya majadiriano na serikali za kigeni HUSUSAN serikali ya Ujerumani. then inafatiwa na neno "Consideration" ikimaanisha serikali "ITAFIKIRIA" kuwa iiombee Miradi ya kanisa misaada pindi itakapofanya mazungumzo na Wahisani wengine.
KAMA HUONI TATIZO KATIKA KIPENGELE HICHO, THEN SIJUI UTAKUWA UMEJIWEKA UPOFU WA NAMNA GANI!- KWA MAANA KWANZA KWA KUFANYA MAZUNGUMZO KWA NIABA YA KANISA MAANA YAKE NI KWAMBA "HAIKUFANYA MAZUNGUMZO KWA NIABA YA TAASISI NYINGINE ZENYE KUTOA HUDUMA KAMA ZINAZOTOLEWA NA KANISA, MFANO TAASISI ZA KIISLAMU, NA WATU BINAFSI" NA HUO NI UPENDELEO KINYUME CHA KATIBA.

MOU NI UPENDELEO WA WAZI KABISA KWA TAASISI ZA KANISA AMBAZO SIYO WAO PEKE YAO WENYE KUTOA HUDUMA ZA SHULE NA AFYA NCHINI.
 
Ivi unaweza kulinganisha context ya lusinde (kwenye jukwaa la kisiasa)wakati wa kampeni na Katibu mkuu wa chama alipoulizwa akadefend na mawazo ya Mtei (sio kiongozi wa chama) tena akiwa nyumbani kwake??

:focus:
Ivi kawa wewe Ritz ni mrefu nikasema wewe ni mrefu natakiwa kuomba radhi sio?? Hebu geuzia upande wa pili wangekuwa ni kina john wamezidi kwenye hiyo tume si kila ijumaa kungekuwa na maandamano?? Humu si kungekuwa hakutoshi? Shukuruni mungu huu upande wa pili kuna ustaarabu na hata mteuzi najua ameliona hilo.

wewe una mahaba makuu.
mtei sio tu ni kiongozi wa chama bali pia ni mjumbe wa kamati kuu ya chama.
 
mou mou mou...na yakitoka matokeo ya form vi utasikia tena necta wanapendelea shule za kikristu...yaani waislamu wamekuwa ni watu kuonewa na kulalamika siku zote...kinachoshangaza ni watu wanajadili matokeo wakati tatizo la msingi linalosababisha yote hayo linajulikana lakini wanashindwa kuli address...heri yake kikwete (alipozungumza kwenye baraza la eid dodoma) aliweza kuwaambia ukweli ingawa ni mchungu kuumeza kama shubiri...

Bandugu, mindset za wafuasi na viongozi wa dini hizi mbili(uislam/ukristo) zipo tofauti sana na mpaka hapo watakapoanza kufanana katika kupanga na kusimamia shughuli za maendeleo(shule/hospitali/vyuo nk) ndiyo hali itabadilika...mfumo wa kikoloni uliwafanya wakristu wawe ahead ya wenzao lakini kinachoshangaza ni zaidi miaka 50 baada ya uhuru, tukiwa na fursa sawa wakristu bado wanakimbia kwa kasi katika kuwekeza kwenye elimu na shughuli nyingine za jamii wakati wenzao waislamu badala ya kukimbia zaidi wenyewe wameamua kwenda kwa mwendo wa matembezi ya ufukweni huku wakilalamika saaaana...

Ndugu zangu waislamu, ili mfumo wenu wa dini na mahusiano yake na jamii uendane na kasi ya maendeleo ya karne hii inabidi ufanyiwe facelift au overhaul ya nguvu...haya bana endeleeni na mjadala wenu...!
 
hiki Kipengele ni Kipengele Hatari sana, ni kipengele kinachoifanya SERIKALI IANZE KUFANYA KAZI KWA NIABA YA KANISA KITU AMBACHO NI KINYUME CHA KATIBA . huko nyuma umejaribu "KUPLAY DOWN SIGNIFICANCE YA NENO ENDEVOUR", wewe unalitafsiri kama "ITAJITAHIDI", Mimi nalitafsiri kuwa "ITAFANYA JUHUDI" kuiombea kanisa misaada kwa ajili ya miradi yake inapofanya majadiriano na serikali za kigeni HUSUSAN serikali ya Ujerumani. then inafatiwa na neno "Consideration" ikimaanisha serikali "ITAFIKIRIA" kuwa iiombee Miradi ya kanisa misaada pindi itakapofanya mazungumzo na Wahisani wengine.
KAMA HUONI TATIZO KATIKA KIPENGELE HICHO, THEN SIJUI UTAKUWA UMEJIWEKA UPOFU WA NAMNA GANI!- KWA MAANA KWANZA KWA KUFANYA MAZUNGUMZO KWA NIABA YA KANISA MAANA YAKE NI KWAMBA "HAIKUFANYA MAZUNGUMZO KWA NIABA YA TAASISI NYINGINE ZENYE KUTOA HUDUMA KAMA ZINAZOTOLEWA NA KANISA, MFANO TAASISI ZA KIISLAMU, NA WATU BINAFSI" NA HUO NI UPENDELEO KINYUME CHA KATIBA.

MOU NI UPENDELEO WA WAZI KABISA KWA TAASISI ZA KANISA AMBAZO SIYO WAO PEKE YAO WENYE KUTOA HUDUMA ZA SHULE NA AFYA NCHINI.

Kuna neno include ambalo unajifanya hulioni. Ni kuwa katika mazungumzo yao na wafadhili kuhusu huduma hizi kwa jumla, watachomekea haja ya kusaidia HUDUMA zinazoendeshwa na taasisi za Kanisa. Hawataondoka kwenda ujerumani kuombea msaada kanisa. Hilo watafanya wamisheni wenyewe na halipo katika MoU hii. Wewe mwenyewe ulitubandikia bandiko linaloainisha kuwa taasisi hizi zinamiliki zaidi ya asilimia 50 ya shule za sekondari, vyuo na hospitali hapa nchini. Hivi zikitetereka, nani atakayeumia zaidi kama sio sisi watanzania wa kawaida (bila kujali dini zao) ambao tunategemea huduma zao? Pamoja na kuona kuwa ninawatukana, hamuwezi kulinganisha mchango wao katika huduma hizi na zile zinazotolewa na taasisi za dini nyingine na watu binafsi. Serikali iliwanyang'anya na ilishindwa kuziendesha. Leo wamewarudishia, huduma zimeboreshwa lakini mnaona soni kwa vile tu ni wakristu?

Serikali imekaribisha taasisi nyingine zishirikiane nae (hata kwa kuweka MoU kama hii) nazo zimekataa. Badala ya kuchangamkia ili wananchi wa kawaida wafaidike, mnabakia kudai hata hicho chema kiharibiwe ili mkose wote.

Halafu mnajifanya si wadini!

Amandla....
 
Tunatakiwa kuzitafakali kwa kina kauli za viongozi wetu hawa ambao tunaimani kila mmoja ana mchango madhubuti juu ya taifa letu kwa sasa. Inaelekea Mh, Zitto na Mzee Mtei wanamapambano ya kila mmoja kutetea kile anachokiamini baada ya kila mmoja kutambua dhamira ya mwingine ndani ya CDM kiasi cha kufanya anayejitokeza kuelezea maono yake mwingine huibuka kumuelezea tofauti.

Mzee Mtei ni muasisi wa CDM na sera zake hivyo anastahiri kupewa, pamoja na yeye binafsi kuilinda heshima yake. Mh, Zitto ni mfuasi na mtekelezaji wa sera za CDM ambaye anaonekana kutaka kuimarisha zaidi sera husika ili kuondoa dhana iliyopo kuwa chama hicho kinajipambanua kuwa cha kitaifa ikiwa tu hakuna athari zinazotishia maslahi ya Muasisi huyo na watu anaowaamini kuyalinda, na pindi inapotokea vinginevyo utaifa wa CDM unatoweka.

Tofauti na waasisi wa vyama vingine Mzee Mtei anabaki kuwa mfano wa pekee kwa kuweza kusimamia sera na mikakati ya kuhakikisha CDM kinadumu na kuwa kimbilio la jamii ya watanzani wote. Mh, Zitto naye anahaha kuimarisha dhana hiyo kwanza ndani ya chama ili kuiaminisha jamii kuwa CDM kweli ni sehemu salama kwa watanzania. Naamini neno Demokrasia lina tafsiri pana kiasi cha kila anayejaribu kuifuata kama inavyotamkwa gharama yake ni kubwa mno hasa kama hukubaliwi na mfumo ulionao karibu. Pamoja na yote yanayotokea Mh, Zitto ameonyesha ukomavu na utayari wa kuutumikia moyo wake kwa kuwa muwazi katika jambo lolote linalogusa maslahi ya Taifa na ndiyo maana hasiti kukosoa au kutii kile kinachoelezwa hata na muasisi wa chama hicho ikiwa tu kinagusa au hakizingatii maslahi ya watanzani.

Kuwepo kwa uwingi wa wajumbe kutoka katika dini fulani kunachangiwa zaidi na jinsi tume hiyo ya kusimamia mchakato wa Maoni ya Katiba ilivyoundwa. Hata kama ingekuwa ni CDM ndiyo wanaoteua Tume hiyo bado uwingi wa wajumbe kutoka dini inayoelezwa kulalamikiwa na Mzee Mtei ingekuwa na wajumbe wengi zaidi ya nyingine la kama angetaka iwe Tume ya Tanganyika kama walivyofanya wazanzibari kabla ya uchaguzi Mkuu wa 2010. Bandugu, Hakuna mwana asiye na kwao, kwani ng'ombe aumiapo hurejea ngamani. Ngama ni zizi, na CUF Zizi lao hasa lipo Zanzibar, CDM zizi lao hasa lipo Kanda ya Kaskazini ijapokuwa kina mhimili mkubwa katika kanda ya Magharibi. CCM inayojipambanua kuwa chama cha Kitaifa sasa kinaonekana kinaogopa mapambano baada ya kupoteza nguvu na hamu ya kupambana kutokana na kutojitambua kwa baadhi ya viongozi wake.

Tunawapongeza Mzee Mtei na Bob Makane kwa kazi waliyoifanya ikiwa ni pamoja na makamanda waliopokea kijiti chao. Muda wa kukijenga chama (CDM) umekwisha na sasa ni wakati wa kukisimika kwa watanzania huku viongozi wake kwa ujumla wakijiepusha na namna yeyote ya ubaguzi au kutoheshimu maoni ya baadhi ya wanachama wake. Kwa sasa CDM kimekuwa ni kimbilio la watu waliojaa matumaini ya kukombolewa na ndiyo maana hata ile dhana ya kwamba CCM wakisimamisha jiwe wanauhakika wa kushinda imegeuka na sasa kuwa CDM hata kama watasimamisha jiwe wanauhakika wa kushinda.

Hiki ndicho kipindi kigumu zaidi ambacho CDM kinatakiwa kuonyesha utayari wake wa kuwaaminisha watanzania kuwa ni chama kwa ajili ya kuwakomboa na siyo cha kuwatumia ili kufikia malengo ya baadhi ya viongozi. Mzee Mtei anastahiri kulindwa na kuilinda heshima yake, na pia Mh, Zitto anatakiwa kulindwa na aongeze bidii za kukabiliana na changamoto kwa kila namna kwani anajitokeza kuwa mhimili wa kuthubutu na kutenda kama ilivyokuwa kwa Hayati Mwl Nyerere ambaye hakuasisi chama bali alijiunga na kuboresha pale alipopakuta, hatua iliyopelekea aonekane kuwa mtu aliyekuwa na mtazamo wa pekee juu ya maslahi ya watanzani.
 
Fundi Mchundo,
Ndugu yangu wee mbona umepotosha zaidi vitu. Grant pamoja na kuwa hairudi hutolewa kwa specific project na hutolewa mara moja sio kitu cha kuendelea kila mwaka kwa chombo au mtu yule yule. JK alisema wazi mwaka jana tu kwamba yeye sio mdini kisha wapa kanisa Billioni 600. Na hata siku moja haiwezi kuwa kitu cha faida yaani kuziwezesha Shule na Hospital zifanye biashara. Hii sio grant kwa ufahamu wangu.

Labda nikukumbushe tu ya kwamba trunachozungumzia ni ARTICAL ONE, the establishment of the institution bila kuwahusisha wadau wengine. Haya unayoongea ya katikati ni miungo tu vya kuwepo kwa chombo hicho. Ni sawa na Muafaka wa CUF haukufaa kuwepo sasa haya ya Maalim Seif kuwa makamu wa rais wa Zanzibar ni kuundwa vyeo na kazi ambazo hazikuruhusiwa kikatiba.

Artical one inasema hivi:-
1. There shall be A GOVERNMENT body to be known as The Chriatian Social Service Commission (herein after to be known as "Commission") whose primary functions shall be:- Blaa blaa blaaa..

Sasa kikatiba huu muundo wa Government body inayoitwa CSSC ndipo tunapokwazwa..Sijui wapi unashindwa kuelewa maana nimechoka kendelea ku bishana wakati kitu kipo wazi kabisa. Ama kweli ndio maana Lowassa anapendwa sana.
BTW Haya tulishayajadili sana huko nyuma na Game Theory unaweza kurudia kupitia Hapa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom