Nitagawana Mali 50/50 na Mke wangu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
NITAGAWANA MALI 50/50 NA MKE WANGU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mali hazikuwa na kamwe hazitakuwa kipaombele changu. Sio mimi tuu bali Watibeli wote. Ikiwa ni mke wangu. Ambaye naye ni Mtibeli. Na ambaye kwake mali sio kipaombele.

Ikiwa itatokea Mimi na mke wangu tukaachana basi tutagawana Mali nusu kwa nusu kama zilivyo sheria na amri za Watibeli. Ni haki yake na yangu kugawana mali nusu kwa nusu sio kwa sababu ya mchango au nguvu kazi au vipawa au Karama au uwezo wa kuzizalisha mali hizo bali kwa sababu sisi tulikuwa wamoja.
Haijalishi mimi ndiye niliyekuwa nafanya kazi au niliyezalisha zaidi.

Ikiwa mmoja ataichukulia hiyo kama nafasi ya bahati kwake hiyo kwetu haitakuwa juu yetu na haitakuwa na maana yoyote ile na wala haitatuzuia Watibeli kumpa Haki yake kwa tamaa yake ikiwa alijiingiza kwenye ndoa kwa uovu.

Watibeli tunajua Mali zipo kwaajili yetu na sio sisi kwaajili ya hizo mali. Tunajua na kufundishwa ya kuwa sisi sio watumwa wa mali. Ila mali zipo kwaajili ya kututumikia na kufurahisishia haja na mahitaji yetu.

Tunajua kuwa chochote tukitakacho tunakipata kwa Mapenzi ya Mungu. Kama vile Mungu alivyotupa mali pasipokuwa Watumwa wa mali hizo ndivyo hivyohivyo hatutaona ugumu kuwapatia haki zao zilizopo kwetu kama Mali.

Taikon kama Mtibeli Halisia, nitagawa Mali nusu kwa nusu, tena ikiwezekana na zaidi ikiwa Mke wangu atataka tugawane na kila mmoja achukue sehemu yake.

Sababu ambazo zitanifanya niachane na mke wangu kama Watibeli wengine kisha kugawana hiyo 50*50 ni kama ifuatavyo;

1. Mke kujihusisha na Uchawi au ushirikina
Ni kosa kubwa kwa Watibeli kujihusisha na tabia ya kuamini, kutumikia na kutumia uchawi na ushirikina.
Taikon ataachana na mkewe pasipo kushauriwa, kushauriana, kufikiria wala mjadala pale ambapo mkewe atakuwa na hatia ya uchawi na ushirikina. Baada ya hapo mgawanyo wa mali utafanywa. Na ni 50*50 na kama atahitaji zaidi ya 50 atapewa.

2. Usaliti wa mapenzi(uzinzi)
Ni kosa ambalo hakuna mambo ya mijadala. Kosa ambalo hata ukipewa msamaha haibadilishi chochote katika kupeana Talaka.

3. Hiyari ya Mwanamke kutaka kuachana
Kwa Watibeli, ndoa ni muungano wa hiari na kamwe sio gereza. Kama ilivyohiyari kuingia pia ni hiyari kutoka.
Ikiwa Mwanamke (mke wangu)kwa hiyari yake atakuja kuomba au kutaka kupewa talaka. Hakutakuwa na muda wa kumuuliza kwa nini au atoe maelezo.

Taratibu za kuachana zitafanyika. Kisha mgawanyo wa mali utafanyika. Na atapata nusu kwa nusu. Na kama atahitaji ziada kama kile akiitacho faida atapewa ziada.

4. Atamkana Mungu
Ikiwa atatumia hiyari yake kumkana Mungu aliyemuumba, na kumtukana na kumkufuru. Basi ataachana na Taikon. Na atapewa sehemu ya haki zake zote. Na tena akihitaji ziada ya haki yake pia atapewa.

Vipi kama atakataa kuchukua haki yake?
Ikiwa atakataa kuchukua haki zake basi haki hiyo itatumiwa na watoto wake. Na ikiwa hakuna watoto basi watapewa ndugu zake.

Watibeli hawaoni sababu hata moja ya Mume kukataa kugawana mali na yule aliyemuita mkewe. Hiyo kwetu ipo kinyume na Haki, upendo, Ukweli na Akili ambao ndio nguzo zetu kuu.

Acha nipumzike sasa.
Nawatakia maandalizi mema ya Sabato.

Robert Heriel
Taikon ww Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hata Mimi nilivyokuwa mdogo ......huko kijijini kwenye umakini mkubwa nilikuwa nawaza ....nikipata pesa ntakuwa nawapa maskini

Kumbe ulikuwa utoto ....now nna pesa ila nikiombwa hata buku nachukia kama mashabiki wa Simba....wanavyochukia namba 5
 
Hata Mimi nilivyokuwa mdogo ......huko kijijini kwenye umakini mkubwa nilikuwa nawaza ....nikipata pesa ntakuwa nawapa maskini

Kumbe ulikuwa utoto ....now nna pesa ila nikiombwa hata buku nachukia kama mashabiki wa Simba....wanavyochukia namba 5

😂😂
Umaskini unaanzia Rohoni, kisha nafsini alafu Akilini. Nje ni matokeo tuu😊😊.

Kilichokuwa kinakusumbua ni ubinafsi na sasa kinajitokeza waziwazi.
 
Hata Mimi nilivyokuwa mdogo ......huko kijijini kwenye umakini mkubwa nilikuwa nawaza ....nikipata pesa ntakuwa nawapa maskini

Kumbe ulikuwa utoto ....now nna pesa ila nikiombwa hata buku nachukia kama mashabiki wa Simba....wanavyochukia namba 5
Utopolo 3 bila

Sent from my Infinix X6816 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom