Mtazamo wangu juu ya suala la Tanzania kujiandaa kuwafanya watu wake kuwa raia wa Dunia "Global citizen"

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,564
3,472
Tanzania inatazamia kuhakikisha raia wake wanatoka nje ya boksi na kushiriki kikamilifu bila kujifungia mipaka juu ya ustawi wa Dunia, yaani Raia wa Dunia.

Kupitia jukwaa hili nimetamani sana kutoa mtazamo wangu ambao unaweza pia kuwa ushauri. Lengo ni kuhakikisha ushiriki wetu kama Taifa hautakuwa wa kupoteza au kufifisha utambulisho wetu. Tukumbuke kipindi tunataka kujitanua kiuraia jamii inalia kuwa miiko yake imeporomoka kutokana na ukasumba na kuiga.

Nadhani kabla ya kukimbila kwa kasi kuwa kuwa raia wa Dunia tukimbilie kwa kasi zaidi kuwa raia wa ndani "local citizen" Kwa kuyaishi maadili na miiko yetu ambayo ndiyo utambulisho wetu Ili tunapoingia kwenye uraia wa Dunia tuingie tukiwa tuna alama yetu.

Msisitizo wangu upo zaidi kwenye dhana ya kulinda vya ndani kwanza (kwa muktadha huu naomba nitumie neno "Glocalization "ambalo linaunganisha maneno "global" na "local." Linahusu mchakato wa kuzingatia mambo ya kimataifa au ya ulimwengu wakati wa kutekeleza au kutengeneza kitu au huduma kwenye ngazi ya kikanda au ya ndani, ili kukidhi mahitaji ya eneo husika kulingana na tamaduni, mahitaji, au mazingira ya mahali hapo. Ni aina ya ushirikiano kati ya mambo ya ulimwengu na yale ya kienyeji.
 
Hatuwezi kuwa na Global citizen wakati mpaka sasa hati za kusafiria ni anasa kwetu na si haki ya kila mtanzania.
Hatuwezi kuwa Global citizen mpaka tutakapo acha kushanga na kujiona kama sisi Tanzania ndio wa lengwa katika suala la kufuta visa kwa nchi zote za africa liliofanywa na Kenya.
Vivyo hivyo serekali yetu nadhani ifikie hatua kama wanazochukua sasa hivi za kutafuta masoko ya ajira kwa watanzania kwenda na si kuweka vikwazo kwa mtu anae taka kutoka kama ilivyokua nyuma.
Sanjari na yote nadhani ni wakati muafaka wa shule zetu za msingi za serekali kutumia kingereza kama nyenzo ya ufundishaji ili kuwaanda watoto vizuri na lugha hii ya kimataifa.
 
Back
Top Bottom