Mtazamo wa jamii kuhusu ushoga kunaupigia chapuo pengine bila kujua

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,530
27,064
Mabibi na Mabwana!

Siku za nyuma kidogo, kulikuwa na wimbi la kuona kila mtu mwenye mafanikio ni Freemason. Hii ilienda kisha ikapotea, sina uhakika ilipotelea wapi ila siku hizi sio habari tena.

Sijui ndo agenda ilishatimilika au ilishakufa!

Kwa sasa upepo umegeuka kwa kasi ya kimbunga, kila mtu maarufu na mwenye mafanikio kwenye tasnia anahusishwa na vitendo vya kishoga.

Stori zimekuwa nyingi na orodha ni ndefu, kuanzia hapa Bongo hadi huko duniani. Utasikia fulani na fulani [wa kiume] usiwaone vile, 'wanaliwa' na kibopa fulani.

Kuendelea kuhusisha mafanikio na vitendo vya hovyo, inaweza kupotosha jamii yetu na kuaminisha kuwa ili 'utoboe' ni lazima 'uliwe'.

Ama kwamba kuliwa ni njia rahisi ya kutoboa, kitu ambacho sio sahihi.

Vijana tufanye kazi, na tuoneshe watu kazi tunazofanya. hii itatujengea heshima na kupigiwa mfano kwenye jamii zetu.

Ncha Kali.
 
Inawezekana mambo wanayofikiria zaidi vijana au hata raia wengi wa bongo ni mpira, dini/ushirikina/freemason na mahusiano ya watu
 
Hii dunia ina mambo mengi sana. Kila kitu kinachopingwa hapa duniani kinapata nguvu kubwa.

Umaarufu wa kitimoto unatokana na kupingwa kwake na dini ya kiislamu na baadhi ya madhehebu ya Kikristo mfano Wasabato.

Madawa ya kulevya ,kupingwa kwake na matokeo tunayaona.

Ushoga sasa ndiyo balaa.
 
Hiyo ni kweli.

Watu wengi wanawaza huo uchafu.

Na ukiona mtu anaongelea ushoga sana jua anajihusisha nao au anakaribia kujihusisha na huo ushoga.

Ni jambo la psychology tu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom