SoC02 Mtazamo usio na tija, maumivu yake ni majuto

Stories of Change - 2022 Competition

ReTHMI

Senior Member
Jul 17, 2022
181
318
Nilikua nasoma kitabu, nikakuta sehemu muandishi anasema, mwanajeshi anaenda vitani sio kwa ajili ya kuua adui bali kwaajili ya kufia nchi yake. Likanijia wazo la ni kwanini mwanajeshi anaapa kufia nchi yake na sio kuishi kwaajili ya nchi yake (to survive for his/her country). Na je akifa vitani bila kuisaidia nchi yake kushinda atakua amesaidia nini?, lakini akipambana kuepuka kifo huenda akaisaidia nchi yake, ni kwanini kufa kuwe kwa muhimu kuliko kuishi (survive).

Nikagundua kumbe watu wengi tunawaza hasi (negative) kuliko chanya (positive). Tumezaliwa na tunaishi katika jamii ambayo imejengewa hofu kuliko ujasiri, na tabia hii inaendelea kurithishwa kizazi hadi kizazi. Na ndicho kinachopelekea wazazi wengi kuamini kwamba shule ndiyo itakayomkomboa mtoto wake. Kwamba ampeleke mtoto wake shule afaulu vizuri baadae apate kazi nzuri. Mtoto akifaulu shuleni basi mzazi anaamini ndiye atakaekuja kua na maisha mazuri baadae, pia mtoto akifeli shuleni basi anaamini na kwenye maisha hatakua vizuri.

Lakini sasa mawazo hasi yanayopelekea wazazi kushindwa kuwapa ujasiri watoto wao wa kupambana na maisha bila kutegemea kigezo cha elimu. Kitu ambacho sicho kabisa, kwenye dunia ya miaka hii iliyojaa ukosefu wa ajira kwa wahitimu kila kona tunaona wanaofanya vizuri kwenye maisha ni wale ambao hawakusoma sana. Mtoto kwakua amemezeshwa kusoma sana ndio atafanikiwa kwenye maisha, basi anapambana kusomea chochote kwakua anajua ataajiriwa. Mwisho wa siku mtoto anafaulu vizuri ila asipoajiriwa anashindwa kupambana mtaani kutokana na alichomezeshwa tokea utotoni.

Ukiangalia pia kwenye upande wa kujiajiri kwa kufungua biashara, kuwekeza kwenye kilimo au ufugaji watu tunakatishana tamaa. Inafikia hatua ni bora ufanye bila kuomba ushauri, kwasababu ukiomba tu ushauri ni mwendo wa kukatishwa tamaa tu. Wanaotia moyo ni wachache sana, unakuta mtu anaomba ushauri mtandaoni kuhusiana na biashara fulani, mwenzake anajibu “ukifanikiwa na hiyo biashara uniite mbwa nimekaa pale”

Untitled.png

Picha 1: ikionyesha baadhi ya maoni ya watu mtandaoni pindi watu wanapoomba msaada wa ujasiriamali

Unabaki kujiuliza kwa nini asifanikiwe kwa hiyo biashara unakosa majibu. Kwakua hata aliyejibu hivyo hajatoa sababu yoyote ya msingi, huenda hata hiyo biashara hajawahi kujaribu.

Nini kifanyike?

1. Toa sababu ya msingi unapopinga kitu fulani.
Mtu anapoomba ushauri usiishie kusema tu “huwezi kufanikiwa kwa hicho kitu”. Toa sababu ni kwanini useme hivyo, labda ulishawahi kufanya ukashindwa kufanikiwa na ilikuaje. Hii itamsaidia muomba ushauri hata kama akifanya hicho kitu ajue ni tahadhari gani achukue ili asipite njia uliyopita wewe. Ikishindikana kabisa kama huna sababu ya msingi ni bora kukaa kimya kuliko kumfanya mtu akate tamaa ya anachotaka kukifanya.

2. Usikariri maisha
Hapa namaanisha usione kwakua mimi nilipata hasara kwenye jambo hili basi kila mtu atapata hasara. Huenda kuna sehemu uliyumba kidogo. Kwaiyo ukimfungukia mwingine ni kwa namna gani ulipata hasara huenda akabaini sehemu ulipoyumba na yeye akapanyoosha na akafanikiwa. Pia kwa upande wa wazazi wasikariri kwakua mtoto wa fulani alifanikiwa kupitia elimu basi na mtoto wao atafanikiwa kupitia hukohuko, La hasha! Kuna njia nyingi za kufanikiwa kimaisha. Huenda huo mchezo anaomkataza mwanaye kucheza (mpira, kuogelea, riadha n.k) ndiko alikopangiwa mwanaye kufanikiwa. Yeye anabaki kumlazimisha kusoma bila kujua anatengeneza ‘jobless’ wa baadae.

3. Matamanio ya ushindi (mafanikio) yazidi hofu ya kushindwa
Kila unapoamua kufanya jambo tamani sana kufanikiwa kuliko kuhofia kushindwa. Ikimbukwe tu kua, ‘hofu ni ishara ya kushindwa hata kama ni kwenye hatua za mwisho za ushindi’. Ukiwa vitani unakaribia kushinda lakini ghafla jeshi lenu likapata hofu ya kushindwa na jeshi pinzani likatambua hilo, nakuhakikishia ni lazima mpigike tu. Wakati mwingine tunajiuliza huyu mtu alikua na pesa sana imekuaje amefilisika. Jibu rahisi ni kuna wakati fulani alipitia misukosuko midogo akaingiwa na hofu ya kufilisika. Kama aliweza kufanikiwa kwa njia halali iweje ashindwe kuzuia kufilisika? Ni kwa sababu ya hofu ya kufilisika. Ukiwa na hofu ya kushindwa utajikuta unafanya jitihada zisizo za lazima kuzuia kushindwa na kuacha kufanya jitihada za kujiongezea faida zaidi.

4. Usikate tamaa
Ni watu wachache sana, naweza nikasema ni chini ya 10% wanaanza kufanya shughuli fulani ya kumuingizia kipato na akafanikiwa moja kwa moja bila misukosuko. Kwaiyo ukipata hasara usikate tamaa, tafuta kilichokukwamisha, ukikigundua basi sahihisha makosa kisha endelea na safari. Ukiwa mtu wa kukata tamaa basi kila siku utakua mtu wa kuanzisha kitu kipya ila baada ya muda mfupi kinakufa.

5. Fanya kile unachokipenda na sio kwasababu umesikia kinalipa.
Mwingine anapenda kufanya biashara ila kwakua amesikia ufugaji wa kuku unalipa basi atakimbilia kwenye kufuga kuku. Mwisho wa siku kuku wanakufa kwa magonjwa anaishia kusema ufugaji wa kuku haulipi. Unapofanya kitu unachokipenda zaidi basi hata hamu au nia ya kujifunza zaidi inaongezeka. Hii inakusaidia kuepukana na matatizo mengi yasababishwayo na uzembe wa kukosa ujuzi kidogo tu.

Natamani niandike mengi, ila ngoja nimalizie kwa kusema, tamaa ya kufanikiwa kwa haraka isitufanye tuone kila kitu hakilipi. Tusitake kuotesha mti leo na kesho tule matunda yake. Lazima tuumwagilie, tuupalilie, tuweke mbolea huku tukiendelea kusubiria ukue na kutoa matunda. Tamaa za utajiri wa haraka inawamaliza vijana wengi kwa kufuata njia zisizosahihi. Mwisho wa siku ni majuto na vilio, wengi wanaishia kwa vifo vya majuto, wachache gerezani.

Mwisho tukumbuke tu, hofu ni ishara ya kushindwa hata kama ni kwenye hatua za mwisho za ushindi.

Ondoa hofu, vaa moyo wa ujasiri/matamanio ya ushindi, fanya kile ambacho unahofia kushindwa ila unahisi pana faida/mafanikio🙂.​
 
Nilikua nasoma kitabu, nikakuta sehemu mwandishi anasema, mwanajeshi anaenda vitani sio kwa ajili ya kuua adui bali kwaajili ya kufia nchi yake. Likanijia wazo la ni kwanini mwanajeshi anaapa kufia nchi yake na sio kuishi kwaajili ya nchi yake (to survive for his/her country). Na je akifa vitani bila kuisaidia nchi yake kushinda atakua amesaidia nini?, lakini akipambana kuepuka kifo huenda akaisaidia nchi yake, ni kwanini kufa kuwe kwa muhimu kuliko kuishi (survive).

Nikagundua kumbe watu wengi tunawaza hasi (negative) kuliko chanya (positive). Tumezaliwa na tunaishi katika jamii ambayo imejengewa hofu kuliko ujasiri, na tabia hii inaendelea kurithishwa kizazi hadi kizazi. Na ndicho kinachopelekea wazazi wengi kuamini kwamba shule ndiyo itakayomkomboa mtoto wake. Kwamba ampeleke mtoto wake shule afaulu vizuri baadaye apate kazi nzuri. Mtoto akifaulu shuleni basi mzazi anaamini ndiye atakaekuja kua na maisha mazuri baadae, pia mtoto akifeli shuleni basi anaamini na kwenye maisha hatakua vizuri.

Lakini sasa mawazo hasi yanayopelekea wazazi kushindwa kuwapa ujasiri watoto wao wa kupambana na maisha bila kutegemea kigezo cha elimu. Kitu ambacho sicho kabisa, kwenye dunia ya miaka hii iliyojaa ukosefu wa ajira kwa wahitimu kila kona tunaona wanaofanya vizuri kwenye maisha ni wale ambao hawakusoma sana. Mtoto kwakua amemezeshwa kusoma sana ndio atafanikiwa kwenye maisha, basi anapambana kusomea chochote kwakua anajua ataajiriwa. Mwisho wa siku mtoto anafaulu vizuri ila asipoajiriwa anashindwa kupambana mtaani kutokana na alichomezeshwa tokea utotoni.

Ukiangalia pia kwenye upande wa kujiajiri kwa kufungua biashara, kuwekeza kwenye kilimo au ufugaji watu tunakatishana tamaa. Yani inafikia hatua ni bora ufanye bila kuomba ushauri, kwasababu ukiomba tu ushauri ni mwendo wa kukatishwa tamaa tu. Wanaotia moyo ni wachache sana, unakuta mtu anaomba ushauri mtandaoni kuhusiana na biashara fulani, mwenzake anajibu “ukifanikiwa na hiyo biashara uniite mbwa nimekaa pale”

View attachment 2298093
Picha 1: ikionyesha baadhi ya maoni ya watu mtandaoni pindi watu wanapoomba msaada wa ujasiriamali

Unabaki kujiuliza kwa nini asifanikiwe kwa hiyo biashara unakosa majibu. Kwakua hata aliyejibu hivyo hajatoa sababu yoyote ya msingi, huenda hata hiyo biashara hajawahi kujaribu.

Nini kifanyike?

1. Toa sababu ya msingi unapopinga kitu fulani.

Mtu anapoomba ushauri usiishie kusema tu “huwezi kufanikiwa kwa hicho kitu”. Toa sababu ni kwanini useme hivyo, labda ulishawahi kufanya ukashindwa kufanikiwa na ilikuaje. Hii itamsaidia muomba ushauri hata kama akifanya hicho kitu ajue ni tahadhari gani achukue ili asipite njia uliyopita wewe. Ikishindikana kabisa kama huna sababu ya msingi ni bora kukaa kimya kuliko kumfanya mtu akate tamaa ya anachotaka kukifanya.

2. Usikariri maisha.

Hapa namaanisha usione kwakua mimi nilipata hasara kwenye jambo hili basi kila mtu atapata hasara. Huenda kuna sehemu uliyumba kidogo. Kwaiyo ukimfungukia mwingine ni kwa namna gani ulipata hasara huenda akabaini sehemu uliyoyumba na yeye akapanyoosha na akafanikiwa. Pia kwa upande wa wazazi wasikariri kwakua mtoto wa fulani alifanikiwa kupitia elimu basi na mtoto wao atafanikiwa kupitia hukohuko, La hasha! Kuna nyia nyingi za kufanikiwa kimaisha. Huenda huo mchezo anaomkataza mwanaye kucheza (mpira, kuogelea, riadha n.k) ndiko alikopangiwa mwanaye kufanikiwa. Yeye anabaki kumlazimisha kusoma bila kujua anatengeneza ‘jobless’ wa baadae.

3. Matamanio ya ushindi (mafanikio) yazidi hofu ya kushindwa.

Kila unapoamua kufanya jambo tamani sana kufanikiwa kuliko kuhofia kushindwa. Ikimbukwe tu kua, ‘hofu ni ishara ya kushindwa hata kama ni kwenye hatua za mwisho za ushindi’. Ukiwa vitani unakaribia kushinda lakini ghafla jeshi lenu likapata hofu ya kushindwa na jeshi pinzani likatambua hilo, nakuhakikishia ni lazima mpigike tu. Wakati mwingine tunajiuliza huyu mtu alikua na pesa sana imekuaje amefilisika. Jibu rahisi ni kuna wakati fulani alipitia misukosuko midogo akaingiwa na hofu ya kufilisika. Kama aliweza kufanikiwa kwa njia halali iweje ashindwe kuzuia kufilisika? Ni kwa sababu ya hofu ya kufilisika. Ukiwa na hofu ya kushindwa utajikuta unafanya jitihada zisizo za lazima kuzuia kushindwa na kuacha kufanya jitihada za kujiongezea faida zaidi.

4. Usikate tamaa

Ni watu wachache sana, naweza nikasema ni chini ya 10% wanaanza kufanya shughuli fulani ya kumuingizia kipato na akafanikiwa moja kwa moja bila misukosuko. Kwaiyo ukipata hasara usikate tamaa, tafuta kilichokukwamisha, ukikigundua basi sahihisha makosa kisha endelea na safari. Ukiwa mtu wa kukata tamaa basi kila siku utakua mtu wa kuanzisha kitu kipya ila baada ya muda mfupi kinakufa.

5. Fanya kile unachokipenda na sio kwasababu umesikia kinalipa.

Mwingine anapenda kufanya biashara ila kwakua amesikia ufugaji wa kuku unalipa basi atakimbilia kwenye kufuga kuku. Mwisho wa siku kuku wanakufa kwa magonjwa anaishia kusema ufugaji wa kuku haulipi. Unapofanya kitu unachokipenda zaidi basi hata hamu au nia ya kujifunza zaidi inaongezeka. Hii inakusaidia kuepukana na matatizo mengi yasababishwayo na uzembe wa kukosa ujuzi kidogo tu.

Natamani niandike mengi, ila ngoja nimalizie kwa kusema, tamaa ya kufanikiwa kwa haraka isitufanye tuone kila kitu hakilipi. Tusitake kuotesha mti leo na kesho tule matunda yake. Lazima tuumwagilie, tuupalilie, tuweke mbolea huku tukiendelea kusubiria ukue na kutoa matunda. Tamaa za utajiri wa haraka unawamaliza vijana wengi kwa kufuata njia zisizosahihi. Mwisho wa siku ni majuto na vilio, wengi wanaishia kwa vifo vya majuto, wachache gerezani.

Mwisho tukumbuke tu, hofu ni ishara ya kushindwa hata kama ni kwenye hatua za mwisho za ushindi.

Ondoa hofu, vaa moyo wa ujasiri/matamanio ya ushindi, fanya kile ambacho unahofia kushindwa ila unahisi pana faida/mafanikio🙂.​
Hili limekua tatizo kubwa sana mkuu
 
Nilikua nasoma kitabu, nikakuta sehemu mwandishi anasema, mwanajeshi anaenda vitani sio kwa ajili ya kuua adui bali kwaajili ya kufia nchi yake. Likanijia wazo la ni kwanini mwanajeshi anaapa kufia nchi yake na sio kuishi kwaajili ya nchi yake (to survive for his/her country). Na je akifa vitani bila kuisaidia nchi yake kushinda atakua amesaidia nini?, lakini akipambana kuepuka kifo huenda akaisaidia nchi yake, ni kwanini kufa kuwe kwa muhimu kuliko kuishi (survive).

Nikagundua kumbe watu wengi tunawaza hasi (negative) kuliko chanya (positive). Tumezaliwa na tunaishi katika jamii ambayo imejengewa hofu kuliko ujasiri, na tabia hii inaendelea kurithishwa kizazi hadi kizazi. Na ndicho kinachopelekea wazazi wengi kuamini kwamba shule ndiyo itakayomkomboa mtoto wake. Kwamba ampeleke mtoto wake shule afaulu vizuri baadaye apate kazi nzuri. Mtoto akifaulu shuleni basi mzazi anaamini ndiye atakaekuja kua na maisha mazuri baadae, pia mtoto akifeli shuleni basi anaamini na kwenye maisha hatakua vizuri.

Lakini sasa mawazo hasi yanayopelekea wazazi kushindwa kuwapa ujasiri watoto wao wa kupambana na maisha bila kutegemea kigezo cha elimu. Kitu ambacho sicho kabisa, kwenye dunia ya miaka hii iliyojaa ukosefu wa ajira kwa wahitimu kila kona tunaona wanaofanya vizuri kwenye maisha ni wale ambao hawakusoma sana. Mtoto kwakua amemezeshwa kusoma sana ndio atafanikiwa kwenye maisha, basi anapambana kusomea chochote kwakua anajua ataajiriwa. Mwisho wa siku mtoto anafaulu vizuri ila asipoajiriwa anashindwa kupambana mtaani kutokana na alichomezeshwa tokea utotoni.

Ukiangalia pia kwenye upande wa kujiajiri kwa kufungua biashara, kuwekeza kwenye kilimo au ufugaji watu tunakatishana tamaa. Yani inafikia hatua ni bora ufanye bila kuomba ushauri, kwasababu ukiomba tu ushauri ni mwendo wa kukatishwa tamaa tu. Wanaotia moyo ni wachache sana, unakuta mtu anaomba ushauri mtandaoni kuhusiana na biashara fulani, mwenzake anajibu “ukifanikiwa na hiyo biashara uniite mbwa nimekaa pale”

View attachment 2298093
Picha 1: ikionyesha baadhi ya maoni ya watu mtandaoni pindi watu wanapoomba msaada wa ujasiriamali

Unabaki kujiuliza kwa nini asifanikiwe kwa hiyo biashara unakosa majibu. Kwakua hata aliyejibu hivyo hajatoa sababu yoyote ya msingi, huenda hata hiyo biashara hajawahi kujaribu.

Nini kifanyike?

1. Toa sababu ya msingi unapopinga kitu fulani.

Mtu anapoomba ushauri usiishie kusema tu “huwezi kufanikiwa kwa hicho kitu”. Toa sababu ni kwanini useme hivyo, labda ulishawahi kufanya ukashindwa kufanikiwa na ilikuaje. Hii itamsaidia muomba ushauri hata kama akifanya hicho kitu ajue ni tahadhari gani achukue ili asipite njia uliyopita wewe. Ikishindikana kabisa kama huna sababu ya msingi ni bora kukaa kimya kuliko kumfanya mtu akate tamaa ya anachotaka kukifanya.

2. Usikariri maisha.

Hapa namaanisha usione kwakua mimi nilipata hasara kwenye jambo hili basi kila mtu atapata hasara. Huenda kuna sehemu uliyumba kidogo. Kwaiyo ukimfungukia mwingine ni kwa namna gani ulipata hasara huenda akabaini sehemu ulipoyumba na yeye akapanyoosha na akafanikiwa. Pia kwa upande wa wazazi wasikariri kwakua mtoto wa fulani alifanikiwa kupitia elimu basi na mtoto wao atafanikiwa kupitia hukohuko, La hasha! Kuna njia nyingi za kufanikiwa kimaisha. Huenda huo mchezo anaomkataza mwanaye kucheza (mpira, kuogelea, riadha n.k) ndiko alikopangiwa mwanaye kufanikiwa. Yeye anabaki kumlazimisha kusoma bila kujua anatengeneza ‘jobless’ wa baadae.

3. Matamanio ya ushindi (mafanikio) yazidi hofu ya kushindwa.

Kila unapoamua kufanya jambo tamani sana kufanikiwa kuliko kuhofia kushindwa. Ikimbukwe tu kua, ‘hofu ni ishara ya kushindwa hata kama ni kwenye hatua za mwisho za ushindi’. Ukiwa vitani unakaribia kushinda lakini ghafla jeshi lenu likapata hofu ya kushindwa na jeshi pinzani likatambua hilo, nakuhakikishia ni lazima mpigike tu. Wakati mwingine tunajiuliza huyu mtu alikua na pesa sana imekuaje amefilisika. Jibu rahisi ni kuna wakati fulani alipitia misukosuko midogo akaingiwa na hofu ya kufilisika. Kama aliweza kufanikiwa kwa njia halali iweje ashindwe kuzuia kufilisika? Ni kwa sababu ya hofu ya kufilisika. Ukiwa na hofu ya kushindwa utajikuta unafanya jitihada zisizo za lazima kuzuia kushindwa na kuacha kufanya jitihada za kujiongezea faida zaidi.

4. Usikate tamaa

Ni watu wachache sana, naweza nikasema ni chini ya 10% wanaanza kufanya shughuli fulani ya kumuingizia kipato na akafanikiwa moja kwa moja bila misukosuko. Kwaiyo ukipata hasara usikate tamaa, tafuta kilichokukwamisha, ukikigundua basi sahihisha makosa kisha endelea na safari. Ukiwa mtu wa kukata tamaa basi kila siku utakua mtu wa kuanzisha kitu kipya ila baada ya muda mfupi kinakufa.

5. Fanya kile unachokipenda na sio kwasababu umesikia kinalipa.

Mwingine anapenda kufanya biashara ila kwakua amesikia ufugaji wa kuku unalipa basi atakimbilia kwenye kufuga kuku. Mwisho wa siku kuku wanakufa kwa magonjwa anaishia kusema ufugaji wa kuku haulipi. Unapofanya kitu unachokipenda zaidi basi hata hamu au nia ya kujifunza zaidi inaongezeka. Hii inakusaidia kuepukana na matatizo mengi yasababishwayo na uzembe wa kukosa ujuzi kidogo tu.

Natamani niandike mengi, ila ngoja nimalizie kwa kusema, tamaa ya kufanikiwa kwa haraka isitufanye tuone kila kitu hakilipi. Tusitake kuotesha mti leo na kesho tule matunda yake. Lazima tuumwagilie, tuupalilie, tuweke mbolea huku tukiendelea kusubiria ukue na kutoa matunda. Tamaa za utajiri wa haraka inawamaliza vijana wengi kwa kufuata njia zisizosahihi. Mwisho wa siku ni majuto na vilio, wengi wanaishia kwa vifo vya majuto, wachache gerezani.

Mwisho tukumbuke tu, hofu ni ishara ya kushindwa hata kama ni kwenye hatua za mwisho za ushindi.

Ondoa hofu, vaa moyo wa ujasiri/matamanio ya ushindi, fanya kile ambacho unahofia kushindwa ila unahisi pana faida/mafanikio🙂.​
Wanaema ukitaka kufika haraka nenda mwenyewe ila ukitaka kufika mbali nenda na mwenza. Ila tatizo ukishirikisha wengine ili ufike mbali wanakatisha sana tamaa mpaka inafikia hatua ni bora kwenda mwenyewe tu
 
Kweli kabisa, inabidi mtu kutolea maelezo kwanini unapinga au unaunga mkono kitu fulani ili imsaidie anayehitaji ushauri kupata uwanja mpana wa kufanya maamuzi sahihi.
 
Habari yako ndugu, ReTHMI.

Hongera kwa nakala nzuri yenye mawaidha na tija kwa jamii.

Kura yangu umepata!!

Nikiamini katika uchakataji wako wa mambo na uwezo wako wa fikra na ubunifu, naomba ukipendezwa, nipate mawazo yako au mapendekezo juu ya nakala ihusuyo

Ahsante!!
Shukrani, nitapita huko
 
Nilikua nasoma kitabu, nikakuta sehemu mwandishi anasema, mwanajeshi anaenda vitani sio kwa ajili ya kuua adui bali kwaajili ya kufia nchi yake. Likanijia wazo la ni kwanini mwanajeshi anaapa kufia nchi yake na sio kuishi kwaajili ya nchi yake (to survive for his/her country). Na je akifa vitani bila kuisaidia nchi yake kushinda atakua amesaidia nini?, lakini akipambana kuepuka kifo huenda akaisaidia nchi yake, ni kwanini kufa kuwe kwa muhimu kuliko kuishi (survive).

Nikagundua kumbe watu wengi tunawaza hasi (negative) kuliko chanya (positive). Tumezaliwa na tunaishi katika jamii ambayo imejengewa hofu kuliko ujasiri, na tabia hii inaendelea kurithishwa kizazi hadi kizazi. Na ndicho kinachopelekea wazazi wengi kuamini kwamba shule ndiyo itakayomkomboa mtoto wake. Kwamba ampeleke mtoto wake shule afaulu vizuri baadaye apate kazi nzuri. Mtoto akifaulu shuleni basi mzazi anaamini ndiye atakaekuja kua na maisha mazuri baadae, pia mtoto akifeli shuleni basi anaamini na kwenye maisha hatakua vizuri.

Lakini sasa mawazo hasi yanayopelekea wazazi kushindwa kuwapa ujasiri watoto wao wa kupambana na maisha bila kutegemea kigezo cha elimu. Kitu ambacho sicho kabisa, kwenye dunia ya miaka hii iliyojaa ukosefu wa ajira kwa wahitimu kila kona tunaona wanaofanya vizuri kwenye maisha ni wale ambao hawakusoma sana. Mtoto kwakua amemezeshwa kusoma sana ndio atafanikiwa kwenye maisha, basi anapambana kusomea chochote kwakua anajua ataajiriwa. Mwisho wa siku mtoto anafaulu vizuri ila asipoajiriwa anashindwa kupambana mtaani kutokana na alichomezeshwa tokea utotoni.

Ukiangalia pia kwenye upande wa kujiajiri kwa kufungua biashara, kuwekeza kwenye kilimo au ufugaji watu tunakatishana tamaa. Yani inafikia hatua ni bora ufanye bila kuomba ushauri, kwasababu ukiomba tu ushauri ni mwendo wa kukatishwa tamaa tu. Wanaotia moyo ni wachache sana, unakuta mtu anaomba ushauri mtandaoni kuhusiana na biashara fulani, mwenzake anajibu “ukifanikiwa na hiyo biashara uniite mbwa nimekaa pale”

View attachment 2298093
Picha 1: ikionyesha baadhi ya maoni ya watu mtandaoni pindi watu wanapoomba msaada wa ujasiriamali

Unabaki kujiuliza kwa nini asifanikiwe kwa hiyo biashara unakosa majibu. Kwakua hata aliyejibu hivyo hajatoa sababu yoyote ya msingi, huenda hata hiyo biashara hajawahi kujaribu.

Nini kifanyike?

1. Toa sababu ya msingi unapopinga kitu fulani.

Mtu anapoomba ushauri usiishie kusema tu “huwezi kufanikiwa kwa hicho kitu”. Toa sababu ni kwanini useme hivyo, labda ulishawahi kufanya ukashindwa kufanikiwa na ilikuaje. Hii itamsaidia muomba ushauri hata kama akifanya hicho kitu ajue ni tahadhari gani achukue ili asipite njia uliyopita wewe. Ikishindikana kabisa kama huna sababu ya msingi ni bora kukaa kimya kuliko kumfanya mtu akate tamaa ya anachotaka kukifanya.

2. Usikariri maisha.

Hapa namaanisha usione kwakua mimi nilipata hasara kwenye jambo hili basi kila mtu atapata hasara. Huenda kuna sehemu uliyumba kidogo. Kwaiyo ukimfungukia mwingine ni kwa namna gani ulipata hasara huenda akabaini sehemu ulipoyumba na yeye akapanyoosha na akafanikiwa. Pia kwa upande wa wazazi wasikariri kwakua mtoto wa fulani alifanikiwa kupitia elimu basi na mtoto wao atafanikiwa kupitia hukohuko, La hasha! Kuna njia nyingi za kufanikiwa kimaisha. Huenda huo mchezo anaomkataza mwanaye kucheza (mpira, kuogelea, riadha n.k) ndiko alikopangiwa mwanaye kufanikiwa. Yeye anabaki kumlazimisha kusoma bila kujua anatengeneza ‘jobless’ wa baadae.

3. Matamanio ya ushindi (mafanikio) yazidi hofu ya kushindwa.

Kila unapoamua kufanya jambo tamani sana kufanikiwa kuliko kuhofia kushindwa. Ikimbukwe tu kua, ‘hofu ni ishara ya kushindwa hata kama ni kwenye hatua za mwisho za ushindi’. Ukiwa vitani unakaribia kushinda lakini ghafla jeshi lenu likapata hofu ya kushindwa na jeshi pinzani likatambua hilo, nakuhakikishia ni lazima mpigike tu. Wakati mwingine tunajiuliza huyu mtu alikua na pesa sana imekuaje amefilisika. Jibu rahisi ni kuna wakati fulani alipitia misukosuko midogo akaingiwa na hofu ya kufilisika. Kama aliweza kufanikiwa kwa njia halali iweje ashindwe kuzuia kufilisika? Ni kwa sababu ya hofu ya kufilisika. Ukiwa na hofu ya kushindwa utajikuta unafanya jitihada zisizo za lazima kuzuia kushindwa na kuacha kufanya jitihada za kujiongezea faida zaidi.

4. Usikate tamaa

Ni watu wachache sana, naweza nikasema ni chini ya 10% wanaanza kufanya shughuli fulani ya kumuingizia kipato na akafanikiwa moja kwa moja bila misukosuko. Kwaiyo ukipata hasara usikate tamaa, tafuta kilichokukwamisha, ukikigundua basi sahihisha makosa kisha endelea na safari. Ukiwa mtu wa kukata tamaa basi kila siku utakua mtu wa kuanzisha kitu kipya ila baada ya muda mfupi kinakufa.

5. Fanya kile unachokipenda na sio kwasababu umesikia kinalipa.

Mwingine anapenda kufanya biashara ila kwakua amesikia ufugaji wa kuku unalipa basi atakimbilia kwenye kufuga kuku. Mwisho wa siku kuku wanakufa kwa magonjwa anaishia kusema ufugaji wa kuku haulipi. Unapofanya kitu unachokipenda zaidi basi hata hamu au nia ya kujifunza zaidi inaongezeka. Hii inakusaidia kuepukana na matatizo mengi yasababishwayo na uzembe wa kukosa ujuzi kidogo tu.

Natamani niandike mengi, ila ngoja nimalizie kwa kusema, tamaa ya kufanikiwa kwa haraka isitufanye tuone kila kitu hakilipi. Tusitake kuotesha mti leo na kesho tule matunda yake. Lazima tuumwagilie, tuupalilie, tuweke mbolea huku tukiendelea kusubiria ukue na kutoa matunda. Tamaa za utajiri wa haraka inawamaliza vijana wengi kwa kufuata njia zisizosahihi. Mwisho wa siku ni majuto na vilio, wengi wanaishia kwa vifo vya majuto, wachache gerezani.

Mwisho tukumbuke tu, hofu ni ishara ya kushindwa hata kama ni kwenye hatua za mwisho za ushindi.

Ondoa hofu, vaa moyo wa ujasiri/matamanio ya ushindi, fanya kile ambacho unahofia kushindwa ila unahisi pana faida/mafanikio.​
Shukrani sana kwa elimu/ ushauri mzuri
Kwa upande wangu nawaza tuchulie mitandao kama jamii zingine mfano unaposikia jamii ya wachanga, wasukuma au wamasai ukienda kuishi na watu wajamii hizo kuna tamaduni zao utaziishi ili uweze kuendana nao
Sasa uku mitandaoni hilo halina nguvu sana hasa kwa kizazi chetu hichi kinachotafutwa sana huku ni umaarufu ( mtu yuko tayari kukujibu vibaya ili andiko lake lipate likes na comment kibao)
 
Ni kweli kabisa, ila inabidi tubadilike kwenye hili kwa sababu mtandaoni ndipo mahali unaweza ukapata ushauri wa watu wengi kwa muda mfupi. Mitandao ikitumika vizuri itasaidia kwenye mambo mengi sana.
 
Back
Top Bottom