Mtangazaji wa Michezo Wasafi FM Maulid Kitenge, Kuzurura kote Ulaya na Marekani bado tu Kiingereza kinakutesa?

Umeniangusha mno leo ambapo hapo Studioni Kwako ulikuwa na Wageni (Wazungu) Wawili akiwemo Mjerumani Mr. Alvaro ambaye ni Mkufunzi wa Soka la Vijana na Wanawake.

Kiingereza chako cha Kumkaribisha Mjerumani Mr. Alvaro kwa Kumwambia ' Welcome Tanzania ' badala ya kusema (Kumwambia) ' Welcome to Tanzania ' kilinifikirisha zaidi na Kusikitika.

Na ulivyo Msanii (Mjanja Mjanja) Kiingereza pekee ulichokielewa haraka wakati Mgeni Mr. Alvaro anaongea ni yale maneno ya ' Show ' na ' Number One ' ila Kwingine kote ulikuwa unabung'aa bung'aa tu. Halafu mwishoni Wageni (Wazungu) hao wakati Wanaaga ukaanza Kujitutumua na kuwaambia ' Thank You ' huku ukitamka kwa nguvu kabisa.

Mtangazaji Maulid Kitenge sasa huko Ulaya na Marekani unakoenda kila mara huwa unaongea na hao Wazungu Kiswahili au Kinyamwezi cha Kwenu Tabora au Kizaramo? Umetuaibisha mno Wanamichezo leo. Sijui Boss wako Nasib Abdul (alias) Diamond Platinumz amejisikiaje na hicho Kiingereza chako Kibovu.

Nampongeza sana Mtangazaji mwana Yanga SC mwenzako Yusuf Mkule Yeye alipoona tu Wazungu wameingia Studioni hapo Wasafi FM kwa kujua Kiingereza hajui (ila anachojua tu ni Kuichukia Simba SC) akajifanya kabanwa na Tumbo la Kuhara la ghafla na kwenda Msalani (Chooni) ambapo aliposikia tu Wazungu wameondoka Studioni Tumbo lake nalo likakata na akarejea Kuendelea na Kipindi.

Ushauri wangu Kwako Mtangazaji Maulid Kitenge punguza sana Mikogo (Sifa) Kupenda Kujionyesha hasa ukiwa huko ng'ambo (Ulaya na Marekani) bali tafuta Chuo kizuri ukajifunze Kiingereza na uweze angalau Kukijua na siyo Kujichoresha kama hivi leo.

Umemuaibisha sana leo Mwanao (Binti) Shadia Kitenge ambaye nakusifia unajitahidi mno kumsomesha Shule nzuri na bora huku nae pia ni Mwerevu (ana Akili) kwani baadhi ya Walimu wake ni Marafiki zangu. Kwa Kiingereza chako hicho Kibovu sijui Binti yako Shadia leo huko aliko anajisikiaje.

Au unaweza pia ukiwa hapa nchini Tanzania ule muda ambao unautumia sana Kutafuta Habari mbaya za Simba SC au Kuichokonoa au Kuiandama basi ukautumia kwenda pale British Council Posta ukajifunze Kiingereza na hatimaye nawe pia kuwa Wordsmith kama wengine.

Na nyie Wasafi FM siku zingine mkijua mna Wageni (hasa Wazungu) muwe mnampa hicho Kipindi Mtangazaji Msomi hasa na anayeijua vyema hiyo Lugha ya Kiingereza Ahmed Abdallah au hata mkamkopa Mtani wangu wa Kihaya Bonge David Runyagira wa Kipindi chenu cha Asubuhi aweze Kukiendesha na Kuwahoji Critically hao Wazungu na siyo kama alivyokuwa akifanya Maulid Kitenge ambaye muda mwingi alikuwa akicheka cheka tu na Kukenua hovyo Minjino yake.

Naamini hatonichukia bali atanielewa.
huu mwandiko mbona kama wa Gentamycin
 
Konda msafi anasema alitamani kurudi bongo maana alichoka kuongea kiingereza kila siku.

Mimi huwa namchukia alieamua hili taifa tutumie kiswahili kama lugha ya taifa,huyo pimbi ndo aliharibu kila kitu ma.Mae zake,na endelee kupata mateso huko aliko.

Kutokujua kidhungu kumenifanya nkose mambo mengi sana.
 
Wanaojua kidhungu walijuaje, kujua lugha ni juhudi zako binafsi
 
Watu wana ma PhD na mavyeo makubwa tu hapa Tz lakini "wanabananga" kizungu, itakuwa huyo mtangazaji?
Ungana nae huyo Mtangazaji katika huo Ujuha ( Uhayawani ) wake tafadhali. Kwahiyo kama wenye Phd's na Vyeo hawajui Kiingereza ndiyo Kigezo au Tiketi ya Wewe pia kutokijua angalau hata kwa kiasi chake? Hivi inaweza Kuingia Akili Mtu kila Uchao unaenda huko ng'ambo ( Ulaya na Marekani ) halafu bado Lugha ya Kiingereza ikawa ni Kikwazo Kwako? Kuna Watu kwa hizi Hoja zenu nikiwa ninawadharau hapa JF msininunie.
 
Bongo zozo anajua kiswahili lakini huwezi kusema kuwa hakosei baadhi ya vitu akiongea.

Na kitenge pia anajua kiingereza japokuwaacanakosea.

Nyie watu mtu anapokosea juu ya lugha fulani mnasema hajui
Tulitegemea ile Mikogo yake anayoifanya hasa akiwa huko Ulaya na Marekani basi hata na Lugha yao pia anaweza Kuwa na Mikogo nayo vile vile katika Kuijua kumbe ni vice versa tu Ndugu.
 
Kama anajua kiingereza angeongea na hao wageni moja kwa moja wote tunajua aina ya mahojiano anayofanya kitenge yeye huwa ni muongeaji zaidi na kuuliza maswali zaidi ila kwa mzungu alinywea kwa sababu lugha zinagongana usimtetee
Huwa nawapenda sana na Kukutana pia na Watu ( JF Members ) Waelewa na wanaojua Kufikiri hadi Kujenga Hoja zao vizuri kama hivi Wewe Ndugu.
 
Ungana nae huyo Mtangazaji katika huo Ujuha ( Uhayawani ) wake tafadhali. Kwahiyo kama wenye Phd's na Vyeo hawajui Kiingereza ndiyo Kigezo au Tiketi ya Wewe pia kutokijua angalau hata kwa kiasi chake? Hivi inaweza Kuingia Akili Mtu kila Uchao unaenda huko ng'ambo ( Ulaya na Marekani ) halafu bado Lugha ya Kiingereza ikawa ni Kikwazo Kwako? Kuna Watu kwa hizi Hoja zenu nikiwa ninawadharau hapa JF msininunie.
Nisome taratibu tu utanielewa. Soma pia post #66 kwa maelezo zaidi.

Naogopa sana (hapa nilipo natetemeka!) kudharauliwa na wewe hapa JF mkuu!
 
Sifa kubwa ya mwandishi wa habari ni kujua lugha mbalimbali at least 2 za kimataifa.

Mojawapo ya kazi zao ni kufanya mahojiano na watu tofauti, wa mataifa tofauti.

Kama kweli amefanya hivyo ni kanjanja najua utopolo watamtetea ila ukweli utabaki kama ulivyo.
Tz waandishi wetu ingilishi inawaumiza sana, huwa najiuliza ukiacha kusoma kuna kujifunza kupitia media kama Ajazeera, BBC,Fox news etc......kama ni muangaliaji lazima ajifunze kitu.......ukitaka uone shida angalia azam tv mechi wanazorusha halafu awepo asiyejua kiswahili wakati wa intavyuuu
 
Konda msafi anasema alitamani kurudi bongo maana alichoka kuongea kiingereza kila siku.

Mimi huwa namchukia alieamua hili taifa tutumie kiswahili kama lugha ya taifa,huyo pimbi ndo aliharibu kila kitu ma.Mae zake,na endelee kupata mateso huko aliko.

Kutokujua kidhungu kumenifanya nkose mambo mengi sana.
Ni Nyerere mzee. Mageuzi ya mwaka 1968. Kale kazee kachawi
 
Back
Top Bottom