Mtangazaji wa Michezo Wasafi FM Maulid Kitenge, Kuzurura kote Ulaya na Marekani bado tu Kiingereza kinakutesa?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Umeniangusha mno leo ambapo hapo Studioni Kwako ulikuwa na Wageni (Wazungu) Wawili akiwemo Mjerumani Mr. Alvaro ambaye ni Mkufunzi wa Soka la Vijana na Wanawake.

Kiingereza chako cha Kumkaribisha Mjerumani Mr. Alvaro kwa Kumwambia ' Welcome Tanzania ' badala ya kusema (Kumwambia) ' Welcome to Tanzania ' kilinifikirisha zaidi na Kusikitika.

Na ulivyo Msanii (Mjanja Mjanja) Kiingereza pekee ulichokielewa haraka wakati Mgeni Mr. Alvaro anaongea ni yale maneno ya ' Show ' na ' Number One ' ila Kwingine kote ulikuwa unabung'aa bung'aa tu. Halafu mwishoni Wageni (Wazungu) hao wakati Wanaaga ukaanza Kujitutumua na kuwaambia ' Thank You ' huku ukitamka kwa nguvu kabisa.

Mtangazaji Maulid Kitenge sasa huko Ulaya na Marekani unakoenda kila mara huwa unaongea na hao Wazungu Kiswahili au Kinyamwezi cha Kwenu Tabora au Kizaramo? Umetuaibisha mno Wanamichezo leo. Sijui Boss wako Nasib Abdul (alias) Diamond Platinumz amejisikiaje na hicho Kiingereza chako Kibovu.

Nampongeza sana Mtangazaji mwana Yanga SC mwenzako Yusuf Mkule Yeye alipoona tu Wazungu wameingia Studioni hapo Wasafi FM kwa kujua Kiingereza hajui (ila anachojua tu ni Kuichukia Simba SC) akajifanya kabanwa na Tumbo la Kuhara la ghafla na kwenda Msalani (Chooni) ambapo aliposikia tu Wazungu wameondoka Studioni Tumbo lake nalo likakata na akarejea Kuendelea na Kipindi.

Ushauri wangu Kwako Mtangazaji Maulid Kitenge punguza sana Mikogo (Sifa) Kupenda Kujionyesha hasa ukiwa huko ng'ambo (Ulaya na Marekani) bali tafuta Chuo kizuri ukajifunze Kiingereza na uweze angalau Kukijua na siyo Kujichoresha kama hivi leo.

Umemuaibisha sana leo Mwanao (Binti) Shadia Kitenge ambaye nakusifia unajitahidi mno kumsomesha Shule nzuri na bora huku nae pia ni Mwerevu (ana Akili) kwani baadhi ya Walimu wake ni Marafiki zangu. Kwa Kiingereza chako hicho Kibovu sijui Binti yako Shadia leo huko aliko anajisikiaje.

Au unaweza pia ukiwa hapa nchini Tanzania ule muda ambao unautumia sana Kutafuta Habari mbaya za Simba SC au Kuichokonoa au Kuiandama basi ukautumia kwenda pale British Council Posta ukajifunze Kiingereza na hatimaye nawe pia kuwa Wordsmith kama wengine.

Na nyie Wasafi FM siku zingine mkijua mna Wageni (hasa Wazungu) muwe mnampa hicho Kipindi Mtangazaji Msomi hasa na anayeijua vyema hiyo Lugha ya Kiingereza Ahmed Abdallah au hata mkamkopa Mtani wangu wa Kihaya Bonge David Runyagira wa Kipindi chenu cha Asubuhi aweze Kukiendesha na Kuwahoji Critically hao Wazungu na siyo kama alivyokuwa akifanya Maulid Kitenge ambaye muda mwingi alikuwa akicheka cheka tu na Kukenua hovyo Minjino yake.

Naamini hatonichukia bali atanielewa.
 
Umeniangusha mno leo ambapo hapo Studioni Kwako ulikuwa na Wageni (Wazungu) Wawili akiwemo Mjerumani Mr. Alvaro ambaye ni Mkufunzi wa Soka la Vijana na Wanawake....
Yaani mtu kakosea kuweka "to" anaambiwa hajui kiingereza wakati neno welcome lilikuwepo ambapo kimsingi ni la kiingereza.

Au welcome ni la kiswahili?

Alafu hapa unawacheka watu hawajui kiingereza wakati hata wewe kiswahili chako tu kinakushinda kutofautisha baina ya kutojua kabisa na kukosea kidogo tu.

Mtu ambaye hajui ni yule ambae hapatii neno lolote la lugha hiyo,mfano wewe leo ukiambiwa tunga sentensi kwa kutumia lugha ya kiitaliano ukawa umejitungia maneno ambayo hayapo ukasema ni sentesi wewe sasa ndo hujui.

Mzungu akisema "naenda kuonana haza" usiseme hajui kiswahili sema kakosea tu kuweka neno "na" kwa sababu maneno yote aliyoyaongea ni ya kiiswahili kuna neno hakuliweka tu kwa makosa,na hayo makosa yapo kwaac kila mtu ambaye anazungumza lugha ambayo sio ya kwake.

Narudia HAYO MAKOSA YAPO KWA KILA MTU AMBAYE ANAZUNGUMZA LUGH AMBAYO SIO YA KWAKE.

Sasa wewe ndugu unatafuuta makosa madogo madogo ya kusahau ama kukosea mtu hajaweka "to" kitu kidogo tu hicho wakati katamka neno "welcome" ambalo ni fefu kuliko hiyo "to" ambayo umeona hajaiweka.

Hebu mpongeze kwa kutamka neno refu "welcome" na msamehje kwa kuliaacha hilo fupi la "to"

Kuandika hivi sina maana kuwa nasema hajakosea hapana,bali ninamaanisha kuwa kuna vikosa vidogo kama hivi sio vya kuanzishia uzi utakuwa una gubu.

Hao wazungu wenyewe hawajawahi kumcheka mtu anaeomgea kiingereza kwa kukosea maadamu wanamuelewa basi wanaishi na wewe hivyo hivyo, WEWE NI NANI UNAWACHEEKA WATU NA KUWAKOSOA?

Hizi ni lugha tu mzee sio unaanzisha uzi kwa mambo kama haya.
 
Dah umeongea kwa hisia kali sana zenye chuki kidogo na za kujenga kwa mbaali japo hazitamfikia mhusika lakini ningependa tu kukujulisha kuwa Lugha ya kingereza hasa cha kuongea ni tatizo kubwa sana hapa nchini sio kwa watu tu wa kawaida bali hata viongozi, wafanyabiashara na watu maarufu wengi.

Tatizo kubwa nilionalo limetokana na lugha zetu mama kutufanya kuwa wagumu sana kunyumbulika na hii lugha labda kwa baadhi ya makabila ambayo ndimi zao ni laini sana ndio kidogo wanaweza kutamba nayo kama wachaga,wakurya ,wazaramo nk lakini watu kama wasukuma,wamasai,nk lugha hii inawasumbua sana.

Kibinafsi mimi sioni tatizo kutokuijua hii lugha au kumpa mtu shida wakati anaitumia shida yangu ni kwa watu hawa wanaocheka wenzao hasa pale anapoonekana kuhangaika katika kuitumia lugha hii ni jambo la kawaida sana katika kujifunza lugha. Kwani hata ukitizama wenzetu wanaokuja huku kutoka mataifa mbali mbali hutamani sana kupata fursa ya kujifunza lugha yetu cha ajabu wao wanapokosea huonekana si kitu cha ajabu kama inavyotokea tunapokosea sisi kwenye lugha zao hasa kingereza .

So inachotakiwa sisi kufanya ni kuacha sasa huu ushamba wa kumuona mtu anakosea kuongea lugha flani na kumcheka ni jambo la kawaida sana katika kujifunza lugha ambayo siyo yako.

Mimi huwa sioni tatizo lolote kawaida tu
 
Back
Top Bottom