Mtangazaji wa Michezo Wasafi FM Maulid Kitenge, Kuzurura kote Ulaya na Marekani bado tu Kiingereza kinakutesa?

Yaani mtu kakosea kuweka "to" anaambiwa hajui kiingereza wakati neno welcome lilikuwepo ambapo kimsingi ni la kiingereza.

Au welcome ni la kiswahili?

Alafu hapa unawacheka watu hawajui kiingereza wakati hata wewe kiswahili chako tu kinakushinda kutofautisha baina ya kutojua kabisa na kukosea kidogo tu.

Mtu ambaye hajui ni yule ambae hapatii neno lolote la lugha hiyo,mfano wewe leo ukiambiwa tunga sentensi kwa kutumia lugha ya kiitaliano ukawa umejitungia maneno ambayo hayapo ukasema ni sentesi wewe sasa ndo hujui.

Mzungu akisema "naenda kuonana hamza" usiseme hajui kiswahili sema kakosea tu kuweka neno "na" kwa sababu maneno yote aliyoyaongea ni ya kiiswahili kuna neno hakuliweka tu kwa makosa,na hayo makosa yapo kwaac kila mtu ambaye anazungumza lugha ambayo sio ya kwake.

Narudia HAYO MAKOSA YAPO KWA KILA MTU AMBAYE ANAZUNGUMZA LUGH AMBAYO SIO YA KWAKE.

Sasa wewe ndugu unatafuuta makosa madogo madogo ya kusahau ama kukosea mtu hajaweka "to" kitu kidogo tu hicho wakati katamka neno "welcome" ambalo ni fefu kuliko hiyo "to" ambayo umeona hajaiweka.

Hebu mpongeze kwa kutamka neno refu "welcome" na msamehje kwa kuliaacha hilo fupi la "to"

Kuandika hivi sina maana kuwa nasema hajakosea hapana,bali ninamaanisha kuwa kuna vikosa vidogo kama hivi sio vya kuanzishia uzi utakuwa una gubu.

Hao wazungu wenyewe hawajawahi kumcheka mtu anaeomgea kiingereza kwa kukosea maadamu wanamuelewa basi wanaishi na wewe hivyo hivyo, WEWE NI NANI UNAWACHEEKA WATU NA KUWAKOSOA?

Hizi ni lugha tu mzee sio unaanzisha uzi kwa mambo kama haya.
Sawa Maulid Kitenge a.k.a Welcome Tanzania.
 
Yaonekana zile safari zake za kwenda ughaibuni kila uchwao zinakutesa sana mtoa uzi, pambana nawe uende kama ni ndoto yako ama mfuate akujuze njia zake nawe uyaishi hayo.
Kwenda Ulaya na Marekani kuwa Chakula cha Watu ndiyo Ufahari? Usinilazimishe nifunguke zaidi kisha Mke mwingine nae akafungasha kama alivyofanya wa Kwanza ile Mitaa ya Slipway Masaki mkabala na Kijiwe cha Bakhressa.
 
Dah umeongea kwa hisia kali sana zenye chuki kidogo na za kujenga kwa mbaali japo hazitamfikia mhusika lakini ningependa tu kukujulisha kuwa Lugha ya kingereza hasa cha kuongea ni tatizo kubwa sana hapa nchini sio kwa watu tu wa kawaida bali hata viongozi, wafanyabiashara na watu maarufu wengi.

Tatizo kubwa nilionalo limetokana na lugha zetu mama kutufanya kuwa wagumu sana kunyumbulika na hii lugha labda kwa baadhi ya makabila ambayo ndimi zao ni laini sana ndio kidogo wanaweza kutamba nayo kama wachaga,wakurya ,wazaramo nk lakini watu kama wasukuma,wamasai,nk lugha hii inawasumbua sana.

Kibinafsi mimi sioni tatizo kutokuijua hii lugha au kumpa mtu shida wakati anaitumia shida yangu ni kwa watu hawa wanaocheka wenzao hasa pale anapoonekana kuhangaika katika kuitumia lugha hii ni jambo la kawaida sana katika kujifunza lugha. Kwani hata ukitizama wenzetu wanaokuja huku kutoka mataifa mbali mbali hutamani sana kupata fursa ya kujifunza lugha yetu cha ajabu wao wanapokosea huonekana si kitu cha ajabu kama inavyotokea tunapokosea sisi kwenye lugha zao hasa kingereza .

So inachotakiwa sisi kufanya ni kuacha sasa huu ushamba wa kumuona mtu anakosea kuongea lugha flani na kumcheka ni jambo la kawaida sana katika kujifunza lugha ambayo siyo yako.

Mimi huwa sioni tatizo lolote kawaida tu
Mwambieni ajifunze Kiingereza Wapuuzi nyie.
 
Kwenda Ulaya na Marekani kuwa Chakula cha Watu ndiyo Ufahari? Usinilazimishe nifunguke zaidi kisha Mke mwingine nae akafungasha kama alivyofanya wa Kwanza ile Mitaa ya Slipway Masaki mkabala na Kijiwe cha Bakhressa.
Duuuuh! Kumbeeeeee!!! Jamaa ni biriani fulani hivi
FB_IMG_1612012763868.jpg
 
Hata mimi nilishangaa sana. Mzungu anawapongeza kwa kuwa kipindi kizuri cha michezo, Maulid anashindwa hata kuitikia "thank you". Imenifikirisha sana
Hamna Mtu hapo Kazi ni Sifa tu Mitandaoni na Mikogo mingi isiyo hata na Tija wala Mantiki.

Angekuwa Mtangazaji mwenye Kujua vyema Lugha ya Kiingereza kwa ule Ugeni wa Mtu kama Mr. Alvaro angalau angemuhoji Maswali ya maana ya Kimpira na Maendeleo yetu Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Ila ikawa ni tofauti na Yeye ( Maulid Kitenge ) akawa anachekacheka tu huku akifanya Upuuzi wake. Nashangaa kuona kuna Wapuuzi baadhi hapa wanaona kafanya sasa.

Nafasi kama hii angeipata Mtangazaji wangu bora wa Vipindi vya Michezo Afrika Robert Marawa sasa yupo SABC ( akitokea Metro FM Radio ) ya huko huko Afrika Kusini angeitumia vyema kwa Kuhoji ya maana ili hata aje na Exclusive Story ila siyo Bumunda lenu hili la Wasafi FM na Boss wa Kipindi hicho cha Michezo hapo.
 
Mimi niliguna nikajua nimesikia peke yangu.....
Hivi vitengo vingine inabidi wahusika wawe wanajiongezea sana hata kwa mazoezi ya mara kwa mara upande wa grammar ,pia tatizo hili huwakuta hawa ndg zetu askari traffic pale wanaposimamisha gari ya mgeni ambaye kiswahili kwake ni zero
Sifa yangu Kuu ni Kufuatilia Jambo kwa Umakini, Kulisikia vyema na Kulichambua kwa marefu na mapana yake.

Yawezekana Somo la Philosophy na hasa lile la Critical Thinking ( Logical Reasoning ) limeniathiri mno kwani napenda zaidi kufanya Observation ya Jambo ( Tukio ) fulani kisha Kulichakata zaidi Kifikra. Yeye ( Maulid Kitenge ) hapa anaweza Kuona nimemsiliba ( nimemsema ) ila kwa wenye Akili watakubaliana nami kuwa nimemsaidia kuelekea katika Kubadilika Kwake ili azidi kuwa Mahiri mno Kitasnia.
 
Back
Top Bottom