GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,646
- 109,022
Ukikutana na Mgeni hasa Mzungu au Mmarekani Mweusi halafu ukataka kufanya nae Mahojiano basi hakikisha Maswali yako yanakuwa ni mafupi mafupi na ya moja kwa moja sawa?
Muda mfupi uliopita nimekusikia Sports Extra ya Clouds FM ukitumia dakika 5 nzima Kuzunguka Kuuliza Swali la Sekunde 10 au 15 tu huku Ukichapia mno hadi Redio yenu nayo ikazima ghafla.
Kama Wakufunzi wako wa Chuo Kikuu ulichosoma ( UDOM ) kama sijakosea kama nao Walikusikiliza nina uhakika watakuwa si tu Wameumia bali watakuwa Wamekasirika mno kwa Kiingereza chako kibovu, cha Kujitafuta na cha Kubabaika.
Na uliponiacha hoi ni pale na Wewe ulipojifanya unaongea Kiingereza cha Kimarekani kwa Kuwaiga Wageni waliokuwepo Studio wakati ukikiharibu kwa Broken yako.
Nilijua nisiyejua Kiingereza Tanzania nzima ni Mimi tu GENTAMYCINE kumbe nina Mwenzangu ( Pacha wangu ) Edgar Kibwana Mchambuzi wa Mpira wa Miguu Clouds FM na Clouds Tv.
Pongezi nyingi kwa Mtani wangu wa Kiha ( kutoka Mkoani Kigoma ) Mtangazaji Prisca Kishamba ambaye Yeye kwa kujua hakijui Kiingereza ( japo anakipenda sana ) aliamua kutokuwa muuliza Maswali ya Kiingereza kwa Wageni na kukaa Kimya na hata Maswali Mawili ya Kiingereza aliyojitutumua Kuyauliza mwishoni alionekana kuwa alitumia muda mrefu Kuyakariri ( Kuyameza ) na aliyauliza kwa haraka sana utadhani kuna Mtu alikuwa anamdai Fedha hivyo anaogopa.