Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,359
- 2,787
Mtandao wa jamii forums ambao uliachiwa Toka mwaka 2006, imekua ni mtandao wa kipekee unaokutanisha vijana kujadili mambo mbalimbali kuhusu Teknolojia, Siasa, maisha, upendo nk.
Sasa katika kuendana na Mitandao ya kijamii kisasa imekua ikileta feature mbalimbali za kisasa na kwa sasa iko mbioni kutambulisha feature mpya inaitwa Regional Communities".
Feature hii itaweza kufanya mambo kadhaa;
✅ Utaweza kuunda Forums au groups za nchi, mikoa au mji fulani mfano Dsm, Mwanza,Tanga nk.
✅ Watu wa ilo Groups wataweza kujadili kuhusu biashara za Karibu, Matukio (Events), Fursa za kazi nk.
Feature hii itapatikana kwenye nchi kuanzia Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, DRC, Zambia pamoja na Zimbabwe.
💡 Faida zake
• utaweza kupata taarifa ya eneo lako moja kwa moja
• itakua rahisi kupata Wateja kama una biashara.
• inajenga jamii Halisi wa eneo fulani hivyo kupunguza matapeli mitandaoni.
Lakini mpaka sasa bado hawajatangaza itaweza kuachiwa lini ila inakuja✍️.