Msikiti wa posta na ubaguzi??

Msikiti wa posta na ubaguzi??

Huu ni Msikiti wa Shia Ithinasharia katika Itikadi hii waswahili huwezi waoma wengi kutokana kuwepo kwa tofauti ya mapokeo. Waswahili ni wachache na wengi wao husalia kwenye Msikiti wao uliopo kule Kigogo.
Hakuna ushia wa kihindi na wa kiafrika,in that case hakuna msikiti wa kihindi na wa kiafrika ,ndiyo maana ukenda msikiti wowote wa shia utaona watu mchanganyiko wakiswali,hata masunni pia wanaswali humo ingawa kuna baadhi ya watu wanajishtukia
 
Inawezekana maana uwezekano wa kubaguliwa katika misikiti yetu ya kawaida hakuna

Huyo aliingia bohora ama Shia
Sina ujuzi na bohora,lakini kwa misikiti ya shia hakuna kitu kama hicho,I'm talking out of experience
 
HUO MSIKITI UPO JILANI NA LILIPODONDOKA LILE GHOROFA...NAZANI NI MTAA WA IDRAGANDI;
ULE MSIKITI KWAKWELI WANAOSALI NI WEUPE TU; NA WALIUJENGA SPECIAL KWA AJILI YAO! RANGI NYEUSI NI MARUFUKU! NAUJUWA
Ni kweli mkuu, misikiti kama hii mbona ipo mingi tu nchini??? Ni hali ya kawaida........
 
Mimi Muafrika. "Kustaarabika" ni kuwa muarabu. Mzizi wa "ku sta arab ika ni kutaka kuwa muarabu.

Sitaki utumwa wa akili wa kutaka kuwa muarabu.

Ndiyo maana hata hizi habari za kuingia msikitini na kusujudu kwa waarabu sizitaki.

Kwa nini nitake kuwa muarabu wakati mimi Muafrika?
Kiranga at his best.............. Amepata exposure kubwa hadi kuwa exposed. Napenda msimamo wako kijana wa zamani wa YESU
 
Sina ujuzi na bohora,lakini kwa misikiti ya shia hakuna kitu kama hicho,I'm talking out of experience

Uko sahihi kabisa.

Mimi husali Kisunni katika msikiti wa Kishiia pale Mtaa wa India na Morogoro Road.

Napapenda kwa kuwa kuna vyoo visafi, na msikiti unaendeshwa vizuri. Kuna gari la mgonjwa, kuna daktari, kuna madrassa na tuition ya kufundisha watoto wao, jioni msikiti unakuwa sehemu ya kufanya sherehe tofauti za kwao na kuna usalama wa vitu vyako na usafi wa hali ya juu.

Sijakutana na ubaguzi wowote na sijakatazwa kusali kisunni. Ila Ijumaa, wanatoa hotuba kwa Kihindi halafu baadae kwa Kiswahili. Sisi tunatoa kwa Kiarabu pale upanga makaburini halafu kwa Kiswahili.

Miaka hiyo ni ya 80 na mpaka leo hamna msikiti wowote unaendeshwa vizuri kama wa Kishiia, kwa maoni yangu, hasa kuhusu usafi wa vyoo.
(Sijaona bado msikiti wa Kisunni chenye choo cha kukaa).
 
nimesala misikiti yote hadi ya mabohora nimeingia na sikubaguliwa acha kisikiliza mambo ya kuambiwa sijui kama kuna ubaguz misikitini labda kubaguliwa kukaa safu ya mbele tena nyuma ya imamu haiwezekan anaekaa nyuma ya imamu lazma awe nae anajua dini vizur imamu akikosea ye anamsahihisha wewe mwenzagu ma mimi hata kutia udhu unageza ukakae nyuma ya imamu lazma utolewe
 
mnafiki mkubwa uislamu hauna ubaguzi kama wengine hata leo nikienda china nitaswali acha wehu wako
 
Weka jina la msikiti nikajaribu...nione huyo atakayenizuia,patachimbika.
Msikiti wa Manyema kuna mtu aliwahi kurusha ngumi pale, kuna watu wa familia flani weupe walishajiwekea kuwa swafu ya mbele ni ya kwao, so wewe kanjangaz ukifika pale unatakiwa ukae ya pili hata kama ya kwanza haijajaa...
 
Hujaeleza umelitoa wapi la kanisani.

Unaokoteza vitu hewani.
We ndiyo mwenye kuokoteza vitu hewani. Kuvua kwa viatu msikitini kuna mahusiano gani na ubaguzi?

Kila sehemu kuna utaratibu wake,hata ofisini kuna taratibu zake. Sasa wewe unataka utaratibu wa sehemu nyengine ndiyo utumike pahala pengine.

We kama ulizoe utaratibu wa kuingia na viatu kanisani basi usitake kufanya na sehemu zengine kuwe na utaratibu huo huo.
 
Uanabaguliwa ndiyo..sasa ulitaka iwaje? Kwani itakuwa ni Mara ya kwanza kubaguliwa?? Ndo maana kuna wazungu,waarabu,waafrika wahindi nk. Similar birds flock together bwana...ulitaka uwe kenge kwny msafara wa mamba? Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba mkuu.. Kwani ukiswali msikiti mwingingine kwani kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi kaka. Hata watoto hucheza na wenzao wanaoendana! Unalalamika kubaguliwa nchini kwako? Ubaguzi ulikuwepo tangu enzi za akina Said Balaghash itakuwa leo?
sasa we unashabikia ubaguzi
 
Back
Top Bottom