Msikiti wa posta na ubaguzi??

Msikiti wa posta na ubaguzi??

Naona wewe haujawahi kukumbana na kimbembe cha ubaguzi wa aina yoyote nadhani, usingetumia hilo neno "patachimbika".
Kwenye ubaguzi, hauwezi kupewa ushirikiano wa aina yoyote na hiyo jamii baguzi. Hadi mwenyewe uta-surrender. Huasemeshwi, haujibiwi! Hauongei ukajibiwa. Haushirikishwi chochote!
Sasa katika mazingira kama hayo utachimbaje mkwara? Utakoromea jamii nzima?
Ubaguzi ni kitu kibaya sana mkuu.
 
Basi huyo alijichanganya akatia timu kwenye msikiti wa wale mabohora waliojazana mjini sahivi.. sijawahi ona mmatumbi akiingia kusali mule na ukizingatia kwamba yule mkuu wa mabohora dunia nzima alikuwepo..
...hata leo wameonyeshwa kwenye TV kibao tu na mkuu wa kaya alikuwepo yani msikiti mzima ni wadosi watupu...
 
Basi huyo alijichanganya akatia timu kwenye msikiti wa wale mabohora waliojazana mjini sahivi.. sijawahi ona mmatumbi akiingia kusali mule na ukizingatia kwamba yule mkuu wa mabohora dunia nzima alikuwepo..
...hata leo wameonyeshwa kwenye TV kibao tu na mkuu wa kaya alikuwepo yani msikiti mzima ni wadosi watupu...
Inawezekana maana uwezekano wa kubaguliwa katika misikiti yetu ya kawaida hakuna

Huyo aliingia bohora ama Shia
 
Kama ndio ivyo basi ninamashaka na.uislam.wao.Misikiti yote niya mwenyez mungu ila huo unaouita uchunguz sio uchunguz coz hujaenda kushuhudia pengine ni porojo za mitaani tu..kama ni uchunguz basi kamilisha uchunguz wako kwa kwenda sio kusikia kwa watu.
 
Wengi hawaendi kuswali bali kwenda kuomba omba kwa wahindi ,wazee wa vibarakhashia huweza kutoka Bunju akiacha misikiti yote huko na kufuata misikiti ambayo huswali matajiri ili baadaye wapate vijisenti vya bure si ajabu jamaa wamewachoka.
 
HUO MSIKITI UPO JILANI NA LILIPODONDOKA LILE GHOROFA...NAZANI NI MTAA WA IDRAGANDI;
ULE MSIKITI KWAKWELI WANAOSALI NI WEUPE TU; NA WALIUJENGA SPECIAL KWA AJILI YAO! RANGI NYEUSI NI MARUFUKU! NAUJUWA
Msikiti wa mashia.
 
Siye waislamu ni vigumu kubaguana. Muislam anaweza kuingia msikiti wowote ambako swala ilimkutia.

Ataingia, Atatawadha, Ataswali , Ataondoka.
Kulingana na mafundisho ya dini ya kiislamu ni vigumu sana kubaguana.

Msikiti wowote hapa duniani ni mahali salama kimwili na kiroho kwa muislamu yeyote.

Nina hakika wewe na uyo aliyekwambia wrote ni wanafiki. Either mna sababu zenu binafsi au mna zile tabia za umbea usio na tija.

Nitashukuru na kukuona wa maana kama utataja jina LA msikiti ili waislam halisi wakahakikishe uyasemayo.
 
Makundi 72 Yatakayoingia Motoni
Aqiydah
SWALI:
assalam aleikum.amma baad namshukuru Allaah kuniwezesha tena kuandika sula hili ambalo natumai litakuwa bayana kwako kwa uwezo wake Allaah. Naomba uanitajie makundi 73 ambayo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)(s.a.w) kayabashiria kuwa yataingia motoni ila moja tu na unifafanulie vizuri tofauti zao? Ahsante wajazakAllaahu kheir.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani kwa swali lako hilo kuhusu makundi yaliyotajwa kwa idadi katika Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa yataingia Motoni. Ieleweke kuwa hapa si mahala pake pa kuweza kuyaeleza makundi hayo kufanya utafiti huo itabidi tusiwe ni wenye kujibu maswali wala kufanya kazi wala shughuli nyengine isipokuwa hiyo. Hivyo ni juu ya mwanafunzi kwenda katika vitabu vingi vilivyoelezea hayo.
Kwa kifupi tu kwa kukupa mwangaza kidogo, utayajua yale makundi yaliyo potofu kwa kuona na kujua itikadi zao. Mfano mzuri leo utaona wanaodai kuna mtume baada ya Mtume wa haki na wa mwisho Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), utawaona pia wale wanaowakufurisha Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) na kuwatukana wake za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), pia utawaona wengine wanaokufurisha Waislam na kuwatoa katika Dini kwa sababu wanaamini kuonekana Allaah Qiyaamah, na wanakufurisha Waislamu kwa sababu ya kufanya baadhi ya maasi, na pia utawaona wengine wanakataa Hadiyth za Mtume na kudai kuwa wao wanafuata Qur-aan pekee, na pia utawakuta wengine wanakwenda kuwaomba watu waliokufa makaburini ili wawasaidie haja zao, na wengi wengine wasio na idadi.
Tutalijua kundi lililookoka na ambalo halipo katika hayo makundi 72, kwa kuitazama ile Hadiyth ya bwana Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo:
((Wamegawanyika Mayahudi katika mapote 71, wakagawanyika Wakristo katika mapote 72 na Ummah wangu utagawanyika mapote 73. Yote hayo yataingia motoni ila moja tu)) Maswahaba waliuliza: Ni lipi hilo, ewe Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wa Allaah! Akasema: ((Ni lile nililokuwemo mimi na Swahaba zangu)) [Ahmad, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ad-Daarimiy].
Kundi hilo litakuwa ni lenye kufuata maagizo ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Makhalifa waongofu (Radhiya Allaahu ‘anhum) na Maswahaba wengine (Radhiya Allaahu ‘anhum) na wema wote waliotangulia (Salafus-Swaalih). Muislam atakayejikita na kuwa imara katika hayo basi atakuwa katika njia nyoofu. Dalili ni nyingi katika Qur-aan na Sunnah. Miongoni mwayo ni kauli ya Aliyetukuka:
((Na anayemtii Allaah na Mtume Wake, bila ya shaka amefanikiwa mafanikio makubwa)) [33: 71].
Pia Amesema Aliyetukuka:
((Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Allaah basi nifuateni mimi, Allaah Atakupendeni na Atakufutieni madhambi yenu. Na Allaah ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu)) [3: 31].
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) naye anatueleza yafutayo katika khutbah yake ya Hijjatul Wadaa: ((Hakika nimewaachia kitu ambacho hamtapotea baada yangu lau mtashikana nacho, Kitabu cha Allaah)) [Muslim].
Sehemu nyengine kasema: ((Kitabu cha Allaah na Sunnah zangu)) [Al-Bukhaariy na Muslim].
Na katika masimulizi ya Abu Najiih al- 'Irbaadh bin Saariyah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba: "Alituwaidhia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yaliyozifanya nyoyo kuingia hofu na macho yakatokwa na machozi. Tukamwambia: "Ewe Mtume wa Allaah! Yaonyesha kama haya ni mawaidha ya kuaga, basi tuusie". Akasema: ((Nawausia kumcha Allaah, Kwani hakika atakayeishi katika nyinyi ataona khitilafu nyingi, basi jilazimisheni kufuata Sunnah zangu na Sunnah za Makhalifa walioongoka, yashikeni kwa magego mambo yao)) [Abu Daawuwd, Ahmad, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah na Ad-Daarimiy].
Mambo muhimu ambayo tunayapata katika dondoo za hapo juu ni kuwa, kuwepo kwetu katika kundi litakaloongoka ni kufuata mwendo aliokuwa nao Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Makhalifa wake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na kushikamana nao kivitendo barabara.
Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Atufanye ni wenye kuyashikilia hayo vilivyo ili tuwe ni wenye kuingia katika Rehma Yake na kuwa ni kundi lililosalimika na moto, kundi lililonusurika na ni kundi liliokoka.
Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Atusahilishie hatua zetu katika kuelekea katika mwendo wa sawa na wa haki.
 
Hawa ndo wezi wa viatu. Wakiona ulinzi wanaanza kusema ubaguzi.
Wacheni hizi tabia za kuiba viati
 
Ingia hapo msikitini uswali alafu utuletelee mrejesho, usipende ku-publish habari za kuadithiwa.
 
Hujui kama unaenda au unarudi.

Unawayawaya.
Unaye wayawaya ni wewe ambaye unataka watu waingie msikitini na viatu kwa sababu tu wewe ulizoea kuingia kanisani na viatu.

Watu wote wanavua viatu msikitini ila wewe unasema ni ubaguzi. Na ndiyo maana nakwambia kuzoea kwako kuingia kanisani na viatu usitake nyumba zote za ibada ziwe hivyo.
 
Misikiti yote ina ubaguzi.

Inabagua wasiotaka kuvua viatu mlangoni.

Sema jingine.
1.Hakuna katazo la kuingia na viatu msikitini. Sayydna Alii anasema kama dini inakwenda kwa rai za watu basi kupaka maji chini ya viatu ingekuwa bora kuliko kupaka juu wakati wa kupata udhu wa swala pale muislam anapotaka kuingia msikitini na viatu kwa ajili ya swala
2. Ibada ya swala hukamilika kwa muislam kukamilisha nguzo ya twahara. Yaani kuwa msafi wa mwili, mavazi (including viatu) na mahala pa kuswalia. Kama muislamu atahisi viatu vyake sio twahara atavivua nje wakatik wa kuingia msikitini
3. Kutomruhusu muislamu kuingia msikitini na viatu si kumbagua Bali ni kumfanya atekeleze ibada ya swala kwa kutimiza masharti (kuwa twahara) kama viatu vyake ni twahara hakatazwi kuingia navyo msikitini
4. Kuvua viatu haiko msikitini peke yake, zipo ofisi na Nyumba watu hutakiwa kuvua viatu.
 
Unaye wayawaya ni wewe ambaye unataka watu waingie msikitini na viatu kwa sababu tu wewe ulizoea kuingia kanisani na viatu.

Watu wote wanavua viatu msikitini ila wewe unasema ni ubaguzi. Na ndiyo maana nakwambia kuzoea kwako kuingia kanisani na viatu usitake nyumba zote za ibada ziwe hivyo.
Hujaonesha ya kanisani umeyatoa wapi.
 
1.Hakuna katazo la kuingia na viatu msikitini. Sayydna Alii anasema kama dini inakwenda kwa rai za watu basi kupaka maji chini ya viatu ingekuwa bora kuliko kupaka juu wakati wa kupata udhu wa swala pale muislam anapotaka kuingia msikitini na viatu kwa ajili ya swala
2. Ibada ya swala hukamilika kwa muislam kukamilisha nguzo ya twahara. Yaani kuwa msafi wa mwili, mavazi (including viatu) na mahala pa kuswalia. Kama muislamu atahisi viatu vyake sio twahara atavivua nje wakatik wa kuingia msikitini
3. Kutomruhusu muislamu kuingia msikitini na viatu si kumbagua Bali ni kumfanya atekeleze ibada ya swala kwa kutimiza masharti (kuwa twahara) kama viatu vyake ni twahara hakatazwi kuingia navyo msikitini
4. Kuvua viatu haiko msikitini peke yake, zipo ofisi na Nyumba watu hutakiwa kuvua viatu.
Kwa nini Allah hajafanya hewa ya Msikitni iwe inasafisha uchafu wote automatically hata kama mtu akingia na viatu vichafu viwe visafi?

Alishindwa kufanya misikiti iwe hivyo?
 
Back
Top Bottom