Msikiti wa posta na ubaguzi??

Aisee mkuu unafikiri saba
 
Habari ndo hiyo, Bilal (Muislaam mweusi) ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuadhini (mwito wa kuita Waislaam kwenda/kuingia msikitini kuswali)
Nabii Luqman pia inadaiwa alikuwa ni mtu mweusi kutoka Ethiopia (Abbyssinia) odbg
Bilal yupi huyo? Ama huyu Bilal Mashauzi??
 
Waarabu wengi ni wastaarabu mana wanapenda taarabu-afande sele(mkuki moyoni)
 
Nani kasema??tena nyie waislamu weusi hamtakiwi uarabuni kabisa..waarabu hawawapendi lakin marekani akiwagonga waarabu mnalia lia na kutaka kuandamana...
Ila afrika ya kati..waislamu weusi wenzenu walikua wanachinjwa... nyie kimyaa...na hata hao waarabu hawakuwasaidia
 
Totally crap...unaandika nonsenses. Hakuna maisha baada ya kifo. Ukibisha lete ushaidi aliyekufa aje atuambie ayo maisha yapoje.
 
Inatia moyo kuona watu wengi zaidi wanajua hili.
Hakuna kitu kibaya kama mental slavery.
Waafrika wengi wana hii kitu..utumwa wa fikra.
Dini zote hizi sio uislamu ama ukristo zimeletwa..
mababu zetu wakazipokea tuu...ukazaliwa...ukamezeshwa . Izo dini zina wenyewe..basi unakuta mwafrika eti yupo ntafia dini yangu..like seriously???

Dini alete mwarabu ama mzungu useme eti "ntafia dini yangu"??? Huezi kua na akili timamu.

Imani yako ndo itayokubeba...naongelea imani yako ktk "right na wrong".
Nafurahi sio muumini wa dini yoyote ile. Napenda imani yangu. Naamini ktk right n wrong ktk maisha.
 
Acha Uongo, hata kama uislam hauruhusu Ubaguzi, Waarabu wanawabagua Wabantu hata katika Ibada.

OVA
Kiufupi waarabu hawawapendi wabantu. ..lakini mwarabu akichapwa na mmarekani basi waislamu wakibantu watalaani na kulia sana na kutishia kuandamana ubalozi wa marekani
 
Siku moja natoka kazini naenda kupanda treni nirudi nyumbani. Kutoka ofisini kwangu mpaka kufika kituo cha treni ilikuwa lazima nishushe Wall St. mpaka Broadway. Basi nimefika kona ya Broad St. na Wall St pale kwenye New York Stock Exchange, katikati ya dunia ya watoza ushuru na waabudu fedha, nikamkuta babu mmoja kwa accent yake anasikika kama Mnigeria hivi. Kakomaa anawahubiria New Yorkers injili wamsikilize anawaletea neno la Yesu. Wakati wazungu ndio wanajua uongo wote ulio katika biblia na ndio walioutumia kwa mamia ya miaka kutuibia mali na uhuru wetu.

Nikaona sasa Afrika tumedanganywa mpaka tunafanya reverse evangelism.

Nikafikiria sana nikasema usikute Mnigeria naye anawapiga kivyaje huko kwenye makodi na misaada na kuwaunganishia watu wa kwao waje huku na yeye anachanganya mingo kivyake.

Bottom line habari za Mungu ambaye hawezi hata ku pass a simple logic test ni uongo wa kitoto unaofaa kuachwa kwani unatudumazia maendeleo.
 
Hujajibu la kanisani umelitoa wapi.

Msikiti haubagui kwa msingi wa wanaoingia kwa kuvaa na kutovaa viatu?
Kwa taarifa yako;Dini na mafundisho yake yanaruhusu kuingia msikitini na kuswali ukiwa umevaa viatu,Pale utapohakikisha ni visafi na havina najisi.Zaidi ni katka hali ya ku maintain usafi kwani watu wanapita ktk mazingira tofauti huko watokako.
Je unaweza kuingia Nyumba yenye Zuria ilhali viatu vyako vina tope???
Al Islam Nadhiif.
 

Umechelewa sana mjadala. Tumejadili hayo yote awali.

Sasa kwa nini huyo Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote hakufanya kwamba ukiingia msikitini tu uchafu wote unaishia mlangoni bila hata kuvua viatu?

Angefanya muujiza huo angeaminika zaidi.

Lakini sasa hivi ama hayupo mnatupiga fix, ama yupo anatubania kutupa favor hata tunapoenda msikitini.
 

Tatizo wewe unataka Mungu afikiri kibinaadamu, Mungu utashi wake ni huo wa kuona Binadamu anakabiliana na Mazingira yake na hali zake, emeweka utaratibu wa Maisha, akatoa uhuru wa kumuamini na kumkataa ndio maan akampa mwanadamu akili ya utambuzi.

Yeye hanufaiki wala hapungukiwi na chochote kwa kuabudiwa wala kutokuabudiwa.

Vilevile kuhusu majanga yanayotokea ni yeye ndiye aliyeumba, hayo majanga yanafaida zake na hasara zake japo sisi wanaadamu hatupendi.

Kwamfano wewe unauwezo wa kununua nguo mpya na hununui unavaa mtumba, kwa kutokununua bado haikuondolei kwamba wewe huna uwezo bali ndio chaguo lako vivyohivyo Mungu kuumba aina hii ya maisha na dunia (imperfect and bungling) hakumfanyi awe hawezi kuumba vinginevyo.

Mfano mwingine Mwanaume anayeowa mke mmoja na kuzaa watoto wawili kisha kwa sababu zake anamfungu uzazi mkewe, kwa kufanya hivyo haina maana hawezi kuowa mke mwingine na kuzaa watoto wengine. vivyo hivyo Allah kwa kuumba Dunia hii hivi ilivyo haimaanishi hawezi kuumba Dunia isiyo na Matatizo wala Mashaka yoyote.

umeng'ang'ania ati kwanini asiumbe Dunia isiyo na inefficiency? hiyo sio Dunia ni pepo na tayari ameshaiumba Pepo ambayo humo hakuna mashaka wala maradhi wala kufa wala hakuna mwisho.

Nilisha kujibu huko lakini unajitia uziwi na kutokuelewa kwa makusudi.
 
Wapi nimeng'ang'ania kwa nini Mungu asiumbe dunia isiyo na efficiency?

Hivi unaelewa hata ninachoandika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…