Je, Makonda ni asset au liability kwa CCM?

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,503
51,098
Katika maamuzi ya hovyo ambayo CCM wamewahi kuyafanya ni kumrudisha huyu kijana katika nafasi kubwa sana ndani ya chama.

Pengine ni katika hali ya kutapatapa kisiasa kwa rais Samia na Pengine kwa sababu ya urafiki wake na Makonda uliomsukuma Rais atumie nguvu na ushawishi wake kumrudisha Makonda katika ulingo wa kisiasa.

Inafahamika vizuri kuwa Tangu Makonda apendekeze kwa wakubwa wa CCM na watawala katika bunge la katiba kuwa Wamfanye Samia kuwa mgombea mwenza wa mgombea uraisi wa mwaka 2015, nadhani Samia amekuwa akiamini kuwa sababu mojawapo ya nyota yake ya kisiasa kung'aa ni pendekezo la Makonda. Hivyo kutoka katika uvungu wa moyo wake amekuwa akidhani kuwa ana deni kwa huyo kijana.

Hata hivyo Samia asichokifahamu, au pengine anakifahamu lakini ameamua kufumba macho kwa sababu ya kumpenda Makonda ni kwamba, Katika watu waliomharibia magufuli na kuiba mtaji mkubwa wa kisiasa wa Magufuli ni huyu Makonda.

Makonda alifanya mambo ya ajabu mno na Magufuli alitumia mtaji wake binafsi wa kisiasa kumlinda na kumkingia kifua huyu kijana. Hii ilipelekea watu kuanza kumchukia Magufuli na kumsema vibaya sana. Umaarufu wa Magufuli umeongezeka zaidi baada ya kifo chake kuliko wakati wa uhai wake hasa kipindi Makonda anafanya mambo ya ajabuajabu.

1. Tukio la Jaribio la Mauaji ya Lissu
Tundu Lissu amekuwa akimtuhumu Makonda katika jaribio la mauaji dhidi yake, hizi ni allegations nzito sana. Haipaswi hata kidogo kwa Chama kikubwa tena kinachoendesha serikali kumpa mtu kama Makonda dhamana kubwa katika chama chao wakati ana tuhuma nzito kama hizo.

Hii inatoa taswira kuwa chama cha CCM nacho kinalinda uhalifu, na kinaunga mkono kilichomkuta Lissu. Otherwise badala ya kumuweka huyu Makonda katika uchunguzi, chenyewe kinamfanya kuwa msemaji wake.

2. Tuhuma za kudhulumu nyumba ya GSM
Pia kuna tuhuma, zimetolewa na Lissu kuwa Makonda amewahi kutumia jina la Rais (Magufuli) ili kufanya utapeli. Mtu aliyetumia nafasi yake ya mkuu wa mkoa na ukaribu na raisi kudhulumu, utampaje mtu kama huyo nafasi kubwa katika chama?

Unampa mtu kama huyu kukisemea chama ili akisemee nini haswa?. Ni dhahiri vetting ya CCM ni ya hovyo au haijielewi kuwa inataka nini, au iko desperate kupata watu wanaoweza kukisaidia kwa merit

3. Kuvamia Studio za Clouds FM kwa silaha
Mtu alionekana katika video, akivamia studio kinyume cha sheria, akakingiwa kifua na mamlaka ya urais, lakini bado akaendelea kufanya mambo ya ajabuajabu. Huyu anafaaje kuwa Msemaji wa Chama. Inamaana CCM nacho kinataka kutwambia kuwa nacho ni chama cha THUGS? Uteuzi wa Makonda kimsingi umeifunua CCM na kuionyesha kuwa ni chama ambacho ni muflisi

4. Kuendesha zoezi la Kumsingizia Lowasa kutelekeza Mtoto
Huyu Makonda ndiye aliitisha zoezi la eti wanawake wakawashitaki wanaume waliowatelekezea watoto. na hapo anatokea binti mwenye miaka kibao eti anaenda kushitaki kwa mkuu wa mkoa kuwa katelekezwa na waziri mkuu mstaafu. mazoezi ya kucheza na hisia za watu, kuwatumia watu kisiasa, kudhalilisha watu. Huyu anawezaje kuwa msemaji wa chama kikubwa kinachoongoza dola?

5. Mtu aliyetajwa na katibu mkuu mstaafu wa CCM kuwa anapwaya katika uongozi
Bashiru Ally aliwahi kutamka wazi kuwa huyu kijana bado hajakomaa katika uongozi, kuna mambo anayafanya ni kinyume cha maadili ya uongozi. Ni lini huyu Makonda karudi tena darasani ili kupigwa tena msasa wa uongozi ili kujua maaili ya uongozi?

MAONI YANGU:
1. Samia tangu alipoingia Madarakani alikuwa anatafuta namna ya kumrudisha Makonda katika mfumo kwa sababu ya urafiki tu lakini alikuwa anasubirisubiri kwanza kutafuta timing.

2. Upepo wa bandari ulipokuwa mkubwa akaona hiyo ni fursa ya kumrudisha swahiba wake katika mfumo lakini wakati huohuo kujaribu kuspin mjadala wa kitaifa wa bandari.

3. Samia anadhani kwa kuwa Makonda alikuwa karibu na Magufuli basi Makonda ataleta upako wa kimagufuli kwake, yaani by virtue ya watu wa kawaida kumkubali Magufuli, basi watafurahi na kumuongezea ratings akimpa nafasi Makonda.

4. Samia anadhani anaweza kupata uungwaji mkono kanda ya ziwa kwa kuwasogeza watu wa kanda ya ziwa katika nafasi kadha wa kadha. Hiyo ndo sababu mojawapo ya kuwaleta karibu akina Biteko na makonda, lakini hata hivyo sidhani kama hili litamsaidia.

NINACHOKIONA KINAFUATA

1. Upepo wa Makonda utakata muda si mrefu, maana aina yake ya ufanyaji siasa ni usanii na vichekesho. Sanaa zinaweza kulipa kwa muda mfupi lakini baadae wananchi wanataka vitu serious.

Wakati bei ya sukari inapanda, watu wana shida ya maji safi na salama, umeme wa manati, ajira kwa vijana tabu, halafu unawaletea wananchi sanaa. Itabackfire tu. CCM waliitaji mtu anayeweza kuelezea Issues za serikali yao vizuri, mwenye charisma, mwenye upeo.

2. It is a matter of time kabla Makonda hajarudi katika ngozi yake ya asili. Kama Samia asipomdhibiti mapema huyu kijana atageuka soon kuwa liability kwake kama alivyokuwa katika siku za mwisho za utawala wa Magufuli.

Ni kweli Makonda aanajua sana kumteka mtu na kumfanya rafiki wa kuaminika. Alifanya hivyo kwa Mzee Sitta, Membe, Familia ya Jakaya, Familia ya Magufuli na sasa Samia. Samia asidhani anamjua Makonda saaaana kuliko Riziwani. Na sote tunajua kilichomkuta Riziwani baada ya Makonda kufanikiwa kumuweka JPM kiganjani. Je Samia ataweza kulirudisha jini katika chupa?- Time will tell
 
mnarudia yaleyale kila uchwao kuhusu Makonda ambayo yanafahamika,lakini jamaa anasonga.

kutoka ukuu wa wilaya,ukuu wa mkoa mpaka nafasi ya kitaifa ya chama,uwenda hata akaukwaa uwaziri huko mbeleni.
jamaa yuko na kitu ndani yake alichopewa na aliyemuumba.

Kwa Bongo lolote linawezekana.
 
Katika maamuzi ya hovyo ambayo CCM wamewahi kuyafanya ni kumrudisha huyu kijana katika nafasi kubwa sana ndani ya chama.

Pengine ni katika hali ya kutapatapa kisiasa kwa rais Samia na Pengine kwa sababu ya urafiki wake na Makonda uliomsukuma Rais atumie nguvu na ushawishi wake kumrudisha Makonda katika ulingo wa kisiasa.

Inafahamika vizuri kuwa Tangu Makonda apendekeze kwa wakubwa wa CCM na watawala katika bunge la katiba kuwa Wamfanye Samia kuwa mgombea mwenza wa mgombea uraisi wa mwaka 2015, nadhani Samia amekuwa akiamini kuwa sababu mojawapo ya nyota yake ya kisiasa kung'aa ni pendekezo la Makonda. Hivyo kutoka katika uvungu wa moyo wake amekuwa akidhani kuwa ana deni kwa huyo kijana.

Hata hivyo Samia asichokifahamu, au pengine anakifahamu lakini ameamua kufumba macho kwa sababu ya kumpenda Makonda ni kwamba, Katika watu waliomharibia magufuli na kuiba mtaji mkubwa wa kisiasa wa Magufuli ni huyu Makonda. Makonda alifanya mambo ya ajabu mno na Magufuli alitumia mtaji wake binafsi wa kisiasa kumlinda na kumkingia kifua huyu kijana. Hii ilipelekea watu kuanza kumchukia Magufuli na kumsema vibaya sana. Umaarufu wa Magufuli umeongezeka zaidi baada ya kifo chake kuliko wakati wa uhai wake hasa kipindi Makonda anafanya mambo ya ajabuajabu.

1. Tukio la Jaribio la Mauaji ya Lissu.
Tundu Lissu amekuwa akimtuhumu Makonda katika jaribio la mauaji dhidi yake, hizi ni allegations nzito sana. Haipaswi hata kidogo kwa Chama kikubwa tena kinachoendesha serikali kumpa mtu kama Makonda dhamana kubwa katika chama chao wakati ana tuhuma nzito kama hizo. Hii inatoa taswira kuwa chama cha CCM nacho kinalinda uhalifu, na kinaunga mkono kilichomkuta Lissu. Otherwise badala ya kumuweka huyu Makonda katika uchunguzi, chenyewe kinamfanya kuwa msemaji wake.

2. Tuhuma za kudhulumu nyumba ya GSM
Pia kuna tuhuma, zimetolewa na Lissu kuwa Makonda amewahi kutumia jina la Rais (Magufuli) ili kufanya utapeli. Mtu aliyetumia nafasi yake ya mkuu wa mkoa na ukaribu na raisi kudhulumu, utampaje mtu kama huyo nafasi kubwa katika chama?. Unampa mtu kama huyu kukisemea chama ili akisemee nini haswa?. Ni dhahiri vetting ya CCM ni ya hovyo au haijielewi kuwa inataka nini, au iko desperate kupata watu wanaoweza kukisaidia kwa merit

3. Kuvamia Studio za Clouds FM kwa silaha.
Mtu alionekana katika video, akivamia studio kinyume cha sheria, akakingiwa kifua na mamlaka ya urais, lakini bado akaendelea kufanya mambo ya ajabuajabu. Huyu anafaaje kuwa Msemaji wa Chama. Inamaana CCM nacho kinataka kutwambia kuwa nacho ni chama cha THUGS?. Uteuzi wa Makonda kimsingi umeifunua CCM na kuionyesha kuwa ni chama ambacho ni muflisi

4. Kuendesha zoezi la Kumsingizia Lowasa kutelekeza Mtoto
Huyu Makonda ndiye aliitisha zoezi la eti wanawake wakawashitaki wanaume waliowatelekezea watoto. na hapo anatokea binti mwenye miaka kibao eti anaenda kushitaki kwa mkuu wa mkoa kuwa katelekezwa na waziri mkuu mstaafu. mazoezi ya kucheza na hisia za watu, kuwatumia watu kisiasa, kudhalilisha watu. Huyu anawezaje kuwa msemaji wa chama kikubwa kinachoongoza dola?

5. Mtu aliyetajwa na katibu mkuu mstaafu wa CCM kuwa anapwaya katika uongozi
Bashiru Ally aliwahi kutamka wazi kuwa huyu kijana bado hajakomaa katika uongozi, kuna mambo anayafanya ni kinyume cha maadili ya uongozi. Ni lini huyu Makonda karudi tena darasani ili kupigwa tena msasa wa uongozi ili kujua maaili ya uongozi?

MAONI YANGU:
1. Samia tangu alipoingia Madarakani alikuwa anatafuta namna ya kumrudisha Makonda katika mfumo kwa sababu ya urafiki tu lakini alikuwa anasubirisubiri kwanza kutafuta timing.

2. Upepo wa bandari ulipokuwa mkubwa akaona hiyo ni fursa ya kumrudisha swahiba wake katika mfumo lakini wakati huohuo kujaribu kuspin mjadala wa kitaifa wa bandari.

3. Samia anadhani kwa kuwa Makonda alikuwa karibu na Magufuli basi Makonda ataleta upako wa kimagufuli kwake, yaani by virtue ya watu wa kawaida kumkubali Magufuli, basi watafurahi na kumuongezea ratings akimpa nafasi Makonda.

4. Samia anadhani anaweza kupata uungwaji mkono kanda ya ziwa kwa kuwasogeza watu wa kanda ya ziwa katika nafasi kadha wa kadha. Hiyo ndo sababu mojawapo ya kuwaleta karibu akina Biteko na makonda , lakini hata hivyo sidhani kama hili litamsaidia.

NINACHOKIONA KINAFUATA

1. Upepo wa Makonda utakata muda si mrefu, maana aina yake ya ufanyaji siasa ni usanii na vichekesho. Sanaa zinaweza kulipa kwa muda mfupi lakini baadae wananchi wanataka vitu serious. Wakati bei ya sukari inapanda, watu wana shida ya maji safi na salama, umeme wa manati, ajira kwa vijana tabu, halafu unawaletea wananchi sanaa. Itabackfire tu. CCM waliitaji mtu anayeweza kuelezea Issues za serikali yao vizuri, mwenye charisma, mwenye upeo.

2. It is a matter of time kabla Makonda hajarudi katika ngozi yake ya asili. Kama Samia asipomdhibiti mapema huyu kijana atageuka soon kuwa liability kwake kama alivyokuwa katika siku za mwisho za utawala wa Magufuli. Ni kweli Makonda aanajua sana kumteka mtu na kumfanya rafiki wa kuaminika. Alifanya hivyo kwa Mzee Sitta, Membe, Familia ya Jakaya, Familia ya Magufuli na sasa Samia. Samia asidhani anamjua Makonda saaaana kuliko Riziwani. Na sote tunajua kilichomkuta Riziwani baada ya Makonda kufanikiwa kumuweka JPM kiganjani. Je Samia ataweza kukirudisha jini katika chupa?- Time will tell
Ndo karudi Sasa!! Mtajua tu kama ni asset au ni liability
 
Watanzania hawaishi mitandaoni.
Toka mtaani chunguza utapata jibu.

NB: Binafsi naona hafai ila mitaa inasema Vingine.
Hii nchi wajinga ni wengi, ukiweza Kwenda nao kijinga unatoboa.
Ni kweli wajinga wanapenda watu wapendao kugombeza, kutisha, kubeza na kulaumu watu wenye vyeo na kujifanya wanawaonea huruma wanyonge. Wajinga wanamuona huyo kijana yuko sahihi.
Anayifanya kama angekuwa naibu waziri mkuu ingekuwa balaa, walio chini wangelazimika kujuuzulu,
Kiukweli katiba mpya ni muhimu sana kuondoa huu upuuzi.
 
mnarudia yaleyale kila uchwao kuhusu Makonda ambayo yanafahamika,lakini jamaa anasonga.

kutoka ukuu wa wilaya,ukuu wa mkoa mpaka nafasi ya kitaifa ya chama,uwenda hata akaukwaa uwaziri huko mbeleni.
jamaa yuko na kitu ndani yake alichopewa na aliyemuumba.
Hitler na wengine kama yeye alipenyapenya hivohivo, hakuna cha talanta hapo
 
mnarudia yaleyale kila uchwao kuhusu Makonda ambayo yanafahamika,lakini jamaa anasonga.

kutoka ukuu wa wilaya,ukuu wa mkoa mpaka nafasi ya kitaifa ya chama,uwenda hata akaukwaa uwaziri huko mbeleni.
jamaa yuko na kitu ndani yake alichopewa na aliyemuumba.

Muaji Makonda, kama ana kitu cha pekee, basi ni uovu uliopindukia.

Punguani huamini kuwa ukiwa na cheo basi umefanikiwa sana. Kuna watu walifanikiwa kuwa mpaka kuwa Marais, lakini kutokana na uovu wao, waliishia kunyongwa mbele ya umma wa wananchi, huku umma ukishangilia. Lakini punguani watasema kwa kuwa alinyongwa mbele ya maelfu ya wananchi wake, basi alifanikiwa sana!!!
 
Ujinga ni kuamini wewe uko sawa tu, ujinga mwingine wa kipumbavu, Ni wasomi kutokuingia kwenye siasa

Sasa nyinyi wasomi mnatakaje kwa mfano, siasa hamuingii na mnataka eti wasomi wawe viongozi? Kwa njia zipi ikiwa kuingia kwenye siasa hamtaki?

Mwacheni Makonda
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom