Mshahara wa Januari vipi mbona unachelewa?

Mshahara wa Januari vipi mbona unachelewa?

Makato ya kutumia Simbanking au NMB mobiles ni mengi na ya hovyo sana.
Hakuna hata sababu ya kuwa nazo.
Hili ndiyo tatizo watu tunalo, kukaririshwa uongo!

Kwani ukiwa na Simbank app ndiyo inakufanya ulazimike kutumia huduma zake zote?

Kwa mfano kutaka kujua transaction na kuuliza salio inakugharimu makato gani?

Je unaelewa ukiwa una app kuuliza salio ni bure na kama hauna app lazima ukatwe salio la vocha na kama hauna salio hauwezi kuhudumiwa?

Mambo simple kama hayo lazima uyaelewe mkuu ipo siku waweza kuwa upo mbali na mji na umekwama ikakusaidia.

Ama hata hapo nyumbani, kutaka kujua mshahara kama umeingia na kutaka kuelewa chochote kwenye acount yako siyo lazima utembee kwenda kuuliza kwenye Atm ama kuuliza mtu wakati kuunganisha sim banking ni bure?

Gharama kubwa ya matumizi yake ni kutoa pesa kwa wakala na kuhamisha pesa tu, ambapo hakuna ulazima labda kwa dharula!
 
Back
Top Bottom