Msajili wa vyama aitaka CHADEMA ijieleze kwanini wanasema wasipochaguliwa wataingia barabarani, Lissu ajibu

Round hii Upinzani wamesimamisha mtu kweli..

Habari za namuachia Mungu wakati Mungu nae anategemea ujasiri wako round hii HAKUNA.
Ni kweli safari hii hakuna cha kugeuza shavu, jino kwa jino, tako kwa tako.💪💪💪
 
Sioni wakujitoa kafara kwa Lissu ,hayupo
hivi ni episode namba ngapi vile? ngoja tuitafutie nafasi yake hapa chini...

Episode 1 (Lissu alivyokuwa Belgium):
Lissu ni kibaraka wa mabeberu, hakuna Mtanzania atakayekubaliana na propaganda za "kuihujumu" nchi

Episode 2 (tetesi za Lissu kurejea nchini ziliposhamiri):
Lissu atakamatwa airport mara tu atakapowasili

Episode 3 (baada ya Lissu kutangaza kugombea urais):
Mbowe atamwengua Lissu kwa vile hana hela kama mwenzie Nyarandu.

Episode 4 (baada ya kuteuliwa na chama chake kuwa mgombea urais):
Atawekewa pingamizi na hatimaye kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha urais

Episode 5 (baada ya kuteuliwa na NEC):
Campaign rallies zake zitadorora kutokana na wananchi kutambua kazi kubwa aliyofanya mgombea wa CCM

Episode 6 (hii ni hii yako uliyoifungulia uzi):
Lissu ajieleze maana ya kuingia barabarani.

Projected Episode 7( hii ni ya kwangu):
Lissu rais October na kuanzia November Magufuli atateuliwa na Lissu kuwa Waziri wa Miundombinu
 
Ofisi ya msajili imekosa weledi mpaka inaanza kutumika kama co...dom ya ccm. Huyu muhaya Mutungi sijui ni mhaya wa wapi mjinga mjinga. Akina jaji Lugakingira walioacha alama hawajui? Shame upon him
 
Nothing Less, Nothing More... Msajili tuonyeshe barua kuionya CCM na kuhubiri ubaguzi kwa kuwatishia wananchi kuchagua wapinzani..
 
Washabiki wa Lissu humu ni maneno tu,nani akajitoe kafara saccos?

Ile siku katus uwanja wa ndege polisi walitangaza Katazo, lakini nyomi ilikuwa ya kutosha. Tusiandikie mate ngoja siku ya uchaguzi tume wazingue.
 
Alichotakiwa kufanya Msajili ni kumhakikishia Lisu kwamba yeye Msajili wa vyama atawasiliana na Tume ya Uchaguzi avihakikishie vyama na ofisi yake kwamba Uchaguzi utakua huru na wa haki.
Anajistukia wanajua ubaya watakaofanya hivyo wanajihami
 
Msajili wa vyama vya siasa amekiandikia barua Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kijieleze kwanini mgombea wao kila siku anasema safari hii hawatakubali kuibiwa kura na wakiibiwa wataingia barabarani, Msajili anasema matamshi hayo ni kutishia amani.

Majibu ya Lissu: Ni kweli uchaguzi huu tukiibiwa tutaingia barabarani, ‘ Nothing less nothing more’.

Kwahiyo msajiri anaona ameingiliwa kwenye mazoea yake ya kuiba kura! Malawi wananchi waliona jinsi time ya uchaguzi ilivyoiba kura, wananchi hawakukubali mpaka ikavunjwa na uchaguzi ukarudiwa. Hapa NEC uko upande wa mgombea wao dhidi ya wananchi huku kanuni za uchaguzi wao hawazifuati.
 
Huyo anayesema wasipomchagua hatawaletea maendeleo wamemfanyaje?
Mzee alijiandaa kwa paper ya geometry akakuta paper yote ni Algebra, halafu waliokuzunguka wanafanya masomo mengine, wa mbele anafanya kiswahili, kulia historia, kushoto geografía, nyuma civics, msimamizi bubu, anatumia ishara tu. Utaishia kuandika jina na kukusanya au ujituingie swali la geometry na kujibu maana hakuna namna, utapigwa tu!!!!. Hivi mzee Pinda yuko wapi bajameni!!!
Yaani JF raha sana . . . jamaa kakuta liear algebra sasa anatafuta pa kutokea ahahaha. Umenikumbusha mbali sana mkuu. Msalimie Kakiko
 
Msajili wa vyama vya siasa amekiandikia barua Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kijieleze kwanini mgombea wao kila siku anasema safari hii hawatakubali kuibiwa kura na wakiibiwa wataingia barabarani
Ajieleze ? Ajieleze nini ? Kuna la kujieleza hapo ? Kama ukiniibia kura na nikawa na ushahidi unategemea nikubali kijinga jinga tu ?
 
Msajili wa vyama vya siasa amekiandikia barua Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kijieleze kwanini mgombea wao kila siku anasema safari hii hawatakubali kuibiwa kura na wakiibiwa wataingia barabarani, Msajili anasema matamshi hayo ni kutishia amani.

Majibu ya Lissu: Ni kweli uchaguzi huu tukiibiwa tutaingia barabarani, ‘ Nothing less nothing more’.
Nothing less nothing more...aione mkurugenzi mkuu tume ya taifa ya kudhibiti upinzani
 
Kwa hiyo ina maana huyu msajili yeye anaunga mkono wizi wa kura. Msajili huyu anashindwa kabisa kututhibitishia kuwa yeye sio kibaraka wa ccm.
 
Back
Top Bottom