Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Hii imevuka mpaka. Chuki iko kwenye mioyo na roho za watu. Hata wakiombewa vipi, hawabadiliki. Cha shetani ni cha shetani...
Na Mungu hadhihakiwi......Si kila alitajae jina na bwana ataingia peponi wengine ni wauaji wakuu na wanyang'anyi wa haki ya kuishi ya watu wengine
 
Sasa wataendaje msibani huku wanashangilia vidole juu km waimba taarabu?

Hyo si kebehi kwa msiba wa Taifa.
Huo sio msiba wa taifa ni wa ccm.......sisi wenye taifa ambao ni malofa haituhusu
 

Makamanda, msibani kwa wastarabu huwa hakuna mwenyewe. Mmefanya sehemu yenu vyema. Sehemu yenu ya nia njema imeonekana na kila mwenye macho na masikio.

Msichoke kuonyesha nia njema. Hiyo ndiyo maturity.

Wanasema, tenda wema wende zako.

Tusisahau wakuu zitakuwapo provocations nyingi na hata mbaya zaidi. Muhimu kujizatiti vilivyo.

Kama kuja nyumbani salama *kulivyoratibiwa vilivyo* tusiangukie kwenye vimitego vya kipuuzi.

Kumbukeni kama msingeenda kuhani, kwa wasiotutakia mema, hiyo mbona ingekuwa habari kubwa?

Ni wazi kuwa walioingilia hilo walikuwa na nia ovu kwa kujua au kutokujua kwao. Tusiwape nafasi za kufanikisha nia zao kwa kujipanga well above the horizon.

Pumzika kwa amani mzee Mkapa.

Mungu ibariki Tanzania.
 
shughulia ya mazishi ya kitaifa.
sasa ndio nini hii!? yaani mtu mzima huwezi hata kutofautisha shughuli za kuaga mwili na shughuli ya mazishi!? nikwambie tu mazishi ni kesho kijijini kwao lupaso sijui, hii ya bongo ilikua ni kuaga!
 
Mbona baada ya kuzuiwa viongozi wa chadema bado watu waliendelea kuingia......

Kwa nn ccm wanaleta siasa kwenye kila kitu?
 
We ng'ombe kwako kifo cha mkapa ndio jambo complex....... kuwaelezea watz ulipo uchumi wa kati ndio swala complex....
 
Viongozi wa CHADEMA mjitahidi sana kuwahi kweye matukio kama haya, mnapofika uwanjani mkuu wa nchi kashaingia tayari, mnakuwa mnawapa nafasi wapinzani wenu kujenga hoja.
 
Jamani mbona Maalim Seif yupo tena kakaa nyuma ya akina Magu?

Hao Chadema walifuata taratibu zilizowekwa au Walifuata taratibu zao binafsi?

Hivi Chadema Magu mpaka leo wameshindwa kucheza naye kweli? Mbona jamaa mwepesi sana???
 
Sawa hata wakenya mmewazuia wasitue kuungana nanyi kwenye msiba hawa nao hawakufata protokali.......

Ni ujingaujinga tu wa maccm
 
Kila kitu mnawaza siasa tu, ndio maana we are one of the poorest countries in the world, now upgraded to lower middle income, with squatters all over the place.
 
Viongozi wa CHADEMA mjitahidi sana kuwahi kweye matukio kama haya, mnapofika uwanjani mkuu wa nchi kashaingia tayari, mnakuwa mnawapa nafasi wapinzani wenu kujenga hoja.

Ok, kaa wamefika Baada ya viongozi wa nchi, walifanya kusudi, wala hawakuwa na nia ya kuomboleza ila kiki. Maana protocol wanaijua.

Kwanini hawakufika kwa muda uliopangwa? Mbona Maalim alifika na kakaa jukwaa kuu, nyuma tu ya Magu?

Ningependa sana kumuona TL karibu na mbaya wake.
 
Na inawezekena hawakukubali mualiko na waandaaji hawakujua kuwa wataenda. Mbona Maalim kapokelewa vizuri, na kakaa nyuma tu ya Magu, tena Hussein Mwinyi yuko nyuma ya Maalim.

Chadema wasipoacha ujinga, ACT- itawazidi kete kwenye uchaguzi huu na kuchukuwa kambi rasmi bungeni. Sijui watasemaje pale Zitto atakapokuwa KUB na mgawaji wa wizara vivuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…