Msaada wa kuandika wosia

Pleasepast

JF-Expert Member
May 30, 2023
325
454
Habarini za usiku wependwa

Naomba msaada kwa anaejua ni utaratibu gani wa kufuata ili mtu aweze kuandika wosia aweze kugawanya mali zake na je.? Inawezekana kumrithisha mtoto wa kuanzia umri gani na uo wosia ukisha andikwa unatuzwa wapi na ikitokea alie andika amefariki walengwa wataupataje.? Kingine ningependa kujua kama mtu ni mwanajeshi anaweza kuandika wosia asizikwe kijeshi azikwe kawaida au haiwezekani.

Naomba kwa wenye kujua mambo haya watoe maoni yao tupate elimu.
 
A: utaratibu wa kuandika wosia,
ili uweze kuandika wosia unapaswa kuwa na;
1: Umri kuanzia miaka 18,mwenye akili timamu na uandike pasipo shiniko la mtu yeyote.
2:utataja mali ulizo nazo na msimamizi wa mirathi baada ya kifo.
3:warithi na viwango vya mgawanyo wa mali .
4:utaeleza utaratibu wa mazishi na mahali utakapotaka kuzikwa.
5:mashahidi walau wawili(inategemea na aina ya wosia kimila,dini au kiserikali-idadi ya mashahidi inaweza kuongezeka)-kila mtu ataandika majina yake na kusaini katika wosia pamoja na mtoa au mwandika wosia
6:lazima kuonyesha tarehe ,mwezi na mwaka uliondikwa.
7:Lazima uandikwe katika maandishi ambayo siyo rahisi kufutika au uchapwe(typed)

B:kwenye mrithi:
mtoa wosia anaweza kumritisha mtu yeyote hata kama ni mtoto ,kwani kama wakati wa kifo cha mtoa wosia akiwa hajafikisha umri wa Miaka 18 basi mali hizo zitakuwa chini ya uangalizi wa mtu mwingine/msimamizi wa mirathi hadi atakapofikia umri wa kisheria wa kurithi mali.

C:Wosia unaweza kutunzwa kwa sehemu zifuatazo;
1:Katika Ofisi ya Vizazi na vifo(RITA)
2:Benki
3:Mahakama kuu
4:Ofisi ya mwanasheria wako,Msikitini,kanisani au sehemu nyingine yoyote utakayoona ni salama

5: Namna ya upatikanaji wa Wosia baada ya kifo cha mtoa wosia.
ni muhimu kuwa na mashahidi kwani miongoni mwa hao mashahidi mtu mmoja(1) atatokea katika ukoo au familia ya mtoa wosia ili inapotokea kifo kutoa taarifa juu ya uwepo wa wosia.

6:Sina ufahamu sana na taratibu za kijeshi,ila kwa mujibu wa sheria za mirathi mtoa wosia anaweza kuandika katika wosia juu ya namna/tartibu za maziko yake na mahali pa kuzikwa ,kwa kusema kuwa angependa kuzikwa kawaida na siyo kijeshi,kwani Wosia ni Last wish ya mtoa wosia hivyo mara nyingi kauli yake au mapendekezo hufuatwa na wote.
 
Nashukuru sana kwa maelezo yako nimeyaelewa vyema kabisa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom