Msaada: Tumetapeliwa!

Msaada: Tumetapeliwa!

nimejaribu kuumiza kichwa tanzania tuna bank nyingi huyo wakala kajuaje kuwa ile namba imeunganishwa crdb ?
 
Aseah pole sana kila siku wezi wanabuni njia mpya ya kufanya wizi hawa mawakala wanaotembea mitaani wengi wanawalalamikia kwavitendo vya wizi wa mitandaoni

Kuna siku mtaan napoishi walipita hawa mawakala wakinadi wanasajili laini kwa alama za vidole sasa mke wangu aliwaita wamsajilie mmoja ya wale mawakala akawa naendelea na zoezi la kumsajilia mke wangu lakin mke wangu katika simu yake kaset typing prediction on alichokua anafanya yule wakala aliingia kwenye menu ya halopesa akawa anafanya muamala mara ikaingia sms kwenye simu sasa yule wakala akawa anataka kuifuta wife analazimisha lazima aisome dah ukawa mzozo kuna jirani akanipigia simu kwakua sikua mbali nikaenda faster kufika nakuta watu washajaa wakala kagoma simu isisomwe sms nikamwambia kama kweli hakuna tatizo kwann simu aikatazie mana hata kumpa mwenye simu hataki mpaka amalize usajili ikabidi nguvu itumike kuitoa lock jamaa kaamisha 765000 tulipompa kibano akaeleza njia mojawapo ni typing prediction yaan kama simu ikiwa na typing prediction on basi hawa vijana wanaibia watu kirahisi sana tuweni makini

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwamba kuna typing prediction ya tarakimu? 😝😝😝 mtapigwa sana kwa mtindo huu hamtaamini
 
VODACOM +255 743 938 273 iliyosajiliwa kwa jina la NYAMIZI MASANJA. Ushapata jina lake na namba ya simu ya evidence afu unashindwa kumpata may be huna shida nae tu, elfu 60 tu ukienda polisi ukaongea na wahusika huyo unampata ndaki ya masaa 6 tu , tena unampata yeye na ukoo wake wote.

Mi nikiamua kumwinda mtu Tanzania hii nampata yeye na ukoo wake wote.
Warning: huyo jamaa ataendelea kupata hela zote zinazoingia bank na tigopesa/mpesa mpaka mmpate au mtelekeze hizo akaunti na laini zote na simu muitupe
Utawapata wasiohusika huwajui vibaka wewe.
Tena unaweza kupata ndugu zako, si wanaenda na vinida vyao kusajili laini au hawaendi? Kama wanaenda hamna jambo mkae kwa kutulia tu
 
VODACOM +255 743 938 273 iliyosajiliwa kwa jina la NYAMIZI MASANJA. Ushapata jina lake na namba ya simu ya evidence afu unashindwa kumpata may be huna shida nae tu, elfu 60 tu ukienda polisi ukaongea na wahusika huyo unampata ndaki ya masaa 6 tu , tena unampata yeye na ukoo wake wote.

Mi nikiamua kumwinda mtu Tanzania hii nampata yeye na ukoo wake wote.
Warning: huyo jamaa ataendelea kupata hela zote zinazoingia bank na tigopesa/mpesa mpaka mmpate au mtelekeze hizo akaunti na laini zote na simu muitupe
UNA AKILI ZA HOVYO SANA....KWA TAARIFA YAKO HAKUNA MWIZI ANATUMIA SIMU ILIYOSAJILIWA JINA LAKE HALISI. NI SAWA NA WALE MAJAMBAZI WANAKURUPISHWA WANAKIMBIA WANAACHA GARI YAO, MTU ANASEMA SI WAFUATILIE TU NAMBA YA GARI TRA WATAMPATA, HAKUNA WEZI WANAOTUMIA GARI WAKAWEKA PLATE NAMBA HALISI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaangu alinisimulia kwamba kipindi yupo lockup (rumande) alipata kuwa na urafiki na jamaa wawili amabo walikuwa na kesi ya cyber crime.

Asa kuna siku akaletwa jamaa mmoja ambaye, jamaa wakataka wampige tukio mulemule ndani. Walichofanya walimuomba simu jamaaa ili wampigie mtu.( pale kituoni ukiwa na mkwanja hadi simu unaruhusiwa kuingia nayo).

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani we jamaa umetuonaje sisi kwamba ni mandezi sana, wazee sana, mirembe sana au?
 
Uyo msajili line kamuibia kijinga sana, alichokifanya uyo msajili line alitumia menu hii *152*00#, then baada ya hapo akabadili password za sehemu zote, kitaalam kwa watu waliosoma cyber security alitumia (social engineering)

Sent using komputa mpakato
Kwamba when you're a social engineer unaweza kutoa hela bila password? Ahahahaha Mungu nisaidie kicheko kitaniua
 
Mtoa mada ni mtu asiyejitambua no wonder anaibiwa na mke wake. Yaani watu wanampa ushauri yeye hata kujibu post moja! Ovyo kabisa
Kumbe kuna muda huwa unazo za kichwani.
Makofi kwako tafadhali
 
Ingia YouTube cheki how to access bank account by using apn utaona kila kitu iyo ishu sio ngumu ata kidogo,

Ushauri usiruhusu mtu kushika simu yako ya uwakala ni tatizo.

Pole mkuu izo pesa zimeenda na utakuta jamaa anatumia dark web security ya Tz haina uwezo wa kumkamata hata wafanyaje ni kama kigogo
Sasa si utumie hiyo njia ya YouTube ufanye kama trial tu uone!
Ukifanikiwa find me i have 2 million cash for ya nigga
 
Wekeni security cameras na muache kufanya biashara ki-zamani. Hapo ungemkata walau sura.
Never trust a stranger next time around.

Sent using Jamii Forums mobile app
Cost ya hizo security cameras ikoje? Mimi fundi nije kukufungia utanilipa ngapi?
.
Biashara yako mtaji wake ni kiasi gani?
Ukishajua unaanguka unakufa
 
Wakuu ninaomba msaada wenu katika hili...

Ilikuwa siku ya Jumamosi ya tarehe 23/05/2020 nilipokea taarifa kutoka kwa wife akinitaarifu kuwa ametapeliwa na wakala wa mitandao ya simu aliyekuwa amevalia mavazi na kitambulisho cha kampuni ya TIGO.

Wakala huyo alifika dukani kwake na kumwambia kuwa anaunganisha vifurushi vya chuo, hapo dukani palikuwa na wateja wawili ambao nao waliomba kupatiwa hiyo huduma kutoka kwa wakala huyo na walionesha kuridhika na huduma yake.

Wife alivyoona wateja hao wamepatiwa huduma na wameprove inafanya kazi vizuri naye aliomba aunganishwe. Alimpatia simu wakala huyo na, kutokana na maelezo yake, alikuwa anashuhudia kila kitu alichokuwa anafanya. Anasema kwamba wakala huyo alitumia muda mwingi katika eneo la 'Access Point Names' (APN).

Baada ya dakika kadhaa alimaliza shughuli yake na kumrudishia wife simu yake na alimtaka ajaribu kama mtandao unafanya kazi ambapo mwanzoni uligoma, akamrudishia simu akaenda tena kwenye APN akarekebisha akamwambia ajaribu ndipo mtandao ukarudi. Alimuaga na kumuhakikishia kwamba kila kitu kipo vizuri na atarudi baadae ili kupata mrejesho. Katika mchakato wote huo, wakala hakuomba wala kuonesha dalili yoyote ya kutaka kufahamu namba ya siri ya TigoPesa wala Bank katika mazungumzo yake.

Baada ya wakala huyo kuondoka wife alipata hitaji la kuhamisha fedha kutoka CRDB SimBanking kwenda kwa mtu aliyemuagiza mzigo. Tatizo lilianza kila anapoingiza menu ya SimBanking (*150*03#) anapata error inayoleta ujumbe 'Try Again Later....'

Baada ya kujaribu muda mrefu bila mafanikio alinipigia na kuniuliza endapo SimBanking yangu inafanya kazi, nilimwambia ipo poa. Pia baada ya kuconfirm na watu wengine na kuambiwa hakuna shida yoyote ndipo alianza kuhisi 'hali ya hatari' kwamba kuna kitu yule wakala amefanya kwenye simu yake.

Alipiga simu Huduma kwa Mteja CRDB akaambiwa kuwa muda si mrefu ametoa fedha (kiasi kimehifadhiwa) kutoka katika akaunti yake kwenda kwenye namba ya VODACOM +255 743 938 273 iliyosajiliwa kwa jina la NYAMIZI MASANJA. Pamoja na wife kuwataarifu watu wa Bank situation iliyotokea still walisisitiza kuwa fedha hizo amezihamisha yeye. Kitu pekee ambacho wameshindwa kukitolea maelezo hadi sasa ni error ya 'Try Again Later....' ambayo ni kama vile wameblock asiweze kuaccess SimBanking yake.

Alipiga simu VODACOM na kutaarifiwa kwamba fedha hiyo imeshatolewa kwa wakala na hivyo hawana cha kufanya. Tuliwarudia tena watu wa TIGO na walisisitiza kuwa endapo Transaction hiyo ingefanyika kwa TIGOPESA basi wangewajibika kuifuatilia lakini kwakuwa ni Bank tufuatilie kwenye taasisi husika!

Pia namba hiyo ya wife imeunganishwa na
NMB Mobile Banking, tulipoangalia salio huko napo tulikuta pesa yote imechukuliwa pia. Na kila akiingiza menu ya NMB Mobile Banking *150*66# nayo inaleta same error ya 'Try Again Later....' Kiufupi ni kwamba Wakala huyo aliweza kubreak Bank Accounts zote ambazo zimekuwa linked na hiyo namba ya TIGO na kuziblock zisiweze kutumika kupitia namba hiyo (hadi sasa)!

To cut the long story short, ni kwamba tangu siku hiyo ya Jumamosi, wife hawezi tena kuingia kwenye SimBanking & NMB Mobile Banking, hapati meseji za TIGOPESA, vifurushi na meseji za aina zote zinazohusiana na huduma za TIGO. Pia Internet haifanyi kazi, App pekee ambayo inakubali mtandao ni WhatsApp tu, but the rest (Google, Facebook, etc) hazifanyi kazi kabisa!

Personally, huwa ni mtundu kiaina kwenye mambo ya IT but this level of crime has amazed me so much. Inakuwaje mtu anaweza kuingia kwenye Bank Accounts na kujitumia pesa bila namba ya siri? How come baada ya kufanya hivyo anakuwa na uwezo wa kublock systems zote zinazohusiana na namba husika in just a matter of few minutes? Nimekuwa nikiamini kuwa Security ya Banking Systems huwa ni Strong sana lakini hii situation imebadilisha mawazo yangu completely!!

Wakuu, ninaomba tujadili inawezekanaje mtu akaweza kubreach systems za Bank kirahisi na ndani ya muda mfupi kiasi hicho. Is it possible mhusika akawa ni mtu mmoja? Au ni hacking device/software ipi ina uwezo wa kuscan log files/strokes za password zilizokuwa typed kwenye simu na kuweza kulock kila kitu kinachohusiana na device husika?

Ninatanguliza shukrani na samahani kwa andiko refu!
View attachment 1459093View attachment 1459092View attachment 1459091View attachment 1459094View attachment 1459097

Sent using Jamii Forums mobile app
poleni sn, hapo mkubali tu mmetapeliwa na sidhan kama kunamsaada. kuhusu hizo line inabidi mzifunge na kurenew zingine.
tuwe makini na matapeli
 
Kuna mdogo wangu nae alipigwa kwa staili hio.......kosa ni kuwapa simu tu wanakumaliza hawaombi password wala taarifa yeyote........ dogo walimpiga tigopesa, crdb sim banking napo walikomba anashtuka anatumiwa mesej tu ya muamala kukamilika watu wameshabeba chao
 
Jombi inawezekana kabisa,Mfumo wa mawasiliano kati ya Mtandao wa Simu na Benki ni kwa kutumia SMS,Password yako ya SIM banking ni kwa ajili ya kuwezesha kutuma SMS tu na SMS ikienda kwenye Bank maana yake ni simu yako imetuma.Kwa maana nyingine mtu anapokuwa na simu yako na kisha kuwa password yako ya kuruhusu menu ya SIM banking itume messeji basi unakuwa tayari na access ya akaunti.

Sasa hapo kwenye Password ya Simbanking yako ndo ambapo panahitaji akili ya ziada na maelezo kutoka benki kwani kutakuwa na namna mtu anaweza pata access ya hio system na kukwiba PESA ambayo sidhani kama inafaa kujadiliwa humu mtandaoni ila zaidi ijadiliwe na wataalamu wa Cybe security kwenye Mabenk.
 
Kuna mdogo wangu nae alipigwa kwa staili hio.......kosa ni kuwapa simu tu wanakumaliza hawaombi password wala taarifa yeyote........ dogo walimpiga tigopesa, crdb sim banking napo walikomba anashtuka anatumiwa mesej tu ya muamala kukamilika watu wameshabeba chao
Noama saba mkuuu watu wanamjaza upepo mwana kama Mkewe kamzunguka lakini hapana aiseee Huu wizi upo sana tuu mimi kuna mwana aliibiwa Mil 1.5 sababu tu alipoteza line yake aliyojiunga nayo Sim banking akapuuzia hakufatilia sijui ikawaje jamaa baada ya kama miezi sita anashangaa bank pesa zimekombwaa na alieiba hakushika hata simu yake na wala hakuwa anajua password balaa sana
 
Noama saba mkuuu watu wanamjaza upepo mwana kama Mkewe kamzunguka lakini hapana aiseee Huu wizi upo sana tuu mimi kuna mwana aliibiwa Mil 1.5 sababu tu alipoteza line yake aliyojiunga nayo Sim banking akapuuzia hakufatilia sijui ikawaje jamaa baada ya kama miezi sita anashangaa bank pesa zimekombwaa na alieiba hakushika hata simu yake na wala hakuwa anajua password balaa sana
Hii kitu kama mtu haijamtokea hawezi kuelewa
 
Back
Top Bottom