Msaada: Tumetapeliwa!

Msaada: Tumetapeliwa!

Afu mtu yoyote anaetapeliwa cha kwanza ni lazima awe mtu wa tamaa, Kwenye swala la kuweka mtu sehemu sensitive za hela ivo mchunguze kwanza kama ni mtu wa tamaa tu ataibiwa afu tumeshatoa angalizo pia smartphone sio secure kabisa katika swala la mawasiliano ziko vulnerable sana na mtu anaetumia smartphone anakuwa targeted kirahisi kuliko anaetumia basic phone, Mimi smartphone kwangu ina chip kwa ajili ya net tu na wala hio chip sipigi simu wala sms ni Kuweka mb tu nakuperuzi tu ila the rest comms nazifanya kwa Vitochi na najihisi niko save and secured, Japo Hivi Vitochi navyo mamlaka ya nchi yanaweza kuwa na calls na Sms logs ila kama sio threat basi haina shida, smartphone zote nazo kwenye izo apps kama whatspp na telegram ni very secured na ziko na end to end encryption
smartphone sio tatizo hata ukiwa na sim ya torch bado una weza ibiwa vile vile usipo kua makini hii game naifahamu nje ndani beware

Sent using Xiaomi Redmi Note7 Pro
 
Hao jamaa waliokuwa dukani na huyo wakala wote lao mmoja na kama wakala alipewa kitambulisho bas huwa wanaangalia mwaka wa kuzaliwa ama tarehe na mwezi ndio wanabahatisha kuwa password. Watu wengi password zao wanaweka miaka ya kuzaliwa ama tarehe na mwezi, ama zile namba za kati kati kwny simu ndogo ya kitoch.

Kosa kubwa mnalolifanya ni kumkabidhi simu wakala, hili ni kosa kubwa sana na hata kampuni za simu linawakataza msiwape wakala simu zenu hata mkitaka huduma gani ni bora kwenda kwny shopping center zao ambapo ni uhakika
Huu ndio ukweli! Wengi sana wanatumia hivo ulizoeleza na ndivyo wizi unapofanyika
 
uyo mkeo kaibiwa kwa njia hii
menu ya malipo ya serikali *152*00#
wakala ame fanya kama ana taka kuangalia bill mara nying hua wana angalia kweny bill ya maji sehem ya kuweka namba ya mita ana mwambia weka namba ya siri sms itarud kua umeingiza namba isiyo sahihi kisha ile namba ita kuja kweny mabano i.e (1965) tayar wakala anakua kesha ona namba ya siri apo ana futa sms kisha ana hamisha pesa pasi ya ww kufahamu na wakat mwngne wana weka na hizo barring kuzuia sms ama kupiga mfano alivo kua ana shindwa kuaccess huduma za bank

Sent using Xiaomi Redmi Note7 Pro
Wakuu ninaomba msaada wenu katika hili...

Ilikuwa siku ya Jumamosi ya tarehe 23/05/2020 nilipokea taarifa kutoka kwa wife akinitaarifu kuwa ametapeliwa na wakala wa mitandao ya simu aliyekuwa amevalia mavazi na kitambulisho cha kampuni ya TIGO.

Wakala huyo alifika dukani kwake na kumwambia kuwa anaunganisha vifurushi vya chuo, hapo dukani palikuwa na wateja wawili ambao nao waliomba kupatiwa hiyo huduma kutoka kwa wakala huyo na walionesha kuridhika na huduma yake.

Wife alivyoona wateja hao wamepatiwa huduma na wameprove inafanya kazi vizuri naye aliomba aunganishwe. Alimpatia simu wakala huyo na, kutokana na maelezo yake, alikuwa anashuhudia kila kitu alichokuwa anafanya. Anasema kwamba wakala huyo alitumia muda mwingi katika eneo la 'Access Point Names' (APN).

Baada ya dakika kadhaa alimaliza shughuli yake na kumrudishia wife simu yake na alimtaka ajaribu kama mtandao unafanya kazi ambapo mwanzoni uligoma, akamrudishia simu akaenda tena kwenye APN akarekebisha akamwambia ajaribu ndipo mtandao ukarudi. Alimuaga na kumuhakikishia kwamba kila kitu kipo vizuri na atarudi baadae ili kupata mrejesho. Katika mchakato wote huo, wakala hakuomba wala kuonesha dalili yoyote ya kutaka kufahamu namba ya siri ya TigoPesa wala Bank katika mazungumzo yake.

Baada ya wakala huyo kuondoka wife alipata hitaji la kuhamisha fedha kutoka CRDB SimBanking kwenda kwa mtu aliyemuagiza mzigo. Tatizo lilianza kila anapoingiza menu ya SimBanking (*150*03#) anapata error inayoleta ujumbe 'Try Again Later....'

Baada ya kujaribu muda mrefu bila mafanikio alinipigia na kuniuliza endapo SimBanking yangu inafanya kazi, nilimwambia ipo poa. Pia baada ya kuconfirm na watu wengine na kuambiwa hakuna shida yoyote ndipo alianza kuhisi 'hali ya hatari' kwamba kuna kitu yule wakala amefanya kwenye simu yake.

Alipiga simu Huduma kwa Mteja CRDB akaambiwa kuwa muda si mrefu ametoa fedha (kiasi kimehifadhiwa) kutoka katika akaunti yake kwenda kwenye namba ya VODACOM +255 743 938 273 iliyosajiliwa kwa jina la NYAMIZI MASANJA. Pamoja na wife kuwataarifu watu wa Bank situation iliyotokea still walisisitiza kuwa fedha hizo amezihamisha yeye. Kitu pekee ambacho wameshindwa kukitolea maelezo hadi sasa ni error ya 'Try Again Later....' ambayo ni kama vile wameblock asiweze kuaccess SimBanking yake.

Alipiga simu VODACOM na kutaarifiwa kwamba fedha hiyo imeshatolewa kwa wakala na hivyo hawana cha kufanya. Tuliwarudia tena watu wa TIGO na walisisitiza kuwa endapo Transaction hiyo ingefanyika kwa TIGOPESA basi wangewajibika kuifuatilia lakini kwakuwa ni Bank tufuatilie kwenye taasisi husika!

Pia namba hiyo ya wife imeunganishwa na
NMB Mobile Banking, tulipoangalia salio huko napo tulikuta pesa yote imechukuliwa pia. Na kila akiingiza menu ya NMB Mobile Banking *150*66# nayo inaleta same error ya 'Try Again Later....' Kiufupi ni kwamba Wakala huyo aliweza kubreak Bank Accounts zote ambazo zimekuwa linked na hiyo namba ya TIGO na kuziblock zisiweze kutumika kupitia namba hiyo (hadi sasa)!

To cut the long story short, ni kwamba tangu siku hiyo ya Jumamosi, wife hawezi tena kuingia kwenye SimBanking & NMB Mobile Banking, hapati meseji za TIGOPESA, vifurushi na meseji za aina zote zinazohusiana na huduma za TIGO. Pia Internet haifanyi kazi, App pekee ambayo inakubali mtandao ni WhatsApp tu, but the rest (Google, Facebook, etc) hazifanyi kazi kabisa!

Personally, huwa ni mtundu kiaina kwenye mambo ya IT but this level of crime has amazed me so much. Inakuwaje mtu anaweza kuingia kwenye Bank Accounts na kujitumia pesa bila namba ya siri? How come baada ya kufanya hivyo anakuwa na uwezo wa kublock systems zote zinazohusiana na namba husika in just a matter of few minutes? Nimekuwa nikiamini kuwa Security ya Banking Systems huwa ni Strong sana lakini hii situation imebadilisha mawazo yangu completely!!

Wakuu, ninaomba tujadili inawezekanaje mtu akaweza kubreach systems za Bank kirahisi na ndani ya muda mfupi kiasi hicho. Is it possible mhusika akawa ni mtu mmoja? Au ni hacking device/software ipi ina uwezo wa kuscan log files/strokes za password zilizokuwa typed kwenye simu na kuweza kulock kila kitu kinachohusiana na device husika?

Ninatanguliza shukrani na samahani kwa andiko refu!
View attachment 1459093View attachment 1459092View attachment 1459091View attachment 1459094View attachment 1459097

Sent using Jamii Forums mobile app
soma hiz quotes kisha muhoji vizuri hakuna cha It wala Ict iliyo tumika apa

Sent using Xiaomi Redmi Note7 Pro
 
uyo mkeo kaibiwa kwa njia hii
menu ya malipo ya serikali *152*00#
wakala ame fanya kama ana taka kuangalia bill mara nying hua wana angalia kweny bill ya maji sehem ya kuweka namba ya mita ana mwambia weka namba ya siri sms itarud kua umeingiza namba isiyo sahihi kisha ile namba ita kuja kweny mabano i.e (1965) tayar wakala anakua kesha ona namba ya siri apo ana futa sms kisha ana hamisha pesa pasi ya ww kufahamu na wakat mwngne wana weka na hizo barring kuzuia sms ama kupiga mfano alivo kua ana shindwa kuaccess huduma za bank

Sent using Xiaomi Redmi Note7 Pro
Haya, umefanikiwa kutengeneza wezi wapya 500, hongera.
 
OK. Mkuu hili ni la kizembe. Sioni tahadhari yoyote uliyochukuwa. Ungemwambia alete mzigo ukiuona ndiyo umkabidhi cash. Na zaidi..... kujiepusha na utapeli siku zote epuka rahisi au short cut.
Kale kaneno...' sipokei hela ya mtu hadi nimkabidhi mzigo wake'.... kalinitoa kwenye umakini.
Hata hivyo ninakubali ulichosema ni uzembe nilifanya.
 
Inavyoonekana jamaa alivuruga mpangilio wa internet halaf akampa sim wife wako na kumwambia ajaribu app ikiwemo hizo za bank na hapo ndipo alipopata password, ilivyogoma ku access internet akamrudishia ili amrekebishie hapo ndipo jamaa alipofanya yake na kuhamisha mpunga, watz weng hatujielew kabisaaa we are so easy trusting everybody tubadilike!!!!!! we mtu haupo chuon unataka kifurush cha chuo cha nin????

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Haya, umefanikiwa kutengeneza wezi wapya 500, hongera.
mimi nime fanya awareness kwa wale ambao hawafahamu na sio jambo la siri kwamba wasijue na hili niliweza fahamu baada ya kuona video ya askari waki muhoji mmoja ya watuhumiwa aelezee jinsi wanavo ibia watu video ipo mtandaoni ime tapakaa..

Sent using Xiaomi Redmi Note7 Pro
 
Kwa ishu ya passcode za bank nina waswas na hao wateja wawili wa mwanzoni kuwa walikuwa hapo kwa muda wakihudumiwa so walimsoma mtoahuduma code anazoingiza na kuna namna waliziwasilisha kwa huyo wakala aliyekujua.Yan kiufupi tukio zima lina dalili ya teamwork.
 
mimi nime fanya awareness kwa wale ambao hawafahamu na sio jambo la siri kwamba wasijue na hili niliweza fahamu baada ya kuona video ya askari waki muhoji mmoja ya watuhumiwa aelezee jinsi wanavo ibia watu video ipo mtandaoni ime tapakaa..

Sent using Xiaomi Redmi Note7 Pro
Mbona kuna video za porno nyingi zipo mtandaoni, umeshaekti ya kwako?
 
Smart phones huwa zina tabia ya kutunza password kwenye app ya Swiftkey sasa alipoomba simu arekebishe mtandao alitumia muda huo kuiba tena kwa haraka. Kwanini atoe simu ya biashara kumpa mtu asiyemjua hilo ni kosa kubwa mno limewagharimu.
 
uyo mkeo kaibiwa kwa njia hii
menu ya malipo ya serikali *152*00#
wakala ame fanya kama ana taka kuangalia bill mara nying hua wana angalia kweny bill ya maji sehem ya kuweka namba ya mita ana mwambia weka namba ya siri sms itarud kua umeingiza namba isiyo sahihi kisha ile namba ita kuja kweny mabano i.e (1965) tayar wakala anakua kesha ona namba ya siri apo ana futa sms kisha ana hamisha pesa pasi ya ww kufahamu na wakat mwngne wana weka na hizo barring kuzuia sms ama kupiga mfano alivo kua ana shindwa kuaccess huduma za bank

Sent using Xiaomi Redmi Note7 Pro
Aisee, hili ni janga kubwa. Angalau tumepata elimu, ilà hapa umetengeneza bomu lingine.
 
Back
Top Bottom