Msaada: Tumetapeliwa!

Kasu

JF-Expert Member
May 3, 2012
382
282
Wakuu ninaomba msaada wenu katika hili...

Ilikuwa siku ya Jumamosi ya tarehe 23/05/2020 nilipokea taarifa kutoka kwa wife akinitaarifu kuwa ametapeliwa na wakala wa mitandao ya simu aliyekuwa amevalia mavazi na kitambulisho cha kampuni ya TIGO.

Wakala huyo alifika dukani kwake na kumwambia kuwa anaunganisha vifurushi vya chuo, hapo dukani palikuwa na wateja wawili ambao nao waliomba kupatiwa hiyo huduma kutoka kwa wakala huyo na walionesha kuridhika na huduma yake.

Wife alivyoona wateja hao wamepatiwa huduma na wameprove inafanya kazi vizuri naye aliomba aunganishwe. Alimpatia simu wakala huyo na, kutokana na maelezo yake, alikuwa anashuhudia kila kitu alichokuwa anafanya. Anasema kwamba wakala huyo alitumia muda mwingi katika eneo la 'Access Point Names' (APN).

Baada ya dakika kadhaa alimaliza shughuli yake na kumrudishia wife simu yake na alimtaka ajaribu kama mtandao unafanya kazi ambapo mwanzoni uligoma, akamrudishia simu akaenda tena kwenye APN akarekebisha akamwambia ajaribu ndipo mtandao ukarudi. Alimuaga na kumuhakikishia kwamba kila kitu kipo vizuri na atarudi baadae ili kupata mrejesho. Katika mchakato wote huo, wakala hakuomba wala kuonesha dalili yoyote ya kutaka kufahamu namba ya siri ya TigoPesa wala Bank katika mazungumzo yake.

Baada ya wakala huyo kuondoka wife alipata hitaji la kuhamisha fedha kutoka CRDB SimBanking kwenda kwa mtu aliyemuagiza mzigo. Tatizo lilianza kila anapoingiza menu ya SimBanking (*150*03#) anapata error inayoleta ujumbe 'Try Again Later....'

Baada ya kujaribu muda mrefu bila mafanikio alinipigia na kuniuliza endapo SimBanking yangu inafanya kazi, nilimwambia ipo poa. Pia baada ya kuconfirm na watu wengine na kuambiwa hakuna shida yoyote ndipo alianza kuhisi 'hali ya hatari' kwamba kuna kitu yule wakala amefanya kwenye simu yake.

Alipiga simu Huduma kwa Mteja CRDB akaambiwa kuwa muda si mrefu ametoa fedha (kiasi kimehifadhiwa) kutoka katika akaunti yake kwenda kwenye namba ya VODACOM +255 743 938 273 iliyosajiliwa kwa jina la NYAMIZI MASANJA. Pamoja na wife kuwataarifu watu wa Bank situation iliyotokea still walisisitiza kuwa fedha hizo amezihamisha yeye. Kitu pekee ambacho wameshindwa kukitolea maelezo hadi sasa ni error ya 'Try Again Later....' ambayo ni kama vile wameblock asiweze kuaccess SimBanking yake.

Alipiga simu VODACOM na kutaarifiwa kwamba fedha hiyo imeshatolewa kwa wakala na hivyo hawana cha kufanya. Tuliwarudia tena watu wa TIGO na walisisitiza kuwa endapo Transaction hiyo ingefanyika kwa TIGOPESA basi wangewajibika kuifuatilia lakini kwakuwa ni Bank tufuatilie kwenye taasisi husika!

Pia namba hiyo ya wife imeunganishwa na
NMB Mobile Banking, tulipoangalia salio huko napo tulikuta pesa yote imechukuliwa pia. Na kila akiingiza menu ya NMB Mobile Banking *150*66# nayo inaleta same error ya 'Try Again Later....' Kiufupi ni kwamba Wakala huyo aliweza kubreak Bank Accounts zote ambazo zimekuwa linked na hiyo namba ya TIGO na kuziblock zisiweze kutumika kupitia namba hiyo (hadi sasa)!

To cut the long story short, ni kwamba tangu siku hiyo ya Jumamosi, wife hawezi tena kuingia kwenye SimBanking & NMB Mobile Banking, hapati meseji za TIGOPESA, vifurushi na meseji za aina zote zinazohusiana na huduma za TIGO. Pia Internet haifanyi kazi, App pekee ambayo inakubali mtandao ni WhatsApp tu, but the rest (Google, Facebook, etc) hazifanyi kazi kabisa!

Personally, huwa ni mtundu kiaina kwenye mambo ya IT but this level of crime has amazed me so much. Inakuwaje mtu anaweza kuingia kwenye Bank Accounts na kujitumia pesa bila namba ya siri? How come baada ya kufanya hivyo anakuwa na uwezo wa kublock systems zote zinazohusiana na namba husika in just a matter of few minutes? Nimekuwa nikiamini kuwa Security ya Banking Systems huwa ni Strong sana lakini hii situation imebadilisha mawazo yangu completely!!

Wakuu, ninaomba tujadili inawezekanaje mtu akaweza kubreach systems za Bank kirahisi na ndani ya muda mfupi kiasi hicho. Is it possible mhusika akawa ni mtu mmoja? Au ni hacking device/software ipi ina uwezo wa kuscan log files/strokes za password zilizokuwa typed kwenye simu na kuweza kulock kila kitu kinachohusiana na device husika?

Ninatanguliza shukrani na samahani kwa andiko refu!
View attachment 1459093View attachment 1459092View attachment 1459091
IMG-20200525-WA0010.jpg
A%2B%20Gallery.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app


UPDATE: Tumefanikiwa kuokoa fedha iliyohamishwa via CRDB SimBanking, tunaendelea kuifuatilia fedha ya NMB.
Asanteni kwa ushauri na miongozo yenu. Mwenyezi Mungu awabariki sana.!
 
khaaaaa...
Kila kukicha watu wanakuja na njia mpya...
Hao watu wawili waliokua pembeni, ni team moja walipangana tuu,

Ukiona mtu anakutangazia fursa halaf from nowhere tuu anatokea mtu anadakia, kimbia...

Japo pia hili suala ukizingatia security ya Bank na mitandao ya simu, basi Inatakiwa uwe na imani kubwa sana kutofikiria nje ya boks, ubaki hapo hapo kwa huyo wakala,

Ngoja na mimi niingie ndani ya 18 Nisije onekana mchawi.

Poleni sanaa..
 
Wakuu hii story kwangu bado nashindwa kuamini kama kweli hao jamaa wame break hizo security kirahisi simaanishi haliwezekani ila sio kirahisi ivo, Nashauri Point muhimu zaidi ni kuanza kuongea na Wife vizuri sana muite Sehemu msisikilize anavyojieleza, I smell something fishy hapo, simaanishi mke kakuzunguka ila watch her steps carefully hawa viumbe hawa hawa hawa hawa.

Ila swala la Internet àcces apo set upya tu au may be jamaa awe ali download firewall ya kuzinyima acces hizo app ila kwa inshu ya bank apo bado naumiza kichwa
 
Wakuu hii story kwangu bado nashindwa kuamini kama kweli hao jamaa wame break hizo security kirahisi simaanishi haliwezekani ila sio kirahisi ivo, Nashauri Point muhimu zaidi ni kuanza kuongea na Wife vizuri sana muite Sehemu msisikilize anavyojieleza, I smell something fishy hapo, simaanishi mke kakuzunguka ila watch her steps carefully hawa viumbe hawa hawa hawa hawa.
Hapana wife hana kosa, ila ni uwizi mpya technology ni pana sana mkuu tusimgombanishae jamaa na mkewe
 
Back
Top Bottom