Mimi hadi sasa nimeruka viunzi kadhaa vya matapeli. Na kiunzi cha mwisho ni abiria niliyekuwa nimekaa naye kwenye siti ya basiMkuu huu msiba ni wa jirani ndiyo maana unasema hivyo.
Hauwezi kupisha chambo cha tapeli, maana haukosi udhaifu wa kibinadamu na ndiyo fursa yao.
Wewe kama upo strong, basi washua hupitia hata kwa mama watoto ili akushawishi ulegee!
Tapeli hana sura wala rangi, yaani ni shetani anayekunasa kwa udhaifu wako wa sekunde1, ana uwezo wa kukulia mingo ya mwaka mzima kusubiria udhaifu wako wa sekunde!
Mimi ni mgumu na ni mjanja, lakini nikikusimulia kisa cha namna nilivyotapeliwa utastaajabu!
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mimi nina duka wanasema: 'la kwa mangi' zaga zaga zote huuza.Yoote uliyosema uko sahihi. Tapeli ni mtu mjanja sana na ana mbinu nyingi. Binafsi mm ni mgumu na hua simuamini mtu yyte, ila siku tumetoka na wife alijikuta mikononi mwa matapeli.
Moro msamvu pale kuna wahuni walkua wanajfanya wana kampuni na wanagawa vitenge bure pamoja na CD ili mkautangaze kampuni. Nkawatilia shaka ila wule kakomaa et twende.
Wahuni wale kufika tu et wanakupa coopon.. Et unashika ile coopon yenye namba, na CD mkononi na kitenge. Yaani unachezeshwa kamari bila taarifa.
Nkamwambia wife ebu tuondoke acha ujinga, kumbe ashatoa buku ten tayar ili ashinde tv. qmmk. Nilitaman nimzabe makofi pale.
Ila niliwakomalia kibabe ile hela waliitoa. Mjini wahuni wengi sana.
Kuna mhuni mwingne niko zangu namsikiliza mbowe akihutubia, ananiijia et nimpe simu yangu aingie youtube chanel ake. Kumkazia akataka nimpe simu ndogo, nkamkata jicho, ikabid asepe tu. Wahuni ukiwapa muda kiduchu umeisha.
Nipe story mkuu, ilikuaje kwa upande wako?
Hakuwai kukuambia mtajie password? Na simu yako ilikuwa kitoch au smart?Pole mkuu wamenipiga hta mm 223000 kwenye simu yangu alikuja km hvyo kwako nkamkabidhi cm akacheza nayo akaniambia huna salio la kawaida nataka mia tu ndio kosa hpo,sijui akafanyaje akahamisha hzo hela
Sent using Jamii Forums mobile app
Wakuu ninaomba msaada wenu katika hili...
Ilikuwa siku ya Jumamosi ya tarehe 23/05/2020 nilipokea taarifa kutoka kwa wife akinitaarifu kuwa ametapeliwa na wakala wa mitandao ya simu aliyekuwa amevalia mavazi na kitambulisho cha kampuni ya TIGO.
Wakala huyo alifika dukani kwake na kumwambia kuwa anaunganisha vifurushi vya chuo, hapo dukani palikuwa na wateja wawili ambao nao waliomba kupatiwa hiyo huduma kutoka kwa wakala huyo na walionesha kuridhika na huduma yake.
Wife alivyoona wateja hao wamepatiwa huduma na wameprove inafanya kazi vizuri naye aliomba aunganishwe. Alimpatia simu wakala huyo na, kutokana na maelezo yake, alikuwa anashuhudia kila kitu alichokuwa anafanya. Anasema kwamba wakala huyo alitumia muda mwingi katika eneo la 'Access Point Names' (APN).
Baada ya dakika kadhaa alimaliza shughuli yake na kumrudishia wife simu yake na alimtaka ajaribu kama mtandao unafanya kazi ambapo mwanzoni uligoma, akamrudishia simu akaenda tena kwenye APN akarekebisha akamwambia ajaribu ndipo mtandao ukarudi. Alimuaga na kumuhakikishia kwamba kila kitu kipo vizuri na atarudi baadae ili kupata mrejesho. Katika mchakato wote huo, wakala hakuomba wala kuonesha dalili yoyote ya kutaka kufahamu namba ya siri ya TigoPesa wala Bank katika mazungumzo yake.
Baada ya wakala huyo kuondoka wife alipata hitaji la kuhamisha fedha kutoka CRDB SimBanking kwenda kwa mtu aliyemuagiza mzigo. Tatizo lilianza kila anapoingiza menu ya SimBanking (*150*03#) anapata error inayoleta ujumbe 'Try Again Later....'
Baada ya kujaribu muda mrefu bila mafanikio alinipigia na kuniuliza endapo SimBanking yangu inafanya kazi, nilimwambia ipo poa. Pia baada ya kuconfirm na watu wengine na kuambiwa hakuna shida yoyote ndipo alianza kuhisi 'hali ya hatari' kwamba kuna kitu yule wakala amefanya kwenye simu yake.
Alipiga simu Huduma kwa Mteja CRDB akaambiwa kuwa muda si mrefu ametoa fedha (kiasi kimehifadhiwa) kutoka katika akaunti yake kwenda kwenye namba ya VODACOM +255 743 938 273 iliyosajiliwa kwa jina la NYAMIZI MASANJA. Pamoja na wife kuwataarifu watu wa Bank situation iliyotokea still walisisitiza kuwa fedha hizo amezihamisha yeye. Kitu pekee ambacho wameshindwa kukitolea maelezo hadi sasa ni error ya 'Try Again Later....' ambayo ni kama vile wameblock asiweze kuaccess SimBanking yake.
Alipiga simu VODACOM na kutaarifiwa kwamba fedha hiyo imeshatolewa kwa wakala na hivyo hawana cha kufanya. Tuliwarudia tena watu wa TIGO na walisisitiza kuwa endapo Transaction hiyo ingefanyika kwa TIGOPESA basi wangewajibika kuifuatilia lakini kwakuwa ni Bank tufuatilie kwenye taasisi husika!
Pia namba hiyo ya wife imeunganishwa na
NMB Mobile Banking, tulipoangalia salio huko napo tulikuta pesa yote imechukuliwa pia. Na kila akiingiza menu ya NMB Mobile Banking *150*66# nayo inaleta same error ya 'Try Again Later....' Kiufupi ni kwamba Wakala huyo aliweza kubreak Bank Accounts zote ambazo zimekuwa linked na hiyo namba ya TIGO na kuziblock zisiweze kutumika kupitia namba hiyo (hadi sasa)!
To cut the long story short, ni kwamba tangu siku hiyo ya Jumamosi, wife hawezi tena kuingia kwenye SimBanking & NMB Mobile Banking, hapati meseji za TIGOPESA, vifurushi na meseji za aina zote zinazohusiana na huduma za TIGO. Pia Internet haifanyi kazi, App pekee ambayo inakubali mtandao ni WhatsApp tu, but the rest (Google, Facebook, etc) hazifanyi kazi kabisa!
Personally, huwa ni mtundu kiaina kwenye mambo ya IT but this level of crime has amazed me so much. Inakuwaje mtu anaweza kuingia kwenye Bank Accounts na kujitumia pesa bila namba ya siri? How come baada ya kufanya hivyo anakuwa na uwezo wa kublock systems zote zinazohusiana na namba husika in just a matter of few minutes? Nimekuwa nikiamini kuwa Security ya Banking Systems huwa ni Strong sana lakini hii situation imebadilisha mawazo yangu completely!!
Wakuu, ninaomba tujadili inawezekanaje mtu akaweza kubreach systems za Bank kirahisi na ndani ya muda mfupi kiasi hicho. Is it possible mhusika akawa ni mtu mmoja? Au ni hacking device/software ipi ina uwezo wa kuscan log files/strokes za password zilizokuwa typed kwenye simu na kuweza kulock kila kitu kinachohusiana na device husika?
Ninatanguliza shukrani na samahani kwa andiko refu!
View attachment 1459093View attachment 1459092View attachment 1459091View attachment 1459094View attachment 1459097
Sent using Jamii Forums mobile app
Dah, mkuu pole sana. Duh hawa jamaa wana akili sana. Yaan ni hatari sana.Mkuu mimi nina duka wanasema: 'la kwa mangi' zaga zaga zote huuza.
Kuna siku moja majira ya saa5 kuna njemba moja ikanikuta dukani huku imevaa tabasamu la kidugu.
Ikanisalimia kwa adabu sana.
Baadae akajitambulisha kuwa ni mtumishi wa railway.
kanambia kwamba yupo kitengo cha karakana, hivyo ofisini kwao huwa wanaletewa mgao wa sabuni kwa ajili ya usafi.
Lakini kila mgao ukitolewa wao huziuza madukani ili wapate pesa na bei wanayouza ni rafiki kwetu wafanyabiashara, maana ni vunja bei.
Nikamuuliza ana katoni ngapi, akaniambia zipo 10.
Ili kujikosha asionekane tapeli akanambia: 'mzee sisi hatupokei hela ya mtu hadi tumemkabidhi mzigo wake'.... 'mzee kwa kuwa una usafiri tupatie kijana wako tukamkabidhi'.
Kijana wangu alikuwepo kweli, nami siku hiyo nilikuwa bize, nikamtuma afuatane naye na kiasi cha pesa tuliyokuwa tumekubaliana akawa nazo kijana!
Walipofika eneo la station habari ikabadilika, kijana wangu akaelezwa asubiri nje, dakika 0 jamaa likarudi, likamwambia kijana: 'boss kasema mzigo hatoi mpaka cash'.
Kijana akakabidhi pesa zote tulizokubaliana akaendelea kusubiri hapo nje.
Akakaa zaidi ya masaa mawili, mwisho akajiongeza,akaingia ndani kufuatilia.
Jamaa hakuwemo na kuna mlango upo wazi uani.
Ndani alikutana na wafanyakazi wapo bize na mambo yao, kuulizia wajihi wa huyo mtu, wakamwambia hawana staff wa hivyo.
Pamoja na umakini wangu, lakini neno moja tu lililonifubaza ni yule tapeli kujishusha na kusema...' sipokei hela ya mtu mpaka nimkabidhi mzigo wake'....
Hivyo ndivyo nilivyotapeliwa mkuu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana mkuu, hawa viumbe akili zao wanazijua wenyewe. Ni waongo na wanafiki kupindukia.ramli chonganishi
Mkuu mimi nina duka wanasema: 'la kwa mangi' zaga zaga zote huuza.
Kuna siku moja majira ya saa5 kuna njemba moja ikanikuta dukani huku imevaa tabasamu la kidugu.
Ikanisalimia kwa adabu sana.
Baadae akajitambulisha kuwa ni mtumishi wa railway.
kanambia kwamba yupo kitengo cha karakana, hivyo ofisini kwao huwa wanaletewa mgao wa sabuni kwa ajili ya usafi.
Lakini kila mgao ukitolewa wao huziuza madukani ili wapate pesa na bei wanayouza ni rafiki kwetu wafanyabiashara, maana ni vunja bei.
Nikamuuliza ana katoni ngapi, akaniambia zipo 10.
Ili kujikosha asionekane tapeli akanambia: 'mzee sisi hatupokei hela ya mtu hadi tumemkabidhi mzigo wake'.... 'mzee kwa kuwa una usafiri tupatie kijana wako tukamkabidhi'.
Kijana wangu alikuwepo kweli, nami siku hiyo nilikuwa bize, nikamtuma afuatane naye na kiasi cha pesa tuliyokuwa tumekubaliana akawa nazo kijana!
Walipofika eneo la station habari ikabadilika, kijana wangu akaelezwa asubiri nje, dakika 0 jamaa likarudi, likamwambia kijana: 'boss kasema mzigo hatoi mpaka cash'.
Kijana akakabidhi pesa zote tulizokubaliana akaendelea kusubiri hapo nje.
Akakaa zaidi ya masaa mawili, mwisho akajiongeza,akaingia ndani kufuatilia.
Jamaa hakuwemo na kuna mlango upo wazi uani.
Ndani alikutana na wafanyakazi wapo bize na mambo yao, kuulizia wajihi wa huyo mtu, wakamwambia hawana staff wa hivyo.
Pamoja na umakini wangu, lakini neno moja tu lililonifubaza ni yule tapeli kujishusha na kusema...' sipokei hela ya mtu mpaka nimkabidhi mzigo wake'....
Hivyo ndivyo nilivyotapeliwa mkuu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo hakuwa wakala.Aisee! Pole kamanda ila hao mawakala wa barabarani, asilimia kubwa ni matapeli
Hii ipo mpaka kwenye mitandao ya simu.. mwezi uliopita nilitoka kuongea tu na kijana wangu wa shambani, tulikuwa tunaongea masuala ya pesa yake ila baada ya dakika chache nikapokea sms ikinielekeza nitume pesa kwenye namba fulani.Hiyo inanitokea mara kwa mara nnapokua nmeshafanya muamala kutuma ela kwa NMB Mobile.
Kuna wapuuz Ela ikishatumwa TU, wanatumia sms.
"Ela itumu kwny hi Namba*****, jina Herman Mnyamisi. Simu yangu inazima chaji."
Nnawasiwasi huu mchezo, watu wa benki wanashiriki.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi naamini kuna sehemu ana ficha mkewe,,, Lazima aliambiwa Weka Namba ya siri hapa ili huduma ikamilike,, narudia tena Lazima Aliambiwa hivyo.. Na kamwe hawezi kusema ukweli ataonekana Mzembe,,,,,,Huo ndo ukweli imewatokea wengi....!!!Mwambie mkeo aeleze ukweli, hayo maelezo aliyotoa hayajitoshelezi kabisa na hayana mashiko.
.
Kwani akijitambulisha mara nyingi wanajitambulisha kuwa ni mawakalaHuyo hakuwa wakala.
Ni mwizi aliyebeba bango la tigo