Msaada: Tumetapeliwa!

Msaada: Tumetapeliwa!

Hapana wife hana kosa, ila ni uwizi mpya technology ni pana sana mkuu tusimgombanishae jamaa na mkewe
Unampaje device mtu comfortably ukijua kuna apps zenye mpunga aisee. Wife mfundishe kudeal na wabongo
 
Aseah pole sana kila siku wezi wanabuni njia mpya ya kufanya wizi hawa mawakala wanaotembea mitaani wengi wanawalalamikia kwavitendo vya wizi wa mitandaoni

Kuna siku mtaan napoishi walipita hawa mawakala wakinadi wanasajili laini kwa alama za vidole sasa mke wangu aliwaita wamsajilie mmoja ya wale mawakala akawa naendelea na zoezi la kumsajilia mke wangu lakin mke wangu katika simu yake kaset typing prediction on alichokua anafanya yule wakala aliingia kwenye menu ya halopesa akawa anafanya muamala mara ikaingia sms kwenye simu sasa yule wakala akawa anataka kuifuta wife analazimisha lazima aisome dah ukawa mzozo kuna jirani akanipigia simu kwakua sikua mbali nikaenda faster kufika nakuta watu washajaa wakala kagoma simu isisomwe sms nikamwambia kama kweli hakuna tatizo kwann simu aikatazie mana hata kumpa mwenye simu hataki mpaka amalize usajili ikabidi nguvu itumike kuitoa lock jamaa kaamisha 765000 tulipompa kibano akaeleza njia mojawapo ni typing prediction yaan kama simu ikiwa na typing prediction on basi hawa vijana wanaibia watu kirahisi sana tuweni makini

Sent using Jamii Forums mobile app
Swift keyboard hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muulize vizuri mkeo isije ikawa huyo aliyemwibia hela ni mchepuko wake unajua namba zake za siri but wamegombana so jamaa akaamua liwalo na liwe
 
Huyo wife wako kuna kitu amekuficha ili usionekane mjinga,muulize vizuri.
Acha uchonganishi mkuu, hii kitu ipo.

Maza angu aliibiwa hela Na wakala ila ye zilikuwa kwenye ac ya airtel money (more than 150k) wanaibaje ibaje me sijui na hapo namba ya siri wala hakumpa
 
Inabidi uanzie bank wakwambie hela imeenda katika account gani
 
Kuna mambo mawili apo maana huwez kuaccess account ya mtu bila kujua namba za siri

1. Moja inawezekana wife alitaja namba za siri bila kujua akajakushtuka kaishaibiwa na kakuficha kama alitaja namba za siri ili asionekana mjinga


2. Inawezekana wife anajua yeye alipo peleka izo pesa na kuamua kufunga sim banking maana unaweza kumuomba simu uingize menyu ya simu banking usipokuta error utashtuka

Zingatia hayo mambo mawili mwisho haiwezekani na haitawezekana kamwe mtu kuibiwa bila namba ya siri hata kwa technologia ya apple au bill gates never ever

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona ishu ya mobile banking kuandika try again later huizungumzii.
 
Wakuu ninaomba msaada wenu katika hili...

Ilikuwa siku ya Jumamosi ya tarehe 23/05/2020 nilipokea taarifa kutoka kwa wife akinitaarifu kuwa ametapeliwa na wakala wa mitandao ya simu aliyekuwa amevalia mavazi na kitambulisho cha kampuni ya TIGO.

Wakala huyo alifika dukani kwake na kumwambia kuwa anaunganisha vifurushi vya chuo, hapo dukani palikuwa na wateja wawili ambao nao waliomba kupatiwa hiyo huduma kutoka kwa wakala huyo na walionesha kuridhika na huduma yake.

Wife alivyoona wateja hao wamepatiwa huduma na wameprove inafanya kazi vizuri naye aliomba aunganishwe. Alimpatia simu wakala huyo na, kutokana na maelezo yake, alikuwa anashuhudia kila kitu alichokuwa anafanya. Anasema kwamba wakala huyo alitumia muda mwingi katika eneo la 'Access Point Names' (APN).

Baada ya dakika kadhaa alimaliza shughuli yake na kumrudishia wife simu yake na alimtaka ajaribu kama mtandao unafanya kazi ambapo mwanzoni uligoma, akamrudishia simu akaenda tena kwenye APN akarekebisha akamwambia ajaribu ndipo mtandao ukarudi. Alimuaga na kumuhakikishia kwamba kila kitu kipo vizuri na atarudi baadae ili kupata mrejesho. Katika mchakato wote huo, wakala hakuomba wala kuonesha dalili yoyote ya kutaka kufahamu namba ya siri ya TigoPesa wala Bank katika mazungumzo yake.

Baada ya wakala huyo kuondoka wife alipata hitaji la kuhamisha fedha kutoka CRDB SimBanking kwenda kwa mtu aliyemuagiza mzigo. Tatizo lilianza kila anapoingiza menu ya SimBanking (*150*03#) anapata error inayoleta ujumbe 'Try Again Later....'

Baada ya kujaribu muda mrefu bila mafanikio alinipigia na kuniuliza endapo SimBanking yangu inafanya kazi, nilimwambia ipo poa. Pia baada ya kuconfirm na watu wengine na kuambiwa hakuna shida yoyote ndipo alianza kuhisi 'hali ya hatari' kwamba kuna kitu yule wakala amefanya kwenye simu yake.

Alipiga simu Huduma kwa Mteja CRDB akaambiwa kuwa muda si mrefu ametoa fedha (kiasi kimehifadhiwa) kutoka katika akaunti yake kwenda kwenye namba ya VODACOM +255 743 938 273 iliyosajiliwa kwa jina la NYAMIZI MASANJA. Pamoja na wife kuwataarifu watu wa Bank situation iliyotokea still walisisitiza kuwa fedha hizo amezihamisha yeye. Kitu pekee ambacho wameshindwa kukitolea maelezo hadi sasa ni error ya 'Try Again Later....' ambayo ni kama vile wameblock asiweze kuaccess SimBanking yake.

Alipiga simu VODACOM na kutaarifiwa kwamba fedha hiyo imeshatolewa kwa wakala na hivyo hawana cha kufanya. Tuliwarudia tena watu wa TIGO na walisisitiza kuwa endapo Transaction hiyo ingefanyika kwa TIGOPESA basi wangewajibika kuifuatilia lakini kwakuwa ni Bank tufuatilie kwenye taasisi husika!

Pia namba hiyo ya wife imeunganishwa na
NMB Mobile Banking, tulipoangalia salio huko napo tulikuta pesa yote imechukuliwa pia. Na kila akiingiza menu ya NMB Mobile Banking *150*66# nayo inaleta same error ya 'Try Again Later....' Kiufupi ni kwamba Wakala huyo aliweza kubreak Bank Accounts zote ambazo zimekuwa linked na hiyo namba ya TIGO na kuziblock zisiweze kutumika kupitia namba hiyo (hadi sasa)!

To cut the long story short, ni kwamba tangu siku hiyo ya Jumamosi, wife hawezi tena kuingia kwenye SimBanking & NMB Mobile Banking, hapati meseji za TIGOPESA, vifurushi na meseji za aina zote zinazohusiana na huduma za TIGO. Pia Internet haifanyi kazi, App pekee ambayo inakubali mtandao ni WhatsApp tu, but the rest (Google, Facebook, etc) hazifanyi kazi kabisa!

Personally, huwa ni mtundu kiaina kwenye mambo ya IT but this level of crime has amazed me so much. Inakuwaje mtu anaweza kuingia kwenye Bank Accounts na kujitumia pesa bila namba ya siri? How come baada ya kufanya hivyo anakuwa na uwezo wa kublock systems zote zinazohusiana na namba husika in just a matter of few minutes? Nimekuwa nikiamini kuwa Security ya Banking Systems huwa ni Strong sana lakini hii situation imebadilisha mawazo yangu completely!!

Wakuu, ninaomba tujadili inawezekanaje mtu akaweza kubreach systems za Bank kirahisi na ndani ya muda mfupi kiasi hicho. Is it possible mhusika akawa ni mtu mmoja? Au ni hacking device/software ipi ina uwezo wa kuscan log files/strokes za password zilizokuwa typed kwenye simu na kuweza kulock kila kitu kinachohusiana na device husika?

Ninatanguliza shukrani na samahani kwa andiko refu!
View attachment 1459093View attachment 1459092View attachment 1459091View attachment 1459094View attachment 1459097

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkeo kuna sehemu kakuficha mwambie akueleze ukweli, kuna mazingira yalitokea akataja namba yake ya siri tu, kuhusu hiyo error anayopata sina utaalamu nayo
 
Back
Top Bottom