Msaada: Tumetapeliwa!

Msaada: Tumetapeliwa!

Aseah pole sana kila siku wezi wanabuni njia mpya ya kufanya wizi hawa mawakala wanaotembea mitaani wengi wanawalalamikia kwavitendo vya wizi wa mitandaoni

Kuna siku mtaan napoishi walipita hawa mawakala wakinadi wanasajili laini kwa alama za vidole sasa mke wangu aliwaita wamsajilie mmoja ya wale mawakala akawa naendelea na zoezi la kumsajilia mke wangu lakin mke wangu katika simu yake kaset typing prediction on alichokua anafanya yule wakala aliingia kwenye menu ya halopesa akawa anafanya muamala mara ikaingia sms kwenye simu sasa yule wakala akawa anataka kuifuta wife analazimisha lazima aisome dah ukawa mzozo kuna jirani akanipigia simu kwakua sikua mbali nikaenda faster kufika nakuta watu washajaa wakala kagoma simu isisomwe sms nikamwambia kama kweli hakuna tatizo kwann simu aikatazie mana hata kumpa mwenye simu hataki mpaka amalize usajili ikabidi nguvu itumike kuitoa lock jamaa kaamisha 765000 tulipompa kibano akaeleza njia mojawapo ni typing prediction yaan kama simu ikiwa na typing prediction on basi hawa vijana wanaibia watu kirahisi sana tuweni makini

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi.Nilimshtukia mmoja hadi leo akiniona hunikwepa.
 
Kuna msemo wa kiswahili unasema "Ukitaka kutafuta nyoka anza kumulika miguuni pako". Mkuu hebu pia mfinye wife kidogo maana kwahiyo attachment uliyoweka hapo naona Kama wife mjanja mjanja kiaina.
Hamna ujanja wowote aliofanya mkewe,omba sana usikutane matapeli kama hao,uwa awakurupuki,itakua walikua wanamlia timing muda mrefu sana mpaka siku ya tukio

Sent from my SM-A705FN using JamiiForums mobile app
 
Wakuu hii story kwangu bado nashindwa kuamini kama kweli hao jamaa wame break hizo security kirahisi simaanishi haliwezekani ila sio kirahisi ivo, Nashauri Point muhimu zaidi ni kuanza kuongea na Wife vizuri sana muite Sehemu msisikilize anavyojieleza, I smell something fishy hapo, simaanishi mke kakuzunguka ila watch her steps carefully hawa viumbe hawa hawa hawa hawa.
Ila swala la Internet àcces apo set upya tu au may be jamaa awe ali download firewall ya kuzinyima acces hizo app ila kwa inshu ya bank apo bado naumiza kichwa
Ambane Mke wake vizuri, Amna wakala mtembea kwa miguu mwenye ujuzi huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haisaidii
Kwa nini haisaidii?
Huoni kama mtoa mada angekuwa na picha ya huyo mtu ingewekwa humu na social media zingine angepatikana na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria?

Sijakuelewa kwa nini unasema HAISAIDII
 
Wife anaogopa kusema ukweli alichofanya kwenye namba ya siri kwa kuhofia kuonekana mjinga.

Kuna binti mmoja aliwahi kunisimulia kuwa kakutana na matapeli wamempora simu na hela, yeye alidai kuwa, walimpulizia dawa na kila walichoongea alikubali. Nilipombana vizuri, nilibaini kuwa, vitu vile alivitoa mwenyewe kwa sababu walimdanganya ana rongwa na shangazi yake na bla bla nyingi mpaka akaingia mkenge.
 
Kwa nini haisaidii?
Huoni kama mtoa mada angekuwa na picha ya huyo mtu ingewekwa humu na social media zingine angepatikana na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria?

Sijakuelewa kwa nini unasema HAISAIDII

Yale majitu ni ngumu sana kukamatika...na simu zetu techno hizo sura inatoka kama sio yeye!
 
Hao jamaa waliokuwa dukani na huyo wakala wote lao mmoja na kama wakala alipewa kitambulisho bas huwa wanaangalia mwaka wa kuzaliwa ama tarehe na mwezi ndio wanabahatisha kuwa password. Watu wengi password zao wanaweka miaka ya kuzaliwa ama tarehe na mwezi, ama zile namba za kati kati kwny simu ndogo ya kitoch.

Kosa kubwa mnalolifanya ni kumkabidhi simu wakala, hili ni kosa kubwa sana na hata kampuni za simu linawakataza msiwape wakala simu zenu hata mkitaka huduma gani ni bora kwenda kwny shopping center zao ambapo ni uhakika
 
Wakuu ninaomba msaada wenu katika hili...

Ilikuwa siku ya Jumamosi ya tarehe 23/05/2020 nilipokea taarifa kutoka kwa wife akinitaarifu kuwa ametapeliwa na wakala wa mitandao ya simu aliyekuwa amevalia mavazi na kitambulisho cha kampuni ya TIGO.

Wakala huyo alifika dukani kwake na kumwambia kuwa anaunganisha vifurushi vya chuo, hapo dukani palikuwa na wateja wawili ambao nao waliomba kupatiwa hiyo huduma kutoka kwa wakala huyo na walionesha kuridhika na huduma yake.

Wife alivyoona wateja hao wamepatiwa huduma na wameprove inafanya kazi vizuri naye aliomba aunganishwe. Alimpatia simu wakala huyo na, kutokana na maelezo yake, alikuwa anashuhudia kila kitu alichokuwa anafanya. Anasema kwamba wakala huyo alitumia muda mwingi katika eneo la 'Access Point Names' (APN).

Baada ya dakika kadhaa alimaliza shughuli yake na kumrudishia wife simu yake na alimtaka ajaribu kama mtandao unafanya kazi ambapo mwanzoni uligoma, akamrudishia simu akaenda tena kwenye APN akarekebisha akamwambia ajaribu ndipo mtandao ukarudi. Alimuaga na kumuhakikishia kwamba kila kitu kipo vizuri na atarudi baadae ili kupata mrejesho. Katika mchakato wote huo, wakala hakuomba wala kuonesha dalili yoyote ya kutaka kufahamu namba ya siri ya TigoPesa wala Bank katika mazungumzo yake.

Baada ya wakala huyo kuondoka wife alipata hitaji la kuhamisha fedha kutoka CRDB SimBanking kwenda kwa mtu aliyemuagiza mzigo. Tatizo lilianza kila anapoingiza menu ya SimBanking (*150*03#) anapata error inayoleta ujumbe 'Try Again Later....'

Baada ya kujaribu muda mrefu bila mafanikio alinipigia na kuniuliza endapo SimBanking yangu inafanya kazi, nilimwambia ipo poa. Pia baada ya kuconfirm na watu wengine na kuambiwa hakuna shida yoyote ndipo alianza kuhisi 'hali ya hatari' kwamba kuna kitu yule wakala amefanya kwenye simu yake.

Alipiga simu Huduma kwa Mteja CRDB akaambiwa kuwa muda si mrefu ametoa fedha (kiasi kimehifadhiwa) kutoka katika akaunti yake kwenda kwenye namba ya VODACOM +255 743 938 273 iliyosajiliwa kwa jina la NYAMIZI MASANJA. Pamoja na wife kuwataarifu watu wa Bank situation iliyotokea still walisisitiza kuwa fedha hizo amezihamisha yeye. Kitu pekee ambacho wameshindwa kukitolea maelezo hadi sasa ni error ya 'Try Again Later....' ambayo ni kama vile wameblock asiweze kuaccess SimBanking yake.

Alipiga simu VODACOM na kutaarifiwa kwamba fedha hiyo imeshatolewa kwa wakala na hivyo hawana cha kufanya. Tuliwarudia tena watu wa TIGO na walisisitiza kuwa endapo Transaction hiyo ingefanyika kwa TIGOPESA basi wangewajibika kuifuatilia lakini kwakuwa ni Bank tufuatilie kwenye taasisi husika!

Pia namba hiyo ya wife imeunganishwa na
NMB Mobile Banking, tulipoangalia salio huko napo tulikuta pesa yote imechukuliwa pia. Na kila akiingiza menu ya NMB Mobile Banking *150*66# nayo inaleta same error ya 'Try Again Later....' Kiufupi ni kwamba Wakala huyo aliweza kubreak Bank Accounts zote ambazo zimekuwa linked na hiyo namba ya TIGO na kuziblock zisiweze kutumika kupitia namba hiyo (hadi sasa)!

To cut the long story short, ni kwamba tangu siku hiyo ya Jumamosi, wife hawezi tena kuingia kwenye SimBanking & NMB Mobile Banking, hapati meseji za TIGOPESA, vifurushi na meseji za aina zote zinazohusiana na huduma za TIGO. Pia Internet haifanyi kazi, App pekee ambayo inakubali mtandao ni WhatsApp tu, but the rest (Google, Facebook, etc) hazifanyi kazi kabisa!

Personally, huwa ni mtundu kiaina kwenye mambo ya IT but this level of crime has amazed me so much. Inakuwaje mtu anaweza kuingia kwenye Bank Accounts na kujitumia pesa bila namba ya siri? How come baada ya kufanya hivyo anakuwa na uwezo wa kublock systems zote zinazohusiana na namba husika in just a matter of few minutes? Nimekuwa nikiamini kuwa Security ya Banking Systems huwa ni Strong sana lakini hii situation imebadilisha mawazo yangu completely!!

Wakuu, ninaomba tujadili inawezekanaje mtu akaweza kubreach systems za Bank kirahisi na ndani ya muda mfupi kiasi hicho. Is it possible mhusika akawa ni mtu mmoja? Au ni hacking device/software ipi ina uwezo wa kuscan log files/strokes za password zilizokuwa typed kwenye simu na kuweza kulock kila kitu kinachohusiana na device husika?

Ninatanguliza shukrani na samahani kwa andiko refu!
View attachment 1459093View attachment 1459092View attachment 1459091View attachment 1459094View attachment 1459097

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah polee sanaaa ,mkuu
 
Tumetapeliwa?? Sema umetapeliwa.
Mkeo mjanja mjanja sana, hapo kama hajakupiga wewe hiyo pesa basi ni lazima alimpa password huyo kijana
NASISITIZA; Hata uwe mtaalam vipi huwezi kutoa pesa bila kuijua password

Mfinye mkeo akueleze vizuri, usiwe boya wewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo mke kajiibia pesa kwa kushirikiana na wakala?
 
Aseah pole sana kila siku wezi wanabuni njia mpya ya kufanya wizi hawa mawakala wanaotembea mitaani wengi wanawalalamikia kwavitendo vya wizi wa mitandaoni

Kuna siku mtaan napoishi walipita hawa mawakala wakinadi wanasajili laini kwa alama za vidole sasa mke wangu aliwaita wamsajilie mmoja ya wale mawakala akawa naendelea na zoezi la kumsajilia mke wangu lakin mke wangu katika simu yake kaset typing prediction on alichokua anafanya yule wakala aliingia kwenye menu ya halopesa akawa anafanya muamala mara ikaingia sms kwenye simu sasa yule wakala akawa anataka kuifuta wife analazimisha lazima aisome dah ukawa mzozo kuna jirani akanipigia simu kwakua sikua mbali nikaenda faster kufika nakuta watu washajaa wakala kagoma simu isisomwe sms nikamwambia kama kweli hakuna tatizo kwann simu aikatazie mana hata kumpa mwenye simu hataki mpaka amalize usajili ikabidi nguvu itumike kuitoa lock jamaa kaamisha 765000 tulipompa kibano akaeleza njia mojawapo ni typing prediction yaan kama simu ikiwa na typing prediction on basi hawa vijana wanaibia watu kirahisi sana tuweni makini

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngoja niiweke off tenaa
 
Back
Top Bottom