Msaada Nimeibiwa Jamani

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Wana JF,napenda kuwapa taarifa kuwa,usiku wa kuamkia jana majira ya saa nane ucku,wezi walivunja mlango wa nyumba yangu na kuiba vitu vyote vilivyokuwepo seating room,
nachoshukuru tu kuwa mke wangu na ndugu walio kuwepo hapo nyumbani hawakudhuriwa na vibaka hao,
kwa kuwa nipo mbali na Nyumbani kwa sasa,naomba msaada wenu wana JF kwa wale waliopo Morogoro-Kihonda-Shule ya msingi Elu(Kihonda lukobe),kama itatoke umepambana na jamaa wanauza Friji,Tv,inveter,Redio,cution za makochi,Tv decoder,hivyo ni baadhi tu basi usisite kunijulisha kwa sms namba ya simu +8615202425864
Ingawaje wife ameshalipoti polisi lakini ni vyema pia kwa atakaye ona biashara ya namna hiyo maeneo ya kihonda morogoro kwa wale walioko morogoro mna weza nisaidia,kwani Nipo china kwa sasa inaniwia vigumu kufuatilia mali zangu

samahani kwa usumbufu wakuu
 
Too bad!
Pole sana broda!
Walitumia nafasi ya wewe kutokuwepo na ku'make advantage!!...
nadhani watu wa Kihonda wapo humu ndani watasaidia kwa lolote!...Je katika ndugu zako wanaoishi hapo, hakuna anayeweza kuuza ishu?...Mara nyingine mambo haya yanakuwa si ya mbali(especially kama hawakumuumiza yeyote!)
 
Pole sana Engineer. Kwa kweli wezi wanaturudisha nyuma sana.
Nashukuru Bitimkongwe,
Yaani yanibidi kuanza upya na tatizo lililopo ni kuwa vitu kwa sasa vipo juu nashindwa hata sielewi wapi pa kuanzia
Naelezwa kuwa baada ya ndugu kuamka asubuhi wakakuta mwarubaini umechomekwa karibu na mlango walio vunja,heheheheh,sasa sijui ndio ulio wafanya kulala fofo,
kwa kweli mwizi akipita ktk anga zangu sitakuwa na msamaa,watanisamehe kwa hilo,
 
Too bad!
Pole sana broda!
Walitumia nafasi ya wewe kutokuwepo na ku'make advantage!!...
nadhani watu wa Kihonda wapo humu ndani watasaidia kwa lolote!...Je katika ndugu zako wanaoishi hapo, hakuna anayeweza kuuza ishu?...Mara nyingine mambo haya yanakuwa si ya mbali(especially kama hawakumuumiza yeyote!)

Yeah,kuna kijana anadai aliamka saa sita kujisaidia na vitu vyote vilikuwepo,ila alivyo amaka tena saa kumi hakuweza kuona kitu zaidi ya sebure kuwa nyeupe
Chakushangaza nimefuga mbwa pale nyumbani lakini kwa siku hiyo hata kelele ya mbwa mmoja haikusikika,
ina uma kwa kweli ni bora uyasikie yakitokea kwa wengine,kwani nipo hatua mia nyuma kwa sasa
 
Pole sana Engineer wangu,
Nimesikitishwa kweli na tukio hilo lakini nadhani vibaka hao hawatauzia Kihonda tu. Naomba wana JF walioko Morogoro wamsaidie kama wataona vibaka wanauza vifaa hivyo.
Naamini kabisa sasa dunia ni kama kijiji na Morogoro inaendelea kwa haraka sana hivyo wanaweza kuuza eneo lolote la Morogoro kwani usafiri upo tu.

Wana JF watakusaidia kadri Mungu atakavyowajalia.

Masomo mema hapo China!

Eng. Dr. Magafu,F.F (Ph.D)
 
Pole sana ndgu yangu. Mungu akutie nguvu. Naamin Mungu atakujalia na utapata vingine zaid ya hivyo. Jaman wezi nyie ndo mana mwachomwa moto kla kukicha
 
Thats too bad.

Pole sana engineer, nachojua siku hizi vibaka wanautaalam wa kupuliza dawa ya usingizi vyumbani kwa kupitia dirishani.
Imemtokea jirani yangu hapa Dar maeneo ya Mbezi beach, wamekomba kila walichokiona sebuleni.

Pamoja na hasara uliyoipata tufarijike kwamba familia haikudhurika. With time Mungu atakuwezesha kupata samani zingine.
 
pole eng., nimeishi Morogoro, ngoja niongee na jamaa mmoja anaweza saidia kwa kuwapa kasi polisi wafuatilie suala hilo.
 
Pole sana mkuu. Unasema kuna kijana aliamka kwenda chooni kujisaidia na vitu vilikuwepo?? Kama alitoka nnje kujisaidia kuna uwezekano alisahau kufunga mlango then jamaa wakavamia na kuvhukua vitu kama vyao vile.

Usijali utapata vingine, shukuru Mungu familia yako haijaguswa na hao maharamia.
 
Pole sana Mkuu. Watu mliopo Morogoro wekeni macho na masikio wazi kuhusu vifaa hivyo.
 
Back
Top Bottom