A
Anonymous
Guest
Askari wa Lukobe, Morogoro wameshindwa kulinda Usalama wa raia, IGP Wambura tusaidie
Mimi ni Mkazi wa Kata ya Lukobe Mkoani Morogoro, miezi miwili iliyopita nivamiwa nyumbani kwangu nikaibiwa vitu vingi ndani hadi viatu vya Watoto, nilitoa taarifa Kituo kidogo cha Polisi Kihonda ila mpaka sasa hivi hakuna hatua zilizo chukulia.
Kabla ya mimi kuibiwa kuna jirani yangu alivamiwa akaibiwa vitu vyandani karibia vyote, akaripoti Polisi ila hakuna chochote kilichofanyika, isitoshe hawa vibaka wanaishi hapahapa Lukobe Makaburini.
Kwa ufupi karibia wavuta bangi wote wanaotajwa kuhusika katika matukio mbalimbali wamevamia Lukobe na kuvuta bangi ni hadharani.
Mtendaji wa Kata na Mwenyekiti wake wote wapo lakini hawachukui hatua zozote, tunashindwa kuelewa cha kufanya na isitoshe wanatuibia Wageni.
Juzijuzi hapa wamevamia mtaa mmmoja unaitwa Kwa Wagogo, wakawakata watu mapanga, wamewaibia vitu wameondoka, sasa tunashindwa tufanyaje.
Tunaomba kilio chetu kifike kwa Kamanda Mkuu wa Polisi Nchini, IGP Camillus Wambura labda tutapata msaada.
Tumeshajenga makazi yetu, kuhama huku inakuwa ngumu na kuendelea kuwa kimya ni kujiharibia sisi wenyewe.