Msaada: Nilifunga ndoa ya kidini, nahitaji cheti cha ndoa cha serikali

Dec 26, 2016
36
82
Habari zenu wadau wenzangu.

Miaka michache iliyopita nilifunga ndoa ya kidini na nikapata cheti cha kidini(BAKWATA), kwa sasa nalazimika kupata cheti cha ndoa kutoka serikalini (kazini kinahitajika), naomba kujua utaratibu ukoje kwa mtu ambae tayari alishafunga ndoa na anahitaji cheti cha serikali na gharama zikoje?

Asanteni
Nimepata maelekezo mazuri, nashukuru kwa ushirikiano wenu.

CLOSED,
 
Mh kwani cheti cha kidini kama ulivyokiita hakitambuliwi serikalini? Kwani hakiandikwi Jamhuri ya muungano wa Tanzania kabla ya hiyo BAKWATA?
 
Kwa kawaida cheti cha ndoa ni cha serikali. Ukifunga ndoa msikitini/Kanisani unapewa cheti cha ndoa cha serikali. Sasa sijui mleta mada alifungia ndoa wapi ambako hawakuwa na vyeti vya serikali...
 
Cheti cha ndoa ni kile kile, haijarishi umefungia ndoa wapi, iwe ni kanisani, bomani au msikitini, cheti ni kile kile kinachotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama hicho cheti kimeandikwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kimesainiwa na wanandoa na mashahidi wawili pamoja na aliyefungisha ndoa basi kinakubalika kokote.
 
Wakuu msiwe wabishi cheti cha Bakwata kwa sasa hakitambuliwi serikalini.
Mimi ni mtumishi nina akili timamu msidhani hapa naandika kitu nisichokijua.
Kama mtu hujui namna ya kunielekeza ni vema ukatulia tu
 
Cheti cha ndoa ni kile kile, haijarishi umefungia ndoa wapi, iwe ni kanisani, bomani au msikitini, cheti ni kile kile kinachotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama hicho cheti kimeandikwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kimesainiwa na wanandoa na mashahidi wawili pamoja na aliyefungisha ndoa basi kinakubalika kokote.
Wakuu msiwe wabishi cheti cha Bakwata kwa sasa hakitambuliwi serikalini.Mimi ni mtumishi nina akili timamu msidhani hapa naandika kitu nisichokijua.
Kama mtu hujui namna ya kunielekeza ni vema ukatulia tu
 
Cheti cha ndoa ni cha serikali, dini ni wakala tu wa kufungisha ndoa, kumbuka ndoa inayokubalika kwa mujibu wa sheria za ndoa ni mke mmoja, hivyo basi kwa waislamu mke wa kwanza tu ndiyo utapewa cheti cha ndoa cha serikali. Kumbuka kuwa mawakala wote wa kufungisha ndoa vyeti wanavyo, makanisani, misikitini na pia bomani.
 
Kwa kawaida cheti cha ndoa ni cha serikali. Ukifunga ndoa msikitini/Kanisani unapewa cheti cha ndoa cha serikali. Sasa sijui mleta mada alifungia ndoa wapi ambako hawakuwa na vyeti vya serikali...
Kama ungeleewa uzi wangu basi usingeandika hayo, alafu nipo serious nahitaji msaada sasa kama hili jambo hulijui just relax uendelee kusoma comments za wenzetu.
 
Nenda na hicho cheti chako kilichotolewa na BAKWATA kwenye ofisi yeyote ya RITA wataisajili hiyo ndoa Kiserikali na kukupatia certificate ya ndoa iliyotolewa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Cheti cha ndoa ni cha serikali, dini ni wakala tu wa kufungisha ndoa, kumbuka ndoa inayokubalika kwa mujibu wa sheria za ndoa ni mke mmoja, hivyo basi kwa waislamu mke wa kwanza tu ndiyo utapewa cheti cha ndoa cha serikali. Kumbuka kuwa mawakala wote wa kufungisha ndoa vyeti wanavyo, makanisani, misikitini na pia bomani.
Naona lugha gongana.
 
Cheti ni kimoja tu kinachotolewa na serikali iwe kwenye dini au Serikali.
 
Nenda na hicho cheti chako kilichotolewa na BAKWATA kwenye ofisi yeyote ya RITA wataisajili hiyo ndoa Kiserikali na kukupatia certificate ya ndoa iliyotolewa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Hii ndio comment ya kwanza niliyoona inatoa msaada, wengine wote wanaleta porojo za kuunganisha maneno mara Jamhuri ya Muungano mara msikiti.

Mkiona mtu kaleta jambo mjue hayo majibu marahisi anayajua tayari.

Nashukuru sana, ushauri wako ntaufanyia kazi.
 
Wakuu msiwe wabishi cheti cha Bakwata kwa sasa hakitambuliwi serikalini.Mimi ni mtumishi nina akili timamu msidhani hapa naandika kitu nisichokijua.
Kama mtu hujui namna ya kunielekeza ni vema ukatulia tu
Serikali ina kazi ya kufanya Kama mtu kama wewe umeajiriwa na serikali halafu kichwa Bomu kiasi hiki.ni hatari kwa maendeleo ya taifa.
 
Nenda na hicho cheti chako kilichotolewa na BAKWATA kwenye ofisi yeyote ya RITA wataisajili hiyo ndoa Kiserikali na kukupatia certificate ya ndoa iliyotolewa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Hicho kinachotolewa na BAKWATA ambacho RITA hawakijui ni cha aina gani?
 
Cheti ulichopewa na bakwata ndio hicho peleka huko kazini maana hicho ndio cheti cha ndoa kilichoidhinishwa na serikali, kama ww ni muislam utapewa na shekh alieidhinishwa na bakwata na kama ww ni mkristo utapewa padri aliekifungisha ndoa huko kanisani na kama ulifungia bomani yaana kwenye office ya mkuu wa wilaya/mkoa au kwa kada utapewa cheti nacho ni cha serikali. Basi usihangaike kutafuta cheti wakati unacho
 
Serikali ina kazi ya kufanya Kama mtu kama wewe umeajiriwa na serikali halafu kichwa Bomu kiasi hiki.ni hatari kwa maendeleo ya taifa.
Umeanza majigambo sasa
Mada inaeleweka unaanza kuleta hoja za kutaka tutoleane matusi.
Nakuacha kwanza ukolee ndo nikujibu unavyopenda
 
Hii ndio comment ya kwanza niliyoona inatoa msaada, wengine wote wanaleta porojo za kuunganisha maneno mara Jamhuri ya Muungano mara msikiti.

Mkiona mtu kaleta jambo mjue hayo majibu marahisi anayajua tayari.

Nashukuru sana, ushauri wako ntaufanyia kazi.
Hicho cheti Cha BAKWATA kimetoka Saudi Arabia mkuu?
 
Back
Top Bottom